Meseji za Vichekesho na Vituko

Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza 🍺 huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili 🍺🍺 kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu 🍺🍺🍺 huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..

Bia ya nne 🍺🍺🍺🍺 huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano 🍺🍺🍺🍺🍺 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; β€˜Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au β€˜ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita 🍺🍺🍺🍺🍺🍺 na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika…….

Hii ndio ndoto ya harusi ya kila msichana anayotamani

GIRL: Baby, hebu niambie harusi yetu itakuwaje?
BOY: Yaani hii haijawahi kushuhudiwa, ngoja nikupe kionjo kidogo tu
GIRL: Enhee…
BOY: Kwanza siku ya kupeleka mahari nitaswaga zizi zima la ng’ombe napeleka kwa babu yako
GIRL: Ooh baby u care..
BOY: Siyo hivyo tu, baba yako ntamnunulia Range Rover Sport na mama mkwe ntampa Range Rover Evoque
GIRL: Baby u are awesome…
BOY: Halagu mdogo wako wa kiume ntampa Prado Tx, na hapo nimesukutua tu mdomo sijaanza kula….
GIRL: Enhee…na sisi??

BOY: Sisi tutachukua mtaa mzima Oysterbay, kila wiki tutaishi nyumba tofauti
Halafu siku ya harusi yetu tutakodi zile meli zinabeba makontena ndiyo iwe ukumbi wetu, itatupeleka hadi Maldives
GIRL: Baby I love you
BOY: Tukitoka hapo tunaenda honeymoon Bahamas….halafu tunaenda Taiwan shopping ya fenicha, kisha Japan shopping ua electronics, halafu tunaenda Dubai nikununulie vito vya thamani
GIRL: Ooh my sweetheart…halafu tukitoka huko??
BOY: Tukitoka huko nachukua ndoo ya maji nakumwagia uzinduke usingizini na ndoto yako imeishia hapo

SOMA HII: Kama wewe ndo baba au mama hapa ungefanyaje!???

Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika. Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit,
boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali. Siku hiyo Bakari alikua jikoni,boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss:- Bakariiii!
Bakari:- Naam baba!
Boss:- Nani anakunywa wine yangu?

Bakari:- Kimyaaaa hajibu kitu! Boss:- Bakariiiii !
Bakari:- naam baba! Boss:- nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!
Bakari:- kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.
Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?
Bakari: Baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.
Bakari:Babaa!
Boss: Naam Bakari!
Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?
Boss:- kimyaaaa!
Bakari:- Baba babaa!
Boss:- Ndio Bakari!
Bakari:- Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?
Boss:- kimyaaaaaaa!

Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.
Mama akasema msinizingue nyie…Mbona siwaelewi..
Bakar: mama kama uamini na ww nenda uone.

Mama akaenda jikoni..
Bakari: akaita mamaa
Mama : bee bakari
Bakari: eti hiyo mimba niya baba au yangu.?
Mama kimya
Bakari; mama nakauliza tena hiyo mimba niyababa au yangu.

Mama akatoka aisee kweli humu unasikia jina tu…..πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„

Tofauti kati ya mwanamke na mwanamme

UTOFAUTI KATI YA MWANAMKE NA MWANAUME
1. Kwenye mshituko; mwanaume hushituka halafu huangalia nini kimemshitua, mwanamke hushituka halafu huzimia hivyo ataambiwa na mwanaume kilichomshituaπŸ˜‚πŸ˜‚
2. Kwenye kupenda; mwanaume huanza kutamani alafu hupenda, mwanamke huanza kupenda moja kwa moja bila kumjua vizuri huyo ampendaeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
3.Kwenye kusaidia; mwanaume hutoa msaada alafu uhuzunika, mwanamke huuzunika badae ndo anakumbuka km msaada unahitajikaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
4.Kwenye maamuzi; mwanaume hufikiri ndipo hutenda, mwanamke hutenda halafu hufikiriπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
5.Kwenye kudanganya; Mwanaume hudanganya ili kumlinda mwanamke, mwanamke hudanganya ili kumkomoa mwanaumeπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
6.Kwenye ugomvi; wanaume hupigana halafu hueshimiana, wanawake hupiga mikelele alafu kila mmoja hurud kwake, kexho tenaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
7.Kwenye ndoa; mwanaume hutafuta maixha ndipo huoa, mwanamke huolewa ndipo atafute maishaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
8.Kwenye kukata tamaa; mwanaume hukata tamaa mapema ili jambo lisimsumbue, mwanamke hajui kukata tamaa hadi aumizweπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
9.Kwenye kula;Mwanaume hushiba alafu huanza madoido, mwanamke huanza na madoido alafu badae hujilaumu hakushibaπŸ˜‚πŸ˜‚
10.Kwenye siri; Mwanaume hutunza siri hasa za aibu, mwanamke humueleza shoga yake badae hugombana nae baada ya kumrudia mwenyewe kwa siku 2 tuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Hizi ni baadhi tu ya sifa tofauti kati ya mwanaume na mwanamke….. VIVA GENTLEMENπŸ‘ŠπŸ½πŸ‘Š

Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza

Zuzu: Mambo Anna!
Anna: Poa!
Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyeshe…
Anna: Kitu gan?
Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda)
Anna: Haya nionyeshe…

Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga)
Anna: Haya nionyeshe sasa!..
Zuzu: Zima taa kwanza (akazima)
Anna: Mhm…nionyeshe sasa!
Zuzu: Haya njoo hapa kitandani…
Anna: Ok, nionyeshe!
Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizani… Acha mawazo mabaya ww???

Tofauti ya mke na mchepuko!!!

Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.

Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.

Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.

Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.

Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.

Tv ina remote lakini Simu haina.

Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.

Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.

Ya mwisho na ya kuzingatia

Tv haina Virusi lakini Simu inayo.

KUWA MAKINI.

Ameniomba nimfungulie akaunt facebook cheki nilichomjibu

Leo nimechoka zangu alafu shangazi amekuja anataka nimuunganishe facebook. Imebidi nimwambie
lazima awe na picha passport size 4 kwaajili ya kuweka profile picture, barua kutoka kwa afisa mtendaji na Atm card ya nmb bank. Alafu awe na marefa wanne ambao wamekuwa facebook for more than 3 years. Amesema
hataki tena kujiunga fb!

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Saa ivi niko zangu nimelala naendelea kupunguza uchovu

Shopping Cart
🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About