Vihoja Vya Xmass
Cheki wanachokisema vichaa baada ya kuona ndege inapita angani
Vichaa wawili walikuwa wamekaa sehemu ghafla ikapita ndege angani kichaa mmoja akasema ndege ile hitakua imembeba rais kichaa mwenzake akajibu hapana ile imebeba wazungu kama ingekuwa imembeba rais ungeona mapikipiki mbele
Hapo sasa!! Ni shida!!
Umeshawahi saidiwa homework na mzazi halafu unapata zero?
Hapo ndio unajua shida siyo wewe
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Jinsi nilivyogundua kuwa nina kipaji leo
LEO NIMEPITA MTAA FULANI NIKAKIMBIZWA NA MBWA, NDIO NIKAJUA NINA KIPAJI KINAPOTEA TUโฆโฆโฆ
SIO CHA KUKIMBIA, NI KUPIGA KELELE๐๐๐๐๐๐
Ukata wa January
Boss;-ย kwa nini umechelewa kazini
Juma;-ย kuna mtu njiani alidondosha elfu1
Boss;-ย ohhoh kwa hiyo ulikuwaunamsaidia kuitafuta
Juma;-ย hapana nilikuwa nimeikanyaga
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Sitasahau mwaka huu
Sitasahau mwaka ule ambapo nilipeleka barua ya maombi yangu ya kazi kwenye kampuni moja maarufu. Wakati nasubiri majibu siku moja nikaenda kwa mama ntilie kununua maandazi akanifungia vizuri, kufika nyumbani hamu yote ya maandazi iliniishia pale nilipogundua karatasi iliyofungiwa maandazi ni barua yangu ya kuombea kazi๐๐
Sipendi ujinga. Cheki nilichokifanya
Nimeingia chumban nikakuta panya wamekula dawa yangu ya minyoo,
Na mimi nimechukua yakwao nikanywa.
Sipendagi ujinga mm!!
๐๐๐
Ulevi noma! Angalia huyu mlevi alichomfanyia huyu jamaa usiku! Ungekua wewe ungefanyaje?
Jamaa alikuwa amelaa na mkewe saa tisa ya usiku akastuka baada ya kusikia mtu anabisha hodi kwenda kufungua mlango
Akamkuta jamaa kalewa sana mlangoni kwao
JAMAA: Nini tena mheshimiwa kuamshana saa hizi?
MLEVI: Naomba uje unisukume.
Jamaa akiamini kuwa pengine kuna gari la huyu mlevi limezima jirani akamwambia subiri nikavae viatu. Baada ya kuvaa viatu akatoka na wakaanza kusindikizana na mlevi. Mlevi akaongoza njia
mpaka kwenye mabembea ya jirani akakaa kwenye bembea moja na kumgeukia jamaa na kumwambia.. Okay nisukume basi.
Sasa Hawa wadada Wapo in Relationship Na Nan!!??
Asilimia 76% Ya Wasichana Kila Ukiwatongoza Wanakwambia Wapo In relationship SAWA ATUKATAIโฆ
Asilimia 98% Ya Mamen Wapo SINGLEโฆ HAPA NDIPO HESABU ZANGU ZINAFELI..
Sasa Hawa wadada Wapo in Relationship Na Nan!?.
Duh! Hii sababu ya huyu mwanaume kulewa ni shida
๐ง: “Mpenzi, nakuomba uache kulewa”
๐จ: “poa, na wewe acha kutumia make up”
๐ง: “Mimi napaka make up ili unione mzuri”
๐จ: “Na mimi nalewa ili nikuone mzuri”
Vodka hatareee๐๐
Njia nne za kufikisha Habari kwa haraka
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniโฆunaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniโฆ๐๐๐๐
Recent Comments