Kulikuwa na semina ya wanawake kuhusu namna ya kuishi kwa upendo katika ndoa.
Mwalimu aliwauliza ni wangapi wanawapenda waume zao? Wote wakanyoosha mikono kama ishara ya kuwa wanawapenda waume zao.
Mwalimu akauliza tena, āNi lini mara ya mwisho umemwambia mumeo āNakupenda Mpenziā?
Majibu yalikuwa kama ifuatavyo:
Wengine wakisema Asubuhi ya leo,
Wengine jana,
Wengine wiki iliyopita
Wengine mwezi uliopita
Na wengine wakasema hawakumbuki!
Mwalimu aliwapa kazi kila mwanasemina achukue simu yake na kumtumia mume wake meseji yenye neno āNAKUPENDA MPENZIā
Baada ya meseji kwenda aliwaamuru kubadilishana simu kila mtu na jirani yake.
Kila mwanasemina aliambiwa kusoma meseji za majibu kwenye simu aliyoshika
Simu ya 1 ā āSamahani, nani mwenzanguā!
Simu ya 2 ā āSamahani, wrong numberā!
Simu ya 3 ā āSi nimekuambia usinitumie messages kwenye namba hiiā!
Simu ya 4 ā āMh! leo mvua itanyeshaā!
Simu ya 5 ā āNikija tutaongea zaidiā!
Simu ya 6 ā āā¦ā¦Imedhibitishwa umepokea Tsh300,000 kutoka kwa ā¦ā¦ā!
Simu ya 7 ā āMe tooā!
Simu ya 6 ā āHuu ujumbe ndio ulikuwa unamtumia huyo hawara yako ee, leo utanikomaā!
Recent Comments