Vituko Vya Jumapili
Mjini shule. Soma hii
Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.
Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!
Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsApp…!
_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang’oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._
—
_*Kisha nikaituma ile message*_
Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yake… Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.
*Akatuma message akiniuliza…*
_Hao wanawake unawajuwa, …mume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweli…!_
Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaa…!
Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaa…! Akaniandikia message nyingine….
*…Nakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupe… Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuri…!*
Nami nikamjibu…
_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipo…!_
Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdai…!
Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaa…. Kama sio mie!
Jinsi nilivyogundua kuwa nina kipaji leo
LEO NIMEPITA MTAA FULANI NIKAKIMBIZWA NA MBWA, NDIO NIKAJUA NINA KIPAJI KINAPOTEA TU………
SIO CHA KUKIMBIA, NI KUPIGA KELELE😆😆😆😆😆😆
Tofauti ya mchaga na mhaya wakipata kazi
Mchaga hata apate kazi bank bado atasema yupo kibaruani.
Acha sasa mhaya apate kazi katka mashine ya kusaga na kukoboa; utaskia i work as a crucial engineer in a monocotyledon finalizing company
😂😂😂
Huyu mwanamke ni noma cheki alichomwambia mme wake baada ya kumnunulia nguo za ndani
Mume kaingia duka la nguo na kamnunulia mke wake chupi dazeni moja zote za rangi nyeusi, akaenda kumzawadia. Mpenzi akashukuru lakini alipogundua kuwa zote ni nyeusi si akaropoka.
MY HONEY: Sasa umeninunulia chupi zote nyeusi, sasa watu si watadhani nina chupi moja tu sibadili,
Jamaa alifura akawa kama mbogo na hapo ndipo zogo kuu lilipoanza
MUME:Watu gani hao watakaokuambia unachupi moje, inamaana unawaonyesha kitumbua changu? Leo utanambia’
Ungekuwa wewe ungefanya nini?
Hakuna mtu mwenye mbio duniani kama huyu
HAKUNA MTU MWENYE MBIO, KAMA MSICHANA ALIYEPAKA MAKE UP ALAFU MVUA INYESHE….. 😂😂
Angalia sababu ya mwanamme kubadili jina na Kuitwa jina la kike, hii dunia ina mambo kweli
Rashidi alimpa ujauzito mwanafunzi, akashtakiwa.
Kumbe Rashidi ana bibi yake mtaalamu wa yale mambo yao ya Sumbawanga, akampachika Rashidi i jinsia ya kike.
Alipofika mahakamani kuhojiwa Rashidi akasema sijampa ujauzito kwa sababu mimi pia nina jinsia ya kike.
Kwa kuthibitisha Rashid wakaenda kumkagua basi akashinda kesi, kufika nyumbani Rashid akawakuta watu wamejaa wanalia, akauliza kulikoni?
Akaambiwa bibi yako amefariki. 😭😭😭😭😭😭😰😰😰😆😆😆😆😆😆
Kwa sasa Rashid anaitwa Leila😀😀😀
Hii ndio ngoma droo kwa wanaume kati ya wanawake
{ NGOMA DROO}
Sikuizi utawasikia wadada wakisema kuachwa na mwanaume asie na pesa nisawa na kuluhusiwa hospital
{Sasa na sisi} wanaume tunasema
Kuachwa na demu mpenda pesa nisawa na kumaliza mkopo benk 😂😂😂😂😂😂
Wanaume atutakagi ujinga!!!! Wanaume heeeeee🏃🏾♂🏃🏾♂🏃🏾♂🏃🏾♂
Ukimuona mbwa kwenye harusi hii ndiyo maana yake
Hili nalo neneo.
Ukimuona mbwa🐶 harusini usimpige mawe wala kumfukuza inawezekana kilichomleta pale ndicho kilichokupeleka na wewe hapo
Angalia huyu jamaa alivyoachika na msichana wake kwa kujidai kuongea kingereza na mwishowe kuchanganya maneno
MSICHANA: Mbona jana nimekupigia simu hujapokea?
JAMAA: please beby forget me.
MSichAnA: eeeh unaniambia hivo mimi?
JAMAA: nakuomba sana forget me.
MSICHANA: aya bwana poa maisha mema.
Msichana anakata simu jamaa ndo ananiuliza.”sasa
sijui amekasirikia lipi?” Mi nikamwambia we zuzu
umemwambia AKUSAHAU, dah, kumbe
ningemwambiaje? hahaha, ungemwambia
ForgivE me! au Ungesema Tu NaombA nSameHe.
Hawa Machizi wamezidi sasa
Chizi kakaa ukingoni mwa bahari analia kwa masikitiko na huku kakamata kijiko cha chai. Mwezake akamuuliza mbona unalia mwenzangu. Chizi akajibu nimetia vijiko vitatu vya sukari baharini, kila nikionja bado ina chumvi. Mwenzake akacheka sanaaaaaa akamwambia. Hujakoroga!!!!😂😂😂😂😂😂
Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta
MUME: Fungua mlango!
MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.
MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!
MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!
MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.
MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.
SMS Mafua ndiyo hii
JE UMESHAWAHI KUONA SMS MAFUA?
Cheki hii hapa……..
“Mabo dugu yagu mziba? Bwada nasubuliwa sada na bafua baka dashindwa kuadika beseji do hayo dugu yagu.
Diobeeni dipone
😂😂😂😂😂😂😂😂
Hapana Chezea
Bafua
Kilichotokea baada ya kichaa kumfumania mke wake na mwanamme mwingine
Jay akaruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na nyumbani kwake, akaulizwa unapakumbuka? akajibu ndio nyumba yangu ileee, mara wakatoka watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto wangu walee wanakwenda shule.. akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee, ghafla akatoka mwanaume Jay akasema na mimi yule naenda kazini. hivi Jay kweli kapona?
Baada ya walevi wawili kuokota kioo hiki ndicho kilifuata
Angalia kilichotokea
Walevi wawili waliokota kioo, mlevi wa 1 akaangalia muda mrefu kisha akasema “hii sura sio ngeni machoni mwangu sema jina tu silikumbuki..! !!
Mlevi wa pili akamnyang’anya kisha nae akaangalia kioo akasema “wee kweli huna akili, si mimi huyu? halafu unajidai hunikumbuki …!!!
Mambo ya pesa haya..
MAMBO YA FEDHA AISEE……. Kuna jamaa alipewa shilingi 983628763600/= …acha uvivu, najua hujasoma ni kiasi gani hicho cha fedha na mbaya zaidi hujagundua kwamba katikati ya namba hizo kuna herufi A… safi sana, najua umeangalia tena kuiona hiyo herufi, bahati mbaya hujaiona. 😜😜😜😜😜😜😜
Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi
*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!
Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.
1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu…”
Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”
🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃😂😂😂😂_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_
Alichokisema mwizi baada ya kushinda bahati nasibu
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda mil.10 za bahati nasibu ??.
Alipoulizwa atafanya nini na hela nyingi hizo
Akasema anataka kupanua shughuli zake. Mimi sijamuelewa na sasa hivi watu wameanza kuhama mtaa…
😂😂
Wabongo ni noma! Angalia huyu mbongo anachokifanya
Basi juzi kati hapa sehemu ndogo ya ukuta wa Ikulu ya Magogoni ilianguka!..
Wakapelekwa contractors watatu ili achaguliwe mmoja atakayejenga vzr na kwa bei nafuu!..
Wakwanza alikuwa MUHINDI, wa pili MCHINA na MBONGO!…
MUHINDI: “ntajenga kwa milioni 90!.., 40 za vifaa, 40 za mafundi na milioni 10 faida yangu”
MCHINA: “mi ntajenga kwa milioni 70!.., 30 za vifaa, 30 za mafundi na milioni 10 faida yangu”
MBONGO kuona vile akamvuta chemba msimamizi wa Magogoni!..
MBONGO: “mi ntajenga kwa milioni 270”
MSIMAMIZI WA MAGOGONI: “we una wazimu nn!.. yaani unathubutu kusema hivyo na unaona wenzako wametaja kiwango kidogo?!.”
MBONGO: “milioni 100 zako, 100 zangu alafu hiyo milioni 70 tunaajiri yule mchina”
Recent Comments