SMS Nzuri: Meseji za Vihoja Vya Kukubadilisha Mudi

Angalia nilichokifanya Jana kumkomoa x-wangu

Mwenzenu nilikatiwa umeme jana basi leo si nikaamua kwenda kununua luku ya 10,000. Kufika njiani nikatamani fursana nikaingia kijisupermarket mara sindo nakutana na ex wangu! Mshenzi yule kaniona mimi sijui alikua na mpango wa kununua vocha ya jero eti kabadili kanunua vocha ya buku tano ilimradi nione maisha yake safi tangu tuachane. Mambo ya kijinga spendi kudadeky nimetoa buku kumi nikanunua mipampers nami nijifanye nimeowa nina mtoto halafu huyoo nikashika njia yangu.

Sasa washkaji zangu tafadhalini mwenye mtoto au shida ya pampers naomba anunue kwangu maana leo nalala tena kiza πŸ™†β€β™‚

Hii mitoto mingine mijinga, cheki alichokifanya huyu

Nimeamka asubuhi nikiwa na elfu 1 tu mfukoni, nikamtuma mtoto wa jirani akaninunulie maandazi nipate kunywa chai. Baada ya muda namuona anarudi huku analamba askrimu ya AZAM kama Simba vile. Nikamuuliza maandazi yako wapi? Akanijibu eti wakati anafika yanapouzwa maandazi akagundua kuwa kapoteza hela yangu, hivyo akaanza kurudi, ila bahati nzuri wakati anarudi ili kuja kunitaarifu kuhusu kupotea kwa hela yangu, njiani akaokota elfu 1 ambayo kuna mtu alipoteza ndio akaamua kununua askrimu….kwa sasa niko polisi na mtoto yuko dispensari na mamakeπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€

Angalia Kiingereza kilivyoniponza

Shikamoo kingereza..!

Baada ya kufika Kempiski nikaona menu imeandikwa:

Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole!

Price: TSH 44,000/=

Nikaagiza!

Nilipoletewa ndio nagundua kwamba:Β ni makande na parachichiΒ ..πŸ€”

hapo ndo unagundua mwalimu wa kiingereza alikuwa sio mtu wa mchezo mchezoπŸ€’πŸ’¨

Huyu jamaa amekomeshwa, majambazi ni shida!

CHEKA KIDOGO
Majambaz waliliteka gar moja lililokua limeshehen abiria
Baada ya abiria kusachiwa na majambaz hao na kukutwa hawana pesa, majambaz wakasema kila m2 atapigwa viboko (bakora) kutokana na namba ya shati alilovaa
Aliyekua hana namba atasalimika
Kaz ikaanza, jamaa alievaa jez ya ROONEY wa Man U akapigwa fimbo 10, mwengine alievaa nguo ya 50cent akapigwa 50, n.k, sasa kwa pemben kulikua na jamaa analia sn yaani kila akijiangalia, kumbe alikua amevaa fulana limeandikwa LOWASA 2015 duuuh! Unajua kilichotokea ngoja niweke cm chaji kwanza.

Alichojibu dalali baada ya kufumwa na mke wa mtu ndani ya nyumba ya kupanga

Dalali aliwatafutia jamaa chumba Buguruni karibu na reli, nyumba nzuri sana. Jamaa na mkewe wakahamia kwa furaha, lakini furaha yao iliisha walipokuja gudundua nyumba ile iko karibu mno na reli treni ikipita mpaka kitanda kinacheza.

Siku hiyo dalali akapita mke akamwita na kumwambia tatizo wakati treni inapita, wakaanza kubishana, yule mama akamwambia dalali kwa kuwa kuna treni itapita sasa hivi… njoo ndani uone mwenyewe.

Bahati mbaya wakiwa wamejilaza kitandani ili dalali aone adhabu wanayopata, Mzee mwenye mali alirudi ghafla, akauliza,

‘Nyie mnafanya nini hapa?’

Masikini dalali kwa woga mkubwa akajibu’ Tunangoja treni’

Kilichowakuta boss, mke wake na mfanyakazi wao

Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue.
Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.
Ilikua ni bahati tu alimvizia na
kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua
anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali.
Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss: Bakariiii!
Bakari: Naam baba!
Boss: nani anakunywa wine yangu?
Bakari kimyaaaa hajibu kitu!
Boss: Bakariiiii !
Bakari: naam baba!
Boss: nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Boss kimyaaaa!
Bakari: Baba babaa!
Boss:ndio Bakari!
Bakari: Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?

Boss kimyaaaaaaa!
Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!

Mke wa Boss akaingilia kati
Mama: nyie msinitanie kabisa mnasemaje?
Bakari: kweli mama ukiwa jikoni husikii kitu nenda uone

Mama akaenda na Bakari akaanza

Bakari: mamaaaa!
Mama: abeee!
Bakari: hebu niambie hiyo mimba ni ya baba au yangu?
Mama kimya

Bakari: mamaaaa!
Mama: abeeee!
Bakari: hebu niambie ukweli hiyo mimba ni ya baba au yangu??
Mama kimya

Mama akatoka nje: kweli humu jikoni kuna tatizo nilikuwa nasikia jina tu

Jinsi ya Kubana matumizi X-mass

Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.

πŸŽ€βœ¨Marry Xmas & Happy new year.βœ¨πŸŽ€

Namna wazazi wanavyoongea na mabinti katika umri tofauti

Miaka 13: Usipende wavulana ni wabaya.
Miaka 18: Sitaki nikuone na yule mvulana tena!
Miaka 23: Lini utatuletea mchumba wako?
Miaka 26: Wenzio wanaolewa.
Miaka 30: Tumekuambia kwamba acha
kuchagua sana wanaume, hutaki kusikia!
Miaka 33: Kuna mtu wa Mungu yupo kule
anaombea unaweza kupata mchumba
Miaka 36: At least pata mtoto mmoja.
Miaka 39: We will take care of all the wedding
bills…yeyote ni sawa sisi tutagharamia kila kitu mwanetu wee mlete tu .
Miaka 45: hivi kweli nani alikuroga.?

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ changamkia fulsa umri ukifika

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About