Mafundisho ya Msingi ya Kanisa Katoliki: Makala za Katoliki

AHADI 15 ZA ROZARI TAKATIFU

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.

1. Yeyote yule atakayesali kwa imani rozari hii takatifu atapokea neema kuu zenye nguvu
2. Naahidi ulinzi wa kipekee na neema za kipekee kwa yule atakayesali rozari hii
3. Rozari itakuwa silaha kubwa dhidi ya nguvu za kuzimu, itaharibu maovu, itapunguza dhambi na kushinda kutofautiana
4. Itafanya fadhila kukua, kazi nzuri kuongezeka, itapatia roho huruma tele toka kwa MUNGU, itaondoa hamu ya wanadamu kupenda mambo ya dunia na majivuno yake na kufanya wapende zaidi mambo ya mbinguni. Ooh, ni kwa namna gani roho hizo zitajifurahisha na kubarikiwa kwa namna hii.
5. Roho zitakazojikabidhi kwangu kwa njia ya kusali rozari, kamwe hazitapotea.
6. Yeyote atakayesali rozari kwa uaminifu huku akiyatafakari matendo makuu ya rozari, kamwe hatashindwa na ubaya. MUNGU hatamwadhibu katika hukumu yake, hatapotea katika kifo asichopangiwa na atabaki katika neema za MUNGU na kustahili kupata uzima wa milele.
7. Yeyote atakayekuwa mwaminifu katika kusali rozari, kamwe hatakufa bila ya kupokea Sakramenti takatifu za Kanisa.
8. Wote watakaokuwa waaminifu katika kusali rozari watadumu katika mwanga wa MUNGU katika maisha yao na saa yao ya kufa na kupata neema zake tele; katika saa yao ya kufa watashiriki fadhila za watakatifu waliopo peponi
9. Nitawatoa toharani wale wote waliokuwa waaminifu katika kusali rozari
10. Watoto wangu waaminifu katika kusali rozari watapata fadhila kuu ya utukufu Mbinguni.
11. Utapata yale yote unayoniomba kwa kusali rozari
12. Wote wale wanaoeneza rozari hii takatifu nitawasaidia katika mahitaji yao
13. Nimepata toka kwa mwanangu Mtukufu kuwa mawakili wote wa rozari takatifu watapata
waombezi toka baraza lote kuu la Mbinguni wakati wa maisha yao na wakati wa saa yao ya kufa.
14. Wote wanaosali rozari hii takatifu ni wanangu, na kaka na dada wa mwanangu wa pekee YESU KRISTO
15. Ibada kwa rozari takatifu ni ishara kuu ya kuelekea ukombozi

Je, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria?

Je, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria?

Ndio, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria kwa sababu yeye ni Mama wa Mungu na Mama yetu pia. Tunaamini kuwa Bikira Maria ni mtakatifu na mwenye nguvu ya kuombea kwa ajili yetu kwa Mungu. Tunaomba Bikira Maria kwa sababu tunajua kuwa yeye anajua mahitaji yetu na anaweza kuwasilisha mahitaji yetu kwa Mungu.

Katika Injili ya Luka, tunasoma kuwa Malaika Gabrieli alimwambia Bikira Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Maria alisema "tazama, mimi ni mtumishi wa Bwana; iwe kwangu kama ulivyosema." (Luka 1:38). Bikira Maria alikuwa mtii kwa Mungu na aliitikia wito wa Mungu kwa unyenyekevu mkubwa. Hivyo, Bikira Maria anatupatia mfano wa kuigwa katika utii kwa Mungu na kujikabidhi kwa mapenzi ya Mungu.

Kanisa Katoliki linatambua kuwa Bikira Maria ni mpatanishi wetu kwa Mungu. Kwa hiyo, tunaweka matumaini yetu kwa Bikira Maria, tunawaomba awakumbuke watoto wake na kutuletea baraka za Mungu. Bikira Maria ni Mama yetu wa huruma ambaye daima yuko tayari kutusaidia. Kupitia sala zetu kwa Bikira Maria, tunaweza kuzidi kuimarisha uhusiano wetu na Mungu.

Kanisa Katoliki linatambua kuwa Bikira Maria ni mtakatifu na ndio sababu tunamwomba. Tunajua kuwa yeye anasikiliza maombi yetu na anatuombea kwa Mungu. Kama vile Yesu alivyomwambia mama yake msalabani "Mama yako" na kumkabidhi kwa wanafunzi wake kuwa mama yao, tunaona kuwa Bikira Maria ni Mama yetu pia (Yohana 19:27).

Kanisa Katoliki limejenga mafundisho ya kuwaomba watakatifu, na hii inajumuisha Bikira Maria. Katika Catechism of the Catholic Church, tunasoma kuwa "katika kumwomba Bikira Maria, tunajiongezea tunaomba kwa watakatifu wote" (CCC 2679). Kama vile tunamwomba Bikira Maria, tunawajibika kuomba kwa watakatifu wengine pia. Kuwaomba watakatifu kunatupa nafasi ya kujifunza kutoka kwao na kusali kwa ajili ya baraka zao.

Kwa hiyo, jibu ni ndio, Kanisa Katoliki linamwomba Bikira Maria. Tunamwomba kwa sababu yeye ni Mama yetu wa Mbinguni na mpatanishi wetu kwa Mungu. Tunajua kuwa yeye anatusikiliza na tunamwamini kuwa anaweza kutuletea baraka za Mungu. Tunamwomba Bikira Maria ili kutia moyo na kuimarisha uhusiano wetu na Mungu. Kwa hiyo, tunasali, "Salamu Maria, Mama wa Mungu na Mama yetu."

Namna Biblia inavyomueleza Bikira Maria

Biblia inashuhudia kuwa watu wanatofautiana

Maandiko matakatifu yanawasifu watu mbalimbali kutokana na jinsi walivyomuamini Mungu na kutenda makuu kwa ajili ya taifa lake.
Abrahamu alimuamini Mungu akawa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18).
Yosefu, mwana mpenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20).
Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale: aliongoza Israeli kutoka [[utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya Agano la Kale yanakiri, β€œWala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musa” (Kumb 34:10-12).
Waliofuata ni Yoshua, Debora, Gideoni, Ruthu, Samweli, wafalme Daudi na Solomoni, manabii Eliya, Isaya, Yeremia, Ezekieli na wengineo.
Mwishoni Yesu Kristo akamsifu Yohane Mbatizaji akisema, β€œNi mkuu kati ya uzao wa wanawake” (Lk 7:24-28).
Elizabeti, mama wa Yohane, alijiona hastahili kutembelewa na Bikira Maria, Mama wa Yesu, akamuita, β€œMama wa Bwana wangu” (Lk 1:43).
Bikira Maria si mtu wa ziada katika mpango wa Mungu bali ni mshiriki mkuu wa ukombozi wa binadamu. Maria amechangia wokovu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa. Msimamo wake ulikuwa mmoja tu: β€œTazama, mimi ni mjakazi wa Bwana; na iwe kwangu kama ulivyosema” (Lk 1:38).
Tukichunguza nafasi yake katika fumbo hilo, tunaweza kukiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49), kwa kuwa, β€œMtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27).
Yale yote ambayo Wakristo wengi wanayasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia bali alijaliwa na Mwenyezi Mungu huku akiitikia kwa hiari fumbo la mpango wake.

Utabiri kuhusu Bikira Maria kwenye Biblia

Biblia inatupatia utabiri uliotolewa na Mungu mwanzoni mwa historia kuhusu mwanamke atakayemshinda nyoka wa kale (Shetani): β€œNitaweka uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chako” (Mwa 3:15). Juu ya [[Eva wa kale, ambaye alidanganywa na kuangushwa na Shetani atende dhambi, imesemwa: β€œAdamu akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio hai” (Mwa 3:20). Hata hivyo Adamu na Eva wa kale wametuletea kifo (Rom 5:12). Mababu wa Kanisa wanamtazama Bikira Maria kama Eva mpya aliyemshinda Ibilisi na kuwa mama wa wote walio hai. Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Mama yake awe Mama wa waliokombolewa kwa kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. β€œPenye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Kleopa, na Mariamu Magdalene. Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, β€œMama, tazama, mwanao”. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, β€œTazama, mama yako”. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake. (Yoh 19:26-27).
Utabiri mwingine ulisema, β€œTazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu pamoja nasi” (Isa 7:14). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:34-35, β€œMariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu”. β€œImba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yako” (Sef 3:14-15). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:28: β€œMalaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, β€˜Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja nawe’”. β€œUmebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika. Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu milele” (Yudithi 14:7; 15:9). Dondoo hilo linalinganishwa na Lk 1:42, β€œAkapaza sauti kwa nguvu akasema, β€˜Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote, na yeye utakayemzaa amebarikiwa’”.
Bikira Maria ni fumbo la ajabu alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Jamaa yake Elizabeti alimpongeza tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, β€œHeri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwana” (Lk 1:45).
Hivyo manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua Maria kwa heshima. Mambo yaliyotabiriwa katika Agano la Kale yalitimia katika Agano Jipya: ukombozi ulianza Bikira Maria alipokubali kwa imani fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu. Bikira Maria hakuwa β€œchombo” tu kilichotumika bila ya kuelewa, bali alikuwa mshiriki huru wa kazi ya ukombozi ya Mwanae, kwa kuwa alipopashwa habari na malaika alikubali kwa hiari mpango wa Mungu akisema, β€œMimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama ulivyonena” (Lk 1:38).

Bikira Maria katika maisha ya Yesu

Yesu, kama mtu yeyote mcha Mungu, aliwaheshimu na kuwatii wazee wake: β€œBasi, akarudi pamoja nao Nazareti, akawa anawatii” (Lk 2:51).
Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara ya Yesu iliongozwa na Bikira Maria katika arusi ya Kana ya Galilaya, akisukumwa na huruma kwa wenye shida: kwa ombi lake Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake wakamwamini. Yohane alisimulia hivi, β€œSiku ya tatu palikuwa na arusi huko Kana, mji wa Galilaya; naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa arusini pamoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu akamwambia, β€˜Hawana divai’. Yesu akamwambia, β€˜Mama tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia’. Mamaye akawaambia watumishi, β€˜Lo lote atakalowaambia, fanyeni’. Basi kulikuwako huko mabalasi sita ya mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu akawaambia, β€˜Jalizeni mabalasi maji’. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, β€˜Sasa tekeni, mkampelekee mkuu wa meza’. Wakapelekea. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale maji yaliyopata kuwa divai, (wala asijue ilikotoka, lakini watumishi walijua, wale walioyateka yale maj), yule mkuu wa meza alimwita bwana arusi, akamwambia, β€˜Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa’. Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya huko Kana ya Galilaya, akaudhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini. (Yoh 2:1-12).
Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake kuu kabisa, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya roho kuliko ya mwili. β€œBasi, mtu mmoja akamwambia, β€˜Mama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema nawe’. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, β€˜Mama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?’ Kisha akanyosha mkono wake juu ya wanafunzi wake akasema, β€˜Hawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na mama yangu’” (Math 12:46-50). Vilevile, wakati wa utume wake, alimsikia β€œmwanamke mmoja katika lile kundi la watu akisema, β€˜Hongera kwa mwanamke aliyekuzaa na kukunyonyesha’. Yesu akamjibu, β€˜Barabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na kulishika’” (Mk 11:27-28).

Bikira Maria alivyoshiriki Mateso ya Yesu

Katika kumfuata Mwanae Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni uchungu kama upanga utakaopenya moyo wake, β€œTazama huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama upanga utauchoma moyo wako” (Lk 2:34-35).
Bikira Maria alishiriki kwanza mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiuawe na Herode Mkuu, β€œHivyo Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka Herode alipokufa” (Math 2:14-15).
Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua kuteswa kwa Yesu; wanafunzi walipokimbia au kumtazama kwa mbali, yeye alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata Mwanae. Kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, alipoyashuhudia yote aliteseka sana katika moyo wake safi, kiasi kwamba Bernardo wa Klervoo akasema, β€œMsalaba wa Yesu uliwasulubisha wote wawili, Yesu mwilini na Mama yake moyoni”. Uaguzi wa mzee Simeoni ulitimia hivyo.
Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, β€œNa sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo” (Kol 1:24). β€œβ€¦ maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wake” (Rom 8:17b).
Pale msalabani Bikira Maria, kwa njia ya mtume Yohane alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae; kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana ameshindwa.

Bikira Maria baada ya kifo cha Yesu

Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, akilivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa sala yake. β€œHao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na ndugu zake” (Mdo 1:14).
Yesu alisema, β€œNinayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli wote” (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa kadiri ya utabiri wake kuwa ataheshimiwa na vizazi vyote, β€œKwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote wataniita mwenye heri” (Lk 1:48).

Uelewa wa namba katika Biblia

Biblia imeandikwa na Mungu kupitia waandishi wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hivyo Biblia ni Neno la Mungu. Hivyo mwandishi wa Biblia ni Mungu kupitia wanadamu (God is the primary author of the Bible while human authors are secondary authors). Mungu aliwavuvia (inspiration by the Holy Spirit) waandishi wanadamu ili waweze kuandika kile tu ambacho Yeye (Mungu) alitaka kiandikwe kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Kusema kuwa Biblia imeandikwa na Mungu kupitia wanadamu haina maana ya kuandikwa kwa njia ya imla (dictation), kana kwamba Mungu anataja sentensi au neno na wao wanaandika. Hapana, pamoja na kuwavuvia Roho Mtakatifu, waandishi wanadamu walikuwa huru kutumia vipawa mbalimbali vya uandishi na mazingira yao ili kufikisha ujumbe ambao Mungu amewavuvia. Hivyo walikuwa β€œactive writers of the Bible, and not passive writers.” Walitumia akili (reason), utashi (will), ujengaji picha (imagination) na vipawa vingine. Lakini vipawa hivi vyote vilikuwa chini ya maongozi ya Roho Mtakatifu ili kuwawezesha waandishi wa Biblia kufikisha ujumbe kwa ufasaha bila makosa.

Hivyo kuelewa kifungu au ujumbe wa Biblia ni lazima kujua yafuatayo:
Maana aliyokusudia mwandishi (the meaning of the human author)
Kusudi/malengo ya Roho Mtakatifu

Na kwa kuwa kwa mara ya kwanza Biblia waliandikiwa Wayahudi na waandishi wengi walikuwa Wayahudi, hivyo tunapaswa kujua yafuatayo ili kufasiri Biblia vizuri:

Tamaduni za Wayahudi
Historia ya Wayahudi
Mambo ya Kijografia
Namna yao ya uandishi n.k

Jambo muhimu kuelewa
Namba, wanyama, rangi, vitu, watu, maeneo, shughuli mbalimbali n.k vilikuwa na maana sana kwa Wayahudi na kwa Wakristo wa kwanza. Hivyo si ajabu kuona vimetajwa au kutumika katika Biblia.

ISHARA NYINGINE TOFAUTI NA NAMBA

Kabla ya kuzungumzia namba tuzungumzie baadhi ya vitu, rangi, watu au mahali kama vinavyoongelewa kwenye kitabu cha Ufunuo na sehemu nyingine za Biblia:

Mwanamke:

kwenye Ufu.12:1+ anamaanisha taifa au mji, na siyo mwanamke kama tunavyojua

Pembe:

neno pembe kwenye Ufu. 5:6; 12:3 linamaanisha β€œmamlaka”. Hata kwenye kiswahili mtu akiambiwa kuwa β€œameota pembe” maana yake anajifanya kuwa ana mamlaka fulani na hivyo ana kiburi.

Mabawa:

kwenye Ufu. 4:8; 12:14 linamaanisha uwezo wa kufika mahali pote (mobility).

Upanga mkali:

kwenye Ufu. 1:16; 2:12,16) linamaanisha Neno la Mungu, ambalo lina hukumu na kuadhibu.

Matawi ya mtende:

kwenye Ufu. 7:9 ni ishara ya ushindi.

Taji:

kwenye Ufu. 2:10; 3:11 ni ishara ya utawala na ufalme.

Bahari:

kama lilivyotumika kwenye Ufu. 13:1; 21:1 linamaanisha sehemu ya uovu, chanzo cha machafuko na kifo.

Nyeupe:

rangi nyeupe inamaanisha furaha ya ushindi (Ufu. 1:14; 2:17)

Zambarau:

rangi ya zambarau huashiria anasa, utajiri na ufalme (Ufu. 17:4; 18:12,16). Kwenye Yohane 19:2,5; Mk. 15:17 vazi la zambarau huashiria β€œufalme”. Kwenye Lk. 16:19 vazi la zambarau la yule tajiri liliashiria β€œmaisha ya anasa”.

Nyeusi:

rangi nyeusi iliashiria kifo (Ufu. 6:5,12).

NAMBA KATIKA BIBLIA

Namba zilikuwa na maana sana kwa Wayahudi kwa sababu za kimazingira, kiuandishi na kilugha. Kila namba ilikuwa na maana. Hebu tutazame baadhi tu ya namba hizo:

Namba 3 na7

Namba hizi kwa Wayahudi (kwenye Biblia) zinamaanisha ukamilifu au utimilifu wa jambo (perfection or completion). Kwa mfano katika Kiebrania (lugha ya Wayahudi) hakuna β€œsuperlative” (kulinganisha kwa kutumia sifa ya juu kabisa) mfano β€œthe tallest, the youngest, the holiest” kama kwenye Kiingereza. Hivyo Myahudi kwa upande wake atatamka neno husika mara tatu kuonesha ukamilifu: God is holy, holy, holy (ambapo kwenye Kiingereza tungesema tu β€œGod is the holiest”). Kwa hiyo akitaja neno mara tatu alimaanisha ukamilifu wa jambo(perfection). Anaposema Mungu ni Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu ana maana kwamba Mungu ana ukamilifu wa utakatifu, yaani ni Mtakatifu kupita viumbe au vitu vyote. Mfano mwingine: Myahudi akisema kwamba nilipigwa viboko vitatu haina maana kuwa lazima vilikuwa vitatu tu. Hapa ina maana kwamba alipigwa katika ukamilifu wake yaani alipigwa barabara, sawia, alipigwa mno,
alipigwa mpaka basi. Hata kwenye Biblia ni vivyo hivyo. Yesu alimuuliza Petro mara tatu kama anampenda (Yohane 21:15-19). Hapa Yesu alitaka kujua kama Petro alimpenda katika ukamilifu wa upendo. Namba 7 imetumika mara 42 kwenye kitabu cha Daniel na Ufunuo: mfano β€œroho saba” ilimaanisha β€œukamilifu wa roho” yaani Roho Mtakatifu. Kwa hiyo namba 3 na7 ni namba za ukamilifu. Yesu anapomwambia Petro asamehe β€œsaba mara sabini” (Mt. 18:21-22) anamaanisha kuwa Petro asamehe β€œkwa ukamilifu, pasipo kukoma”.

Namba 4

Namba 4 kwenye Biblia inamaanisha β€œulimwengu mzima” (universality of the visible world). Kwa hiyo aya isemayo β€œmalaika wanne waliokuwa wamesimama katika pembe nne za dunia” (Ufu.7:1; 21:16; Rejea pia Is.11:12) ulimaanisha malaika walikuwa wameenea katika ulimwengu mzima. Pia aya hiyo hiyo inamaanisha kuwa jukumu lao lilikuwa ni kwa ulimwengu mzima.

Namba 6

Hii namba inasimama kumaanisha β€œmapungufu, isiyo kamilifu”. Namba hii ilihusianishwa na maadui wa Mungu kwenye Biblia. Kitendo cha mtu kuwa adui wa Mungu kilimaanisha mtu huyo si mkamilifu na ana mapungufu (Rejea 1 Nyakati 20:6; Daniel 3:1; Ufu.13:18).

Namba 12, 24

Hizi mara nyingi kwenye Biblia zinawakilisha kabila kumi na mbili za Israeli. Wapo wataalam wa Maandiko wanaosema kuwa Mitume 12 waliwakilisha makabila 12 ya Israel, yaani kila mmoja alitoka miongoni mwa makabila 12 ya Israel. Pia namba 12 inawakilisha Kanisa zima. Lakini pia 12 ni namba ya ukamilifu. Kwa hiyo Mitume 12 walikamilisha taifa zima la Israeli.

Namba 40, 175

Namba hizi kwenye Biblia zinamaanisha β€œurefu wa jambo” (longevity). Mfano wakisema fulani amekuwa mgonjwa kwa siku 40 ina maana amekuwa mgonjwa kwa kipindi kirefu, haina maana kuwa ni lazima zilikuwa 40 (huenda hata zilizidi). Kusema kuwa gharika ilidumu siku 40 mchana na usiku, ni kusema kuwa gharika ilidumu kwa kipindi kirefu; kusema kuwa Yesu alifunga siku 40 ni kumaanisha kuwa alifunga kwa muda au kipindi kirefu, yawezekana hata zaidi ya siku hizo 40. Kusema kuwa Waisraeli walikaa jangwani miaka 40 ni kusema kuwa walikaa jangwani kwa kipindi kirefu. Kusema kuwa Ibrahimu aliishi miaka 175 ina maana aliishi miaka mingi au kipindi kirefu, si lazima kwamba alifikisha miaka 175 lakini kwamba aliishi miaka ya kutosha, aliishi kipindi kirefu. Haya yote Wayahudi walielewa vizuri, hawakuhitaji kuuliza.

Kuanzia maelfu

Kwenye Biblia ikitajwa namba ya maelfu inamaanisha β€œumati mkubwa” wa watu. Yohane anaposema β€œβ€¦na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye..” (Ufunuo 14: 1) anamaanisha kuwa aliona umati mkubwa wa watu wasio na idadi. Hivyo Ufunuo 14:1 haimaanishi watu 144,000 tu bali umati mkubwa wa watu wasio na idadi. Hata kwa Kiswahili kuna wakati tunasema β€œakihubutia maelfu ya watu” tukiwa na maana kwamba alihutubia umati mkubwa wa watu.

N.B. Hapa nimeeleza baadhi ya namba tu. Zipo nyingine nyingi sana na zina maana yake. Hivyo tusitafsiri Biblia kwa maana sisisi tu (Literal interpretation), yaani kile kilichoandikwa tu. Twende zaidi ya hapo.

UFAFANUZI WA NAMBA 666 (Ufu.13:11-18)

Kuelewa maana ya namba hii ni lazima kuelewa mazingira na sababu za kuandikwa kitabu cha Ufunuo. Kitabu cha Ufunuo kiliandikwa karne ya kwanza (kati ya 90-96 AD) ambapo dini ya Ukristo ilianza kuenea kwa kasi. Hivyo tawala za Warumi na Wayahudi ziliona Ukristo kama dini mpya na tishio kwa imani, siasa na tamaduni zao. Ili kuifutilia mbali Warumi na hata Wayahudi waliendesha madhulumu (persecutions) dhidi ya Wakristo: kuwaua, kuwafunga, kuwatesa na kuwalazimisha wakane Ukristo. Yohane mwenyewe anaandika kitabu cha Ufunuo akiwa gerezani (uhamishoni) katika kisiwa cha Patmos kama matokeo ya madhulumu. Yohane anaandika kitabu cha Ufunuo kuwatia moyo Wakristo katika madhulumu wanayopata, wasikate tamaa, wasikane imani kwa kuwa baada ya madhulumu watapata utukufu katika Yerusalem mpya (mbinguni) na damu watakayomwaga katika madhulumu ndiyo itawatakasa (Ufu. 7:14).

Kwa kuwa madhulumu yalikuwepo ilikuwa ni vigumu Wakristo kuwasiliana kwa lugha ya wazi ili kuepuka kuuawa au kufungwa. Hivyo Wakristo walitumia lugha ya namba na mafumbo kufikishiana ujumbe kwa waandishi (they used coded language). Kumtaja mfalme wa dola ya Kirumi kwa jina ilikuwa ni dharau na hivyo sababu tosha ya kuuawa. Yohane anatumia lugha ya namba kumtaja mmoja wa wafalme wakatili wa dola ya Kirumi aitwaye NERO kwa kutumia namba 666. Wakristo na wataalamu wa Maandiko Matakatifu walijuaje kuwa 666 inamwakilisha mfalme NERO? Mpaka leo kwa Warumi na Wagiriki kila herufi imepewa thamani ya namba. Walipojumlisha herufi zinazounda jina β€œNERO” walipata jumla ya 666. Kwa Warumi jina la NERO liliandikwa NERON (likiwa na β€œN” mwishoni). Walijumlisha herufi za jina NERON na kupata 666 na hivyo kugundua kuwa mnyama aliyetajwa kwenye Ufu. 13:11-18 alikuwa NERO. Kwa nini amezungumziwa mnyama halafu sisi tunazungumzia mtu? Ni kwa sababu Yohane mwenyewe anasema: β€œHapa ndipo penye hekima. Yeye aliye na akili, na aihesabu hesabu ya mnyama huyo; maana ni hesabu ya kibinadamu [for it is man’s number]. Na hesabu yake ni mia sita, sitini na sita” (Ufu. 13:18).

Utaalamu wa kuzipa herufi thamani ya namba unaitwa β€œgematria”. Mfumo wa kuzipa herufi thamani ya namba unafanana na kutofautiana kwa kiasi fulani kwa Warumi na Wagiriki. Utaratibu wa kuthaminisha herufi na namba upo bado. Ndiyo maana tukiwa shule ya msingi tulifundishwa β€œNamba za Kirumi”. Tunajuaje kuwa MM ni 2000 au MMIX ni 2009. Ni kwa sababu kwa Warumi kila herufi ina thamani ya namba: M ni 1000, hivyo M+M ni sawa na kusema 1000+1000, na hivyo 2000. Tuone sasa kwa jina NERO na thamani ya kila herufi.

Gematria kwa Kirumi: NERON
N = 50
E = 6
R = 500
O = 60
N = 50
neron (50 + 6 + 500 + 60 + 50) = 666

Gematria kwa Wayunani (Waebrania): KAISER NERON

Wayunani walitamka jina ya mfalme kwa kuanza na jina la heshima β€œtitle” yaani Kaisari (Ceaser). Hivyo NERO aliitwa qsr nrwn (Kaiser Neron, kwa Kigiriki). Mwanzoni Kiebrania (Kiyunani) hakikuwa na irabu (vowels). Herufi zilizounda neno qsr nrwn (Kaiser Neron) zilipewa thamani ya namba kama ifuatavyo:
q = 60
s = 100
r = 200
n = 50
w = 6
Hivyo basi neno qsr nrwn (60 + 100 + 200 + 50 + 200 + 6 + 50) = 666.

Na Fr. Kelvin O. Mkama

Huruma ya Mungu: Upendo Usiokuwa na Kifani

Huruma ya Mungu ni upendo usiokuwa na kifani ulioelekezwa kwetu sisi binadamu. Tunapokea huruma hii kwa neema ya Mungu, ambaye daima yuko pamoja nasi katika safari yetu ya kiroho. Kwa njia ya huruma yake, Mungu anatupatia msamaha na uponyaji wa dhambi zetu. Ni muhimu kuelewa maana ya huruma ya Mungu, na jinsi inavyoweza kutusaidia katika maisha yetu ya kila siku.

  1. Huruma ya Mungu inamaanisha kusamehe dhambi zetu. Mungu anatualika kumwomba msamaha kwa makosa yetu, na kwa neema yake atatusamehe. β€œLakini Mungu, kwa sababu ya rehema yake kuu aliyo nayo, alituokoa, kwa kuoshwa kwa maji, na kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu” (Tito 3:5).

  2. Huruma ya Mungu inatupatia nguvu za kushinda majaribu na dhambi. Tunapata neema ya Mungu kwa njia ya Sakramenti ya Kitubio, ambapo tunamkiri Mungu dhambi zetu na kupokea msamaha wake. β€œMungu ni mwaminifu, naye hatawaacha mjaribiwe kuliko mwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kuvumilia” (1 Wakorintho 10:13).

  3. Huruma ya Mungu inatufariji katika mateso yetu. Tunajua kwamba Mungu yuko pamoja nasi katika kila hali, na tunaweza kumwomba aondoe mateso yetu au atupatie nguvu ya kuvumilia. β€œMungu ni wetu wa faraja yote, atufariji katika taabu yetu, ili sisi tuweze kuwafariji wale wamo katika taabu yoyote, kwa faraja hiyo ile ile ambayo sisi tunafarijiwa na Mungu” (2 Wakorintho 1:3-4).

  4. Huruma ya Mungu inatupatia upendo usio na kifani. Tunajua kwamba Mungu anatupenda bila kikomo, na kwamba upendo wake ni wa kudumu. β€œKwa kuwa Mungu aliupenda ulimwengu hivi, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

  5. Huruma ya Mungu inatupatia tumaini la uzima wa milele. Tunajua kwamba mwisho wa maisha yetu sio kifo, bali uzima wa milele pamoja na Mungu. β€œKwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, lakini karama ya bure ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu” (Warumi 6:23).

  6. Huruma ya Mungu inatufundisha kusamehe wengine. Tunapokea huruma ya Mungu kwa sababu ya neema yake, na tunapaswa kuwa na huruma kwa wengine pia. β€œBasi, kama Mungu alivyowasamehe ninyi katika Kristo, vivyo hivyo ninyi mnapaswa kusameheana” (Wakolosai 3:13).

  7. Huruma ya Mungu inatufundisha kutoa msamaha bila kikomo. Tunapaswa kusamehe wengine mara kwa mara, bila kujali makosa yao. β€œBasi, ikiwa ndugu yako akakosa dhidi yako mara saba katika siku moja, na akaja kwako akisema, Naungama, usamehe, utamsamehe” (Mathayo 18:21-22).

  8. Huruma ya Mungu inatufundisha kumpenda jirani yetu. Tunapaswa kuwa na huruma kwa wengine kama vile Mungu anavyotupa huruma. β€œKwa maana huu ndio upendo wa Mungu, kwamba tuzishike amri zake, na amri zake si nzito” (1 Yohana 5:3).

  9. Huruma ya Mungu inatufundisha kuishi kwa uadilifu na upendo. Tunapaswa kuishi kwa uadilifu na upendo, kama vile Mungu anavyotuonyesha huruma. β€œBasi, iweni wafuatao wa Mungu kama watoto wake wapendwa, na enendeni katika upendo, kama vile Kristo naye alivyowapenda sisi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato” (Waefeso 5:1-2).

  10. Huruma ya Mungu inatupatia neema ya kufikia utakatifu. Tunapokea huruma ya Mungu kwa neema yake, na tunapaswa kutumia neema hiyo kufikia utakatifu. β€œLakini kama alivyo mtakatifu yeye aliyewaita ninyi, ninyi nanyi iweni watakatifu katika mwenendo wenu wote; kwa maana imeandikwa, Iweni watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu” (1 Petro 1:15-16).

Katika Catechism ya Kanisa Katoliki, tunajifunza kwamba huruma ya Mungu ni β€œupendo wa Mungu unaotenda katika maisha yetu kadiri ya hali yetu ya dhambi na uhitaji wetu” (CCC 1846). Tunapokea huruma hii kwa njia ya Sakramenti ya Kitubio, ambapo tunamkiri Mungu dhambi zetu na kupokea msamaha wake. Katika Diary ya Mtakatifu Maria Faustina Kowalska, tunajifunza kwamba huruma ya Mungu ni kubwa zaidi ya dhambi zetu, na kwamba tunapaswa kuomba huruma yake kila siku.

Je, unajisikiaje kuhusu huruma ya Mungu? Je, unajua kwamba Mungu anatakia mema yako na anataka kukupa upendo na neema yake? Tunaweza kumwomba Mungu kwa moyo wote na kumwomba aonyeshe huruma yake kwetu sisi, na kwa wale wote tunaowapenda. Tumaini katika huruma ya Mungu na utaona mabadiliko makubwa katika maisha yako!

Mambo manne ya mwisho katika maisha

Mambo manne ambayo ni ya mwisho katika maisha ni;
  1. Kifo
  2. Hukumu
  3. Mbinguni
  4. Motoni
Mambo haya yote yanaweza kutokea wakati wowote bila kujua wala kutarajia

Kifo

Kifo ni kitu ambacho kinaweza kumpata mtu yeyote wa umri wowote awe mtoto kijana au mzee na kwa wakati wowote.
Maranyingi watu hawapendi kuongelea kuhusu kifo kwakua ni kitu ambacho kinampata kila mtu na hakipingiki wala hakina mjadala.

Hukumu

Baada ya kifo, inafuata hukumu, kila mtu atahukumiwa kulingana na matendo yake kama ulitenda mema utaenda mbinguni, na kama umetenda mabaya utaenda motoni.

Mbingu

Kama mtu akifa akiwa katika hali usafi wa moyo anaelekea mbinguni. Haijalishi ni kwa kipindi gani aliishi hivyo. Ila ni kwa hali gani kifo kilimkuta. Kwa sababu hii kila mtu anatakiwa aishi katika hali ya usafi wa moyo kwani hajui ni wakati gani atakutwa na kifo.

Motoni

Kama mtu akifa katika hali ya dhambi anaenda motoni. Kwa hiyo inatupasa tutumie vyema msamaa na huruma ya Mungu katika maisha yetu ili mwishi wetu uwe mzuri wakati bado tukiwa na muda.
Kila unapoishi ni lazima ufikirie mambo haya ukizingatia hujui wakati yanaweza kukupata. Kwa hiyo, nilazima uishi ukiwa unatafakari haya
ili uwe na mwisho mzuri.

Ni nini maana ya Ekaristi Takatifu katika imani ya Kanisa Katoliki?

Ekaristi Takatifu ni moja ya Sakramenti muhimu katika imani ya Kanisa Katoliki. Sakramenti hii huadhimishwa kwa kutumia mkate na divai, ambavyo vinageuka kuwa mwili na damu ya Yesu Kristo. Ni matukio muhimu sana katika ibada za Kanisa Katoliki, kwa sababu Ekaristi Takatifu ni chakula cha kiroho ambacho kinawapa waumini nguvu na neema ya kumtumikia Mungu.

Kanisa Katoliki linatambua Ekaristi Takatifu kama Sakramenti, ambayo ni ishara ya uwepo wa Yesu Kristo. Kwa njia hii, mtu anayepokea Ekaristi Takatifu anakuwa na umoja na Yesu Kristo, ambaye ni Bwana wa maisha yote. Kwa hiyo, Ekaristi Takatifu ni chanzo cha maisha ya kiroho ya kila Mkristo.

Ekaristi Takatifu pia ina maana ya kumbukumbu ya kifo cha Yesu Kristo msalabani. Kristo alitia damu yake kwa ajili ya wokovu wa wanadamu wote. Kwa hiyo, kila tunapoadhimisha Ekaristi Takatifu, tunakumbuka dhabihu ya Kristo na tunashukuru kwa ajili ya upendo wake kwetu sisi.

Kwa mujibu wa Kitabu cha Matendo ya Mitume 2:42, Kanisa la mwanzo lilikuwa likifanya mkutano kila siku "kwa kula chakula chao pamoja kwa furaha na kwa unyofu wa moyo, wakimsifu Mungu". Kanisa Katoliki linatambua Ekaristi Takatifu kama chanzo cha umoja na mshikamano wa waumini. Katika Ekaristi Takatifu, waumini huwa na uzoefu wa kuwa sehemu ya familia ya Mungu.

Kanisa Katoliki linatambua umuhimu wa kuenenda kwa uungwana wakati wa maadhimisho ya Ekaristi Takatifu. Kwa sababu Ekaristi Takatifu ni Sakramenti ya uwepo wa Kristo, ni muhimu kuheshimu Sakramenti hii kwa kutumia vitu vizuri, kama vile chombo cha kuwekea Ekaristi Takatifu.

Kwa kumalizia, Ekaristi Takatifu ni Sakramenti muhimu katika imani ya Kanisa Katoliki. Ni ishara ya uwepo na upendo wa Yesu Kristo, na inatupa neema ya kuwa sehemu ya familia ya Mungu. Kwa hiyo, tunapaswa kuheshimu na kuenenda kwa uungwana katika maadhimisho ya Ekaristi Takatifu. Kama inavyoelezwa katika KKK 1324, "Ekaristi ni chanzo na kilele cha maisha ya Kikristo".

Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

Utangulizi

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu.
Na wakati ndiyo sasa. Wakati ni sasa, Yesu anatuhubiria na Kwaresima imewadia, na ndiyo maana siku ya Jumatano ya majivu, kwa kuitikia mwito wa maneno ya Yesu kanisa linatualika kuingia katika kipindi cha Kwaresma, ambacho ni kipindi cha kujikusanya, kujitayarisha, kijitengeneza na kujikarabati hasa kwa toba, kufunga, kusali na kujitoa sadaka zaidi mambo yanayorutubishwa kwa tafakari ya kina ya Neno la Mungu.

Nini maana ya Jumatano ya majivu?

Jumatano ya majivu ni mwanzo wa kipindi cha kwaresima katika kanisa, Ni mwanzo wa siku arobaini za kutafakari kwa undani fumbo kuu la upendo wa Mungu linalofunuliwa kwa kujitoa kwake na kufa msalabani, kifo cha aibu cha Msalaba ili kuichukua aibu yetu au dhambi zetu.

Kwaresma ni nini?

Kwaresma ni kipindi cha siku 40 cha kujiandaa kuadhimisha Sherehe kuu ya PASAKA yaani kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Tunajiandaa kwa Kufunga Kusali, Kutubu, na Matendo mema.
Mama kanisa anatupatia kipindi hiki ili tuweze kutafakari njia na mienendo yetu na kubadilika kama haimpendezi Mungu
Tunapofunga tunatakiwa kuzuia vilema vyetu na kuviacha kabisa, tunaomba kujaliwa moyo wa toba, tunainua mioyo yetu na tunaomba Mungu atujalie nguvu na tuzo. Haitoshi tu kukiri makosa yetu bali tunahimizwa kuungama na kutubu hayo makosa na kuwa tayari kuanza upya. Kipindi cha Kwaresima huanza tangu Jumatano ya majivu. Mwanzoni mwa kazi yake ya kuhubiri Habari njema Yesu anaanza kwa kusema tubuni na kuiamini Injili – Mk 1,15. Maneno haya haya tunayasikia/tumeyasikia kila tunapopakwa majivu. Mwaliko huu wa Yesu unatuingiza katika kipindi cha toba – tubuni na kuiamini Injili. Huu ni mwaliko wa uzima. Ni mwaliko ili tuongoke, tuanze maisha mapya, maisha ya sala, kufunga na kutoa sadaka.

Kwa nini ikaitwa Jumatano ya majivu?

Jina linatokana na desturi ya kumpaka mtu majivu kichwani pamoja na kumtamkia maneno ya kumhimiza afanye toba inavyotakiwa na kipindi hicho cha liturujia kinachoandaa Pasaka.
Kwa kawaida siku ya Jumatano ya majivu unaanza mfungo unaofuata kielelezo cha Yesu kufunga chakula siku arubaini jangwani baada ya kubatizwa na Yohane Mbatizaji na kabla ya kuanza utume wake mwenyewe.

Nini maana ya majivu tunayopaka?

Majivu ni ishara ya majuto, nayo hufanywa visakramenti kwa kubarikiwa na kanisa. Tunapopakwa majivu katika paji la uso hutusaidia kutafakari na kutukumbusha kuwa wanadamu sisi tu mavumbi na mavumbini tutarudi. Hutukumbusha zaidi kuwa maisha ya hapa duniani tunapita na safari yetu itakamilika pale tutakapoungana na Bwana na mwokozi wetu katika ufalme wako.
Angalia; Isaya 61:3, Ester 4:1-3, Yeremia 6:26, Ezekieli 27:30, Mathayo 11:21 na Luka 10:13.

Kwa nini majivu yanapakwa kwenye paji la uso na si vinginevyo?

Ishara yoyote iwekwayo katika paji la uso huonesha umiliki (soma Ufunuo 7:3, Ufunuo 9:4, Ufunuo 14:1, Ezekieli 9:4-6, ). Tunapochorwa ishara ya msalaba katika paji la uso ni ishara kwamba sisi tupo chini yake yeye aliyekufa msalabani kwa ajili yetu.
Hali kadhalika hutukumbusha ishara ya msalaba tuliyochorwa na mafuta matakatifu siku ya ubatizo wetu, hutukumbusha ahadi tuliyoiweka siku hiyo ya ubatizo na kutuita tuishi maisha ya utakatifu

Padri hutamka maneno gani wakati anapaka majivu?

Tunapopakwa majivu Padre husema; Mwanadamu kumbuka u mavumbi na mavumbini utarudi AU Tubuni na kuiamini Injili.

Maneno anayosema padre yana maana gani?

Maneno haya kwa upande mmoja hutukumbusha tunapoelekea, tusisikitike kwamba siku moja tutarudi mavumbini bali tuwe na furaha kwani wakati miili yetu unarudi mavumbini roho zetu zitakwenda kuungana na Mungu Baba mbinguni.
Hivyo maandalizi tunayoalikwa kuyafanaya si maandalizi ya kuelekea mavumbini bali maandalizi ya kuelekeza roho zetu mbinguni. Ndio maana pia twaambiwa tubuni na kuiamini Injili.

Majivu tunayopakwa yanatoka wapi?

Majivu tunayopakwa hutoka katika matawi yaliyotumika katika jumapili ya matawi ya mwaka jana. Majivu haya hubarikiwa na kuwa visakramenti. Hivyo majivu yanapoashiria toba na majuto pia hutukumbusha wema wa Mungu na utayari wake wa kutusamehe.

Kwa nini unatumia matawi ya Jumapili ya Matawi?

Matawi haya yalimkaribisha Yesu Yerusalemu akiwa tayari kufa kwa ajili ya dhambi zetu, yalimpokea mfalme kwa furaha na shangwe kuu. Matawi haya yanapochomwa na sisi kupakwa majivu yetu yanatukumbusha kuwa ni kwa ajili ya dhambi zetu Mungu alimtoa mwanae wa pekee kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zetu sisi wanaadamu. Hivyo hututafakarisha kuacha dhambi.

Kanisa limekataza nini siku ya Jumatano ya majivu?

Tumekatazwa kula chakula siku ya Jumatano ya Majivu na kula nyama siku ya Ijumaa Kuu katika Amri ya Pili ya Kanisa.

Nani analazima kufunga siku ya Jumatano ya majivu na Kwaresma?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula Jumatano ya Majivu

Tunaposema kujinyima wakati wa Kwaresma tunamaana gani?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k.

Mwisho

Wakati wa Kwaresma Waamini wanapaswa kujitakasa zaidi kwa kusali, kufunga, toba na matendo mema
Kipindi cha Kwaresima ni fursa makini ya kumkimbilia Mwenyezi Mungu, kwani kwa njia ya dhambi wamejikuta wakiwa mbali na Uso wa huruma ya Mungu, kiasi hata cha kupoteza imani na matumaini kwa Mwenyezi Mungu. Hii ni changamoto ya kumpenda Mungu na jirani badala ya kukumbatia malimwengu yanayoendelea kuwatumbukiza katika utupu wa maisha ya kiroho. Kwaresima ni kipindi cha waamini kukimbilia na kuambata huruma ya Mungu inayoganga na kuponya dhambi. Ni wakati wa sala, upendo na kufunga.

Ahadi kumi na mbili za Moyo Mtakatfu wa Yesu

Bwana Yesu mwenyewe kwa kutumia kinywa cha Mtakatifu Margareta Maria Alakoki aliahidi Baraka na neema zifuatazo kwa wale wote watakaouheshimu Moyo wake Mtakatifu.

Na kwa maneno yake mwenyewe, Bwana Yesu aliahidi:

1. β€œNitawajalia neema zote watakazozihitaji katika hali yao ya maisha

2. Nitawajalia amani katika familia zao

3. Nitawafariji katika magumu yao yote

4. Nitakuwa kimbilio lao salama wakati wa maisha yao, na zaidi sana katika saa yao ya kufa

5. Nitawapa baraka tele katika shughuli zao zote

6. Wakosefu watapata katika Moyo wangu chanzo na bahari ya huruma isiyo na mwisho

7. Waumini walio vuguvugu watakuwa na bidii

8. Waumini wenye bidii watakwea kwa upesi katika ngazi za juu za ukamilifu

9. Nitabariki kila mahali ambapo picha au sanamu ya Moyo wangu Mtakatifu itawekwa na kuheshimiwa

10. Nitawajalia mapadre karama ya kuigusa mioyo migumu

11. Wale wote watakaoeneza Ibada hii kwa wengine majina yao yataandikwa ndani ya Moyo wangu na sitawasahau kamwe

12. Wale wote watakaopokea Sakramenti ya Ekaristi kila Ijumaa ya kwanza ya mwezi kwa miezi tisa mfululizo wakiwa katika hali ya neema ya utakaso, hawatakufa wakiwa na uadui nami, nitawapa neema ya kudumu katika uaminifu hadi mwisho na hawatakufa bila kupokea Sakramenti za mwisho”.

Swala la Mapadri kutooa limeandikwa wapi katika Biblia?

JE,SHERIA YA MAPADRE KUTOOA NA KUISHI USEJA IMEANDIKWA WAPI KATIKA BIBLIA AU IMETUNGWA TU NA PAPA?

Pengine umewahi kuulizwa swali hili wakati fulani.Na jibu lake ni kama ifuayavyo:
Mtu anapouliza kila kitu kimeandikwa wapi katika Biblia ni kudhihirisha kutokuijua au kuielewa vizuri Biblia Takatifu na historia yake.Mtu anapong’ang’ania “nionyeshe kitu fulani kimeandikwa wapi kwenye Biblia”ni kutaka kujiona ya kwamba yeye anaielewa sana Biblia na ameisoma yote kwa hiyo kila kitu kilichopo kwenye Biblia anakifahamu kumbe haijui Biblia bali anakariri Biblia!
Na hili suala la kushupalia swala la kuoa linadhihirisha jinsi gani tulivyo kizazi cha zinaa,ni kama tunadhani kuwa UZIMA upo katika kujamiiana!La hasha.
Paulo anasema “Kwasababu ya zinaa ni bora kuoa na kuolewa”(1Wakorintho 7:2.9) haya sio maneno ya kufurahia na kuchekelea tu maana “YANAWALENGA WALE WALIOSHINDIKANA KATIKA YALE YAPENDEZAYO”(1Wakorintho 7:1.8)sasa ni lazima tujiulize je tumeshindikana kiasi hicho?,hiyo sio sifa!
1Wakorintho 7:1.8
“Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo”
Na Paulo Mtume anasema “Ni bora kuoa au kuolewa” lakini hakusema “Ni LAZIMA kuoa au kuolewa”
Suala la kutooa kwa mapadre kadiri ya historia lilianza tangu zamani kabisa mwanzoni mwa milenia ya pili katika mtagusi wa pili wa Laterani mwaka wa 1139 ili waweze kumtumikia Mungu kwa uhuru na bila mawaa wala pasipo vikwazo(1wakorintho 7:32-35)
1wakorintho 7:32-35
“32Lakini nataka msiwe na masumbufu.Yeye asiyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya Bwana ampendezeje Bwana;33.bali yeye aliyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendeza mkewe.34-Tena iko tofauti kati ya mke na mwanamwali.Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili apate kuwa mtakatifu mwili na Roho.Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendezesha mumewe.,35.Nasema hayo niwafaidie ninyi,si kwamba niwategee tanzi,bali kwaajili ya vile vipendezavyo,tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”
Maandiko hayo hapo juu yanajieleza wala sidhani kama yanahitaji kufafanuliwa zaidi ya yanavyojifafanua yenyewe.
Watu wengine wanafikiri kwamba kutooa ni dhambi,kama ni hivyo basi hata Yesu mwenyewe alikosa maana hata yeye mwenyewe hakuoa.
Yesu mwenyewe anafundisha kuhusu ubikira(Mathayo 19:10-12)
Mathayo 19:10-12,
“Wanafunzi wake wakamwambia,kama mambo ya mme na mke yakiwa hivyo ni afadhali kutuooa kabisa.Lakini Yeye akawaambia ‘SI WOTE WAWEZAO KULIPOKEA NENO HILO,ILA TU WALE WALIOJALIWA,maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi,tena wako Matowashi WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI’,awezaye kulipokea neno hili na alipokee”
Yesu mwenyewe analifafanua jambo hili kwa mapana,katika orodha ya matowashi Yesu aliowataja,Mapadre ni Matowashi waliojifanya hivyo kwaajili ya huduma ya kanisa na ufalme wa Mungu.
Tena Yesu anatuambia waziwazi kwamba”sio wote wawezao kulipokea neno hilo”yaani sasa sio wote wawezao kuwa Matowashi(Mapadre)bali ni wale tu waliojaliwa na Mungu neema hiyo.wale wasioweza kuishi upadre huoa na kuwa na familia.Tena Yesu anamalizia kwa kusema “Awezaye kulipokea fundisho hili na alipokee”,kwa maana nyingine ni kusema “Fundisho au Utowashi huu sio wa lazima”anayeweza kuishi maisha hayo basi na ayapokee na yule asiyeweza basi aache!
Vilevile Mitume ili kumfuata Yesu kikamilifu waliyaacha yote waliokuwa nayo ikiwepo familia zao ili wamtumikie Bwana(Mathayo 19:27.29)
Mathayo 19:27.29:
“Ndipo Petro akajibu akamwambia ‘Tazama sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe,tutapata nini basi?29.Amini nawaambia,kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu wa kiume au wakike,au baba au mama au watoto au mashamba KWAAJILI YA JINA LANGU,atapokea mara mia zaidi na kuurithi uzima wa milele”
katika injili hiyo,Yesu anadhihirisha kwamba aliyeacha hayo yaliotajwa si kwasababu hawezi kuyapata la hasha,bali ameyaacha hayo yote KWAAJILI YA JINA LA YESU atapokea mengi hapa duniani halafu tena ataurithi ufalme wa mbinguni.
Mapadre wameyaacha hayo yote,wameacha nyumba,familia zao na kila kitu SIO KWASABABU HAWANA UWEZO AU HAWAWEZI KUPATA MAMBO HAYO bali WAMEACHA KWASABABU YA KUMTUMIKIA MUNGU KWA KADIRI YA MAANDIKO MATAKATIFU na kwakutaka kwao kuyaishi kimamilifu MASHAURI YA INJILI ikiwepo USEJA.
Maneno ya Paulo na yale ya Yesu mwenyewe kuhusu kumtumikia Mungu bila kuoa sio ya bahati mbaya bali ndiyo njia bora na inayofaa sana na kukubalika mbele ya Mungu.
Kwahiyo unapowaona mapadre hawaoi ujue sababu yake ni hiyo kwamba “Wamejitoa kwaajili ya kulihudumia kanisa”
(Na pia huwa nawashangaa mno watu wanaowapiga vita Mapadre kwamba kwanini hawaoi,najiuliza je,hao Mapadre wamewakataza wao kwamba wasioe?.)..na kama jibu ni hapana,sasa Je,”Pilipili ya shamba usiyoila inakuwashia nini?”
TUMSIFU YESU KRISTO!

Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha kuwa tunaweza kuwaombea wafu ili wapate neema na amani ya Mungu?

Je, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha kuwa tunaweza kuwaombea wafu ili wapate neema na amani ya Mungu? Ndio, Kanisa Katoliki linaamini kuwa tunaweza kuwaombea wafu ili wapate neema na amani ya Mungu. Imani hii imetokana na imani ya watakatifu wa kanisa na imani ya mapokeo ya kanisa kuhusu maombi kwa ajili ya wafu.

Kanisa Katoliki linatumia kifungu cha Waraka wa 2 Macabees 12:46 kuthibitisha kuwa tunaweza kuwaombea wafu. Katika kifungu hiki, inasimuliwa kuwa Judas Macabees aliwaombea wafu waliokuwa wamepoteza maisha yao vitani. Kanisa Katoliki linaamini kuwa maombi ya Judas yaliwasaidia wafu hao kupata nafuu na kumpendeza Mungu.

Pia, Kanisa Katoliki linatumia mfano wa Mtakatifu Paulo kufundisha juu ya umuhimu wa kutumia wakati wetu kuwaombea wafu. Katika Waraka wake kwa Timotheo, Paulo aliandika "Mimi nimekamilisha mbio, nimeumaliza mwendo, nimeilinda imani. Kuanzia sasa, taji ya haki imewekwa kando kwa ajili yangu, ambayo Bwana, hakimu mwenye haki, atanipa siku ile, wala si mimi peke yangu, bali na wote wao wanaopenda kufunuliwa kwake" (2 Timotheo 4:7-8). Paulo anahitimisha nafasi yake katika maisha na kuwa na uhakika wa kupokea taji ya haki. Kanisa linatumia mfano huu kuonyesha kuwa tunaweza kupokea taji ya haki kupitia maombi yetu kwa ajili ya wafu.

Kanisa Katoliki linatumia kifungu cha Kitabu cha Mithali 31:20 kufundisha juu ya umuhimu wa kuwaombea wafu. Kifungu hiki kinasema "Ananyosha mkono wake kwa wahitaji, ndiye anayewanyoshea watu wake mikono yake" na kanisa linatumia kifungu hiki kuonyesha kuwa tunahitaji kuwaombea wafu wetu ili waweze kupata amani na neema ya Mungu.

Kanisa Katoliki pia linasisitiza juu ya umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya kifo. Kanisa linaitwa kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya wafu, kama kupata Sakramenti ya Kitubio, kutolewa kwa Komunyo Takatifu na kutumia maombi maalum ya kwa ajili ya wafu. Kanisa linatufundisha kuwa, kwa kufanya hivyo, tunawasaidia wafu wetu kupata neema na amani ya Mungu katika maisha ya milele.

Kanisa Katoliki linatambua kuwa maombi kwa ajili ya wafu yanaweza kuwa na manufaa kwa wafu wenyewe, lakini pia kwa sisi waliobaki. Maombi haya yanaweza kutupa faraja na amani katika kipindi cha majonzi yetu. Kanisa linatuhimiza kwa maombi kwa ajili ya wafu wetu ili waweze kupata amani na neema ya Mungu.

Kwa kuhitimisha, Kanisa Katoliki linahubiri na kufundisha kuwa tunaweza kuwaombea wafu ili wapate neema na amani ya Mungu. Imani hii inatokana na imani ya watakatifu na mapokeo ya kanisa. Kanisa linatumia Biblia na Catechism ya kanisa kuthibitisha umuhimu wa kuwaombea wafu. Kanisa linatuhimiza sisi sote kufanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya wafu na kuwaombea kupata amani na neema ya Mungu. Maombi kwa ajili ya wafu siyo tu kwa manufaa yao, lakini pia kwa ajili yetu waliobaki. Tuombe kwa ajili ya wafu wetu ili waweze kupata amani ya Mungu katika maisha ya milele. Amina.

Mambo 7 ya kubadili katika maisha ili ubadilike

1. Huwezi kubadili namna watu walivyokutendea mpaka ubadili namna unavyowatendea.​

Matayo 7:12;
“Basi yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.”

​2. Huwezi kubadili tabia mpaka ubadili marafiki.​

1Wakorintho 15:33
“Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.”

​3. Huwezi kubadili ulichovuna mpaka ubadili ulichokipanda.​

Wagalatia 6:7;
“Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.”

​4. Huwezi kubadili mwelekeo wa maisha yako mpaka ubadili dereva.​

Kutoka 23:1-3;
“Msivumishe habari za uongo; usishirikiane na mwovu kwa kuwa shahidi wa uongo. Usiwafuate walio wengi katika kutenda uovu; wala usitie ushahidi wako katika neno lolote kwa kugeukia kando na kuandamana na mkutano ili kupotosha hukumu; wala usimpendelee mtu mnyonge katika neno lake”.

Maisha yako yaweza ongozwa na mkumbo wa watu au ​MSIMAMO​ wako ​BINAFSI​ kwa ​UNACHOKIAMINI.​

​5. Huwezi kubadili hali yako ya kifedha mpaka ubadili tabia yako ya kifedha.​

Mithali 21:17;
Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; yeyote apendaye mvinyo, kula na manukato hatakuwa tajiri.”

​Mtindo wa maisha ya ufukara ndiyo busara kwa wengi.​

​6. Huwezi kunibadili mpaka ujibadili mwenyewe.​

Matayo 7:3-5.
“Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huioni? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.”

​7. Huwezi kubadili mtazamo wako wa kifikra mpaka ubadilipo usikiacho.​

Mithali 23:7;
“Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Akuambia haya kula, kunywa; lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.”

​(Waache wenye Hekima wasikilize na kuongeza ufahamu wao.)​

Huyo anayesikiliza, huashiria na kuamua kile anachojifunza.

Kile unachojifunza, huashiria uelewa ulio nao kichwani mwako.

Uelewa ulionao kichwani mwako, huashiria maamuzi yako.

Na maamuzi yako, huashiria ​mwelekeo wa maisha yako.​

Mafundisho (Dogma) ya Kanisa Katoliki kuhusu Bikira Maria

Kuna mafundisho makuu manne kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na ufunuo wa Mungu: 1. B. Maria mkingiwa dhambi ya asili 2. B. Maria Mama wa Mungu 3. B. Maria Bikira daima 4. B. Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho

Mkingiwa Dhambi ya Asili

Malaika alimsalimia Maria β€œumejaa neema” (Lk 1:28) maana ndiye tunda bora la ukombozi ulioletwa na Yesu. Ni imani ya Wakatoliki kwamba kwa stahili za Mwanae alikingiwa asirithi kwa wazazi dhambi ya asili na madonda yanayotokana nayo, wala asitende dhambi maisha yake yote. Kwa maneno mengine, Bikira Maria tangu atungwe mimba Mungu alimkinga na kila doa la dhambi kwa kutazamia stahili za Yesu Kristo aliye Mkombozi wa binadamu wote. Ndiye aliyekombolewa kwa namna bora kushinda viungo vyote vya Kanisa. Maisha yake yote hakutenda dhambi hata moja. Mapokeo ya mashariki yanamuita β€œA Panagia” = β€œMtakatifu tu”. Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX mwaka 1854, halafu mwaka 1858 Bikira Maria alijitambulisha kama Mkingiwa kwa Bernadeta Soubirous huko Lurdi (Ufaransa). Tena mwaka 1917 huko Fatima (Ureno) aliwafunulia Lusia, Fransisko na Yasinta Marto moyo wake safi usio na doa.

Mama wa Mungu

Injili ya Yohane inaanza kwa kishindo, β€œHapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu” (Yoh 1:1). Huyo Mungu Mwana alitwaa ubinadamu katika Bikira Maria akazaliwa mtoto, jina lake Yesu, maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni binadamu kama sisi katika yote isipokuwa dhambi. Ubinadamu wa Yesu unategemea Nafsi yake ya Kimungu: akisema, β€˜Mimi’, ni kwa Nafsi yake hiyo. Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi, β€œKweli nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, nalikuwepo” (Yoh 8:50). β€œKama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhai” (Yoh 5:26).
Mtume Paulo akaeleza, β€œWakati maalumu ulipotimia Mungu alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamke” (Gal 4:4). Bikira Maria ni Mama wa Mungu kwanzia wakati huo: tangu Bikira Maria alipojaliwa kumchukua mimba, kumzaa, kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye kwa asili ni Mungu. Cheo hicho kimemuinua juu kuliko hata malaika. β€œMalaika alimwambia, β€˜Hicho kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Mungu’” (Lk 1:35).
Dogma ilitangazwa mwaka 431 kwenye Mtaguso wa Efeso uliomuita β€œMzazi wa Mungu”, ukisema Maria anastahili kuitwa hivyo kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: β€œUmebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?” (Lk 1:42-43). Ungamo hilo la Elizabeti likakamilishwa na Mtume Thoma aliyemuambia Yesu mfufuka: β€œBwana wangu na Mungu wangu!” (Yoh 20:28).

Bikira na Mama

Wakristo na Waislamu wote wanakiri kuwa Yesu alitungwa bila ya mchango wa mwanamume. La ajabu zaidi katika imani hiyo ni kwamba hata uzazi wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali uliutakasa: ni Bikira daima. Ingawa akili inasita, ni lazima kukiri na malaika, β€œHakuna lisilowezekana kwa Mungu” (Lk 1:38). Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa.
Ni imani ya Wakatoliki na Waorthodoksi kuwa Mama wa Yesu anastahili kuitwa β€œBikira daima” kwa sababu alimchukua mimba akiwa bikira, akamzaa bila ya kupotewa na ubikira, akabaki bikira hadi mwisho wa maisha yake. Hamu yake ya kuwa bikira hata kisha kuchumbiwa inajitokeza katika jibu alilompa malaika aliyemtabiria mimba: β€œLitakuwaje neno hili, maana sijui mume?” (Lk 1:35). Ni kielelezo cha Wakristo ambao Mtume Paulo aliwaandikia: β€œNawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi” (2Kor 11:2), β€œmpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine” (1Kor 7:35).
Wanaosemwa katika Injili β€œndugu zake Yesu” si watoto wa Bikira Maria, bali ndugu wa ukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, Yesu angekuwa amefanya kosa la kuwanyang’anya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, β€œβ€˜Mwana, tazama Mama yako’. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake” (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo β€œndugu yake Bwana” (Gal 1:19): Yakobo huyo alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na mama yao kwenye Injili anaitwa β€œMaria mwingine”, si Maria Mama wa Yesu. β€œWalikuwepo pia wanawake waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo na Yose” (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue kuwatofautisha kwenye Injili, ambazo zinamtaja Bikira Maria kama β€œMama wa Yesu”.

Kupalizwa Mbinguni mwili na roho

Baada ya maisha haya ya duniani Bikira Maria alipalizwa mbinguni mwili na roho, ishara ya mwanamke mshindi. β€œIshara kubwa ikaonekana mbinguni, ambapo mwanamke aliyevikwa jua, pia na mwezi chini ya miguu yake, na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake” (Ufu 12:1). Maneno ya shangilio lake yametimia: Mungu β€œamewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi; na wanyonge amewakweza” (Lk 1:52).
Imani hiyo ya mapokeo ya kale, yanavyoshuhudiwa na Mababu wa Kanisa, ilitangazwa rasmi na Papa Pius XII kwa niaba ya maaskofu wote mwaka 1950.

Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?

Jibu fupi ni kwamba Bikira Maria hakuzaa watoto wengine na hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu
Hapo zamani hakuna mkristu au dehebu lolote lililokuwa linapinga kuwa Bikira Maria sio Bikira Daima hata Waprotestanti/walokole waliamini Bikira Maria ni Bikira Hata Baada ya Kumzaa Yesu. Kwenye Miaka ya 1400-1600 Watu wote wakwanza waliopinga Kanisa Katoliki walikubali kuwa Bikira Maria ni Bikira daima wakiwemo Martin Lutha aliyeanzisha kanisa la Lutheran, John Calvin aliyeanzisha Ulokole/Protestanti, Mchungaji Ulrich Zwingli, Heinrich Bullinger, and Thomas Cranmer. Kwa miaka zaidi ya 350 Waprotestant/walokole waliendelea kuamini kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.
Lakini baadae wakristo wengi walianza kupinga kuwa Bikira Maria ni Bikira Daima.

Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;

1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu

Biblia inatuambia wazi kwamba Bikira Maria alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu Kama tunavyosoma katika Luka 1:26-35
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)

2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi

19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
Kama wangekuwepo wadogo zake Yesu Biblia ingetuambia kwamba walikuwa wapi wakati huo na walikuwa na Yesu au la.

3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12

Wakati wa Maria, Yoseph na Yesu walipoenda Yerusalemu Yesu akiwa na miaka 12 Biblia haituambii kuwa Yesu alikuwa na wadogo zake na walikuwa wapi. Kumbuka walikuwa na Desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka kwa ajili ya Pasaka familia nzima kama familia. Je hao watoto wengine walikuwa wapi. Kwa nini walikuwa na Yesu Mwenyewe? Maana yake ni kwamba Yesu hakuwa na Wadogo zake.
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
Kwa hiyo Biblia haionyeshi kuwa Yesu alikuwa na kaka na dada wakati akiwa na miaka 12. Kama wangekuwepo wangetajwa hapa kuwa walikuwa pamoja na Wazazi wao kama Yesu au walikuwa na Yesu wakati anapotea. Biblia haituambii chochote kwa hiyo wakati huo hapakuwa na wadogo zake Yesu.

4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu

Wakristu wa kwanza pamoja na Yesu aliongea Kiaramaiki au Kiebrania. Katika lugha zote hizo hakuna neno “Binamu” kwa hiyo mabinamu walijulikana kama dada na kaka wa mtu. Kwenye Agano jipya Neno kaka na Dada lilitumika pia kuwakilisha binamu.
Biblia inapotuambia kuwa Kaka na dada zake Yesu haimaanishi kaka wa kuzaliwa bali ndugu au Binamu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kwa hiyo wanaotajwa hapa ni ndugu wa Yesu kwa maana maneno kama; ndugu, kaka au dada lilitumika badala ya Binamu yaani mtoto wa shangazi au mjomba. Hapa juu Yosefu ametajwa kama kaka yake Yesu lakini tunajua kuwa Yosefu ni Baba yake Yesu. Baba na mwana hawawezi kuwa na jina sawa.

5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja

Sio mara zote Biblia imetumia neno Ndugu kumaanisha ndugu (Dada na Kaka) wa kuzaliwa yaani kaka na dada kwa mfano
Kwa kuangalia lugha ya Kiswahili na Kiingereza 1 Wakorintho 15:6 tunaona tafsiri tofauti.
KISWAHILI 6 Kisha aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano kwa mara moja; wengi wao wanaishi bado, lakini baadhi yao wamekwisha kufa.
ENGLISH 6 After that, he appeared to more than five hundred of the brothers and sisters at the same time, most of whom are still living, though some have fallen asleep.
Kwa hiyo hapa neno kaka dada na ndugu linaonekana wazi halikumaanisha ndugu au kaka wa damu.

6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

Wasemao kuwa Bikira maria alikuwa na wana zaidi ya Yesu wananukuu kifungu hiki;
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
Kumbuka kulikuwa na Yakobo wawili wakati wa Yesu, Vifungu vifuatavyo yunaweza kuona kuwa kulikuwa na yakobo wawili ambao walikuwa ndugu za Yesu lakini sio kaka wa kuzaliwa kwa mama.
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
Tunaweza kuona Undugu huu na Yesu kwa kusoma;
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
Lakini Yuda anasema;
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
Kwa hiyo Yakobo na Yohane walikuwa watoto wa Mama mwingine ambao baba yao ni Zebedayo. Na Yakobo na Yosefu walikuwa watoto wa Maria Mwingine. Kwa hiyo ni Yakobo wa wili wa Mama wengine Tofauti na Maria. Yuda alikuwa ni ndugu yake Yakobo. Yakobo vilevile alikuwa ndugu yake Yesu.
Kuthibitisha kuwa Hawa kina Mama ndio waliokuwa Mama zao kina Yakobo wote hao wawili na wengine tunaweza kusoma;
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
Kwa hiyo kwenye (Yohana 19:25) tunaona Kuwa ni kwenye Msalaba wa Yesu alikuwepo Mama yake Yesu (Bikira Maria), Dada yake Bikira Maria, Mke wa Cleopa na Maria Magdalena. Na kwenye (Matayo 27:55-56) wamwtajwa ni Mama za kina nani kama inavyoonekana kwenye kifungu kifuatachi;.
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
Kwa hiyo hii ina maanisha kulikua na wanawake watatu wenye majina sawa ya Maria waliokuwa chini ya Msalaba. Yakobo na Yuda walikuwa watoto wa Maria Mke wa Cleofasi, na sio Mama wa Yesu, na hivyo sio kaka za Yesu.

7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye

26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Ndiyo maana Bikira Maria tangu siku ile alihamia kwa Yohani kwa kuwa hakuwa na watoto wengine.

Maana ya Zaka, Sababu za Kutoa Zaka na Faida zake kulingana na Mafundisho ya Kikatoliki, Katekisimu, na Biblia

Tumsifu Yesu Kristo…

Nakualika tujifunze pamoja kuhusu maana ya Zaka, Sababu za Kutoa Zaka na Faida zake kulingana na Mafundisho ya Kikatoliki, Katekisimu, na Biblia

Maana ya Zaka

Zaka ni sehemu ya kumi ya mapato au mazao ambayo Mkristo anatoa kwa ajili ya kazi ya Mungu. Katika Biblia, zaka inatajwa kama sehemu ya lazima kwa kila Mwisraeli kutoa kwa ajili ya kuendeleza kazi ya Mungu na kuwasaidia wasiojiweza.

Sababu za Kutoa Zaka

  1. Agizo la Mungu:
  • Katika Kitabu cha Mambo ya Walawi 27:30, Mungu anatoa amri kwa Waisraeli kwamba zaka ni takatifu na ni mali ya Bwana.
  1. Shukrani kwa Baraka za Mungu:
  • Kutoa zaka ni ishara ya kumshukuru Mungu kwa baraka na mafanikio tunayopata (Kumbukumbu la Torati 8:18).
  1. Kutoa kwa moyo wa hiari:
  • Biblia inasisitiza umuhimu wa kutoa kwa hiari na kwa moyo mkunjufu (2 Wakorintho 9:7).
  1. Kuwezesha Huduma za Kanisa:
  • Zaka zinatumika kusaidia kazi za kanisa kama huduma za kiroho na kimwili (Malaki 3:10).
  1. Kuwasaidia Watu Wenye Mahitaji:
  • Zaka hutumika pia kusaidia maskini, yatima, wajane na wale walioko kwenye mahitaji (Kumbukumbu la Torati 14:28-29).

Faida za Kutoa Zaka

  1. Kubarikiwa na Mungu:
  • Mungu anaahidi kumimina baraka nyingi kwa wale wanaotoa zaka kwa uaminifu (Malaki 3:10).
  1. Kukuza Imani na Kumtegemea Mungu:
  • Kutoa zaka ni njia ya kukuza imani yetu na kumtegemea Mungu zaidi kwa mahitaji yetu (Mithali 3:9-10).
  1. Kupata Neema na Fadhila za Mungu:
  • Kutoa zaka kunaleta neema na fadhila za Mungu katika maisha yetu (Luka 6:38).
  1. Kujenga na Kuimarisha Jamii ya Wakristo:
  • Zaka zinasaidia katika kuimarisha huduma na shughuli mbalimbali za jamii ya Wakristo, kuleta umoja na upendo (Matendo ya Mitume 2:44-45).
  1. Kusafisha Nafsi na Kujenga Roho ya Ukristo:
  • Ni njia ya kujisafisha na kujenga roho ya ukarimu, unyenyekevu na upendo (2 Wakorintho 8:12).

Marejeo ya Biblia

  • Mambo ya Walawi 27:30: “Kila zaka ya nchi, ikiwa mbegu za nchi, au matunda ya miti, ni ya Bwana; ni takatifu kwa Bwana.”
  • Kumbukumbu la Torati 14:28-29: “Kila mwisho wa miaka mitatu utatoa zote zaka za maongeo yako katika mwaka ule, nawe utaziweka ndani ya malango yako…”
  • Malaki 3:10: “Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa hayo, asema Bwana wa majeshi…”
  • Luka 6:38: “Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa na kusukwa sukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu…”
  • 2 Wakorintho 9:7: “Kila mmoja na atoe kama alivyoamua moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.”

Kwa ujumla, kutoa zaka ni tendo la utii kwa Mungu na njia ya kuonyesha shukrani, upendo na kujitoa kwa ajili ya kuendeleza kazi ya Mungu na kusaidia wengine katika jamii.

Asili na matumizi ya Neno “AMINA” kama kiitikio muhimu katika Liturujia

Kiitikio hicho tunakifahamu sisi sote; tunaitikia mara nyingi lakini je, tunaelewa umuhimu wake? Binafsi nikichunguza wakati wa maadhimisho mbalimbali ya Liturujia hasa Adhimisho la Ekaristi, ni baadhi tu ya waamini wanaoitikiaAmina sehemu mbalimbali wakati wa Misa. Waamini wengine huitikia  kwa sauti  ya kuungama dhambi na wengine hawaitikii kabisa.

Asili yake 

Kwa asili Amina ni neno la kiebrania na maana yake ni: ni kweli kabisa.  Neno hilo lililotumika kukubali au kuthibitisha ukweli wa maneno au jambo lililokuwa limesemwa. Kwa hiyo mtu aliyesema Amina alitakiwa kusikia nini kilichosemwa na ndipo akubalie:    Amina.
Neno hilo limetumika katika Agano la Kale hasa katika Zaburi. Katika Agano Jipya Bwana Yesu alilitumia mara nyingi alipotaka kusisitiza siyo tu ukweli wa lile alilolisema bali pia uzito wake. Kwa namna hiyo Bwana Yesu alidhihirisha pia mamlaka yake katika lile alilosema.
Katika kitabu cha Ufunuo Yesu mwenyewe anaitwa Amina, kwani yeye ni mwaminifu kabisa katika maneno yake na kwamba yale anayosema kwa uhakika yatatimia. Tunasoma hivi: β€œHaya ndiyo anenayo yeye aliye Amina. Shahidi aliye mwaminifu na wa kweli…” (Ufu 3:14). Yesu mwenyewe anajiita  β€œnjia, na  ukweli na  uzima”(Yn 14:6).

Katika Liturujia

Katika Liturujia yetu Amina ni kiitikio muhimu sana. Tunapoanza Sala zetu na kuhitimisha tunafanya Ishara ya Msalaba na kuitikiaAmina.Tunaposema Amina tunasisitiza umuhimu wa kuanza Sala au Liturujia tunayoadhimisha kwa jina la Utatu Mtakatifu. Kwa Sala hiyo msingi tunautukuza Utatu Mtakatifu na kuomba utuongoze katika Liturujia yetu tunayoadhimisha au Sala yetu tunayoitoa. Kwa kupiga Ishara ya Msalaba tunajiweka mikononi mwa Utatu Mtakatifu tunapoanza Sala zetu au kuadhimisha Liturujia, na tunapomaliza tunapiga tena Ishara ya Msalaba na kusemaAmina. Katika Adhimisho la Liturujia kwa kawaida kuhani huhitimisha kwa Baraka ndipo waamini hujiandika Ishara ya Msalaba.
Hata hivi katika Adhimisho moja la Liturujia kuna Sala mbalimbali ambazo kuhani au atazitamka kwa sauti peke yake kama mwongoza Adhimisho ili waamini wasikie na hatimaye waitikie Amina lakini kuna Sala ambazo kuhani hutakiwa kusali pamoja na waamini na wote watazihitimisha kwa pamoja kwa kiitikio hichohicho Amina. Tufuatane kuangalia Aminakatika Adhimisho la Ekaristi, yaani Misa.

Mwanzo wa Misa  

Mwanzoni kuhani huanza: Kwa Jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu. Kama tulivyosema hapo juu hii ni Sala ya msingi ambayo inatuweka mikononi mwa Utatu Mtakatifu tunapoanza kuadhimisha Liturujia yetu. Kuhani akishasema vile Wakristo wote wanatakiwa kuitikia Amina. Wale wasioitikia wanafanya kosa kubwa la kutokukiri imani kwamba tunajiweka mikononi mwa Utatu Mtakatifu. Wanatakiwa kujiuliza wamefika kanisani kufanya nini?
Kuhani huwasalimu waamini na kisha hutualika kukiri dhambi zetu. Hapo kuna namna mbalimbali za kukiri dhambi, lakini zote huishia na Sala anayotamka kuhani: Mungu mwenyezi atuhurumie, atusamehe dhambi zetu, atufikishe kwenye uzima wa milele. Waamini wote hutakiwa kuitikia  Amina. Kwa nini wengine basi hawaitikii?
Hata hivi tukumbuke tendo hilo ni la kukiri dhambi na kuomba msamaha wa jumla katika kujiweka tayari kuadhimisha mafumbo matakatifu kama mwaliko wa kuhani unavyosema. Hiyo siyo nafasi ya Sakramenti ya Kitubio na Upatanisho. Mkristo mwenye dhambi kubwa lazima aende kuungama kwa kuhani yaani padri au Askofu.
Baada ya tendo la kukiri dhambi na kuomba msamaha hufuata Utenzi wa Utukufu ambao huimbwa au kusemwa siyo na kwaya peke yaobali na waamini wote pamoja na kuhani. Utenzi huishia na Amina. Waamini wote pamoja na kuhani hukiri kwamba walivyoimba au kusali ni ukweli kabisa.
Sehemu ya Mwanzo wa Misa huhitimishwa na Sala iitwayo Kolekta, kutokana na neno la kilatini lenye maana ya kukusanya. Kuhani akishasema: Tuombe, inampasa kunyamaa kitambo ili kila Mkristo na kuhani mwenyewe wasali kimya ndipo kuhani ahitimishe maombi yao kwa sala iliyomo katika kitabu cha Misa. Sala anayosali kuhani ni kama inakusanya na kuhitimisha maombi ya Wakristo wote wanaoshiriki Misa hiyo. Mwishoni mwa Kolekta hiyo wote hutakiwa kuitikia Amina. Asiyeitikia huwaza nini moyoni mwake?

Liturujia ya Neno

Wakati wa Liturujia ya Neno, kabla ya Injili, kuhani hujiandaa kwa Sala fupi  ili kutangaza Injili. Iwapo Misa huongozwa na Askofu, shemasi au padri iwapo shemasi hayuko huomba Baraka kwa Askofu. Anapopata Baraka hupiga ishara ya Msalaba na kutikia Amina.
Baada ya mahubiri, siku za Dominika na Sherehe hufuata Kanuni ya Imani ambayo, kama utenzi wa Utukufu kwa Mungu juu, huimbwa au husemwa na Wakristo wote, na mwishoni wote humaliza kwa Amina.
Tunapomaliza sehemu ya Liturujia ya Neno kuhani huwaalika waamini kusali: Salini ndugu, ili sadaka yangu na yenu ikubalike kwa Mungu Baba mwenyezi. Wakristo wakishasali hawasemiAmina kwa sababu kuhani huendelea mara na Sala iitwayo Sala juu ya Vipaji (oratio super oblata) ambayo ni ya kuombea dhabihu. Baada ya Sala hiyo ndipo Wakristo wote huitikia Amina.Tujibidishe kufanya vile.

Sala Kuu ya Ekaristi

Sala ya kuombea vipaji huhitimisha sehemu ya kuandaa vipaji. Hufuata Sala Kuu ya Ekaristi inayoanza na dayalojia: Bwana awe nanyi,… Inueni mioyo .. Mwishoni mwa Sala Kuu ya Ekaristi hufuata kiitikio cha Amina, ambayo huitwa Amina Kuu. Waamini wote hutakiwa kuitikia kwa nguvu Amina hiyo Kuu. Katika Sherehe  waamini wote siyo kwaya peke yao, waimbe Amina mara tatu. Wanamuziki wazingatie hilo wakitunga muziki.
Baada ya Amina kuu hufuata sehemu ya kujiandaa kwa Komunyo Takatifu, inayoanza na Sala ya Bwana: Baba yetu uliye mbinguni. Baada ya sala hiyo hatuitikii Amina kwa sababu kuhani huendelea`mara :Ee Bwana, tunakuomba utuopoe β€¦hatimaye wote huitikia: Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu…
Hufuata mara Sala ya kuomba Amani ambayo kuhani husali na mwishoni wote huitikia Amina. Wakati wa kupokea Ekaristi kila Mkristo hutakiwa kuitikia Amina kabla ya kupokea Mwili wa Bwana. Ni tendo la kukiri imani kwamba unasadiki huo ni Mwili wa Kristo. Wote huitikiaAmina mwishoni mwa Sala baada ya Komunyo.

Hatima

Mwishoni mwa Misa wakati kuhani anapowabariki waamini ndipo wote wakiinamisha vichwa vyao, hupiga Ishara ya Msalaba na kuitikia Amina ya mwisho.Wito kwa Wakristo wote: Tuitikie AMINA wakati wa Liturujia, bila kusita.Kwa kufanya vile tunashiriki na kusali  na kuhani tena tunakiri imani yetu kwamba alivyotamka kuhani ninakubali, ni kweli kabisa na Sala hiyo huwa Sala yetu pia.

Kilichowapata Watu 8 waliowahi kumdhihaki Mungu

1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)

Wakati alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa habari wa gazeti la #American alinukuliwa akisema hivi “Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya #Yesu yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake (Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966.
Wiki moja baada ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu, akapigwa risasi sita na kufariki.

2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)

Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa Brazil na kuwa rais, hata #MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo. Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya kuapishwa, akafariki dunia.

3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)

Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la #Rio #De #Janeiro, alichukua sigara, akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema #Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute”
Alifariki akiwa na miaka 32 kwa ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa yeyote yule.

4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.

Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, Mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani ilikuwa salama nae akajibu “Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata #Mungu hawezi kuizamisha”
Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.

5. BON SCOTT (MUIMBAJI)

Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979 wenye maneno haya
“Don’t stop me; I’m going down all the way, down the highway to hell’.
Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya kupaliwa na matapishi yake.

6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa Mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na kumwambia “Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu” Yule binti akajibu “Gari imejaa Mama, huyo #Mungu labda akae kwenye boneti la gari”.
Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi, trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.

7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)

Huyu alikaririwa akisema hivi “Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna kitabu kibaya…kibaya na kibaya kama #Biblia”
Siku chache baada ya kusema maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka leo ule moto ulisababishwa na nini.

8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)

Huyu alifuatwa na #Bill #Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza akasema “Simhitaji #Yesu wako, unaweza kuondoka nae”. Wiki moja baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu.

#share Ujumbe huu Kwa Ndugu na jamaa,ujumbe huu utawasidia kumuheshimu Mungu na kumtii.

Mungu ni pendo

27. Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti ya Daraja Takatifu?

Kwa wale ambao wamechagua njia ya Kikatoliki katika maisha yao, kanisa linaamini kuwa sakramenti ya Daraja Takatifu ni muhimu sana katika utendaji kazi wa maisha ya kanisa. Wakati wa kupokea sakramenti hii, wanaume wanapokea daraja ya Uaskofu, Upadri, na Ushemasi. Lakini ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu sakramenti hii? Hapa chini ni maelezo fulani:

Kwa kuanza, Kanisa Katoliki linashikilia kuwa sakramenti ya Daraja Takatifu ni mojawapo ya sakramenti saba za Kanisa. Kwa mujibu wa Catechism ya Kanisa Katoliki, sakramenti hii inampa mwanamume mamlaka ya kuwa kiongozi wa kiroho katika kanisa. Kwa hivyo, wanaume ambao wamepokea sakramenti hii wanakuwa na wajibu wa kuongoza kundi la waamini katika kufanya mambo ya kiroho.

Kuhusu ushirikishwaji wa Mungu katika sakramenti hii, Kanisa Katoliki linashikilia kwamba ni Mungu pekee ndiye anayeweza kuwapa wanaume mamlaka ya kuwa viongozi wa kiroho. Katika 1 Timotheo 4:14, kanisa linakumbuka maneno haya: "Usichukue tu kwa kiburi nafasi yako ya uongozi. Shughulika kwa bidii kila wakati, ukiendelea kujitahidi kufuata mafundisho ya Kanisa."

Kwa kuongezea, sakramenti ya Daraja Takatifu inahusiana sana na sakramenti nyingine za Kanisa. Kwa mfano, wanaume ambao wamepokea sakramenti hii wanaweza kutoa sakramenti ya Ekaristi Takatifu na kuwasamehe waamini dhambi katika sakramenti ya Kitubio. Kwa hiyo, sakramenti hii inahusiana sana na utendaji kazi wa kanisa kwa ujumla.

Mwishowe, Kanisa Katoliki linashikilia kuwa kuna wajibu mzito kwa wanaume ambao wamepokea sakramenti hii. Kwa mfano, wanapaswa kufuata maadili ya kikristo na kuheshimu mistari ya mamlaka. Katika Mathayo 23:11-12, Yesu anasema: "Mwenye kutawala kwenu, na awe mtumishi wenu. Kila mtu anayejitukuza mwenyewe atashushwa, na kila mtu anayejishusha atainuliwa."

Kwa hivyo, sakramenti ya Daraja Takatifu ni muhimu sana katika utendaji kazi wa kanisa. Wanaume ambao wamepokea sakramenti hii wanapaswa kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha kuwa kanisa linaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na kuzingatia maadili ya kikristo. Kwa hivyo, sakramenti hii ni muhimu sana katika kufikia malengo ya kiroho ya kanisa.

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu utunzaji wa mazingira?

Kanisa Katoliki limekuwa likitangaza utunzaji wa mazingira kama jukumu la kikristo kwa miaka mingi. Ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha kwamba tunalinda na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo. Utunzaji wa mazingira ni kazi yetu sote na inatokana na imani yetu ya kikristo na maadili tunayoyafuata.

Katika kitabu cha mwanzo 2:15, Mungu anamwamuru Adamu awatunze na kuilinda bustani ya Edeni. Kwa hivyo, imani ya Kanisa Katoliki inaamini kwamba sisi ni wasimamizi wa mazingira na tunapaswa kulinda kila aina ya uhai uliopo. Kwa kufanya hivyo, tunawajibika kwa Mungu na kwa vizazi vijavyo.

Kanisa Katoliki linategemea falsafa ya kiekumene katika kutunza mazingira. Falsafa hii inasema kwamba binadamu na mazingira ni sehemu moja ya ulimwengu mmoja. Tunapata maisha yetu kutoka kwa mazingira na kwa hivyo, tunapaswa kuilinda mazingira kama sehemu ya jukumu letu la kibinadamu.

Vilevile, imeandikwa katika KKK 2402, "uharibifu wa mazingira ni kinyume cha maadili na inaweza kuathiri maisha ya watu." Kwa hivyo, Kanisa linasisitiza umuhimu wa kutunza mazingira kama sehemu ya maadili yetu.

Katika Mkutano wa Mazingira wa Vatican uliofanyika mnamo 2019, Baba Mtakatifu Francis aliwataka watu wote kuchukua hatua za kuhifadhi mazingira. Aliwataka wakristo kuhakikisha kwamba wanawajibika kwa kufuata mafundisho ya kanisa na kuishi maisha yenye kuheshimu mazingira.

Kwa hivyo, tunapaswa kulinda mazingira kwa kufuata kanuni za utunzaji wa mazingira kama vile kupunguza utumiaji wa plastiki na kukuza utumiaji wa nishati mbadala. Tunapaswa pia kuhakikisha kwamba tunatumia rasilimali za dunia kwa njia yenye uwajibikaji na kwa kuzingatia mahitaji ya vizazi vijavyo.

Kwa kuhitimisha, Kanisa Katoliki linatukumbusha kwamba utunzaji wa mazingira ni jukumu letu kama wakristo. Tunapaswa kuhakikisha kwamba tunatumia rasilimali za dunia kwa njia yenye uwajibikaji na kuheshimu kila aina ya uhai uliopo. Tunapaswa kuwa wasimamizi wa mazingira na kutoa mfano wa maisha yenye kuheshimu mazingira kwa vizazi vijavyo.

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu maisha ya kuwa mtakatifu?

Ni nini imani ya Kanisa Katoliki kuhusu maisha ya kuwa mtakatifu? Hili ni swali muhimu sana kwa wakristo wote. Kuwa mtakatifu ni kielelezo cha maisha ya kujitolea kwa Mungu, kuishi katika mapenzi yake na kufuata maagizo yake yote. Ni kuitikia wito wa Mungu kwetu sisi wote kuishi maisha ya utakatifu.

Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa kila mmoja wetu ameitwa kuwa mtakatifu. Katika barua ya kwanza ya Mtume Petro, anasema "Muwe watakatifu, kwa kuwa mimi ni mtakatifu" (1 Petro 1:16). Lakini ni vipi tunaweza kuwa watakatifu? Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa njia pekee ya kuwa mtakatifu ni kwa kufuata maagizo ya Mungu, kuishi maisha ya sala, na kumtumikia Mungu na wenzetu.

Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa kuwa mtakatifu ni jambo linalowezekana kwa kila mmoja wetu. Kwa mfano, tunaweza kuwa watakatifu kwa kuishi maisha ya kuwajali wengine, kwa kusameheana, kuwapenda na kuwatumikia wengine. Kanisa linatufundisha kuwa kuwa mtakatifu ni kumfuata Yesu kwa karibu, kufuata maagizo yake na kuwa na imani thabiti kwa Mungu.

Kanisa Katoliki linatukumbusha kuwa tunapokuwa watakatifu, sisi ni sehemu ya jumuiya ya watakatifu na kwamba utakatifu ni karama inayotolewa na Mungu. Utakatifu unatokana na neema ya Mungu na hakuna mtu anayeweza kuwa mtakatifu kwa nguvu zake mwenyewe. Kwa kufanya hivyo, Kanisa linatufundisha kuwa tunahitaji kudumisha maisha yetu ya kiroho, kwa kuishi maisha ya sala, kuwahi sakramenti na kufanya kazi ya kiroho.

Kanisa Katoliki linatufundisha kwamba kila mtu ana wajibu wa kutafuta utakatifu. Hii ina maana kuwa tunapaswa kutafuta kumjua Mungu zaidi, kumtii na kumtumikia. Katika Catechism ya Kanisa Katoliki, tunasomwa kwamba "Mtakatifu ni mtu aliyejisalimisha kikamilifu kwa Mungu. Kwa hiyo, kuishi maisha ya utakatifu ni kuwa na urafiki wa karibu na Mungu" (CCC 2013).

Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa ili kuwa mtakatifu lazima tujifunze kutawala tamaa zetu, kutetea ukweli, kusamehe, kuwa na msamaha na kujitolea kwa kazi ya Mungu. Tunahitaji kuwa jasiri na kuwa na nguvu za kiroho ili kupambana na ulimwengu wa dhambi na uovu.

Katika hitimisho, Kanisa Katoliki linatufundisha kuwa kila mmoja wetu ana wajibu wa kuitikia wito wa Mungu wa kuwa mtakatifu. Kwa kufanya hivyo, tunahitaji kuwa karibu na Mungu, kuishi maisha ya sala na kutumia maisha yetu kujitolea kwa kazi ya Mungu. Tunahitaji kuwa na imani thabiti katika Mungu na kujitahidi kutimiza mapenzi yake. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kufikia utakatifu wa kumjua Mungu na kuishi maisha ya utakatifu.

Shopping Cart
28
    28
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About