SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Kuwaadisia
Kilichotokea wakati mchungaji akifungisha ndoa ya Mashoga
Mchungaji mmoja baada ya kuwafungisha ndoa “MASHOGA” wawili alipata wakati mgumu kutamka kuwa “sasa ninyi ni MKE na MUME”
atafanyaje wakati wote ni wanaume? mchungaji akapiga moyo konde na kusema “tangu sasa ninyi ni MAN UNITED”
Tofauti ya mchaga na mhaya wakipata kazi
Mchaga hata apate kazi bank bado atasema yupoΒ kibaruani.
Acha sasa mhaya apate kazi katka mashine ya kusaga na kukoboa; utaskiaΒ i work as a crucial engineer in a monocotyledon finalizing company
πππ
Β
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbeleπππππ
Nilichokifanya wakati naangalia taarifa ya habari
Jana wakati naangalia taarifa ya habar mtangazaji akasema “mpenz mtazamaji nataka nikupeleke moja kwa moja had marekani” nikazima TV kwa haraka nikaenda kuvaa viatu. Hadi sahv bado nmekaa hapa seblen nahisi bado wanaihangaikia Visa yangu
ππππππ
Wasichana wa leo
Jamaa yupo ndani ya Range rover yake mpya na msichana ambaye ni mpenzi wake.
#Jamaa: kuna siri flani nimeitunza moyoni mwangu kwa muda mrefu na nikaona kama nitakuambia lazima utaniacha.
#Msichana: siri gani hiyo mpenzi wangu?
#Jamaaa: nimeoa.
#Msichanaa: HΙΙΙΙΙΙΙΙ! We umenishtua sana,mm nilifikiri hili gari sio lako!
πππ€π€
Sasa Hawa wadada Wapo in Relationship Na Nan!!??
Asilimia 76% Ya Wasichana Kila Ukiwatongoza Wanakwambia Wapo In relationship SAWA ATUKATAIβ¦
Asilimia 98% Ya Mamen Wapo SINGLE⦠HAPA NDIPO HESABU ZANGU ZINAFELI..
Sasa Hawa wadada Wapo in Relationship Na Nan!?.
Ndoa zina mambo, cheki haya mambo ya mtu na mke wake
Mke: mume wangu leo 2badilishe stail kwani nimechoka kla siku hiyo hiyo tu
Mme: kwel mke wang hata mimi nilikuwa nataka nikuambie hivyo hivyo
Mke: sasa stail ya leo wewe utaosha vyombo mimo nitaangalia tv
Mme: huna haya wala hujui bayaβ¦!!!
we unadhani ni xtail gani mume aldhani???
Kuwa na Binti aliyeacha shule
Kuwa na binti aliyeacha shule ni BALAA.
Anaweza kukuacha kwa staili ileile alotumia kuacha SHULE
π π π π π
Duh! Hii sababu ya huyu mwanaume kulewa ni shida
π§: “Mpenzi, nakuomba uache kulewa”
π¨: “poa, na wewe acha kutumia make up”
π§: “Mimi napaka make up ili unione mzuri”
π¨: “Na mimi nalewa ili nikuone mzuri”
Vodka hatareeeππ
Alichokisema mwizi baada ya kushinda bahati nasibu
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??.
Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo
Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaaβ¦
ππ
Cheka kidogo: Majibu ya mhindi kwenye mtihani wa Kiswahili alipoambiwa ajibu methali
Mhindi kwenye mtihani wa kiswahili anaambiwa amalizie methali:
(a)Nyani haoniβ¦..valisa miwani!
(B)Debe tupuβ¦.weka dengu!
(c)Masikini akipataβ¦.iko acha iba!
(d)Penye kuku wengiβ¦chinja bili,tatu!
(e)Asiyesikia la mkuuuβ¦.peleka yeye polisi!
(f)Penye wengiβ¦β¦iko kutano ya chadema!
Ungekua wewe ndio boss wa huyu jamaa ungempa kazi? Ungemjibu nini?
*Boss*:-kijana unataka nini ndani ya ofisi zangu?
*Jamaa*:-Samahani naomba kazi ya ulinzi ndugu.
*Boss*:-umesoma mpaka wapi?
*Jamaa*:-mpaka form four.
*Boss*:-unajua kingereza?
*Jamaa*:-kwani hao wezi wanakuja na wazungu???.
π
π
π
π
π
π
Alichofanya maasai baada ya kupanda Tax
Baada ya kupanda daladala aina ya DSM kutoka Mbagala chalambe mpaka Mwenge na kulipa sh 500.Masai akachukua tax wakati wa kurudi.walipofika sasa shughuli ilikuwa hivi.
Masai: we dureva? Naulisa Ng’ombe na mbusi ipi ngali?
Dereva: Ni ng’ombe ghali Masai.
Masai: kwanini Ng’ombe ngali?
Dereva: kwa sababu ni mkubwa zaidi ya mbuzi
Masai: umepata..na mbusi na kuku ipi ngali
Dereva: ni mbuzi kwa sababu nae ni mkubwa kuliko kuku.
Masai: Umepata..
Masai: sasa me nimekwenda kule mwenge kwa ngali kubwa nikalitoa sh. 500 hii yko ndogo unasema nikupe 40,000 wewe acha wizi.. Nitakupa 250 Tu..wee acha lbia moraniβ¦!!!
Haya ndiyo madhara ya kulala kanisani
Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia
Huyu mgeni wa huyu jamaa ni shida
Pale unapokuwa umefulia sanaβ¦
Mgeni anakutembelea Maskani kwakoβ¦.Unaamua Kuchukua Ile Sh 600 iliyobaki na kwenda Dukani Kumnunulia Soda Unaondoka na Chupa Mbili Unanunua Fanta Moja kwaajil ya Mgeni na Ile Chupa ya Sprite Unaijaza Maji ili Ukirudi Uweze kumpa Kampani Mgeniβ¦β¦Unafika Seblen Unampa Ile soda ya Fanta Mgeni anakuambia Fanta huwa situmii Nipe hiyo sprite β¦..Bwanaβ¦.Bwana. β¦Bwanaβ¦.Weee ππππππππ
Tenda Wema Uende Zako
Nimekuta panya ana struggle kuingia chini ya mlango wa jirani yanguβ¦
Nikagonga mlango Jirani kafungua panya akapenya mi nkaenda zanguβ¦..
Tenda Wema Uende Zako!!! Sipendi Ujinga mimi kwanini panya wa watu apate shida
Huyu kashauzwa!! Angalia kilichomkuta sasa
Jamaa alionekana Mnyooooonge sana ikabidi mpita njia amuulizeβ¦
Kaka, mbona u mnyonge hivyo?”
Jamaa : ‘aaaaah we niache tu, kuna rafiki yangu nimemkopesha laki tano akafanye PLASTIC SURGERY ya uso, Mwanaharamu sasa nashindwa kumtambua!!!
ππππππ
Maujanja ya kumkalisha mwanamme wako nyumbani weekend haya hapa
Siku hizi wa naume licha ya kukimbia nyumba zao kwa kisingizio cha kazi maajabu weekend hasa Jumamosi utasikia wanaaga nafika hapo njiani naja naenda kununua gazeti.
Kumbe wanaenda kunywa supu unasubiri wee mpaka alasiri au jioni
Hivyo wanandoa wengi hili limekuwa tatizo mwanaume kiguu na njia asb mchana na njia kumuacha mama na watoto.
Nini kifanyike hasa weekenda Mwanaume ashinde NYUMBANI akikupumzikia??
Zipo njia nyingi mojawapo SUPU YA WEEKEND NA MAZUNGUMZO NA MKAO
Ni kweli wanawake wengi hamjuagi kuwakalisha waume home.
Anza hivi
Siku uko home wewe amka mapema kabla yake anza makeke jikoniβ¦
Mara blenda priiiiiβ¦ juiceβ¦ ama milk shakeβ¦. hahahaha..Utaona anasogea jikoni..
Wakati anakunywa juice ama milk shakeβ¦Anza kukuna naziβ¦
Chambua mnafuβ¦
Hapo jikoni kuna kanyama kanachemka⦠katia kitunguu tupia viazi 2 na ndizi.Hahaha..
ile harufu ikianza kutoka utasikia anafuata maji jikoni⦠hahahaha kwenye friji⦠wala hatumi..
Hahaahha⦠utasikia nini kiko jikoni?Hahahaa.
Mmiminie supuβ¦
Na ndizi mbili na kiazi kimoja kapilipili mbuzi pembeni..
Muulize kuna chapatiβ¦Mpe.. hahahahaha..Akimaliza supu nakuapia atasinzia..
.Akishtuka ugali na mnafu na nyama umeivaβ¦Mpe ale..Mshushie na glass ya mtindiβ¦Hahahaha..
analewa full Hata kama kuna mama junior anaambiwa usipigeβ¦
Hahahahahahaβ¦.Baada ya hapo acha apumzikeβ¦ aogeβ¦
Kisha funga ka khanga kako kepesi jilaze pembeni.. woiiiiiiiii..
Mkimaliza muombe pesa ya sokoniβ¦
NAKUAPIA HATA KAMA JANA YAKE ALIKUPA ATAKUPA TENA.
Hahahahaha.. jamaniβ¦
Hahahahaha⦠yani kwa raha ya supu⦠nakuapia utaambiwa hata mama alipiga simu jana⦠hahahaha.. ama utasikia mamii.. njoo uone njoo⦠unaitiwa kitu cha kwenye tv.. hahaha.
Hata hujaona mwanzo ila kwa raha yakasupu utaitwaβ¦
Hata kama huna kalio nakuambia utapigwa kibao hata cha mgongoβ¦. hahahahahahahahahaha.
Sasa wewe unaamka chai na mkate kama chuo cha uhaziliβ¦
Wali maharage kama jeshi la j
Recent Comments