Vituko Vya Kutumia Watu
Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua
Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..
Kwa wanywaji wazuri wa bia,
chupa ya kwanza 🍺 huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.
chupa ya pili 🍺🍺 kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….
Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.
Bia ya tatu 🍺🍺🍺 huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..
Bia ya nne 🍺🍺🍺🍺 huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.
Bia ya tano 🍺🍺🍺🍺🍺 ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’
Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.
Kuanzia bia ya sita 🍺🍺🍺🍺🍺🍺 na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. ……. …Kuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.
Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjika…….
Soma hii, Nani haelewi kati ya hawa?
Dogo: Bro naomba nitumie hela.
Bro: Tumia tu mpaka uchoke.
Dogo: Hujanielewa,nitumie hela.
Bro: We ndo hunielewi, nimesema tumia tu…!!!
Wanandoa wa Kijapani wakibishana
*Wanandoa wa Kijapan wakiwa wanabishana hadharani*
*Husband: Takamushi jiku.*
*Wife :hashi jiku mishihe*
*Husband: inamoto kushini hat a pi*
*Wife: jejeta takuna mota shinita*
*Husband: kituya sitina kutara*.
*Wife: totori yatika miniya*
_Uko busy kusoma utadhani unaelewa kijapan kuwaga serious saa zingine_
😂😂😂😂😂😂
Nilichokifanya wakati naangalia taarifa ya habari
Jana wakati naangalia taarifa ya habar mtangazaji akasema “mpenz mtazamaji nataka nikupeleke moja kwa moja had marekani” nikazima TV kwa haraka nikaenda kuvaa viatu. Hadi sahv bado nmekaa hapa seblen nahisi bado wanaihangaikia Visa yangu
😂😂😂😂😂😂
Angalia huyu jamaa anavyojiona msomi, huyu kamuotea, hapa amekwama
USIJIONE MJUAJI SAAAA…NA.
Jamaa kamaliza chuo anarudi nyumbani kwa wazee, kufika
nyumbani.
kwa furaha waliopata wazazi, mama aliamua
kurosti kuku WAWILI(2) kwa ajili yao.
Mezani jamaa akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi,
akawaambia “hawa kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia
sheria za arthematic na geometric kuna kuku watatu mezani”
mama”hee embu tuoneshe mwanangu”
jamaa akachukua kuku ya kwanza akainua juu “ngapi?”
wazazi”moja” akainua wa pili “ngapi?” wazazi “mbili”
akawarudisha akisema”wazee wangu nadhani japo shule
hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu so tuna kuku watatu
mezani”
baba”mmh kweli mwanangu umesoma. SASA TUFANYE IVI
MIMI NACHUKUA KUKU MOJA NA MAMA YAKO WA PILI WE
UTAKULA UYO WA TATU ULIYOSEMA”
Ungekua wewe ni mwalimu ungemshauri nini huyu mwanafunzi?
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe James??
JAMES: mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa James.!!
Angalia huyu mgeni anachokifanya, wageni wengine ni hatari
Hata kama ni Mgeni this is too much.
Mwenyeji: Karibu mgeni karibu ukae,utapenda chai au soda?
Mgeni: Nipe nianze na soda wakati chai inachemka.
Mwenyeji: Utakunywa fanta au sprite?
Mgeni: Nipe fanta wakati sprite inapoa.
Mwenyeji: Utakunywa na keki au mkate?
Mgeni: Nipe keki mkate nitanywea chai ikishachemka.
Mwenyeji: Utapendelea ndiz au machungwa,
Mgeni: Nipe machungwa ndizi ntakula na wali
mchana.
Chezea mgeni ww.!!!
Haya mawazo ya huyu Mtu kuhusu Shetani ni kiboko
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuni…unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuni…😂😂😂😂
Staili nyingine za michepuko ni shida
Mtu na mkewe walikuwa bado wamelala asubuhi, mtu akapiga hodi mke akaenda kufungua mlango, si akakuta mchepuko wake,
MKE: Unataka nini we mpumbavu?
MUME: Nani huyo unamtukana?
MKE: Kuna mtu hapa anakichwa kama nenda urudi badae
MCHEPUKO:Nawewe pua kama poa
MKE:Miguu kama masaa mawili
MCHEPUKO:Masikio kama sichelewi
MKE: Ondoka hapa mjinga we. …… Akafunga mlango
MUME: mwambie ana macho kama sitoki leo ng’oo
SIPENDI UJINGA MM nikiwa na my love pr
Angalia huyu ticha wa Hesabu alichofanyiwa
Looku Looku* 👀👀
*Ama Kweli Mkuki Kwa Nguruwe kwa Binadamu Mchungu Skia Hii….!!*
*Ishawahi kutokea Pale nilipokutana njiani na mwalimu aliyekufundisha MATHS secondary afu akaniambia nimuelekeze njia ya kwenda sehemu fulani.*
*_Nenda mbele kama 2KM hivi kisha kata kushoto,ila hakikisha ANGLE inakuwa ni 30.5 KUSINI MASHARIKI.Kisha tumia PYTHAGORAS na hakikisha una FOUR FIGURE ili kupata thamani ya ANGLE._*
*Mwalimu alisonya na kuondoka.*😏😏😏😒😒
*Stakagi ujinga kabisa mimi, wakati ananichapa alifikiri sifa*😂😂
😅🙌🏽🙌🏽 *Mniache Tuu Mimi Sio Kwa Bifu Ilo Aiseee*🏃🏾
Angalia huyu mgonjwa
Mngojwa: daktari Nina tatizo la kusahausahau kila dakika.
Daktari: hilo tatizo lilianza lini?
Mngojwa:tatizo lipi?
😂😂😂😂😂😂😂
Sababu ya watu kupenda mapenzi kuliko vita
Mwalimu aliuliza swali
“Kwanini watu wanapenda MAPENZI kuliko VITA?
Mwanafunzi mmoja akajibu:-
“Kwa sababu CONDOM ni bei rahis kuliko BUNDUKI.
Wanafunzi wote: Ndiooooo…!!
Kichekesho cha mtalii na mbongo
Duh! Sikubali bora mbavu zituume wote!
Watalii wana dharau sana bana, Mtalii alikodi boti akazunguka nayo kwenye mto Rufiji kuangalia mandhari, akamuuliza kijana anayeongoza boti, “Do you know Biology, Psychology and Anthropology?” Kijana akajibu “NO,” Mtalii akamwambia “nothing you know under the sun? You are useless, and u’ll die with your illiteracy!” baada ya muda boti ikaanza kuzama, kijana akamwambia mtalii “Do you know kuogelealogy and kusepalogy from mambalogy? Mtalii akajibu huku ametoa macho “No” kijana akamwambia “You will kufalogy and mambalogy wil eat your matakology because of your bad-mdomology..😂😂😂😂😂😂
Angalia alichokifanya huyu mkaka alipoenda benki 🏦
At the bank..
Teller: Hii pesa ni fake
Mkaka: Shida iko wapi..pesa ni yangu..account pia ni yangu..weka tu!!!😂😂😂
🏃🏃🏃🏃
Misemo ya kina dada
Misemo ya kina dada
walianza na halohalooo!
Wakaja unalo babu weee!
Ikafuata utajijuuu!
Ikafupishwa utajiJJ!
Mara ghafla kantangazeee!
Haikukaa sana kansajiriii!
Ikatoka nyingine nishiiiiida!
Unaijua iliyotoka Leo?
Heh! Heh! Heeeh! MB zenyewe 8 nikudownload unanini?
Sababu ya mke kupewa dawa badala ya mumewe
Dokta: Mama tumemchunguza mumeo kwa makini sana, jopo lote la madaktari tumekubaliana mumeo anahitaji mapumziko japo ya mwezi. Sasa tafadhali chukua hivi vidonge vya usingizi vitasaidia sana.
Mama: Asanteni sana, sasa niwe nampa mara ngapi?
Dokta: Unatakiwa wewe uwe unakunywa vidonge hivi kutwa mara tatu kwa mwezi mzima, mumeo atapona.
Angalia alichokifanya huyu sharobaro kanisani
Huu usharobaro mwingine uchizi. Jamaa kamzimia demu kanisani,
mara ukafika mda wa kutoa sadaka, eti jamaa akamwambia ”dont worry bby” ntakulipia!!
Cheki jamaa alivyoumbuka baada ya kuhudhuria semina isiyomuhusu
Jamaa kavamia semina ya wasomi iliyokua inafanyika maeneo ya ubungo plaza bas wakaanza kujitambulisha
1. Naitwa Anna niko SUA mwaka3 nasoma agriculture
2. Naitwa Stella niko UDSM mwaka2 nasoma public relation
3. Naitwa Emmanuel niko UDOM mwaka3 nasoma computer science
bas jamaa nae akainuka kwa kusuasua huku akijishtukia akasema”Naitwa Elisha niko Tanesco mwaka wa 7 nasoma mita”











I’m so happy you’re here! 🥳



































































Recent Comments