1000+ Vichekesho vipya: Vichekesho vya AckySHINE
Angalia nilichomfanyia huyu dereva sasa
Tulikua kwa basi tunaelekea arusha,ile namcheki dereva kumbe ni best yangu na basi ilikua kwenye spidi hatari, nikaenda kumziba macho nkamuuliza otea mi ni nani, kabla hajanijibu nikasikia kishindo kikubwa sana
NA SASA HIVI NIMEZINDUKA NIMEONA ABIRIA WOTE TUPO WODI NAMBA 3 HAPA KCMC MOSHI. 🤕🤕🤕🤕
SODA ZA WAGONJWA PLIIIZ!!! 🙏🙏🙏🙏🙏
Utoto bwana. Raha sana!
Utoto buana! eti mnacheza mpira wa makaratasi(chandimu) unapiga chenga kibao afu ukifika golini ufunge unakuta goli hamna kumbe mwenye ndala zake ameitwa kwao😆
Hii sasa kali kweli kweli! wazazi wanachofanya pale binti yao anapochelewa kuolewa
Wazazi wengine wanaandika MBWAMKALI kwenye geti lao kama binti wao ana miaka 18..
Binti akifika miaka 30 na hajaolewa wanapabadilisha na kuandika TUNAUZA BARAFU
😂😂😂😂😂😂😆
😆😆😆😆😆😆😆
Angalia huyu mwalimu alichomfamya huyu mwanafunzi
*Hadith ya Shemdoe na Mwalimu wa English:*
*Teacher:* `Who is a pharmacist?`
*Shemdoe:* 👆🏿 _(raised up his hand.)_
*Teacher:* `So it’s only Shemdoe that can tell who a pharmacist is in this class? Thus, no body else to answer the question except Shemdoe?`
_(There was no reply from the students)_
*Teacher:* `Ok. now Shemdoe, chukua hii fimbo, charaza vilaza hawa wote kila mmoja viboko 3.`
*Shemdoe* _(akiwa amevimba kichwa, akawatwanga viboko vitatu vitatu vya kushiba darasa nzima)_
*Teacher:* `Now, my dear Shemdoe tell this dumb students, who a pharmacist is…?`
*Shemdoe:* `Yes, sir. a Pharmacist is a farmer who assists people.`
_*Shemdoe sasa hivi amelazwa MOI kwa wataalam wa mifupa*_😀😀😀
SOMA HII! Baba kampaka Sumu mkewe kafa Houseboy
Baba mmoja Juzi alimpaka Sumu Mke wake kwenye Matiti akiwa amelala ili Mtoto akinyonya afe kwani alihisi sio wa kwake, akaondoka kwenda kazini aliporudi akakuta house boy amekufa, usiniulize alikufaje. Mie mambo ya umbea sipendi niliondoka zangu mapemaaa!!😅😅😅😅
😝😝😝😝😝😝
Huyu jamaa kawaweza polisi watatu, cheki alichowaambia
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: kimya
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: we nani kwani?
Polisi::: sisi polisi
Jamaa::: mnataka nini?
Polisi::: kuongea na wewe
Jamaa::: kuongea na mimi?!
Polisi::: ndio
Jamaa::: mko wangapi?
Polisi::: tuko watatu
Jamaa::: kama mko watatu si muongee wenyewe…!!!
Hii sasa kali kweli kweli!!
MCHUNGAJI alitangaza kila mwanaume aliye na mke atoe sadaka kulingana na uzuri wa mke wake…bac watu wakaanza kutoa 50,000/= 30,000/= na 20,000/=.
Kuna jamaa akatoa 500/=.
MCHUNGAJI akamuita ofisin akamuuliza.
MCHUNGAJI:Ina maana mkeo siyo mzuri?. Jamaa akajibu: Ukimuona utanirudishia na chenji.
😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆
Makonda wana mambo, Kila mtu ni ndugu yao
Hakuna m2 mwenye ndugu wengi kama konda wa daladala.
Utasikia,
“HAYA, DADA HAPO MBELE, MJOMBA KULE MWISHO.
MA-MDOGO UNAENDA?,
NGOJA ASHUKE BIBI.
HAYA SHEMEJI UMEIKUTA YA KUWAH.
Babu njoo ukae!
Baba angu hapo tusogee kidogo,
Shangazi maliza ngazi,
Swaiba geukia mbele,
Kaka hapo shika upande wa pili,
Mdogo wangu mpishe Ma Mkwe akae.
Subiri Shemeji yako apande…
Duh… makonda noma…!!
Mshahara usiobadilika
PAMOJA NA HALI NGUMU YA UCHUMI NCHINI HUWEZI AMINI MSHAHARA WA DHAMBI HAUJABADILIKA HATA KIDOGO…BADO NI MAUTI VILEVILE
😊😊😊😊
Kizungu nacho ni sheeeedeer
Mtalii: Do you have vegetables here.
Mtafsiri: Mnavyo vijimeza hapa.
Waiter: Vijimeza vidogo hatuna.
Mtafsiri: No sir, they don’t have.
Mtalii: OK, fine, do you have hot dogs.
Mtafsiri: Sawa, je mnao mbwa wa moto.
Waiter: Loh! Bwana we, hatupiki mbwa hapa.
Mtafsiri: They don’t cook here
Mtalii: What type of snacks do you have here.
Mtafsiri: Aina ngapi ya nyoka mnao hapa,
Waiter: We bwana we hapa hatupiki aina yeyote
ya nyoka, mwache akale nyumbani kwao.
Mtafsiri: They don’t cook any type of snacks
here,
maybe you can go back and eat at home.
Mtalii: OK, at least give us a cocktail juice.
Mtafsiri: OK, tupatie hata juisi ya mkia wa jogoo.
Waiter: Hebu tokeni na bangi zenu hapa, tena
sasa hivi kabla sijakasirika.
Mtafsiri: Lets get out of here
😝😝😝😂😂😂
Usicheke pekeyako
Dongo kwako kama una degree moja Halafu unachagua kazi
Mtu una degree 1 unachagua kazi! Wakati thermometer ina degree 100, inafanya kazi kwenye kwapa.
😃😄😆😆😆
Ni Utani tuuuuu!
Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU” 😂😂😂 Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapo *Sipendagi Ujinga mimi* 🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽
Angalia huyu house girl wa mzungu alichokifanya na anachokisema
House girl mmoja alipewa kazi na mzungu mara akavunja sahani.
Mzungu aliporejea,kazin akamuuliza ‘what happened to my plate?
House girl akajbu: ‘The dog wow wow friji paaa, mchuzi mwaaaa the vyombo pangalapangala the sahan ngelengenjee……the pasuka paaaaaaaa
😂😂😂😂hadi saiz mzungu bado anasoma dictionary hajui lugha gani imetumika
Cheka na methali
1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(…..)
Kali ya mwaka iliyotokea Benki Baada ya wezi kuiba
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuni…unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuni…😂😂😂😂
Angalia huyu mvulana anachomwambia huyu daktari baada ya rafiki yake wa kike kupata ujauzito
😂😂😂😂
MVULANA: Daktari, rafiki yangu wa kike ni mjamzito, lakini mara zote nimekua nikitumia kinga. Inawezekanaje hii?
DAKTARI: Ngoja nikusimulie hadithi. Kulikua na Muindaji ambaye alikua anabeba bunduki kila aendako. Siku moja, alichukua mwamvuli badala ya bunduki na akaenda nayo. Ghafla akatokea Simba mbele yake. Ili amtishie Simba, muindaji akatumia mwamvuli na kummiminia risasi Simba. Simba akafa palepale!
MVULANA: Sio kweli!! Lazima kulikua na mtu mwengine pembeni aliyempiga risasi Simba.
DAKTARI: Nashukuru umeelewa somo!!😂
😂😂😂😂😂😂😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃
Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja
Ujinga wa ndoto ndio huu
👉Ujinga wa ndoto ndiyo huu
••Utaota umeokota dolla ukiamka empty…
••Utaota umeokota dhahabu ukiamka kitandani patupu daadeeki OTA Sasa UMEKOJOA…..
😂😂😂😂😂😂
Huyu bwana leo kapatikana, Jamani nyodo nyingine mbaya
Baada ya kumaliza Degree yake ya sheria Bwana Rwegashora aliamua kurudi nyumbani Bukoba mjini na kufungua ofisi yake kwa ajili ya huduma kwa wateja.
Siku moja akiwa ndani ya ofisi yake alimuona mtanashati na mdada mmoja mrembo anakuja ofisini kwake akajua ni mteja anamletea kesi.
Ndipo akanyanyua mkoni wa wa simu ya TTCL na kuanza kuongea huku anajizunguusha kwenye kiti cha kuzunguuka.
Wakati mdada alipokaribia Rwegashora alimkaribisha kwa ishara maana alijifanya yupo busy na kuongea na simu ya umuhimu.
Wakati anaongea na simu akisikika akisema No, No, No….. Absolutely No. Wajuulishe hao lay person wa New York kua siwezi kushuhulika na kesi ambayo itanilipa chini ya 50 million. Mimi ni profesional lawyer and im crossing the border to sarve international community.
Aka pose kidogo na akanywa maji kisha akaendelea…..
Naweza kuanza kukusanya primary evidence next weak but tell them watume kwanza ten million kwa kuanza…
Hahahahaha you dont know my Account
Mr Roger. Ok waambie watume kwenye Account ileile walionitumia million 100 last month…
Aka pose tena akameza fundo la maji na kurekebisha tai yake kisha akaendelea… Ok usisahau kumueleza muendesha mashtaka mkuu wa marekani kua nitakuja New York mwezi ujao maana nitapita kwanza Amsterdam kuwasilisha utetezi wa yule mteja wangu mholanzi kisha nitaenda Tokyo kulipia ile gari yangu niloagiza.
Wakati anaongea hayo yote yule mdada alikua ametulia na anamuangalia Bwana Rwegashora anavyojizunguusha kwenye
kiti chake huku akiongea kwa tambo kwenye ile simu ya TTCL.
Baada ya kumaliza kuongea na simu Bwana Rwegashora aliweka mkono wa simu yake ya TTCL chini kisha akamgeukia mdada mrembo.
Samahan sana kwa kukupotezea muda wako unajua tena kazi zetu zinaumiza kichwa sana kama unavyoona mwenyewe yaani niko busy sana ninapokea simu sana mpaka nimechoka na simu nyingi ni za wateja wa njee ya nchi.
Anyway nikusaidie nn? Mdada akajibu mimi ni mfanyakazi wa kampuni ya TTCL nimekuja kuunganisha line yako ya simu kwani haipo hewani tangu wiki iliyopita…!!!
Unadhani Bwana Rwegashora alifanyaje…???
Recent Comments