SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Usiruhusu tabia hii itawale akili yako

Tabia ya kijidharau na kujiona hufai ama huwezi kufanya lolote ukafanikiwa maishani, hakuna mwanadamu aliyeumbwa ili ashindwe,, sote tu washindi zaidi, tunatofautiana njia za kufikia huo ushindi.

Rafiki yawezekana umeshajidharau… na kujitamkia maneno kadha wa kadha ambayo kimsingi yamekukatisha tamaa kabisa ya kufikia lengo fulani maishani… na ukabaki kushuhudia mafanikio ya wengine kila siku maishani.

Embu ondoa dhana ya kushindwa na kujidharau katika kila hatua upitiayo maishani haijalishi umeshindwa mara ngapi, jifunze kuwa na moyo mgumu na wa subila kwa kila hatua upitiayo maishani,, haijalishi upo katika hali gani? Maishani.

Kama ni maskini sana, usijidharau na umaskini wako ukaona wewe ni wa hali hiyo hiyo maisha yako yote,, no.. hapana, haukuumbwa ili uje kuwa maskini. Ila ni juhudi zako mwenyewe ndizo zitakazokutoa katika umaskini ulionao, haijalishi wewe una ulemavu wa aina yeyote ukajidharau na kujiona huwezi fanya lolote mbele ya jamii likakubalika.

Rafiki kuna walemavu kama wewe, wamejitambua na wameamua… hakika wamefikia mafanikio makubwa maishani. Ondoa dharau katika nafsi yako amini unaweza. Kuna walioshindwa kama wewe wakadharauliwa na kutemewa mpaka mate… ila walitambua kusudi la maisha yao na leo hii wamefikia mafanikio makubwa sana maishani, kwa nini?? Wewe ukate tamaa na kujidharau katika hali uliyopo ukajiona hauna maana? Hakika unaweza ukiamua,

Umuhimu wa kufanya Masaji

Kufanya Masaji kuna faida hizi zifuatazo;

Masaji uongeza kinga ya mwili

Masaji kushuka kwa homoni inayohusika na kupunguza maambukizi mbalimbali homoni ijulikanayo kama ‘cytokines’ vile vile masaji inashusha homoni inayohusika na matendo ya mashari homoni ijulikanayo kama ‘cortisol’.

Kufanya masaji hakukufanyi ujisikie ni mtulivu peke yake, bali pia kunaweza kukuongezea kinga yako ya mwili.

Masaji ya dakika 45 kwa siku imethibitika kuongeza uwingi wa seli nyeupe za damu (lymphocytes) ambazo ndizo hupigana dhidi ya vijidudu nyemelezi vya magonjwa mbalimbali mwilini.

Kufanya masaji huondoa tatizo la kukosa usingizi

Tafiti nyingi zinasema masaji inao uwezo wa kuamsha mawimbi ndani ya ubongo yanayohusiana na kutengenezwa kwa usingizi mzito (delta waves) na hii ndiyo sababu kwanini wengine hupitiwa na usingizi mzito mara tu baada ya mazoezi ya masaji.

Tatizo la kukosa usingizi linaweza kutibika kwa kufanya masaji tu kwakuwa masaji husaidia kupunguza uchovu na kuongeza uwezo wa kupata usingizi mtulivu kwa watu wa rika zote yaani watoto wadogo mpaka wazee ikihusisha wale wenye matatizo ya akili, kansa na magonjwa ya moyo, machache kati ya magonjwa mengi yawezayo kutibika kwa masaji tu.

Kuondoa mfadhaiko wa akili au Stress

Masaji huondoa hamaki na maumivu huku yakiongeza uwezo wa kupata usingizi mzuri na wa uhakika.

Masaji huondoa huzuni

Watafiti wanasema kuwa masaji kuongezeka homoni ijulikanayo kama ‘oxytocin’ na kupungua kwa homoni nyingine iitwayo ‘adrenocorticotropin’.

Oxytocin inahusika na matendo ya huruma, maono, upendo na ushirikiano wa kijamii. Wakati adrenocorticotropin yenyewe huhusika na kupungua kwa mfadhaiko (stress) moja kwa moja.

Kuondoa maumivu mbalimbali mwilini

Masaji hupunguza maumivu hasa ya mgongo na maumivu ya kichwa na maumivu ya kwenye mishipa.

Masaji huongeza uwezo wa kujiamini

Masaji hutuliza mwili na kuongeza concentration

Faida za kila kitu kwenye mti wa papai

Watu wengi hulitumia tunda la papai kwa sababu ya utamu wake. Hata hivyo mbali na kuwa na ladha nzuri, tunda la papai lina faida lukuki kwa afya ya mwanadamu.

Utajiri wa vitamin.

Tunda la papai lina vitamini A,B,C,D, na E jambo linalo liweka tunda hili katika kundi la matunda na vyakula vyenye utajiri mkubwa wa vitamin.

Faida zitokanazo na papai kiafya.

Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa :

Mbegu za Papai:

1. Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni.

2. Kutibu Udhaifu wa tumbo.

3. Kutibu Kisukari na asthma au pumu.

4. Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni.

Mizizi Ya Papai:

· Kutibu Kifua kikuu

· Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku

· Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda

· Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto

· Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)

Majani Ya Mpapai:

· Pia yanasaidia kutofunga choo

· Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.

· Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.

· Majani yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.

· Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.

· Papai likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani linaweza kutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.

· Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.

· Mbegu za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona bila dawa nyingine.

· Mizizi yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika.

Faida za kula mayai asubuhi

Mayai ni kitu kilichozoeleka na kinachopatikana kwa gharama nafuu. Kutokana na kuzoeleka huku watu wengi wamekuwa wakipuuza umuhimu au nafasi ya mayai katika afya zao. Pengine kupuuza huku kunatokana na mazoea au ukosefu wa elimu juu ya faida zinazopatikana kutokana na ulaji wa mayai.

Zifuatazo ndizo faida za kula mayai wakati wa kifungua kinywa;

Hutunza shibe

Protini zilizoko ndani ya mayai hukufanya kutohisi njaa mapema. Ina maana kuwa ukila mayai unaweza kukaa muda marefu zaidi bila kula ikilinganishwa na mikate au vyakula vingine vya ngano.

Husaidia ukuaji wa ubongo na uwezo wa kumbukumbu

Kirutubisho kinachojulikana kama “Choline” kinachopatikana kwenye mayai ni muhimu katika ukuaji na maendeleo ya ubongo. Pia kinahusishwa katika kuongeza uwezo wa ubongo wa kutunza kumbukumbu.

Hulinda macho

Kemikali za leutin na zeaxanthin zinazopatikana kwenye mayai zinaaminika kulinda macho dhidi ya madhara ya mionzi mibaya. Pia inaaminika kuwa zinazuia kutokea kwa tatizo la mtoto wa jicho uzeeni.

Husaidia kupunguza uzito

Ulaji wa mayai husadia kupunguza uzito wa mwili. Utafiti uliofanyika umeonyesha kuwa watu wanaokula mayai wamefanikiwa kupunguza uzito wa miili yao kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na wasiokula.

Mayai ni bei rahisi

Ukilinganisha na vyakula vingine vya protini kama vile nyama, mayai ni bei rahisi zaidi. Hivyo basi, mayai yanaweza kupatikana na kuandaliwa kwa urahisi wakati wa kifungua kinywa kuliko vyakula vingine.

Mayai ni chanzo kikubwa cha protini

Kama nilivyotangulia kusema kuwa mayai yana kiasi kikubwa cha protini kinachohitajika katika kujenga miili yetu. Hivyo basi ni vyema kula mayai asubuhi wakati wa kifungua kinywa ili kujipatia virutubisho hivi.

Kumbuka hili ni sawa na kusema kuwa amino asidi zote muhimu tunazozihitaji katika mlo zinapatikana kwenye mayai.

Mayai hayaongezi lehemu (Cholesterol)

Ni dhahiri kuwa mayai yana kiwango fulani cha lehemu. Lakini utafiti uliofanyika hivi karibuni umebaini kuwa lehemu iliyoko katika mayai inapoliwa haina athari kwenye kiwango cha lehemu kwenye damu. Hivyo hakuna haja ya kuhofu juu ya magonjwa ya moyo yatokanayo na lehemu.

Kumbuka afya yako ni muhimu sana. Jali afya yako kwa kuzingatia ulaji bora wenye tija. Kumbuka kuwa huwezi kuwa na tija katika shughuli zako bila kuwa na afya njema. Badili mtazamo wako leo; tafuta mayai na ule kwa ajili ya afya yako.

Staili nyingine za michepuko ni shida

Mtu na mkewe walikuwa bado wamelala asubuhi, mtu akapiga hodi mke akaenda kufungua mlango, si akakuta mchepuko wake,
MKE: Unataka nini we mpumbavu?

MUME: Nani huyo unamtukana?
MKE: Kuna mtu hapa anakichwa kama nenda urudi badae
MCHEPUKO:Nawewe pua kama poa
MKE:Miguu kama masaa mawili
MCHEPUKO:Masikio kama sichelewi
MKE: Ondoka hapa mjinga we. …… Akafunga mlango
MUME: mwambie ana macho kama sitoki leo ng’oo
SIPENDI UJINGA MM nikiwa na my love pr

Kuwa na mahusiano na msichana kama huyu ni changamoto, Mabinti bwana!

Binti: Hallow mpenzi, Mambo

Jamaa: Poa baby

Binti:Uko wapi?

Jamaa: Niko town napata lunch

Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi

Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?

Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.

Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.

Binti: Kwanini dear?

Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!

Madhara ya dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu

Dawa za kuulia wadudu maarufu kama viwatilifu zimetengenezwa kwa lengo la kuangamiza wadudu wanaoharibu mazao au wanaomdhuru binadamu. Hata hivyo kutokana na sababu kuwa lengo la dawa hizi ni kuangamiza, huathiri pia viumbe hai vingine akiwemo binadamu.

Takwimu kutoka shirika la afya duniani WHO zinabainisha kuwa kuna zaidi ya vifo 220,000 vitokanavyo na athari za sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu—viwatilifu.

Ikiwa unataka kuweka afya yako salama, basi karibu nikushirikishe athari 8 kiafya za dawa za kuulia wadudu — viwatilifu.

1. Husababisha saratani.

Watafiti mbalimbali wa maradhi ya saratani wanaeleza kuwa dawa za kuulia wadudu zinachangia kwa kiasi kikubwa kusababisha seli za saratani mara zinapoingia kwenye mwili wa binadamu.

Hatari hii hutokea zaidi pale ambapo mtu anakula vyakula vilivyoathiriwa na sumu za dawa za kuulia wadudu.

2. Huvuruga mfumo wa homoni.

Mwili wa binadamu huzalisha homoni mbalimbali zinazowezesha viungo mbalimbali kufanya kazi vyema.

Dawa za kuulia wadudu zinapoingia mwilini huathiri mfumo wa homoni wa binadamu na kuufanya usifanye kazi vyema.

3. Huathiri mfumo wa uzazi.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa matatizo ya uzazi kati ya wanaume na wanawake huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.

Inaelezwa kuwa sumu hizi zinapoingia mwilini kupitia matunda au mbogamboga huharibu mfumo wa uzazi na kusababisha ugumba au utasa.

4. Huharibu ubongo.

Madawa ya kuulia wadudu — viwatilifu huathiri pia mfumo wa ubongo hasa kwa watu wanaoyapulizia au kukaa nayo karibu kwa muda mrefu.

Maradhi kama vile Mild Cognitive Dysfunction (MCD) ambayo humfanya mtu ashindwe kutambua vyema maneno, rangi au namba huchangiwa kwa kiasi kikubwa na athari za dawa za kuulia wadudu.

5. Huathiri mama mjamzito na mtoto

Mama mjamzito anatakiwa kuchukua tahadhari nyingi sana wakati wa ujauzito ili kulinda afya yake na mtoto aliyeko tumboni.

Matumizi ya viwatilifu ndani ya nyumba au karibu na makazi kwa lengo la kuua wadudu kama vile mbu, chawa, kunguni, au utitiri kunaweza kumwathiri mama mjamzito na mtoto kwa kiasi kikubwa.

Inaelezwa kuwa sumu hizi zinaweza kusababisha mtoto kuzaliwa bila viungo vyote, kuzaliwa kabla ya wakati au hata kifo.

6. Huharibu viungo muhimu vya mwili

Kumekuwa na taarifa mbalimbali ulimwenguni zikieleza kuwa dawa za kuulia wadudu huharibu viungo muhimu vya mwili kama vile figo na ini.

Utafiti uliofanyika huko India ulibaini kuwa watu wengi waliokufa kutokana na maradhi ya figo waliishi katika mazingira yenye sumu za kuulia wadudu au kula vyakula vyenye mabaki ya sumu hizo.

7. Huathiri mfumo wa upumuaji

Kutokana na watu wengi kutumia dawa za kuulia wadudu bila kuvaa vifaa vya kujikinga, wengi huvuta sumu zilizoko kwenye dawa hizo na kusababisha kuathiri mfumo wa upumuaji hasa mapafu.

Hivyo ili kujikinga na athari hii inashauriwa kuvaa vifaa bora vya kuzuia kuvuta sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu.

8. Huathiri ngozi

Kama ilivyo kwenye swala la kuathiri mfumo wa upumuaji, watumiaji wengi wa dawa za kuulia wadudu hawakingi ngozi zao kwa mavazi au vifaa maalumu vinavyoepusha athari za dawa hizo kwenye ngozi zao.

Ikumbukwe kuwa sumu zilizoko kwenye dawa za kuulia wadudu zinaweza kuingia mwilini kirahisi kupitia ngozi na kusababisha athari nyingi za kiafya.

Naamini umeona jinsi ambavyo dawa za kuulia wadudu — viwatilifu zinavyoweza kuathiri afya ya binadamu ikiwa hazitatumiwa kwa uangalifu na kwa kufuata kanuni muhimu za matumizi yake.

Ikumbukwe kuwa vifo vingi na matatizo mbalimbali ya kiafya hutokana na mwili wa binadamu kukutana na sumu mbalimbali, hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About