Ni vizuri kujua haya
ππΏDegree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
ππΏUzuri ulio nao hauwezi kukupeleka kwenye ndoto zako.
ππΏUsipobadilisha hao marafiki ulio nao hutofika mahali popote.
ππΏUsipobadilisha vitendo unavyovifanya kila siku hivyo hivyo mafanikio utayasikia kwa wengine.
ππΏKazi au ajira unayoifanya usipojiongeza haiwezi kukupeleka kwenye maisha unayoyataka.
ππΏHuo mshahara unaolipwa usipoutumia vizuri na kujiwekea akiba au kuwekeza kidogokidogo hutoacha kulalamika kila siku mshahara mdogo au hautoshi.
ππΏUsipoacha kukopa bila malengo mafanikio ni ngumu kuyapata.
ππΏUsipowekeza muda kwa ajili ya kujifunza na kuelewa mambo mengi ya biashara na ujasiriamali kwa ujumla na kufahamu dunia imetoka wapi,iko wapi na inaelekea wapi huytoacha kulalamika.
ππΏUsipolipia gharama za kujifunza na ukajifunza kweli kile unachoelekezwa ikiwa ni pamoja na Pesa na muda haya mambo waachie wengine.
ππΏUsipobadili fikra na mtazamo wako huwezi kubadilisha chochote katika maisha yako.
ππΏUkiacha kusikiliza kila aina ya ushauri unaopewa na ndugu zako,jamaa zako,marafiki zako,familia yako,majirani zako na kujisikiliza wewe mwenyewe utahangaika sana.
ππΏUsipofanya bidii na juhudi na ukakubaliana na changamoto zozote utakazokutana nazo maisha yatakuwa magumu sana kwako.
Kumbuka mtu pekee Wa kuyabadilisha maisha yako na kukusaidia kufikia malengo na ndoto zako wala sio mwingine ni mmoja tu nae ni WEWE.
Badilisha fikra zako,badilisha mtizamo wako,badilisha maisha yako.

I’m so happy you’re here! π₯³













































































Recent Comments