SMS Nzuri: Meseji za Visa Vya Kushangaza

Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station

“Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…”

Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?

John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura “MAJANGA” umfikie popote pale alipo…!!!

Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?

RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?

JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, β€œHuyo nguruwe umeshamuondoa?’ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja

Angalia hawa kina mama, ni shida..!

Mama mdaku alishangaa kila siku mchungaji anaingia nyumba ya jirani yake ambaye hana mume, akawa anajiuliza anakwenda kufanya nini? Uzalendo ukamshinda akamuuliza “Mwenzangu, mbona kila siku mchungaji anakuja kwako, vipi anakuja kukuombea?” Akajibiwa “Nyoo, umbea tu! Mbona kwako kila siku anakuja mwanajeshi kuna vita! chefuuuu 😳😳😳😳😳

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hawa wanaume wanaopenda wanawake hovyo barabarani wamepatikana, hawatarudia πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Marafiki wawiliΒ (Jose na Ben)Β walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.

Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:

Ben:Β Muone yule mrembo amenirushia busu

Jose:Β tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..

(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)

Ben:Β yule mwanamke ameniita!

Jose:Β Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.

Ben:Β Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu

Jose:Β Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kuleΒ (akihisi kutotiliwa maanani)

(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini).. πŸ”ŠπŸ”Š

Lady:Β _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!

Ben:Β Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!

Lady:Β Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo

(akimuonyesha lundo la nguo)

(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)

(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)

Ben:Β Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???

Jose:Β Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha,Β Nilizifua Mimi Juzi!!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

When an experienced person speaks … πŸ‘‚you must listen..!

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi… njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote

Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoido…..leo nimetoka Likizo Moshi,

“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!

Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!…kamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?…kwa Style ipi?

Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!…sasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,…hakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,….hapa sasa nikapata wazo!

“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”

“Mia mbili tu Kaka!”

”Ok”

Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,

“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)

“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’

Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!…Sasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!…My God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!

“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”

Kimya…

“Dogo huu Mzani vipi?”

Kimya…

Dogo ana dharau huyu!…Sasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!….ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!…Dogo hakuwepo!….na Mabegi pia hayapo!…lap top haipo!….NIMEPIGWA!

Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!….sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!…yaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!…niitieni Ambulance!

πŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌπŸ™†πŸΌ

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About