Ufufuko wa wafu maana yake nini?
Ufufuko wa wafu maana yake mwisho wa dunia watu wote watafufuka na miili yao na kwenda nayo katika furaha ya milele au moto wa milele. (Ayu 19:25-26, Mt 22:30-32, Yh 28-29)
Mbinguni ni mahali pa namna gani?
Mbinguni ni makao mema ya heri na furaha (2Kor 5:1, Ufu, 2:17).
Waendao mbinguni ni wale wanaokufa katika hali ya neema ya utakaso na urafiki na Mungu na waliotakaswa kikamilifu
Motoni ni nini?
Motoni ni makao mabaya kwa Shetani walaaniwa wakaapo mbali na Mungu wakiteswa milele. (Mt 25:41, Mik 9:42-43, 1Yoh 14:15)
Uzima wa milele ni nini?
Uzima wa milele ni maisha ya kukaa mbinguni na Mungu yasiyokua na mwisho.
Toharani ni mahali gani?
Toharani ni mahali pa mateso zinakosafishwa roho ambazo hazikutimiza kitubio vizuri baada ya kuungama dhambi. (1Kor 3:15, 1Pet 1:7).
Je, hatuwezi kupunguza mateso ya roho za marehemu waliokwenda toharani?
Ndiyo: twaweza kupunguza hata kuyamaliza kwa kuwasalia na kuwapatia rehema na hasa kwa kuadhimisha Misa kwa ajili yao. (2Mik 12:38-46)
Mambo makuu manne ya mwisho ni yapi?
Mambo hayo ni;
1. Kifo
2. Hukumu
3. Jehanamu (Motoni)
4. Paradiso. (Toharani/Mbinguni)
Je, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia?
Ndiyo, ufufuko wa Yesu ni muhimu kwetu pia, kwa sababu kwa njia yake tu tunatiwa uzima: sasa rohoni kwa kuondolewa dhambi, na siku ya mwisho mwilini pia kwa kufufuliwa.
Mwenyewe alisema, โMimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi ajapokufa, atakuwa anaishi; naye kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata mileleโ (Yoh 11:25- 26).
โKristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala. Maana kwa kuwa mauti ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtuโ (1Kor 15:20-21).
โAlitolewa kwa ajili ya makosa yetu, na kufufuka ili tupate kuhesabiwa hakiโ (Rom 4:25).
Je, ni muhimu tujiandae kufa?
Ndiyo, ni muhimu tujiandae kufa wakati wowote na namna yoyote kwa kuishi kitakatifu sasa na kwa kujiombea neema tutakazohitaji saa ya kufa kwetu, tukijua tumewekewa โkufa mara moja, na baada ya kufa hukumuโ (Eb 9:27).
โKatika mambo yako yote uukumbuke mwisho wako, hivyo hutakosa kamwe hata hatimaโ (YbS 7:36).
โHamjui yatakayokuwako kesho! Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutowekaโ (Yak 4:14).
โKesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuniโ (Math 26:41).
Je, ina thamani machoni pa Bwana mauti ya mtu aliyemcha?
Ndiyo, โina thamani machoni pa Bwana mauti ya wacha Mungu wakeโ (Zab 116:15).
Hasa utiifu wa Yesu msalabani umegeuza laana ya kifo iwe baraka kwa waamini wake.
โHeri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana naoโ (Ufu 14:13).
Je, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu?
Ndiyo, sisi wanyonge tunaweza kushiriki uzima wa milele wa Mungu: hapa duniani katika mwanga hafifu wa imani, na kisha kufa katika uangavu wa utukufu usiofifia kamwe. Kwa kuwa lengo la Baba ni kwamba tuungane na Yesu Mwanae kwa uwezo wa Roho Mtakatifu ili tuwe na utukufu wake.
โNa uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtumaโ (Yoh 17:3).
โKwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaaโ (2Pet 1:3-4).
Sisi tuliobatizwa tunaitwa โwana wa Mungu; na ndivyo tulivyo!โ (1Yoh. 3:1).
Kwa sababu tumesadiki kwamba โMungu ni upendoโ (1Yoh 4:8) na kwamba โhakuna lisilowezekana kwa Bwanaโ (Lk 1:37).
โNa kwa kuwa ninyi mmekuwa wana, Mungu alimtuma Roho wa Mwanawe mioyoni mwetu, aliaye, โAba!โ yaani, โBaba!โ Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Munguโ (Gal 4:6-7).
Aliyezungumzia moto wa milele ni nani?
Aliyezungumzia moto wa milele ni hasa Yesu: akitufunulia ukuu wa upendo wa Mungu, aliye heri yetu pekee, alituangalisha juu ya hatari ya kutengana naye milele kwa dhambi. Mwenyewe atatoa hukumu hiyo:
โOndokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zakeโ (Math 25:41).
โHumo funza wao hafi, wala moto hauzimikiโ (Mk 9:48).
โNa moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usikuโ (Ufu 14:11).
Toharani maana yake nini?
Toharani maana yake kuna hali ya muda ambayo huruma ya Mungu inawatakasa marehemu waliofariki dunia katika urafiki naye lakini bila ya usafi kamili unaotakiwa kwa kuingia mbinguni. Sisi tunaweza kuharakisha utakaso wao kwa kumtolea Mungu sala na sadaka, hasa ekaristi. Yuda Mmakabayo โalichanga fedha kwa kila mtu jumla drakma elfu mbili, akazipeleka Yerusalemu kutoa sadaka ya dhambi.
Kwa kufanya hivi alitenda vema na kwa haki, kwa kuwa aliukumbuka ufufuo wa wafu. Maana kama asingalitumaini ya kuwa wale waliokufa watafufuka, ingalikuwa kazi bure isiyo na maana kuwaombea wafu. Lakini kwa kuwa aliufikiri utukufu wa thawabu waliowekewa wale wafao katika utauwa, wazo lake lilikuwa takatifu na la kicho. Ndiyo sababu alifanya upatanisho kwa wafu ili wafunguliwe dhambi zaoโ (2Mak 12:43-46). Imani hiyohiyo iliongoza Wakristo wa kwanza kuwafanyia marehemu ibada ambayo haieleweki vizuri, lakini hailaumiwi na Mtume Paulo: โKama wafu hawafufuliwi kamwe, kwa nini kubatizwa kwa ajili yao?โ (1Kor 15:29).
Je, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa?
Ndiyo, mwili utakaofufuliwa ni huuhuu tulionao sasa, lakini katika hali tofauti: > โhupandwa katika uharibifu; hufufuliwa katika kutokuharibikaโ (1Kor 15:42).
Siku ya ufufuo โndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu pamoja na nguvu na utukufu mwingiโ (Lk 21:27).
โSaa yaja ambayo watu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake. Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuko wa uzima, na waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumuโ (Yoh 5:28-29).
โNa hao watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele; bali wenye haki watakwenda katika uzima wa mileleโ (Math 25:46).
Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu vipi?
Siku ya ufufuo Kristo mfalme atatuhukumu kwa kudhihirisha misimamo ya watu wote ambao, kwa kupokea au kukataa upendo wa Mungu moyoni mwao, wametenda mema au la.
โImetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyopenda, kwamba ni mema au mabayaโ (2Kor 5:10).
โBasi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulikisha yaliyositirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Munguโ (1Kor 4:5).
โHapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake. Na mataifa yote watakusanyika mbele zake; naye atawabagua kama vile mchungaji abaguavyo kondoo na mbuzi; atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, na mbuzi mkono wake wa kushoto. Kisha Mfalme atawaambia wale walioko mkono wake wa kuume, โNjoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu; kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkaninywesha; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha; nalikuwa uchi, mkanivika; nalikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nalikuwa kifungoni, mkanijiaโฆ Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimiโโ (Math 25:31-36,40).
โHeri wenye rehema, maana hao watapata rehemaโ (Math 5:7).
Baada ya hukumu ya mwisho itakuwaje?
Baada ya hukumu ya mwisho, waadilifu watatukuzwa mwili na roho pamoja na Yesu, na ulimwengu pia utageuzwa.
โKama ilivyo ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yakeโ (2Pet 3:13).
โNa Roho na Bibi arusi wasema, โNjoo!โ naye asikiaye na aseme, โNjoo!โโฆ Yeye mwenye kuyashuhudia haya asema, โNaam, naja upesiโ. Amina. Na uje, Bwana Yesu! Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi nyote. Aminaโ (Ufu 22:17,20-21).
References:
Google ScholarResearchGateSemantic ScholarAckySHINE
Neema na amani iwe nawe.
Upendo wa Mungu haukosei kamwe.
Nguvu hutoka kwa Bwana
Rehema hushinda hukumu
Mwamini Bwana kwa moyo wako wote, na usitegemee ufahamu wako mwenyewe