Vihoja Vya Kukubadilisha Mood

Cheka kidogo, angalia anachosema huyu mchaga

Mchaga baada ya kufa akaulizwa na malaika anayetoa roho: Mangi hapa ni njiapanda kulia ni Mbinguni na kushoto ni Jehanamu, Je unachagua kwenda wapi?

MANGI: Bwashee, mi nabaki hapa hapa njiapanda aisee.
MALAIKA: Kwa nini?
MANGI: Aisee, nikifungua duka hapa si nitapata wateja wa Mbinguni na Jehanam. Yani patakuwa senta ya hatari, supu na nyama choma muda wote. Hata we utafaidi, unavyoenda kuchukua roho unaniletea stock nakupa hela yako cash mkononi. Na kila ukipita hapa unapiga mchemsho wako wa ulimi na bia mbili chap kabla ya kuingia mbinguni.
Kwanza nashangaa Shirima alipitaje hapa bila kushika ploti, au alikufa amelewa sana?

Huu ndio mlolongo wa michepuko kuwahi kutokea kati ya mke, mume mwanafunzi na boss

BOSS anamwambia sekretari wake: Wiki hii tutaenda wote Serena Hotel kwenye mkutano fanya mipango yote.
SEKRETARI (anamuaga mumewe): Tunaenda na bosi Serena hotel kwenye mkutano for 1 week.
MUME (anampigia mpango wa kando): Mambo safi, wife anaenda kikazi Serena, jitayarishe tujipe raha for 1 week
(Mpango wa kando) anamwambia mwanafunzi wake wa tution: wiki hii nina kazi fulani hakuna tution mpaka week ijayo.
MWANAFUNZI anampigia simu sugar daddy wake ambaye ndo (BOSS): Dear hakuna tution wiki hii nakuja kwako…..

BOSS anamwambia sekretari wake: Siendi Serena tena coz mjukuu wangu atanitembelea.
SEKRETARI: Mume wangu hatuendi Serena
MUME (anampigia Mpango): dah! mpenzi, huyu mke wangu haendi tena. Shit! So hadi next time plz
Mpango wa kando a.k.a teacher (anampigia mwanafunzi): Darasa kama kawaida sorry for the earlier message.
MWANAFUNZI: darling tution inaendelea kumbe, so nakuja wiki ijayo!!
BOSS: Sekretari sorry jitayarishe ile safari ya Serena iko palepale……

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂

Angalia huyu jamaa anavyojiona msomi, huyu kamuotea, hapa amekwama

USIJIONE MJUAJI SAAAA…NA.
Jamaa kamaliza chuo anarudi nyumbani kwa wazee, kufika
nyumbani.

kwa furaha waliopata wazazi, mama aliamua
kurosti kuku WAWILI(2) kwa ajili yao.
Mezani jamaa akataka kuwadhihirishia kuwa yeye ni msomi,
akawaambia “hawa kuku unaona wako wawili ila kwa kutumia
sheria za arthematic na geometric kuna kuku watatu mezani”
mama”hee embu tuoneshe mwanangu”
jamaa akachukua kuku ya kwanza akainua juu “ngapi?”
wazazi”moja” akainua wa pili “ngapi?” wazazi “mbili”
akawarudisha akisema”wazee wangu nadhani japo shule
hamkwenda ila mnajua moja+mbili=tatu so tuna kuku watatu
mezani”
baba”mmh kweli mwanangu umesoma. SASA TUFANYE IVI
MIMI NACHUKUA KUKU MOJA NA MAMA YAKO WA PILI WE
UTAKULA UYO WA TATU ULIYOSEMA”

Angalia huyu msichana alichonifanyia

Kuna siku nilichalala kipesa nikaamua kuomba dem wangu aniazime 10,000/= akanipa.
Baada ya siku mbili nikapata pesa zaidi ya laki nne hivi, nikaamua kumpa 100,000/= mpenzi wangu bila yeye kuniomba.
Baada ya siku 3 akaja kuniambia:- “Bae, ile 10,000/- niliyokuazima mwenyewe amekuja kunidai, so kama unayo naomba unipe nimrudishie maana ananisumbua leo siku ya 3.”
SAA HIZI NIPO ZANGU SINGLE NATAFUTA DEM MWINGINE

Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta

MUME: Fungua mlango!

MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.

MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.

MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!

MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!

MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.

MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.

MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About