Vichekesho Vya Weekend
Cheki huyu mzee alichomfanyia muuzaji wa pharmacy
Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?….Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka …majimaji yaliyomo kwenye
kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo
Sifa 10 za mwanaume ambaye kila binti anayetaka aolewe angependa aolewe naye!!
1. Awe na pesa nyingi
2.Siyo lazima awe mzuri wa sura
3. Ajenge ukweni
4.Awe mpole
5.Asimuonee wivu mke wake
6.Awe mwenye upendo wa dhati
7.Asishike simu ya mke wake.
8.Akimkuta na mwanaume apite tu, akitaka kujua ni nani asubiri nyumbani
9.Awe anamskiliza mke wake kwa kika kitu.
10.Asipende mwanamke mwingine zaid yake
UKIMPATA MWANAUME MWENYE SIFA HIZO KAPIME DNA LAZIMA ATAKUWA NI BABA AKO.
😂😂😂😂😂😂😂😂
Angalia huyu mgeni anachokifanya, wageni wengine ni hatari
Hata kama ni Mgeni this is too much.
Mwenyeji: Karibu mgeni karibu ukae,utapenda chai au soda?
Mgeni: Nipe nianze na soda wakati chai inachemka.
Mwenyeji: Utakunywa fanta au sprite?
Mgeni: Nipe fanta wakati sprite inapoa.
Mwenyeji: Utakunywa na keki au mkate?
Mgeni: Nipe keki mkate nitanywea chai ikishachemka.
Mwenyeji: Utapendelea ndiz au machungwa,
Mgeni: Nipe machungwa ndizi ntakula na wali
mchana.
Chezea mgeni ww.!!!
Kweli shilingi yaua, Huyu jamaa kapatikana, angalia anachomjibu mke wake,
Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
“Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..
Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia
“Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo”.Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,”eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu “Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue”.
Angalia Kiingereza kilivyoniponza
Shikamoo kingereza..!
Baada ya kufika Kempiski nikaona menu imeandikwa:
Sauteed white corn, rare lucy beans, garnished with rift potatoes & topped with organic unprocessed guacamole!
Price: TSH 44,000/=
Nikaagiza!
Nilipoletewa ndio nagundua kwamba: ni makande na parachichi ..🤔
hapo ndo unagundua mwalimu wa kiingereza alikuwa sio mtu wa mchezo mchezo🤒💨
Hizi swaga za huyu jamaa ni shida, Google!
Jamaa alikuwa kwenye daladala pembeni kuna
dada mrembo kakaa. Kamlia timing kwa muda
kisha halafu akamuuliza “Samahani dada
unaitwa Google?”.
Dada: “hapana, kwanini umedhani naitwa
hivyo?”. Jamaa: “Una kila kitu nnachokitafuta
“😅😃😃😃😃😃😃😃😃😃
Angalia kilichompata huyu mwanafunzi kilaza anayejiamini
Teacher: Who is a pharmacist?
Shemdoe raised up his hand.
Teacher: So it’s only Shemdoe that can tell who a pharmacist is in this class? So there is no body else to answer the question except Shemdoe? (There was no reply from the students)
Teacher: Ok now Shemdoe, chukua hii fimbo, charaza vilaza hawa wote kila mmoja viboko kumi…. Shemdoe akiwa amevimba kichwa, akawatwanga viboko kumi kumi vya kushiba darasa nzima
Teacher: Now, my dear Shemdoe tell this dumb students who a pharmacist is…
Shemdoe: Yes, sir. A Pharmacist is a farmer who assists people. Shemdoe saiv amelazwa MOI kwa wataalam wa mifupa 🏃
Huyu mwanafunzi kweli kiboko
Ticha: Wa kwanza kujibu swali langu ataenda Home mapema..
John kusikia hivyo….Karusha begi la daftari nje…..`
`Ticha akauliza: Nani karusha begi nje!?!`*
`John: Mimi….. Kwa herii Mwalimu……` 😂😂,😂😂
Balaa la mitoto isiyopenda shule
SINA MBAVU NA HIKI KISA;
BALAA LA MITOTO ISIYOPENDA SHULE!
Baada ya mwiz kuvamia nyumba moja usiku na kuiba vitu vngi wakati anajiandaa kuondoka ghafla akadakwa mguu na dogo
DOGO: Usipoondoka na begi langu la shule NAPIGA KELELE….😂😂😂
Baada ya mwanamke kukataa kufungua mlango angalia kilichomkuta
MUME: Fungua mlango!
MKE: Leo sifungui! Nimechoshwa na ulevi wako.
MUME: kama hufungui najitupa kwenye hili shimo nife kabisa.
MKE. Kufa huna faida yoyote duniani!
MUME kachukua jiwe kubwa kalitupa kwenye shimo chubwiiiiiii!
MKE kajifunga kanga, kafungua mlango. Ghafla mume kaingia ndani na kumfungia mke nje.
MKE: Nifungulie la sivyo nitapiga kelele majirani waje.
MUME: Piga kelele na wakija uwambie unakotoka usiku huu na khanga moja.














































































I’m so happy you’re here! 🥳
Recent Comments