Mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI, anaweza kuzaa mtoto?

Na anaweza kumwambukiza mtoto aliye tumboni au wakati wa kumnyonyesha?
Ndiyo, mama mwenye virusi vya UKIMWI na UKIMWI anaweza kubeba mimba kama mwanamke mwingine yeyote. Ila ni muhimu kukumbuka kwamba kuna uwezekano wa mtoto kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI.

Lakini siyo watoto wote waliozaliwa na mama mwenye maambukizi watabeba virusi. Kuwa moto ataambukizwa au hataambukizwa i itategemea na i idadi ya virusi ambavyo viko kwenye damu ya mama na sababu nyingine. Tafiti zimeonyesha kwamba watoto wawili kati ya watoto watatu waliozaliwa na akina mama wenye maambukizi ya Virusi huambukizwa na hivyo virusi.
Pamoja na hayo, mama mwenye virusi vya UKIMWI anaweza kumwambukiza mtoto wake wakati wa kumnyoshesha kwa sababu ya kuwepo virusi kwenye maziwa ya mama. Akina mama walio na maambukizi ya UKIMWI na UKIMWI wanashauriwa kuacha kuzaa na kutumia njia za uzazi wa mpango

Je, nikitoa au kupata damu hospitalini, itakuwepo hatari ya kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Katika swali hili lazima tutofautishe kati ya kutoa damu na kuwekewa damu. Kutoa damu hakuleti hatari, kama mtaalamu wa afya aliyechoma sindano kwa ajili ya kutoa damu anatumia sindano na vifaa vilivyochemshwa.
Kwa kawaida hakuna matatizo kuongezwa damu, kwa sababu damu i inapimwa kabla ya kumuongeza mgonjwa hospitalini. Iwapo damu i imepimwa na sindano zilizochemshwa zimetumika hakuna ubaya wowote katika kuongezwa damu.

Je, nikila na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI, nitaambukizwa na virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Hapana, ukila na mtu mwenyemaambukizi ya Virusi vya UKIMWI huwezi kuambukizwa Virusi vya UKIMWI wala UKIMWI, isipokuwa pale ambapo wote wawili mna vidonda mdomoni na mnachangia kijiko kimoja. Lakini uwezekano huu ni mdogo sana, kiasi tunachoweza kusema kwamba huwezi kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI ukila sahani moja na mtu aliyeambukizwa na virusi.
Lakini, kufuatana na kanuni za afya, ni vizuri zaidi kila mtu atumie vifaa vyake na baada ya kuvitumia avioshe kikamilifu.

Je, ninaweza kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI kwa kuumwa na mbu?

Hapana, mbu na wadudu wengine hawawezi i kukuambukiza virusi vya UKIMWI kutokana na mfumo wa mii li yao. Virusi vya UKIMWI haviwezi kuishi kwenye mii li yao, kwa sababu siyo mazingira vinavyoyapenda. Virusi vya UKIMWI vinajilisha na kuzaliana katika chembechembe nyeupe za damu, lakini chembechembe za aina hii hazipo katika mwili wa mbu. Kwa hiyo, virusi vya UKIMWI vinakufa mara baada ya mbu kufyonza damu na aking‘ata mtu mwingine baadaye hakuna hatari ya kuambukizwa.
Thibitisho jingine la ukweli huu ni kwamba sisi sote tungekuwa tumebeba virusi vya UKIMWI kama mbu angelikuwa anaambukiza kwa sababu sisi sote tunaishi katika mazingira yenye mbu na karibu na watu wengine.

Nikitumia nyembe kali au sindano pamoja na mtu mwenye Virusi vya UKIMWI ninaweza kupata Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Ndiyo, unaweza kuambukizwa ukitumia nyembe kali au sindano kwa kuchangia pamoja na mtu mwenye virusi i vya UKIMWI. Matumizi ya vyombo vyenye makali, kama sindano, visu au nyembe yana hatari. Kama baada ya kutumika damu husalia katika vyombo hivi, na endapo vitatumika bila kutakaswa au kuchemshwa, matumizi yake yanaweza kusababisha maambukizi ya magonjwa mbalimbali, pamoja na UKIMWI.
Kwa hiyo ni muhimu sana kutochangia vifaa vyenye makali na watu wengine au lazima kuvitakasa na kuchemsha kila baada ya kuvitumia.

Kwa nini nao watu wanaishi kwenye ndoa wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Kuna sababu kuu mbili i kwa wana ndoa kupata maambukizi i ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI.
Kwanza, i inawezekana kuwa mmoja kati yao alikuwa tayari na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kabla ya siku ya kuoana. Kwani hata mtu aliyeambukizwa na Virusi vya UKIMWI anaweza kuonekana mwenye afya nzuri i na kuwa navyo mwilini siku ya harusi. Hii ni pale ambapo awali alifanya ngono na mtu aliyeambukizwa Virusi i ama alivipata kwa kupitia njia nyingine kwa mfano, njia ya damu i siyo salama..
Kama mtu aliwahi kufanya ngono kabla, njia pekee ya kuhakikisha kuwa hana virusi kabla ya kufunga ndoa ni kwenda kupima damu.
Pili, wanandoa hao wanaweza kuambukizwa baada ya kufunga ndoa, pale ambapo mwenzi mmoja atafanya mapenzi na mtu mwingine. Kama mmoja wao au wote wawili watafanya ngono na mpenzi mwingine (mahusiano nje ya ndoa) wanaweza kupata maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Je, nitaweza kupata virusi vya UKIMWI na UKIMWI nikijamiiana na msichana au mvulana wa umri mdogo sana?

Ndiyo, utaweza kuvipata virusi vya UKIMWI. Uwezekano wa kuambukizwa hautegemei umri wa mpenzi wako, lakini unategemea afya yake! Kama huyu msichana au mvulana tayari ameshapata virusi vya UKIMWI na unajamii ana naye utaweza kuambukizwa.
Mara nyingi huwezi kufahamu kama mtu ana virusi vya UKIMWI au hapana, kwa sababu katika hatua ya mwanzo baada ya kuambukizwa hakuna dalili zozote za kuugua.
Vilevile ni tabia mbaya sana kushawishi wasichana au wavulana wadogo kujamii ana. Kwa usalama na faida ya wote, mnashauriwa kuacha mapenzi na wasichana au wavulana wadogo.

Je, Virusi vya UKIMWI na UKIMWI vinaambukiza kwa kujamiiana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni?

Ndiyo, kuna hatari kubwa ya kuambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana kwa njia ya sehemu ya haja kubwa au mdomoni.
Ngozi ya ndani ya sehemu ya haja kubwa ni laini sana na uwezekano wa kupata michubuko wakati wa kujamii ana ni mkubwa, kwa sababu hakuna majimaji kama ukeni yanoyorahisisha uume kuingia. Kwahiyo virusi vya UKIMWI ni rahisi sana kuingia mwilini mwa mwanamke kupitia kwenye michubuko hii ..
Pia ngono kwa njia ya mdomoni ( „kula koni, chumvi chumvi , kulamba ukeni) hatari sana kama mwanamke ana vidonda au michubuko mdomoni na mwanaume au vidonda au michubuko uumeni, wanaweza kuambukizana.
Watu wote wanashauriwa kutumia kondomu i ili kuzuia maambukizi.

Je, nikijamiiana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI bila kutumia kondomu, nitapata virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Uwezekano wa kuambukizwa na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI ukijamii ana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI bila kutumia kondomu ni mkubwa.
Mpaka leo, kondomu ni njia pekee ya kuzuia kuambukizwaVirusi vya UKIMWI na UKIMWI wakati wa kujamii ana. Kama kondomu i inatumiwa i ipasavyo na kila unapojamii ana na mtu mwenye virusi vya UKIMWI, uwezekano wa kuambukizwa ni mdogo sana. Kutumia kondomu ipasavyo i i ina maana kutumia kondomu mpya, kuivaa vizuri uumeni na kuitoa kabla ya uume kulegea.

Je,mwanaume akitoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga shahawa anaweza kuambukizwa yeye au mwanamke na Virusi vya UKIMWI na UKIMWI?

Ndiyo, hata akitoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga mbegu anaweza akaambukizwa Virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ni hatari kwa mwanamke na pia kwa mwanaume, kwa sababu vijidudu vimo ndani ya majimaji ukeni na uumeni. Hasa kama mmoja kati ya wapenzi ana vidonda au michubuko midogo sehemu za siri, Virusi vya UKIMWI. huingia kwa urahisi.

Kutoa uume nje ya uke kabla ya kumwaga shahawa siyo njia salama ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI.

Je, ni tabia zipi zinazochangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI?

Virusi vya UKIMWI kwa kiasi kikubwa vinaenea kwa njia ya kujamii ana. Kama mtu ana wapenzi wengi wa kufanya ngono, uwezekano wa kupata maambukizi unaongezeka,. Hi ni kwa sababau kila mpenzi anaweza kuwa chanzo cha maambukizi endapo watashiriki ngono za aina yeyote (ukeni au sehemu ya haja kubwa) bila kutumia kondomu.
Pia kuchelewa kutibu magonjwa mengine ya zinaa, i inachangia kuenea kwa virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Kwa mfano, kama mtu anaugua ugonjwa wa zinaa, vijidudu vya UKIMWI vinaweza kuingia mwilini kwa urahisi zaidi kwa sababu ya vidonda sehemu zake za siri.
Mwisho, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na ulevi wa pombe wa kupindukia yanaweza kuchangia kufanya maamuzi yasiyo sahihi katika matendo ya ngono.

Je, mtu mwenye kuonekana na afya nzuri, anaweza kuwa na virusi vya UKIMWI?

Ndiyo, mtu anayeonekana na afya nzuri anaweza kuwa na virusi vya UKIMWI. Katika hatua ya mwanzo baada ya kuambukizwa mtu anakuwa na virusi vya UKIMWI kwenye damu lakini haonyeshi dalili zozote za kuumwa. Hatua hii i ii inaweza kuchukua zaidi ya miaka kumi! Hii ni hatari sana, kwa sababu kama unajamii ana na mtu mwenye kuonekana na afya nzuri, lakini ndani ya mwili tayari anavyo virusi vya UKIMWI, anaweza kukuambukiza.
Njia pekee ya kuwa na uhakika kama mtu ameambukizwa na VVU au la ni kwa njia ya kupima damu katika Vituo maalamu vya kupima au hosipitalini. Kwa hiyo, kujamii ana bila kujikinga kwa kutumia kondomu i inawezekana kuhatarisha maisha yako, hata kama mpenzi wako ni mtu mwenye kuonekana na afya nzuri.

Je, watu wote wenye virusi vya UKIMWI watapata UKIMWI? Na kama ndiyo, itachukua muda gani?

Ndiyo, baada ya muda fulani karibia watu wote wenye maambukizi ya Virusi vya UKIMWI wataanza kuugua UKIMWI. Lakini muda kati ya kuambukizwa na kuanza kuugua UKIMWI unatofautiana. Wengine wanaishi muda mrefu. Kwa wastani watu wazee wazima wanaendelea kuishi miaka kumi kabla ya kupata dalili za awali. Watoto wanaopata virusi kabla ya umri wa miaka mitano kwa wastani wanendelea kuishi mwaka moja hadi mitatu.
Hakuna jibu la ujumla ni miaka mingapi ataishi tena mtu aliyeambukizwa na virusi vya UKIMWI. Idadi ya miaka ya kuishi baada ya kuambukizwa i inategemea vitu vingi, kinga asilia i inayomkinga mtu, hali ya lishe ya mtu, wakati muafaka na usahihi katika kutibu magonjwa nyemelezi na wakati muafaka na usahihi wa kutumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI kwa Kiingereza Anti-Retro-Viral drugs (ARVS )

Nini kinatokea wakati Virusi vya UKIMWI (VVU) vinapoingia mwilini na vinakwenda wapi katika sehemu ya mwili?

Virusi hivi vinakaa katika chembechembe nyeupe zilizopo kwenye majimaji ya mwili i wa binadamu hasa kwenye damu, shahawa na maji maji ya ukeni na maziwa ya mama anayenyonyesha. Ndani ya chembechembe nyeupe ndiyo mahali virusi vinakaa na kuendelea kuzaliana. Vikiwa ndani ya chembechembe nyeupe hizi, virusi huendelea kuzaliana hadi kusababisha chembechembe nyeupe hizi kupasuka.

Virusi hivi hupata nafasi ya kuendelea kushambulia chembechembe nyingine nyeupe za damu. Kwa kadri chembechembe nyeupe zilizoshambuliwa zinavyoendelea kupasuka ni kwa kiwango hicho hicho chembechembe nyeupe zinaendelea kuharibiwa na kupungua. Matokeo yake ni kupungua kwa kinga mwilini na mtu kuendelea kudhoofika.

Kinga ya mwili ni nini?

Kinga ya mwili ni mpangilio wa mwili kujikinga na maradhi. Chembechembe nyeupe zilizopo katika damu ya mwili mzima wa binadamu zina kazi maalum katika kuhakikisha kinga ya mwili i i ipo. Kama askari jeshi wanaolinda nchi yao, chembechembe hizo kwa pamoja zinalinda mwili dhidi ya magonjwa. Hivyo, kama chembeche-mbe hizo zikishambuliwa, mwili hauwezi kujikinga na maradhi au magonjwa.

Nitafanya nini kuzuia dawa za kulevya na jinsi gani nitaepukana na marafiki wabaya?

Wakati mwingine ni vigumu kusema hapana ukiwa na
maana ya hapana. Jaribu kuwa mpole na usiwe mgomvi.
Jaribu kueleza sababu zako kwa upole na uwaeleze rafiki zako kile unachokijua na nini unachofanya. Hivyo utapata heshima kutoka kwa wanarika wenzako na rafiki zako. Kama vijana wenzako watakushawishi utumie dawa za kulevya wakati wewe hutaki, wanaweza kuwa marafiki wabaya. Kumbuka kwamba rafiki ni mtu ambaye anajali, analinda na kuthamini maisha ya rafiki yake. Kwa maana hiyo, kwa nini mtu anayekushawishi kwa makusudi kufanya kitu chenye madhara kwa afya yako awe rafiki wa kweli?!

Kumbadilisha mtu aliyeathirika na dawa za kulevya

Endapo rafiki au jamaa anaomba msaada wa kuacha kutumia dawa za kulevya unaweza kumsaidia kwa kumpatia nasaha. Jitahidi kumpatia taarifa zote muhimu kuhusu dawa za kulevya. Muhimu zaidi mweleze athari za matumizi ya dawa hizo. Hata wazazi unaweza kuwapatia ushauri endapo watatambua umuhimu wako wa kujali.
Wakati mwingine waathirika wa dawa za kulevya hawako tayari kusikiliza ushauri na msaada wako. Inaweza kutokea muathirika akawa na hasira na hata kuvunja urafiki wenu na hata kufa. Usijilaumu!!! Kwa sababu ulijitahidi kumsaidia kadri ya uwezo wako. Wakati mwingine ni vyema kuvunja urafiki kwa usalama wako na kwa faida ya rafiki yako. Rafiki huyo anaweza kugundua kuwa utumiaji wa dawa za kulevya unamletea mwisho mbaya na hatimaye kuchukua uamuzi wa kueleza matatizo yake.
Kama itatokea rafiki au ndugu yako ambaye ni teja ameathirika sana kiafya usijaribu kumsaidia peke yako. Inaweza kuwa muhimu kumtafutia msaada wa kitaalamu kutoka kwa mtaalamu.

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About