Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha
Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejengaย GHOROFAย na yule anayejengaย Nyumba ya KAWAIDA.
Anayejengaย Ghorofaย anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza
kuinuaย Ghorofaย yake juu. Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka, unaweza kukuta yule anayejengaย Ghorofaย bado yuko kwenye Msingi.
Ila siku akianza kuinuaย Ghorofaย lake, kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.
Kwenye maisha ndivyo ilivyo-ย “If want to go so high, you need to go so deep” (Kama unataka kwenda juu sana ni lazima ukubali kwenda chini sana).ย Ni lazima ufanye kitu cha tofauti kitakochokujengeaย Future imara.
Ukweli ni kuwa Watu wengi wanaokuzunguka wanajenga maisha ambayo ni kamaย Nyumba ya kawaida.
Na wewe kama unataka kujenga maisha yanayofanana naย Ghorofa,
Ni lazima ukubali kuonekana unachelewa kwenye baadhi ya mambo.
Hii inamaanisha nini?โฆ
Hii inamaanisha kuwa utalazimika kufanya vitu vyaย TOFAUTIย na kuwaย TAYARIย kusubiri.
Utatakiwaย Kuwekezaย wakati wengine wanaenda kununua nguo mpya waendane na Fashion,
Utatakiwaย Kusoma vitabuย wakati wengine wanaangalia movie na kupiga stories,
Utatakiwaย Uanzishe Biashara yakoย wakati wenzako wamesharidhika na mshahara wanaopata n.k
Unachofanya kuanzia unapoamka hadi unapoenda kulala kitajulisha kama unajengaย Maisha GHOROFAย amaย Maisha KAWAIDA.
Ukijiona unapoteza muda hovyo,
ukiingiaย Facebook/instagramย ni kusoma umbea tu,
Unalalamika unasema utafanya na hakuna unachofanya, ujue unajengaย Maisha ya KAWAIDAย tena ni kamaย Nyumba ya UDONGO.
Ukitaka kujenga maishaย GHOROFA;
1.ย _Jifunze kitu kipya leo._
2.ย _Chukua hatua kuelekea Ndoto yako._
3.ย _Usiwe mtu wa kulalamika bali tafuta suluhisho kwa kila changamoto._
Je, LEO utajiunga na wanaojengaย Maisha GHOROFAย ama wale wanaojengaย Maisha ya KAWAIDA?
Twende zetu tujengeย Maghorofa !!!
Recent Comments