Vituko Vya Xmass
Bangi si mchezo, Angalia kilichowakuta hawa
Bangi si mchezo!
Jamaa kaikoleza si ikamtuma avue nguo!
Akavua nguo zote akaenda kwenye kioo, kujitazama akaona kama kavaa suti!
then akaenda kama alivyo zaliwa kwa masela wenzake akawauliza vp suti imenikaa? Mvuta bangi mwenzie akamwambia “imekutoa kinyama ila tai umeifunga chini sana”.
Njia nne za kufikisha Habari kwa haraka
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuni…unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuni…😂😂😂😂
Kuwa na mahusiano na msichana kama huyu ni changamoto, Mabinti bwana!
Binti: Hallow mpenzi, Mambo
Jamaa: Poa baby
Binti:Uko wapi?
Jamaa: Niko town napata lunch
Binti: Wow unarudi saa ngap? Nina njaa dear naomba uniletee msosi
Jamaa: Narudi baada ya nusu saa nikuletee nini?
Binti: Niletee chipsi kuku, soseji, mayai manne ya kukaangwa pembeni, baga, piza, coke take away baridi, mkate wa moto kwenye ile bekari ya wapemba na maji ya kunywa ya kiimanjaro.
Jamaa:Umesahau viti, meza, masufuria, sahani na beseni na vijiko.
Binti: Kwanini dear?
Jamaa: Naona hutaki kula unataka kufungua hoteli!
Huu ndio Umuhimu wa English katika mapenzi
HUU NDO UMUHIMU WA ENGLISH KATIKA MAPENZI
jaribu kumwita mpenzi wako “my sweet potato” atakuelewa ila mwite kwa kiswaili ” *kiazi wangu mbatata*”hiyo itakuwa vita ya tatu ya dunia😁😁
Mlevi kazua tafrani, angalia alichokifanya hapa
MLEVI mmoja aliingia baa akavuta kiti na kukaa mhudumu akatokea kumsikiliza.
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni “nikusaidie nini?”
MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia
Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapo… teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu
Mvua zazua kasheshe! Soma hii..
Baba- : Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumban, daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi dar haiwezekani
MAMA:- Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ?
BABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia
MAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia
BABA:- Unasemaje! We uko wapi kwan
MAMA:- Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi.
BABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15
Baada ya dk 15 Baba kafika nyumban.
MAMA:- Haya umefkaje kutoka morogoro?
BABA:- Nimepewa lift na helkopta ya Mbowe..
Kama umeipenda shea na rfiki zakooo…..
Angalia huyu mke wa mtu anavyojichanganya hadi kwa mme wake
MUME: “Mke wangu nasikia John katembea na wake za watu wooote hapa mtaani kasoro mmoja tu!”
MKE: “Mmmh! basi huyo aliebaki atakuwa MAMA MBILINGE KISIKI, maana yule mama ndo ANAJIFANYAGA MGUMU sanaaa.!!”
Je, huyu mama angekuwa mkeo ungekuwa na swali lingine la kumuuliza?
Huu mchezo hautaki makeup
Mama mwenye nyumba anajipodoa anashinda saloon kujipodoa lakini house girl hata mafuta usoni hapaki lakini akipita na khanga yake moja tuu nyumba inatetemeka😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 huu mchezo hautaki mekapu
Angalia wanachokifanya Zuzu na msichana chumbani kwenye giza
Zuzu: Mambo Anna!
Anna: Poa!
Zuzu: Kuna kitu nataka nikuonyeshe…
Anna: Kitu gan?
Zuzu: Twende chumbani kwako (wakaenda)
Anna: Haya nionyeshe…
Zuzu: Funga mlango na madirisha kwanza (akafunga)
Anna: Haya nionyeshe sasa!..
Zuzu: Zima taa kwanza (akazima)
Anna: Mhm…nionyeshe sasa!
Zuzu: Haya njoo hapa kitandani…
Anna: Ok, nionyeshe!
Zuzu: Ona nimenunua saa ambayo inawaka yenyewe gizani… Acha mawazo mabaya ww???
Cheki nilichomfanyia huyu dereva tax
Nilipanda tax leo.dereva tax akaanza kuongea…
Naipenda sana kazi yangu nimejiajiri hakuna wa kunipangia nn cha kufanya
….nikamwambia_ ..KATA KUSHOTO 😂😂
Balaa la mitoto isiyopenda shule
SINA MBAVU NA HIKI KISA;
BALAA LA MITOTO ISIYOPENDA SHULE!
Baada ya mwiz kuvamia nyumba moja usiku na kuiba vitu vngi wakati anajiandaa kuondoka ghafla akadakwa mguu na dogo
DOGO: Usipoondoka na begi langu la shule NAPIGA KELELE….😂😂😂
Angalia nilichomjibu huyu kuhusu kabila langu
Kuna mtu kanikera et nmemkubalia urafiki Leo tu Facebook anataka kujua kabila langu
Bac akajifanya mjanjaa et akaniuliza mbu kwenu mnawaitaje
Mimi nkamjibu hatuwaiti wanakujaga wenyewe
😂😂😂😂😂😂😂
Si kwamba cjamuelewa ila sipendagi Ujinga Mimi
Dunia ina mambo! Angalia kilichotokea baada ya mgonjwa kuwekewa macho ya paka
Kuna jamaa alipata ajali akapofuka macho👀, akaenda hospital akawekewa macho ya paka🐈🐱,
dokta akamuuliza: vipi saizi unaona?
jamaa: naona ila naona panya tu
👀🐀🐁🐀👀
Huyu jamaa kawaweza polisi watatu, cheki alichowaambia
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: kimya
Polisi::: hodi, hodi
Jamaa::: we nani kwani?
Polisi::: sisi polisi
Jamaa::: mnataka nini?
Polisi::: kuongea na wewe
Jamaa::: kuongea na mimi?!
Polisi::: ndio
Jamaa::: mko wangapi?
Polisi::: tuko watatu
Jamaa::: kama mko watatu si muongee wenyewe…!!!
Kilichompata huyu jamaa mroho wa nyama, Hata kaa arudie tena
Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;
JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi
Mimi ndio nimeelewa hivi!
Leo nimepishana na Vitz imeandikwa, “Never trust women”
Nikajua huyu mtu lazima alikuaga na Range Rover
😂😂😂😂😂😂
Sitasahau mwaka huu
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kazi😂😂
Padri Akimbia wakati wa kuungamisha, chanzo ni hiki
Padri alikuwa amekaa katika confession booth kanisani
peke yake.
Mara kukaingia jamaa mmoja akapiga magoti upande wa
pili, akafanya ishara ya msalaba kisha akaanza kuungama
{confess}
“Padri nimekuja kuungama dhambi zangu, leo nimefanya
dhambi kubwa sana.”
Padri, “Endelea…”
“Bosi wangu aliniita nyumbani kwake, akaniambia
amegundua nimeiba shilingi millioni 100 kazini. Akasema
nisipozitoa atanipeleka polisi, sa kwa ukweli mi naogopa
kufungwa.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu,nikatoa bastola nikamuua….. Yesu atanisamehe?”
Padri: “Utasamehewa.”
“Basi wakati nataka kuondoka nikasikia mlango
unafunguliwa kutazama, Loh! Mke wa bosi, alipoona
kilichotokea akasema anapiga polisi simu.
Kutazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua na yeye pia… Yesu atanisamehe hilo?”
Padri: “Utasamehewa.”
Nikatoka nje, nikawasha gari niondoke, lakini mlinzi
akakataa kunifungulia, ati amesikia mlio wa
bastola. Nikaona ataniletea kizuizi huyu.
Nikatazama huku na huku nikagundua tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe?”
Padri:”Utasamehewa.”
“Nikajifungulia geti mwenyewe nikaenda
nyumbani, wakati napanga kuja kuungama mtoto wa bosi
akabisha hodi, nikawaza mambo gani tena, akasema alirudi
nyumbani na kukuta yaliyotokea akanionesha diary ya
babake, inayoonesha nilikuwa na appointment naye
wakati nilipomuua. Nikamuuliza nani mwingine anayejua?
Akasema ameanzia kwangu kisha anaenda polisi.
Nikatazama huku na huku nikakuta tuko wawili peke
yetu, nikamuua….. Yesu atanisamehe na hilo?”
Kimyaa….
“Padri yesu atanisamehe?”
kimya….
Jamaa akatazama kwenye confession booth padri
hayupo, lakini kwenye kona moja akaona kabati la nguo
za mapadri linatikisika. Kufungua akaona padri kajificha ndani anatetemeka huku akitokwa na jasho.
Jamaa, “Sasa baba mbona umekimbia?”
Padri kwa taabu akajibu, “Nilitazama huku na huku
nikagundua tuko wawili peke yetu…….”
Recent Comments