Vihoja Vya Kukubadilisha Mood
Angalia nilichomfanyia huyu dereva sasa
Tulikua kwa basi tunaelekea arusha,ile namcheki dereva kumbe ni best yangu na basi ilikua kwenye spidi hatari, nikaenda kumziba macho nkamuuliza otea mi ni nani, kabla hajanijibu nikasikia kishindo kikubwa sana
NA SASA HIVI NIMEZINDUKA NIMEONA ABIRIA WOTE TUPO WODI NAMBA 3 HAPA KCMC MOSHI. 🤕🤕🤕🤕
SODA ZA WAGONJWA PLIIIZ!!! 🙏🙏🙏🙏🙏
Huyu dogo nimsaidieje? Cheki alivyojichanganya
Nimekutana na dogo mmoja hivi hapa analia,namuliza analia nin??ananambia ”ALIPEWA MIA TANO ZIPO MBILI,MIA TANO MOJA YA NYANYA na MIA TANO NYINGINE YA VITUNGUU sasa KAKOSEA KAZICHANGANYA HAJUI TENA IPI NI YA NYANYA na IPI NI YA VITUNGUU!!!
.
.
NA PESA ZOTE ANAZO KAZISHIKA MKONONI,
Angalia nilivyoingizwa mjini na ujanja wangu wote
Ndio nilikuwa nimeshuka kwenye basi la SAI BABA pale Ubungo, nina Begi kubwa Mgongoni na begi Dogo la Lap Top mkononi, sura inatazama Mbele Very Serious kama nipo kwenye Gwaride la Uhuru!..Mabega juu yanafanya Cheers na Mawingu!, natembea kwa madoido…..leo nimetoka Likizo Moshi,
“Brother Simu ya ukweli hii..kitu cha Tecno C9 bei poa” hii ilikuwa sauti ya Teja mmoja hivi!
Yaani huyu Teja Bwege kweli,anataka kumuuzia nani sabuni? mimi sio wa kuja!…kamwe Siwezi kuibiwa hapa Town,hakuna wizi au utapeli nisioujua!, Mimi nimezaliwa Mwananyamala kwa Manjunju, nikalelewa Tandale kwa Mtogole, Shule ya msingi nimesoma Turiani Magomeni, Hivi Mbwa gani aniibie?…kwa Style ipi?
Sipendi kabisa Upuuzi!, Wajinga ndio wataibiwa, sio Mimi!…sasa Kwa mwendo wa haraka nikatoka nje kabisa ya Stendi ya Ubungo straight mpaka Stendi ya dala dala za Kariakoo, hapo ndipo nikakutana na Vijana wawili wadogo wakiwa na mzani wa kupimia uzito,…hakika napenda sana vijana wanaojituma kama hawa na sio ile Mijizi ya kule ndani Stendi!!,….hapa sasa nikapata wazo!
“Dogo mnapima uzito kwa shilingi ngapi?”
“Mia mbili tu Kaka!”
”Ok”
Kwa mwendo wa kikakamavu nikapanda juu ya mzani,lengo hapa ni kujua uzito wangu, Mtori niliokula mwezi mzima kule kwa Mshekuu sio mchezo, hapa nahisi nacheza kwenye kg za John Cena,
“Mama wee! Dogo mzani mzima huu kweli? Mbona nina kilo 134?” (Nilihamaki)
“Aaah! Brother huoni umepanda na Mabegi juu ya mzani?”’
Hahaha! kweli nimechanganyikiwa!…Sasa nikatoa mabegi yote mawili na kurudi juu ya Mzani, hapa ndipo Uzito ukashuka kutoka kg 134 mpaka kg 56!…My God kweli Body la “One Pack ” haliongopi! thats means mabegi yaliniongezea kg 78! duh hii ni hatari!
“Yaani we Dogo kitambi chote hiki kg 56? huu Mzani Mzima kweli?”
Kimya…
“Dogo huu Mzani vipi?”
Kimya…
Dogo ana dharau huyu!…Sasa ndio nikabandua macho yangu toka kwenye kioo cha mzani ili nimtazame huyu dogo asiyejibu!….ndipo macho yangu yakakutana na Kigoda tupu kilichochongwa Mvomero!…Dogo hakuwepo!….na Mabegi pia hayapo!…lap top haipo!….NIMEPIGWA!
Ni dhahiri watoto wa Mjini walikuwa wameniacha juu ya Mzani, wamechukua Lap top ya Milioni na wameniachia Mzani chakavu wa elfu 40, what a stress!….sasa nilirudisha macho kwenye kioo cha uzito na sasa kilisoma KG 38!…yaani dakika hii hii nimepungua kilo zingine 18, Hakiyamama nahisi hata utumbo wangu wamebeba!…niitieni Ambulance!
🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼🙆🏼
Angalia alichokifanya huyu sharobaro kanisani
Huu usharobaro mwingine uchizi. Jamaa kamzimia demu kanisani,
mara ukafika mda wa kutoa sadaka, eti jamaa akamwambia ”dont worry bby” ntakulipia!!
Watu wana vimaneno
Eti linalo jamba ni tumbo makalio ni spika tu
Dah!!
Nimecheka hadi basi leo
😸😸😹😹
Duh! Hiki nacho chombo cha moto?
_Sheria inasema kila anaetembea na chombo cha moto barabarani sharti awe na leseni._
_Sasa hawa wauza kahawa mbona wanatembea na chombo cha moto lakini hawakamatwi 😡._
_Hizi sheria zinapendelea._
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Tofauti ya mchaga na mhaya wakipata kazi
Mchaga hata apate kazi bank bado atasema yupo kibaruani.
Acha sasa mhaya apate kazi katka mashine ya kusaga na kukoboa; utaskia i work as a crucial engineer in a monocotyledon finalizing company
😂😂😂
Jinsi ya Kubana matumizi X-mass
Badala yakupika PILAU tutapika TAMBI kwenye Xmas maana tutakua tumeokoa sh.15,000/= Vitunguu swaumu 2000, Vitunguu maji 1000, hiliki 1000, Magome 1000, Michele wa 2000, Soda 3000, Nyama 5000 . Fedha hizi zitatumika kununua mfuko wa cement ili tuanze kujaza kibubu cha ujenzi wa nyumba badala ya kupanga. Karibuni saana maji ya kunywa tumechemsha ndoo nzima.
🎀✨Marry Xmas & Happy new year.✨🎀
Soma alichojibiwa huyu mzee baada ya kudai kutaka kumsikiliza Nyerere
Mzee: Dereva ongeza sauti tumsikilize Mwalimu Nyerere!!
Dereva: ungemsikiliza mwalimu wako miaka iyo saivi ungekua na gari yako
😅😅😅😅😅😅😅😅😅
Mke alichomfanyia mme wake kabla ya kwenda safari, Chezea mawaifu walokole wewe!
JAMAA alimuaga mke wake mlokole kuwa anaenda semina ya siku tatu, kumbe anakwenda kwa bi mdogo.
Mke akamwambia mumewe; “Tupige magoti tusali”,
Wakapiga magoti…:
MKE: Eee baba msaidie mume wangu afike salama safari yake.
MUME: Emen…
MKE: Mpe nguvu katika yote atakayoyafanya huko.
MUME: Emen…
MKE: Akitaka kufanya uasherati ashindwe.
MUME: Kimya…
MKE: Akifanya uasherati apatwe na janga baya kwa uwezo wako bwana.
MUME: …….!!
MKE: Yaani akifanya uasherati afie hukohuko kwa mateso makali.
MUME: Maombi gani sasa hayo!!?. Haya basi siendi semina ufurahi wewe.
Chezea mawaifu walokole wewe!
Recent Comments