Vichekesho Vya Tanzania

Huyu jamaa bonge la bwege, ungekua wewe ndiyo rafiki ake ungemwambiaje?

RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?

JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, “Huyo nguruwe umeshamuondoa?’ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja

Usichokijua kuhusu sungura, panya na jamii yao

JE WAJUA?

Sungura, panya na Jamii zao huwa na mwendo wa kukimbia na kuruka muda wote na umri wao wa kuishi ni miaka 15. Kobe ni mnyama mwenda pole, asiye na papara wala pilika, muda mwingi hujificha na kupumzika ndani ya jumba lake akikwepa maadui. Umri wa kuishi kobe hufikia hadi miaka 300.
FUNZO: Mazoezi ni kiinimacho na uongo mtupu. Jipumzikie mwaya!!!
🏃🏾🏃🏿‍

Alichokifanya jamaa baada ya kuokota wallet yenye pesa za kumwaga

Jamaa aliokota wallet, alipofika nyumbani akapiga simu kwenye radio station

“Naitwa John nimepiga simu kutangaza kuwa nimeokota wallet ndani ina laki 7, ATM Card na kikaratasi chenye PIN ya ATM Card na kijimkufu cha dhahabu kinene hivi…”

Mtangazaji akasema:- Akhasante sana John, kwa hiyo ungependa kumrudishia mwenyewe kama ana kusikiliza akutafute kwa No. Gani!?

John: Hapana, mi nilikuwa namshukuru tu maana amenitoa kwenye matatizo na ninapenda kumuombea Dedication wimbo wa Snura “MAJANGA” umfikie popote pale alipo…!!!

Ndege ya Tanzania

Kuna maprofesa 40 walipanda AIR TANZANIA ili wasafari. Kabla ndege haijaanza kuondoka, Lilipita tangazo kama ifuatavyo:

Ndugu wasafiri wote, ndege unayotarajia kusafiri nayo imetengenezwa na wanafunzi wa Kitanzania.
Baada ya tangazo maprofesa wote waliteremka isipokuwa mmoja alibaki kwenye kiti chake
Walipomuuliza ni kwanini hakuondoka akajibu kwa haraka na furaha kuwa:
Kama ndege hii imetengenezwa na watanzania, hata kuwaka haitawaka!

Jamaa mpenda michepuko kapatikana

…Upo kazini umeacha familia yako nyumbani mara ghafla unapigiwa simu kutazama unakutana na no ngeni na kuamua kuipokea ndipo unakutana na Sauti ya msichana ya kuvutia lakin kabla hajasema shida yake anaamua kukata simu. Unashikwa na hamu ya kujua ni nani. Tamaa ya mchepuko inakujia ghafla na kuamua kuipiga ile no tena kwa mara nyingine inakuwa haipatikani.

Siku hiyo hiyo usiku ukiwa umelala chumba kimoja na mkeo meseji inaingia tena kwenye cm yako kwa ile namba iliyokupigia mchana ikikuomba umpigie kwa mida ule na kusisitiza kuwa ana hamu ya kukufahamu. kila ukimtumia meseji ya kumdanganya upo sehemu mbaya hasikii anakubipu mara nyingi. Uzalendo unakushinda, unamuangalia pembeni mkeo kalala fofofo kajifunika shuka hadi usoni. Unaamua kuondoka kwa kunyata mpaka sebuleni kwenda kuipiga Ile namba kwa lengo la Kumwambia kesho mkutane. Ile unafika sebuleni na kuanza kuipiga ile cm ndipo unakutana na sauti hii:- MUME WANGU ACHA MCHEPUKO, NILIKUWA NAKUPIMA TU RUDI TU CHUMBANI TULALE 😋😋😋😋😋😋😋😋 Hapo ndo utajua kwann bata hata ale kokoto anaharisha 😂😂😂😂😂😂😂😂

Cheki hawa washikaji wanachokifanya baada ya kuvuta bangi, Bangi si mchezo

Kuna washikaji walikuwa wakivuta bangi… kiberiti kikawaishia… wakamtuma mwenzao akatafute kingine… bangi lilikuwa limemkolea… akazungukazunguka hatimaye akarudi palepale kijiweni…

MSHIKAJI: oyaaa wanangu eeeh… niazimeni kiberiti mwanangu mwenyewe …..

WENZAKE: baharia ee subiria kimtindo kuna mwana tumemtuma akatafute kiberiti.

Unakumbuka hizi Sheria zetu za mpira utotoni?

1.Mwenye mpira Lazima acheze ata kama hajui mpira
2.Dogo mnene Lazima awe golikipa
3.Mwenye mpira ataamua nan acheze na nan asicheze

4.kama haujashiriki kufuma mpira unaweza ucpate namba
5.Ukichaguliwa mwishon ujue uwezo wako ni mdogo kuliko wote
6.Mwenye mpira akikaclika mpira umeisha
7.Inaruhusiwa kubadili golikipa kama ikitokea penat na baada ya apo ataendelea kudaka yule yule
8.Mechi itaisha pale giza linapoingia
9.wale ambao wamekosa namba kazi yao ni kufata mpira ukitoka
10.yule mtaalam wa soka {KM MIMI } huwa hakoc namba ata cku moja!
Ukiikumbuka lazima utabasam!

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About