SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Kukuchangamsha

Wanaume wote ni waaminifu

Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.

Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.

Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?

Jamaa: NDIYO.

Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.

Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?

Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.

Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”

Jamaa: NDIYO.

Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?

Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!

Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.

*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Kizungu nacho ni sheeeedeer

Mtalii: Do you have vegetables here.
Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa.
Waiter: Vijimeza vidogo hatuna.
Mtafsiri: No sir, they don’t have.
Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs.
Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto.
Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa.
Mtafsiri: They don’t cook here
Mtalii: What type of snacks do you have here.
Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa,
Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote
ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao.
Mtafsiri: They don’t cook any type of snacks
here,
maybe you can go back and eat at home.
Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice.
Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo.
Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena
sasa hivi kabla sijakasirika.
Mtafsiri: Lets get out of here
πŸ˜πŸ˜πŸ˜πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Usicheke pekeyako

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Hii ndiyo bongo sasa!!

Hii ndio Bongo

Ilikuwa Ijumaa mida ya saa 10 jioni, mzee mmoja aliingia na kibinti kizuri kwenye yard ya magari mapya.

MZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi….kabinti akazunguka yard yote mwisho akachagua Verrosa metallic .

BINTI: Mi naitaka hii

MZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima upate gari uloichagua mwenyewe. Mzee akatoa kitabu cha cheki na kuandika palepale na kumpa mwenye yard

MUUZAJI: Sasa Mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa Account yako ina pesa benki. Naomba namba yako ya simu Mzee

MZEE: Hakuna tatizo (akampa namba). Haya twende zetu sweetie Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako…

Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.

MUUZAJI: We Mzee kavu sana, akaunti yako haina hata senti tano.

MZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

πŸ’¦πŸ˜†πŸ’¦

Haya mapenzi jamani! Umewah kumpenda kwa kihivi??

Sijui Kama ushawai fall in love ile haswaa..

yani unampenda mtoto hadi akikupigia ile sauti ilivo tamu unajiskia kutafuna na kuimeza hiyo simu

Akikuita tu “my love”unajiskia tu kuvua nguo mwenywe
..
hicho kiupendo ukiwa nae unajskia unaweza piga wanaume 8 kwa pamoja

Yani ile love mtashinda pamoja kutwa nzima afu usiku unakopa salio umpigie muongee

Yani yale mapenz kiasi ukiona love story za romeo na Juliet unaona hakuna wanachofanya coz mapenz yao hayafikii yenu..

ile true love akikuangalia machoni akuguse mashavu afu akwambie,”I love u”
Unajishikilia kwenye ukuta usizimie..

yani ukimfikiria unaweza kulala chini ya kitanda Ku dilute hiyo feeling coz ni too much..

Umewahi kufeel hivyo??

Kama ushawai experience hivyo?? Basi HIYO SIYO “LOVE” NI “BANGI” PLZ ACHA KUTUMIA!
#ishakua_biashara_kichaa

Angalia nilichomfanyia huyu dereva sasa

Tulikua kwa basi tunaelekea arusha,ile namcheki dereva kumbe ni best yangu na basi ilikua kwenye spidi hatari, nikaenda kumziba macho nkamuulizaΒ otea mi ni nani, kabla hajanijibu nikasikia kishindo kikubwa sana
NA SASA HIVI NIMEZINDUKA NIMEONA ABIRIA WOTE TUPO WODI NAMBA 3 HAPA KCMC MOSHI. πŸ€•πŸ€•πŸ€•πŸ€•
SODA ZA WAGONJWA PLIIIZ!!! πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.

Angalia jamaa alivyouweza huu mchepuko wake

Kuna mchepuko nilimtumia nauli jana ili aje,.kwang sasa leo kaniambia eti ” nimesahau ile line yenye M-pesa home plz nitumie tena kwa tigo mpenz””!! Me nikajifanya chizi nikatuma Kule kule kwenye voda (aliosema kaacha home) Nikatuma huko message ivi “nikuongezee Sh. Ngapi tena mpenz..!!” Akanjbu “elfu 20,000 tu mpenzi” Mtuhurumie jamani πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Mzunguko wa elimu kiafrikaafrika

01.πŸ‘‰ Wale wanafunzi walioongoza Mashuleni, wanaenda kwenye Engineering na Medical school.

02.πŸ‘‰ Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.πŸ‘‰ Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia Siasa na kuwaongoza wote hapo juu. Yaani wa kwanza na wa pili.
04.πŸ‘‰ Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu wote hawana raha.
05.πŸ‘‰ Wale waliopata Zero na waliokataa shule wanakuwa waganga wa kienyeji, wote hapo juu watamtafuta huyu, pale mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‰πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸƒπŸƒπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œπŸ˜œ

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About