SALA ZA KUMWABUDU YESU KATIKA EKARISTI TAKATIFU

SALA YA KUMWABUDU BWANA YESU KATIKA SAKRAMENTI TAKATIFU

Ee Yesu Kristu,/ Bwana wangu na Mungu wangu/ ambaye ninasadiki kuwa upo hapa/ katika Sakramenti Takatifu ya Altare;/ pokea kitendo hiki cha kukuangukia kifudi fudi/ kama ishara ya tamaa niliyonayo ya kukuabudu Wewe/ bila kuchoka/ na kukushukuru kwa mapendo yako makubwa/ yasiyo na kipimo/ ambayo Moyo wako Mtakatifu sana/ unawaka katika Sakramenti Takatifu hii./ Siwezi kukushukuru vizuri zaidi/ kuliko kama ningetolea kwako/ matendo yangu yote ya kukuabudu/ unyenyekevu wangu/ uvumilivu na mapendo/ ambayo huu Moyo Mwabudiwa ulifanya,/ bado unafanya/ na utaendelea kufanya katika uzima wa milele mbinguni./ Ninaahidi kupitia Moyo huu,/ nitakupenda,/ nitakutukuza,/ na nitakuabudu kama nitakavyoweza./ Ninajiunganisha na hii Sadaka Takatifu/ ambayo unatoa kwa Baba Mungu/ na ninatolea kwako utu wangu./ Ninakuomba kuangamiza ndani yangu/ dhambi zote pamoja na majeraha yake/ na usikubali kunitenga nawe milele./ Amina.

(Na Mt. Margareta Maria Alakoki)


SALA MBELE YA SAKRAMENTI KUU I

Utukuzwe ee Bwana wangu Yesu Kristo./ Uliagua kifo chako./ Katika karamu ya mwisho ulitumia mkate wa kidunia/ ukafanya mwujiza na kuugeuza/ kuwa Mwili wako azizi./ Kwa mapendo ukawapa Mitume Mwili huo/ uwe kumbukumbu la mateso yako mastahivu./ Uliwaosha miguu kwa Mikono yako Mitakatifu./

Uheshimiwe, ee Bwana wangu Yesu Kristo./ Kwa kuhofu mateso na kifo,/ Mwili wako usio na kosa ulitoka jasho la damu/ badala ya maji./ Juu ya hayo uliutimiza wokovu wetu/ uliokuwa umetaka kuufanya./ Hivyo ulionyesha waziwazi mapendo yako/ uliyo nayo kwa wanadamu./

Utukuzwe, ee Bwana wangu Yesu Kristo./ Ulipelekwa kwa Kayafa,/ Wewe uliye Hakimu wa wote./ Ukaruhusu kwa unyenyekevu kutolewa kwa Pilato/ uhukumiwe naye./

Utukufu uwe nawe, Bwana wangu Yesu Kristo,/ kwa kuwa ulivumilia kuchekwa tena/ uliposimama huko,/ umevaa joho jekundu,/ umetiwa taji ya miiba mikali sana Kichwani,/ ukavumilia kwa saburi kubwa/ kutemewa mate katika Uso wako mzuri,/ kufumbwa Macho,/ na kupigwa mno na wajeuri/ ngumi na makofi Mashavuni na Shingoni./

Sifa iwe nawe, Bwana wangu Yesu Kristo,/ Kwa uvumilivu mkubwa ulikubali kufungwa nguzoni,/ kupigwa mijeledi kijeuri,/ kujaa damu na hivyo kusukumwa barazani kwa Pilato./ Ulionekana kama mwanakondoo asiye na kosa./

Heshima iwe nawe, Bwana wangu Yesu Kristo./ Umehukumiwa Mwili wako mzima/ Mtukufu wenye kutoka damu/ ufe msalabani./ Ulichukua msalaba kwa Mabega yako Matakatifu/ na kuumwa sana./ Kwa ghadhabu walikusukuma mbele/ mpaka mahali pa mateso,/ wakakunyang’anya nguo zako./ Hivyo ulikubali kupigiliwa msalabani./

Heshima ya milele upate Wewe,/ Bwana wangu Yesu Kristo./ Ulipokuwa katika taabu kubwa hii,/ ulimkazia Mama yako mstahivu/ Macho yako ya hisani na mapendo/ na unyenyekevu,/ ndiye Mama yako asiyekosa hata mara moja/ wala kukubali dhambi yeyote./ Ulimweka katika ulinzi mwaminifu/ wa Mfuasi wako ili kumtuliza./

Milele utukuzwe, ee Bwana wangu Yesu Kristo./ Ulipokuwa mwenyewe taabani,/ uliwapa wakosefu wote/ matumaini ya kuondolewa dhambi/ kwa kumwahidia mnyang’anyi aliyekuendea/ utukufu wa paradisi kwa huruma yako./

Sifa ya milele iwe nawe, Bwana wangu Yesu Kristo,/ kwa kila saa ulipovumilia uchungu/ na taabu kubwa mno msalabani kwa ajili yetu sisi wakosefu,/ maumivu makali sana/ yaliyotoka katika majeraha yako,/ yakapenya bila huruma Roho yako Takatifu./ Yakaingia kikatili katika Moyo wako Mtakatifu/ hata ukakatika,/ ukapumua Roho yako,/ ukainama Kichwa,/ ukaweka Roho yako mikononi mwa Mungu, Baba yako./ Na baada ya kufa uliacha nyuma Mwili baridi./

Utukuzwe, ee Bwana wangu Yesu Kristo,/ kwa Damu yako azizi na kwa kifo chako kitakatifu/ ulizifidia roho za watu,/ ukazitoa ugenini/ na kuzipeleka kwa hisani yako katika uzima wa milele./

Milele uheshimiwe, Wewe Bwana wangu Yesu Kristo./ Siku ya tatu ulifufuka katika wafu,/ ukajionyesha kwa wafuasi wako,/ ukapaa mbinguni/ mbele ya macho yao siku ya arobaini./

Shangilio na sifa ya milele upate Wewe, Bwana wangu Yesu Kristo,/ kwa kuwa umewapelekea wafuasi wako mioyoni mwao/ Roho Mtakatifu,/ ukawasha rohoni mwao mapendo makuu ya Mungu./

Pia, utukuzwe, usifiwe na kushangiliwa milele, Bwana wangu Yesu Kristo./ Umekaa katika ufalme wako wa mbinguni/ juu ya kiti cha enzi cha Umungu wako,/ ukaishi pamoja na Viungo vyako vyote Vitakatifu./ Na hivyo utakuja tena/ kuzihukumu roho za wazima na wafu wote./ Unaishi na kutawala/ pamoja na Baba na Roho Mtakatifu,/ milele. Amina.

(Na Mt. Birgita wa Sweden)


SALA MBELE YA SAKRAMENTI KUU II

Yesu, Mungu wangu mpenzi,/ upo hapa katika Altare mbele yangu;/ na mimi napiga magoti mbele yako.// Waniangalia sana,/ siyo kwa kunipeleleza,/ lakini kwa sababu wapenda kuniona hivi karibu na wewe,/ wafurahiwa nikija kukuabudu./ Wayasikiliza maneno yangu yote/ yenye kutoka mdomoni mwangu,/ na zaidi wapokea maneno yangu yanayotoka moyoni./ Nataka kuzungumza na wewe peke yako,/ na kusahau mambo mengine yote/ na watu wengine walioko kanisani pamoja nami./

Yesu wangu,/ nakushukuru/ kwa sababu umekubali kutupa Sakramenti hii kuu kabisa,/ ukitaka kukaa pamoja na sisi,/ na hata ukakubali kuwa chakula chetu/ chenye nguvu ya ajabu./ Mfalme wangu Yesu,/ Sultani wangu Mkuu,/ naamini kabisa kwamba upo katika Altare/ na kwamba umejificha chini ya umbo la mkate./ Ulipokuwapo bado hapa duniani mbele za watu,/ ulikuwa hujifichi kama sasa;/ lakini hata siku zile/ watu hawakuweza kukuona vile ulivyo./ Hawakuweza kuutambua Umungu wako,/ ikalazimu kukuamini tu sawa kama sisi./ Wakainama kichwa wakisema,/ “Bwana wangu na Mungu wangu”./ Na mimi kadhalika naungama/ U Bwana wangu na Mungu wangu/ na Mkombozi wangu/ na salama yangu yote./ U Yesu wangu tu,/ siwezi kusema zaidi./ Nakuabudu ee Yesu./ Najua sana, mimi ni mdogo kabisa,/ sina maana hata kidogo./ Mimi ni dhaifu na maskini mno./ Lakini Wewe katika hruuma yako kubwa/ waniita nije kwako./ Wewe huuangalii umaskini wangu,/ bali wanivuta katika mapendo yako./

Nasikia maneno yako usemayo:/ “Njooni kwangu ninyi nyote mnaoelemewa na mizigo/ nami nitawasaidia”./ Kwa ajili ya maneno hayo/ nakuja kwako bila hofu./ Najua kwamba wanipenda,/ najua wataka kunisaidia na kuniponya,/ najua kuwa wataka kunitakasa./

Nahitaji sana msaada wako, hakika./ Unaniona katika mwendo wangu wa kila siku,/ Jinsi ninavyohangaika na vishawishi mara nyingi;/ jinsi nilivyo na lazima ya kushindana kila siku/ nikitaka kukaa mwema na safi katika utumishi wako./ Naungama mbele yako Wewe Mkombozi wangu,/ kwamba sikukaa imara siku zote vile nilivyopaswa./ Naungama kwamba nimeshindwa mara nyingine/ na kwa hivi naomba toba./ Lakini kwa nini nimeshindwa mara nyingine?/ Kwa nini nikakosa?/ Ni kwa sababu nalikuwa nimekwenda mbali nawe;/ nalianza kujitegemea mwenyewe./ Katika majivuno yangu nikajisifu mwenyewe,/ nikajiona mwema,/ nikasahau udhaifu wangu./ Na kwa ajili hiyo nikajitia katika hatari bure,/ sikujilinda tena,/ nikampa shetani nafasi ya kunishambulia kwa hila zake zote./ Unihurumie ee Yesu wangu./

Sasa nafahamu jinsi nilivyokuwa mjinga kwelikweli./ Ndiyo maana nakuabudu kwa moyo wangu wote./ Najiweka mikononi mwako/ ufanye nami vile unavyotaka./ Wewe utanitunza;/ Wewe utanilinda vema;/ Wewe utaniongoza nijue namna ya kuepa hatari zote,/ na jinsi ya kufukuza kila kishawishi./ Chukua moyo wangu kabisa,/ kwa sababu ni mali yako kamili;/ Wewe ndiwe uliyeniumba,/ ndiwe uliyenipeleka katika Ukristo,/ nawe ndiwe utakayenihukumu siku ya mbele./ Ndivyo ninavyojitolea kwako./ Ndivyo ninavyokuabudu,/ wala sijui njia nyingine ya kukusifu zaidi./

Yesu wangu mpenzi,/ naomba upokee kwa uzuri heshima hiyo yangu./ Angalia: naitolea pamoja na heshima yote/ unayopewa daima na watakatifu wako/ na malaika wako./ Nikipiga magoti hapa mbele yako sasa,/ siko peke yangu,/ nakuabudu pamoja na Mama yako Bikira Maria,/ ambaye sala zake zinakupendeza kabisa./ Sala zangu naweka pamoja na sala zake yeye,/ uzipokee zote pamoja,/ zikupendeze zote sawa./ Ee Mama Maria!/ Nifundishe maneno ya kumsifu Mwanao Yesu vizuri./ Nipeleke kwa Yesu tumwabudu pamoja./ Nifunike na utakatifu wako/ kusudi Yesu asiangalie tena umaskini wangu/ na makosa yangu,/ aniponye katika huruma yake./

Sasa najisikia vizuri, Yesu wangu./ Sasa nina moyo wa kuweza kuendelea vema/ katika njia njema./ Sasa ninatumaini kwamba/ nitakaa mkristo mwema,/ nitakuwa mtumishi wako mwaminifu./ Nasikia amani kubwa sana moyoni mwangu,/ kwa kuwa nimo mikononi mwako./ Baada ya dakika chache/ nitaondoka tena kanisani,/ nitarudi nyumbani kwangu,/ lakini hatutaachana,/ hapana./ Mapendo yetu yatatuunganisha pamoja daima./ Wewe utanikumbuka nikiwa kazini,/ nikilala usingizi,/ nikienda njiani,/ kila mahali nilipo,/ Wewe utaniona,/ utafuatana na mimi./ Kadhalika nitakukumbuka tu./ Nitafanya bidii nisikuache kabisa./ Amina.


SALA YA KUANGUKA MIGUUNI PA BWANA YESU KATIKA EKARISTI

Ee Yesu Mfungwa wa Upendo wa Mungu,/ ninapofikiri Upendo wako na jinsi ulivyojitolea kwa ajili yangu,/ nashindwa kuelewa./ Unaficha Ukuu wako usiofahamika/ na kujidhihirisha kwa ajili yangu mimi mnyonge./ Ee Mfalme wa utukufu,/ unaficha uzuri wako,/ lakini jicho la moyo wangu/ linapenya pazia na kuona Majeshi ya Malaika/ wakikuimbia kwa heshima bila kukoma/ na nguvu zote mbinguni zikikusifu bila mwisho zikisema:/ “Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu..”/

Ni nani awezaye kufahamu Upendo wako/ na huruma yako isiyo na kipimo kwa ajili yetu!/ Ee Mfungwa wa Upendo,/ nafungia moyo wangu masikini/ kwenye Tabarnakulo hii/ ili niweze kukuabudu usiku na mchana bila mwisho./ Najua hakuna kizuizi/ na hata kama naonekana kukaa mbali,/ lakini moyo wangu u pamoja nawe/ katika ibada hii./ Hakuna kinachoweza kuzuia upendo wangu kwako./ Kwangu hakuna kizuizi chochote./

Ee Utatu Mtakatifu,/ Mungu Mmoja usiyegawanyika,/ utukuzwe kwa zawadi yako hii kuu/ na agano hili la huruma!/

Nakuabudu,/ Bwana na Muumba uliyefichika katika Sakramenti Takatifu!/ Ee Bwana,/ nakuabudu kwa kazi zote za mikono yako/ zinazonifunulia Hekima yako kuu,/ Wema wako na Huruma yako kuu./ Uzuri uliousambaza hapa/ Uzuri ulio nao Wewe mwenyewe/ ambaye U Uzuri usioelezeka;/ na ingawaje umejificha na kusitiri uzuri wako,/ jicho langu,/ kwa mwanga wa imani linafika kwako,/ na roho yangu inapata kumtambua Muumba wake/ aliye Uzuri usiopimika,/ ulio juu ya kila uzuri,/ na moyo wangu unazama kabisa katika sala ya kukuabudu./

Bwana wangu na Muumba wangu,/ wema wako wanitia moyo wa kuongea nawe,/ Huruma yako huondoa kiambaza/ kitenganishacho Muumba na kiumbe./ Furaha ya moyo wangu,/ ee Mungu, ni kuongea na Wewe./ Yote ambayo moyo wangu unayatamni nayapata kwako./ Hapa ndipo mwanga wako unaponiangaza akili yangu/ na kuiwezesha kukujua Wewe zaidi na zaidi/ – ndipo mikondo ya neema inapoutiririkia moyo wangu,/ ndipo roho yangu inapochota uzima wa milele./ Ee Bwana na Muumba wangu,/ licha ya mapaji yote haya,/ unajitoa mwenyewe kwangu,/ ili uweze kujiunganisha na kiumbe dhaifu na maskini./

Ee Kristu,/ nafurahi sana nionapo kwamba unapendwa/ na kwamba sifa na utukufu wako vinaongezwa/ hasa ya Huruma yako./ Ee Kristu,/ sitaacha kamwe kuutukuza wema wako na huruma yako,/ hadi dakika ya mwisho ya maisha yangu./ Kwa kila tone la damu yangu/ na kwa kila pigo la moyo wangu/ naitukuza Huruma yako./ Natamani kugeuzwa kabisa/ na kuwa utenzi wa utukufu wako./ Naomba siku ya kufa kwangu/ popote nitakapokuwa nimelala,/ pigo la mwisho la moyo wangu/ liwe utenzi mpendevu/ usifuo Huruma yako isiyo na kipimo./ Amina

(Na Mt. Faustina Kowalska).


SALA YA KUUABUDU MOYO MTAKATIFU WA YESU KATIKA EKARISTI TAKATIFU

Kwa nguvu zangu zote za moyo wangu/ ninakuabudu ee Moyo Mtakatifu/ na Mwabudiwa sana,/ Moyo Mtakatifu wa Bwana wetu Yesu Kristu/ ambao ninataka kumpenda/ na kukusalimu kwa usikivu unaoendelea./ Kamwe nisikuudhi tena/ kwa sababu Wewe ni Mwema sana;/ Ee Mwema sana./ Ee Moyo Mtakatifu sana/ ninakupenda/ na ninataka kukupenda zaidi ya vitu vyote,/ kwa nguvu zangu zote/ na kwa uwezo wangu wote,/ ninatamani kuwa mali yako/ Wewe uliyejitoa Msalabani kwa ajili yangu/ kwa mateso makali./ Unionee huruma na udhaifu wangu/ na usiniruhusu kupotea./

Ninajitoa kabisa kwako/ ee moyo wa mapendo,/ kwa makusudi kuwa utu wangu,/ maisha na mateso yangu/ yalipie kukupenda,/ kukuheshimu/ na kukutukuza Wewe sasa na milele./ Ninakupenda ee Moyo Mwabudiwa wa Mwokozi wangu,/ ninakuomba kwako/ uamuru moyo wangu na kila kitu ndani yangu/ kikutukuze sasa na milele./ Amina.

(Na Mt Margareta Maria Alakoki)

If you have any question or need more information, ask/search it here

More results...

Generic selectors
Exact matches only
Search in title
Search in content
Post Type Selectors
Filter by Categories
1000+ Best Jokes That You Will Find Absolutely Hilarious
1000+ Best Quotes to Brighten your Day
1000+ Inspiring Real Stories
1000+ Riddles with Answers
Afya na Ustawi wa Wanaume
Afya na Ustawi wa Wanawake
Afya ya Akili na Ustawi
Afya ya Mwili na Mazoezi
All you need to Know About Virgin Mary Mother of God Jesus Christ
Amazing Real African Stories
Best Christian Quotes to Support your Faith
Best Health and Wellness Improvement Tips
Business and Entrepreneurship Secrets
Business Innovations Development Secrets
Business Planning and Strategic Management Tips
Career Development and Success Techniques
Chemsha Bongo: Maswali na Majibu
Christian Articles to Build your Faith
Christian Reflections to Build your Faith
Christian Teachings to Strengthen Your Faith
Climate and Environment
Communication and Interpersonal Skills Techniques
Community and Social Development
Decision Making and Problem Solving Strategies
Detailed Elaboration of Global Contemporary Issues
Dhana ya Muungano wa Mataifa ya Afrika: Mikakati ya Kuunda "United States of Africa"
Digital Marketing Tips
Disease Prevention and Management
Dondoo za Mapishi na Lishe
Dondoo za Urembo na Mitindo
Emotional Well-being Techniques
Entrepreneurship Development: Secrets of Becoming a Successful Entrepreneur
Fahamu kwa Undani Kuhusu Bikira Maria: Mama wa Yesu Kristo na Mama wa Mungu
Family/Parenting, Love and Relationship Techniques
Finance and Money Matters Techniques
Financial Management and Wealth Creation Tips
Financial Management Tips for Your Business
Fitness and Exercise
Funny Questions with answers
Global Cooperation for Peace and Unity
Global Poverty Alleviation and Sustainable Development
Global Sustainable Resources Utilization and Environment Conservation
Hadithi nzuri za Mafundisho kwa Ajili ya Watoto
Hadithi za Kiswahili: Historia, Mapenzi na Maisha
Hadithi za Kusisimua za Matukio ya Kweli ya Kihistoria
Hadithi za Kusisimua: Hadithi za Biblia
Hali ya Hewa na Mazingira
Health and Lifestyle Tips and Techniques
Healthy Aging and Longevity
Healthy Cooking and Meal Preparation
Healthy Habits and Behavior Change
Ifahamu Huruma ya Mungu
Injili na Mafundisho ya Yesu
Inspiring Historical Stories From all Over the World
Inspiring Stories From All Over the World
International Relations and Cooperation
Intimacy and Connection Building Tips
Jinsi ya Kuboresha namna Unavyowasiliana: Ujuzi wa Mawasiliano
Jinsi ya Kujijengea Mtazamo na Fikra Chanya
Kujenga Jamii na MIji Endelevu
Kupunguza Umaskini na Maendeleo Endelevu
Kuvunjika kwa Mahusiano ya Mapenzi: Kuvunjika na Uponyaji
Kuzuia na Usimamizi wa Magonjwa
Lishe na Ulaji wa Afya
Maendeleo ya Jamii na Kijami
Mafundisho Makuu ya Dini: Makala za Dini
Mafundisho Makuu ya Upendo Wa Kipekee Wa Mungu
Mafundisho ya Katekisimu
Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki
Mafundisho ya Nguvu ya Damu ya Yesu
Mahusiano ya Kimataifa na Ushirikiano
Maintenance of Spirituality and Inner Peace
Makala za Tafakari Kwa Wakatoliki
Malezi na Afya ya Familia
Mambo Muhimu ya Msingi Unayopaswa Kufahamu Kuhusu Afrika
Mambo ya Sasa ya Amerika ya Kaskazini na Kusini
Management of African Natural Resources for African Economic Development
Masomo ya Misa ya Kanisa Katoliki
Mastering Leadership and Human Resources Management
Matumizi Endelevu ya Rasilimali na Uhifadhi wa Mazingira
Mbinu za Kilimo na Ufugaji Kukuongezea Mapato
Mbinu za Kubadilisha Mfumo wa Mawazo na Kujenga Tabia Chanya ya Waafrika
Mbinu za Kuboresha Afya na Ustawi wako Binafsi
Mbinu za Kuboresha Afya ya Kihisia Katika Mahusiano
Mbinu za Kufanya Maamuzi na Kutatua Matatizo: Uamuzi na Ushughulikiaji wa Matatizo
Mbinu za Kujengea Afrika na Waafrika Uhuru na Uwezo wa Kujitegemea
Mbinu za Kukufanya Uwe Mjasiriamali Mwenye Mafanikio: Maendeleo ya Ujasiriamali
Mbinu za kukuza Ujasiri wa Kibinafsi na Heshima ya Kujiamini
Mbinu za Kuongeza Ukaribu na Ushirikiano
Mbinu za Kupangilia Biashara na Usimamizi Mkakati
Mbinu za Kusimamia Pesa na Mambo ya Kifedha kwenye Mahusiano
Mbinu za Kutunza Familia na Malezi ya Watoto
Mbinu za Kuwa na Maendeleo ya Kazi na Mafanikio
Mbinu za kuwa na Maisha Mazuri ya Kikristo
Mbinu za kuwa na Misingi imara ya Upendo na Mapenzi
Mbinu za Mauzo na Masoko Kuboresha Biashara Yako
Mbinu za Mawasiliano na Ujuzi wa Mahusiano
Mbinu za Ubunifu Katika Biashara na Maisha: Maendeleo ya Ubunifu
Mbinu za Ujasiriamali na Biashara Kufanya tofauti
Mbinu za Uongozi na Ushawishi
Mbinu za Uongozi na Usimamizi wa Rasilimali Watu
Mbinu za Usimamizi wa Fedha Katika Biashara
Mbinu za Utatuzi wa Migogoro
Mbinu za Uwezo wa Kihisia na Ujuzi wa Kujitambua
Meditation and Yoga
Men’s Health and Wellness
Mental Health and Well-being
Methali za Kiswahili na Maana zake
Mikakati ya Uhifadhi wa Utamaduni na Urithi wa Kiafrika
Mipango na Mikakati ya Usimamizi wa Maliasili za Afrika
Misemo ya AckySHINE
Misingi ya Ndoa Yenye Mafanikio: Ndoa na Kujitolea
Nguvu na Uwezo wa Roho Mtakatifu
Njia za Kujenga Udini na Amani Yako ya Ndani
North and South America Contemporary Issues
Nukuu ya Mistari ya Biblia
Nukuu za Dini
Nutrition and Healthy Eating
Parenting and Family Health
Pembejeo Bora za Kilimo: Bidhaa za Kilimo
Personal Development Strategies and Tips
Promotion of Good Governance and Management of Social Services
Promotion of Sustainable Cities and Communities
Recommended African Development Strategies for Building Independent and Self Reliance Africa Community
Recommended Beauty and Fashion Tips
Recommended Christian Daily Readings
Recommended Conflict Resolution Tips
Recommended Emotional Intelligence and Self-Awareness Tips
Recommended Family and Parenting Techniques
Recommended Leadership and Influence Techniques
Recommended Relationships and Social Skills Techniques
Recommended Strategies for Preservation of African Culture and Heritage
Recommended Technique to Build Self-Confidence and Self-Esteem
Relationship Breakups and Healing Tips
Sala za Katoliki: Sala Muhimu Kwa Mkristu Mkatoliki
Sales and Marketing Tips for Your Business
Sayansi, Teknolojia, na Ubunifu
Science, Technology and Innovation
Selected Christian Prayers to Support your Prayer Life
Shine Ads
Siri ya kuwa na Familia Nzuri ya Kikristo
Siri za Familia, Mapenzi na Mahusiano
Siri za Kuwa na Afya Bora na Utimamu
Siri za Mahusiano Bora na Ujuzi wa Mambo ya Kijamii
Siri za Nguvu ya Jina la Yesu
Siri za Usimamizi wa Fedha na Utengenezaji wa Utajiri
SMS za AckySHINE: SMS Nzuri za Mapenzi na Mahaba Kwa Mpenzi Wako
Special Dedications: 1000+ SMS Messages to Build your Love Life
Stadi za Maisha: Mbinu za Maisha ya Kipekee
Strategies on Changing Mentality and Building Positive Mindset
Strategies to Strengthen your Marriage and Build Commitment
Strategies to Unite Africa: Building a Better World for African Community
Strategies Towards Formation Of The United States Of Africa
sw-picha
Tabia Njema za Afya na Badiliko la Mwenendo
Tafakari ya Kina na Yoga
The Best Love and Romance Techniques
Tips to Develop Positive Mindset and Positive Thinking
Ujana na Makuzi | Mapenzi na Ngono Salama
Ukombozi kutoka Utumwa Wa Dhambi na Shetani
Umoja na Ushirikiano wa Jumuiya ya Kanisa
Umoja wa Afrika: Mikakati ya Kuunganisha nchi na Watu wa Afrika
Understanding African Development: All You Need to Know About Africa
Understanding Communication Skills and Technics
Upishi na Maandalizi ya Milo yenye Afya
Usawa wa Kazi na Maisha
Ushirikiano wa Kimataifa kwa Amani na Umoja
Usimamizi wa Uzito na Taswira ya Mwili
Utawala Bora na Usimamizi wa Huduma za Kijamii
Uzee Mwema na Maisha Marefu
Vichekesho vipya 1000+: Vichekesho vya AckySHINE
Videos in English
Videos za Kiswahili
Weight Management and Body Image
Women’s Health and Wellness
Work-Life Balance
Yafahamu kwa Undani Mambo ya Sasa ya Kimataifa
Melkisedeck Leon Shine

Editor: Melkisedeck Leon Shine. About Me | Contact Me | LinkedIn | TikTok | WhatsApp

Read and Write Comments

Views: 112

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Shopping Cart