Visa Vya Wikiendi

Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure

Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA : Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU : Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA : Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU: Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA : Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
😂😂😂😂😂😂😂

Angalia sababu ya mke Mtarajiwa kuzimia kabla ya harusi

*Jihadharini* na wachapaji wa kadi za harusi. Hakikisha unasoma maandishi yaliyochapwa kabla ya kadi kuchapwa na kusambazwa!

Mchapaji aliombwa aweke 1 Yohana 4:18 katika kadi ya harusi lakini mchapaji kwa makosa aliweka Yohana 4:18.

1 Yohana 4:18 panasema, “Katika pendo hakuna hofu, lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu…”

Lakini Yohana 4:18 tunasoma, “Kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako.”

🏃🏃🏃🏃🏃🏃🏃😂😂😂😂_MKE MTARAJIWA AKAZIMIA HAPA, TUNAMPEPEA_

Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy

Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?….Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka …majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;

MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

Angalia kilichonikuta nilipoenda kwa mganga

Usije ukaenda kwa mganga, mwenzako yamenikuta, yani masharti niliyopewa, acha tu,
yalikua hivi:-

1.Jasho la nyoka.
2.Manyoya ya mende.
3.Sisimizi Shoga.
4.Mbwa mjane.
5.Kuku aliye single.
6.Samaki mwenye miaka miwili bila kuoga
7.Mti wenye ujauzito.
8.Mbavu za Nzi.
9.Nywele za Kiroboto.
10.Mwanya wa Mbu.
Duuh..!! mwanangu kwa hali hii mbona itakula kwako.
Wengine wanasemaga
IGA UFE! Rizik anagawa Mungu tu shetan simuelew!

Mkalimani alivyoharibu ibada ya leo

Leo nikaamua niingie misa ya asubuhi kwenye kanisa moja la kilokole kulikua na ugeni wa mchungaji kutoka Bulgaria, Mahubiri yameanza saa 1 asubuhi hali ikawa kama hivi:

MCHUNGAJI: My name is Pastor Livingstone
MKALIMANi: Kwa jina naitwa mchungaji Jiwe linaloishi
MCHUNGAJI: We thank God for All goals we set by our hands
MKALIMANI: Tunamshukuru Mungu kwa Magoli yote tuliyoweka kwa Mkono

Hivi navyoongea kanisa halina viti waumini wote tumekimbia nje naona Mkalimani amebaki na kiatu cha kushoto tu.
Sunday joke

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About