Visa Vya Krismass
Huyu mama mkwe kazidi sasa
Eti kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi. Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya. Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata. Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol. Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacy๐๐
Usichokijua kuhusu shamba lako
Je wajua?.. Shamba lako likipatikana na dhahabu ni mali ya serikali..ila likipatikana na bangi ni mali yako
๐๐๐๐
Huyu Jamaa kaona bora afe kuliko mke wake ajue Siri zake
Jamaa Mmoja Alimwambia Mke Wake Wasiliana Na Kitengo Cha Dharura Hospitali, Niko Taabani Nahisi Kama Ninakufa.
Mke Akamwambia Nipe Namba Yako Ya Siri Nifungue Simu Yako.
Mume Akasema๐๐ Basi Acha Tu; Kila Nafsi Itaonja Mauti
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Hili nalo neno kwa wavulana
Hili nalo neno
Demu wako anakuja kwako kasuka nywele za 30,000 na hujampa hata mia,we unakalia kusema waooo waoooo kama king’ora cha ambulance.
Shauri yako we endelea kusema waoooo waooo na atakuwa wao kweli.
๐๐๐๐๐๐๐
Jinsi Baba na mtoto wanavyoweza kuwaziana
Duh! Maisha
Ile time unawaza baba angekua MO DWEJI baba ako na ye anawaza mwanangu angekua MBWANA SAMMATA
Ni shetani tu anajaribu kucheza na akili zenu
๐๐๐๐
Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana
Alifanya hivi;
Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikieโฆ..mkeยญ akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja
Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili
Siku sita baadaeย mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi
Huyu bibi kazidi sasa
Bibi kapigwa mtama na Kibaka na kuporwa simu,
Kainuka na kuanza kumkimbiza kibaka,
Kibaka kuona Bibi hakati tamaa akatupa simu,
Bibi kaikota na kuendelea kumkimbiza kibaka,
Kibakaย “Bibi kama ni simu yako si tayari umechukua”,
Bibi kajibuย “Bado Mtama”
bibi ujinga hapendagi”๐ก๐ก๐ก๐ก๐ก
Alichokisema mtoto baada ya kusikia baba na mama wakiongea mambo yao usiku
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
MUME: Ntakununulia gari
MKE: Sitakiโฆ.mtoto wao aliyekuwa kalala alisikia haya maneno ya mwisho
MTOTO: Baba basi nibusu mimi uninunulie baiskeli
BABA: Pumbafu lala huko mjinga mkubwa
Mme amemfuma fundi wa kitanda na mke wake, cheki walichokua wanafanya
Kuna mama mmoja ameolewa na wanapendana sana na mmeo. siku moja mme wake alisafiri kikazi (safari ya zaidi ya mwezi) nje ya mkoa. Siku mmeo anarudi, yule mama alimtafuta fundi seremala amrekebishie chaga za kitanda zilikuwa zimeharibika, kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya above +18.
Wakati fundi anaendelea na kazi kumbe mmeo huyu dada alishafika. hakutaka kumjulisha mkeo, kwa nia nzuri tu ya kumfanyia suprise, kwani alikuja na mazaga zaga kibao. Hiyo aliingia kwa kunyatia hadi kwenye mlango wa chumbani kwao. Ghafla akasikia mazungumzo ya mkeo na fundi ndani. Mazungumzo yalikuwaje? fuatilia hapa chini
Mama X: Fanya haraka mme wangu amekaribia
Fundi: Nakaribia kumaliza, nisaidie kuchomeka vizuri upande wako (akikusudia chaga)
Mama X: Mbona haiingii
Fundi: Ingiza kwa upande upande
Mama X: Sukuma kwa nguvu
Fundi: Angalia usiumie
Mama X: Hamna shida imeingia
Wakati jamaa akiendelea kusikiliza mlangoni, fundi akaweza godoro juu ya kitanda na mama x akajitupa kitandani kujaribu kama kimetengamaa. mara chaga akachomoka na kuanguaka chini. Nini kilifuata
Mama x: Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii iiiii(miguno) “my God, mbona hivi”
Fundi : Pole sana
Mama X: sasa?
Fundi: Ngoja nichomeke tena
Mama X: Yaan wewe, utaacha mme wangu afike hatujamaliza
Fundi: Usijali namaliza sasa hivi
Baada ya dakika chache, fundi akamuaga mama na kumwambia tayari, sasa naona umefurahi. Kutoka tu mlangoni akakutana uso kwa uso na jamaa amekunja ndita kama matuta ya viatu. Gues what happened?
Kitu gani kitatokea kisia toa maoni yako kama ni ww ungefanyaje?
Utajuaje kama unachoangalia ni filamu ya kibongo!!!!
Angalia hivi
-Mlinzi wa Getini lazima awe chizi
-Mtu yupo kijijini, maisha magumu ana Wave
kichwani.
-Kama bosi atakuwa na kampuni basi ni lazima
itakuwa ya Clearing and Forwading au ya uuzaji
Magari.
-Lazima waende Kununua nguo.
-Jambazi lazima avae koti lefu jeusi na Miwani.
-Mtu akichapwa kofi huangukia kwenye kochi
ama kitandani.
-Actress huwa hawapiki hata chai.
-Kwa mdada akiishi maisha ya kitajiri lazima
avae nguo inayoishia mapajani.
-Actress even after 5 yeas utakuta staili ya
nywele na rangi za kucha ni zile zile.
-Anaweka Sumu alafu anaonja kama imekolea.
-Movie zote wapenzi huitana Baby..
-Main actor wote ni wafanya biashara na lazima
wataongelea mizigo kutoka bandarini.
-Wakinywa Soda basi lazima wabakishe.
Recent Comments