Vihoja Vya Kukubadilisha Mood

Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?

RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?

JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja

Angalia uhuni wa huyu dereva

Dereva alikamatwa kwa kosa la kusababisha ajari ya watu wa5 aliowagonga. Trafik akamuliza kwanin umewagonga awa watu? Jamaa akajibu,”nilikua mwendo wa kasi sana, alafu nimejaza abiria ndani, gari likawa linakuja mbele yangu nilipokanyaga breki zikakatika, sasa ningefanya nin?” Trafki akamwmbia, kwanin ucngeenda upande ambao una watu wachache ili uokoe wengi? Jamaa akajibu, “nilifanya hivo, huku kushoto alikua m1 na kulia walkua wa4, nikamfuata uyu wa kushoto et akakambilia upande wakulia akazani cjamwona, nikamfata huko huko alipoenda, nikampa kitu mbwa yule”

Wanaume wote ni waaminifu

Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.

Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.

Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?

Jamaa: Hapana.

Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?

Jamaa: NDIYO.

Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.

Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?

Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.

Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”

Jamaa: NDIYO.

Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?

Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!

Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.

*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.

WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
😀😀😀😀

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About