Ujasiriamali: Kujitambua na Kuwa na Mafanikio Katika Maisha

Jipe moyo kamwe usikate tamaa

Nilikuwa naangalia mpira wa miguu katika uwanja wa
shule.
Nilipokaa, Nilimuuliza kijana mmoja juu ya Matokeo ya mchezo.

Kwa tabasamu, alijibu “Wako mbele yetu 3-0”!
Nikasema, Kweli!
Mbona huonekani kukata tamaa..?

“Kukata tamaa?
“Yule mvulana aliuliza kwa mshangao….”!?

Kwanini nikate tamaa wakati bado refa hajapuliza kipenga cha mwisho?

Nina imani na timu yangu na meneja wa timu; Nina hakika tutashinda!

Na kweli, mchezo uliisha 5-4 timu ya kijana ikiwa mbele!

Alinipungia mkono taratibu, na tabasamu zuri akiondoka uwanjani; nilishangaa, mdomo wazi, ujasiri mkuu kiasi hiki; such beautiful faith;

Nilipofika nyumbani usiku ule, swali lake lilizidi kuja kwangu zaidi:
“Kwanini niogope wakati refa hajapuliza kipenga cha mwisho?”

Maisha ni kama mchezo.
Kwanini ukate tamaa wakati mwenyezi Mungu ndiye meneja wako?

Kwanini ukate tamaa wakati kungalipo uhai ndani yako?

Kwanini ukate tamaa wakati kipenga chako cha mwisho bado hakijapigwa?

Ukweli ni kwamba watu wengi hujipulizia wenyewe vipenga vyao vya mwisho.

Lakini maadamu ungalipo uhai, hakuna kisichowezekana muda haujakuacha.

Nusu kipindi si kipindi kizima na ratiba ya Mungu kwa mwanadamu si ratiba ya mwanadamu kwa Mungu.

Usijipulizie kipenga chako cha mwisho we mwenyewe.

JIPE MOYO USIKATE TAMAA!

KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA.

KAMWE USIKATE TAMAA.

Una thamani gani?

Kazi au shughuli unayoifanya ina thamani gani kwa wengine?unawasaidia au unawaumiza??
Biashara unayoifanya ina thamani gani kwa wengine?ni lazima uwaumize ndipo ufaidike au uwasaidie ili nawe upate faida?

Elimu yako uliyo nayo ina faida au thamani gani kwako na kwa wengine?unawadharau na kujiona wewe ndiye msomi pekee au unawasaidia?

Una thamani gani kwa ndugu,jamaa,marafiki na majirani zako?unasaidiana nao katika kila kitu au unajiona wewe ndiye matawi ya juu unyenyekewe?

Una faida au thamani gani kwa wasiojiweza??umewahi kuwasaidia chochote?kuwatembelea watu wenye Shida mbalimbali kama wagonjwa,wafungwa nk

Kila unachokifanya kina thamani yoyote kwa wanaokuzunguka??
Kumbuka mafanikio ni kugusa maisha ya watu wengi kwa kuwasaidia wao kwanza wafanikiwe ndipo Baraka za mafanikio zitamwagika kwako.
Mafanikio sio wengine waumie ndipo uyaone mafanikio.

Jifunze kuwasaidia wengine waweze kutimiza malengo na ndoto zao ndipo nawe Mungu atakubariki kufikia ndoto zako.

Kumbuka kuna watu wengi wapo nyuma yako wanakusubiri wewe ubadilike ndipo nao waweze kuungana na wewe muweze kufanya kitu cha maana na chenye thamani kwa wengine.

Hichi ndicho unatakiwa uwe nacho kulingana na umri wako

20 – 25 =Iwe kama ni kielimu hujafikia malengo yako,sitisha mara moja tafuta kazi/biashara ya kufanya,pigana kufa na kupona ili kama vipi urudi shule kwa pesa yako.

25 – 30 = Hakikisha uwe na angalau na SHUGHULI RASMI kama umeajiliwa au umejiajili.

30 – 35 = Uwe na angalau kama sio nyumba basi kiwanja,tena ujitahidi uwe umeoa/umeolewa kama sio kuishi nae,tena si mbaya ukawa umeshatengeneza familia,kwa maana ya kuwa na watoto kama mungu kakuwezesha.

35 – 40 = Ni umri wa kama kiwanja kiwe kimejengwa, na kama ni tayari basi nenda step nyingine ya kumiliki kama ni Gari au kuongeza nyumba na hakikisha vinaenda sambamba na ongezeko la familia.

40 – 45 = Ni umri wa masahihisho, kama hukuwahi kununua kiwanja au kujenga basi hapa pambana afe kipa afe beki,kama umegundua mkeo hazai fanya mchakato kwingine kama ni mwanaume na kama mwanamke umegundua mumeo ndio mwenye shida basi tafuta nje umletee mtoto. Kifupi ni umri wa masahihisho.Ila kwa wale ambao wameenda vizuri huko nyuma basi hapa kama ni wale watoto wapo kwenye level tofauti za elimu,kwahiyo ni muda wa kuwawekea malengo ya kimasomo watoto wao.

45 -50 = Kwa yule ambaye hakukosea huko nyuma,basi umri huu ni wa kuanza kuwatengenezea mazingira watoto wako,kama ni shuguli zako ni kuanza kuwahusisha,huku wewe ukijiweka pembeni taratibu na kuangalia fulsa za umri wako. Lakini kwa wale waliokosea hapa ni kupitia zile hatua za 35 -40.

50 – 60 = Ni kujiandaa na maisha mapya ya kustaafu au kujiweka mbali na shughuli za shulba.Na kama ulijitenga na msikiti/kanisa huu ndio muda wako.

60 – 70 = kula matunda yako huku ukiangalia misingi ya wanao inaendaje.

70 – 80 = kula matunda.

80 – n.k= unamsikilizia Mungu anasemaje

Ni vizuri kujua haya

πŸ‘‰πŸΏDegree au vyeti ulivyo navyo haviwezi kukupa mafanikio.
πŸ‘‰πŸΏUzuri ulio nao hauwezi kukupeleka kwenye ndoto zako.
πŸ‘‰πŸΏUsipobadilisha hao marafiki ulio nao hutofika mahali popote.

πŸ‘‰πŸΏUsipobadilisha vitendo unavyovifanya kila siku hivyo hivyo mafanikio utayasikia kwa wengine.

πŸ‘‰πŸΏKazi au ajira unayoifanya usipojiongeza haiwezi kukupeleka kwenye maisha unayoyataka.

πŸ‘‰πŸΏHuo mshahara unaolipwa usipoutumia vizuri na kujiwekea akiba au kuwekeza kidogokidogo hutoacha kulalamika kila siku mshahara mdogo au hautoshi.

πŸ‘‰πŸΏUsipoacha kukopa bila malengo mafanikio ni ngumu kuyapata.

πŸ‘‰πŸΏUsipowekeza muda kwa ajili ya kujifunza na kuelewa mambo mengi ya biashara na ujasiriamali kwa ujumla na kufahamu dunia imetoka wapi,iko wapi na inaelekea wapi huytoacha kulalamika.

πŸ‘‰πŸΏUsipolipia gharama za kujifunza na ukajifunza kweli kile unachoelekezwa ikiwa ni pamoja na Pesa na muda haya mambo waachie wengine.

πŸ‘‰πŸΏUsipobadili fikra na mtazamo wako huwezi kubadilisha chochote katika maisha yako.

πŸ‘‰πŸΏUkiacha kusikiliza kila aina ya ushauri unaopewa na ndugu zako,jamaa zako,marafiki zako,familia yako,majirani zako na kujisikiliza wewe mwenyewe utahangaika sana.

πŸ‘‰πŸΏUsipofanya bidii na juhudi na ukakubaliana na changamoto zozote utakazokutana nazo maisha yatakuwa magumu sana kwako.

Kumbuka mtu pekee Wa kuyabadilisha maisha yako na kukusaidia kufikia malengo na ndoto zako wala sio mwingine ni mmoja tu nae ni WEWE.
Badilisha fikra zako,badilisha mtizamo wako,badilisha maisha yako.

Ujumbe wa leo kwa mtu anayetaka kufanikiwa katika maisha kiuchumi

Kila mtu aliyefanikiwa ukifuatilia historia yake pengine unaweza kukata tamaa kabisa Na kusema mimi hii njia siiwez.

Lakin siri ya mafanikio ni uvumilivu Na kujituma ktk kazi uifanyao.

Ni kweli vijana wengi humaliza vyuo Na kusubiri ajira wanashindwa kusoma alama za nyakati, hawatambui kuwa sasa wasomi ni wengi sana ajira chache.

Mimi pia ni mwanafunzi wa Chuo kikuuu lakini ni mjasiri amali vilevile.

Vijana wenzangu tubadilike fursa zipo tuache kuchagua kazi eti kisa unashule kichwani!

Tumia vyeti vinapo hitajika pia viweke pemben unapohitaji kutumia nguvu.

Jaman mungu ni wawote hana upendeleo utatoka tu!!! Tusijitenge eti kwasababu tumeingia darasan uonekane wakipekeee ila tujichanganye Na watu tuliowaacha mtaani tutaongeza maarifa Na watatuonesha fursa tusizozijua.

Shule ni nzuri sana ila pia ni mbaya hasa ya Tanzania maana haitufundishi kujitegemea bali inatufanya tuwe tegemezi cku zote

Chamsingi vijana wenzangu tuamini maarifa tuliyonayo kuwa ndo muhimu kuliko vyeti tulivyo navyo

“Tafuta maarifa ustafute shule tafuta pesa ustafute vyeti”

Kuna watu wameajiriwa lakn hadi Leo wanaishi nyumba za kupanga

Mwisho wa yote niambie uliwahi kuona wapi tajiri aliyeajiriwa? Wote wanamaisha ya kawaida tu.

Angalist ya matajiri Tanzania Na duniani kote hamna aliye ajiriwa hata mmoja.

Yatie akilini hayo jali mafanikio katika maisha yako

Mizigo tuliyoibeba ambayo haina faida

1.πŸ’₯Umejipa jukumu la kuwa “mpelelezi” wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

2.πŸ’₯Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.

3.πŸ’₯ Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!

4.πŸ’₯Umeweka mbele zaidi “watu watanichukuliaje” kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.

5.πŸ’₯Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna. Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.
6.πŸ’₯Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii. Huna siri hata moja! Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema “umefulia”

7.πŸ’₯Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.

8.πŸ’₯Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia “hapa umekosea” kwa sababu ya ujuaji wako.

9.πŸ’₯Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni “Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe” Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi “life skills” wala ujuzi mwingine.

10.πŸ’₯Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.

ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele!

AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA

AMINI UNA AKILI YENYE UWEZO MKUBWA WA KUBUNI WAZO LA KUWEZA KUKUSAIDIA KUFANIKIWA KIMAISHA.

Huwa nikikaa na kufikiri ni namna gani binadamu aliweza kubuni ndege, meli kubwa hasa za mizigo, gari na vitu vinginevyo na badae kuja kuwa msaada mkubwa katika dunia yetu ya siku leo hata kurahisisha maisha katika eneo fulani lililokuwa na ugumu kwetu, basi nauona uwezo wa Mungu aliouweka ndani ya binadamu huyu ingawa yeye binafsi kama binadamu wakati mwingine hatulitambui hilo na kama tunalitambua basi ni wachache na wakati mwingine hatujakaa vizuri kuitumia hii fursa ya uwezo huo tuliopewa. Hii inaonyesha ni jinsi gani binadamu alivyo na uwezo mkubwa wa kufanya ubunifu kwa kupitia akili aliyonayo na kuleta mageuzi na mshangao mkubwa katika ulimwengu tunaoishi.

Hebu tazama wengi wa wabunifu waliojitoa kwa kuumiza akili na kubuni vitu vipya katika ulimwengu huu tunaoishi leo hii, ndio tunaowaona matajiri katika dunia hii ya leo kuliko watu wengine waliokataa kutumia uwezo na akili zao walizopewa na Mwenyezi Mungu na zaidi sana kubakia kulalamikia watu wengine wanaofanikiwa. Nataka nikuambie unauwezo mkubwa sana ndani yako unaoweza kuutumia ili kubuni jambo kubwa litakaloleta matokeo chanya na kuwa msaada mkubwa katika jamii yako unayoishi na kwako pia.

Ndio. Una uwezo mkubwa sana tena sana unaoweza kuleta matokeo chanya na makubwa katika ulimwengu wako na ukasahau hata habari ya kuajiriwa na kuanza kujiajiri binafsi kupitia jambo ulilobuni. Tatizo ni kwamba hupendi kutumia akili yako kufikiri kwa upana na kwa kiwango cha juu kwa hofu ya kupoteza muda, kuumiza akili, kutokutaka matatizo (stress), nakadhalika. Kila siku umekuwa ni mtu wa kusema β€œmimi sitaki kuumiza akili yangu” mara unasema β€œmimi masuala yanayochosha akili yangu siyataki” unataka kufanya mambo marahisi marahisi ili utoke kimaisha, ni gumu sana kwa namna hiyo rafiki.

β€œIf you do what is easy your life will be hard, but if you do what is hard your life will be easy.” – Les Brown

Nataka nikuambie akili yako inauwezo mkubwa sana, narudia β€œinauwezo mkubwa sana” tena sana wa kubuni biashara ya kukutoa kimaisha, kutatua matatizo yaliyo magumu kwa jamii iliyokuzunguka, kuleta mbinu na mikakati mipya kwenye kazi au ofisini ili kusaidia kampuni kusimama, nakadhalika. Tatizo unajitetea na kujenga hofu kubwa ndani yako ya kujitoa na kufikiri ili kuhakikisha unaleta matokeo mapya na makubwa mahali ulipo muda huu. Hebu fikiri kama binadamu huyu huyu unayemjua na aliye kama wewe alibuni balbu za umeme anaitwa Thomas Edison kutoka nchini Marekani; na zaidi sana binadamu huyu huyu kama wewe aliweza kugeuza historia ya muonekano wa magari na kuja na kitu kipya zaidi anaitwa Henry Ford, na binadamu huyu huyu aliweza kubuni biashara ya kuuza kuku walioandaliwa kama chakula na hatimaye kuwa na mgahawa mkubwa wa KFC uliosambaa karibu nchi 123 duniani kote anaitwa Harland Sanders. Na wengine wengi sana ambao sitaweza kuwamaliza kwa kuwataja wote mahali hapa siku ya leo.

Naamini wapo watu wanaoweza kujitetea na kusema kwa kuwa hao ni watu weupe yaani wazungu na sijaona mtu mweusi hata mmoja hapo. Hebu fikiri ni watu wangapi wanabiashara ambayo leo hii inawaingizia mabilioni ya pesa na wakati mwingine biashara wanazozifanya ni za kawaida na zilizokuwa zikidharaulika na watu kwenye jamii zao na wapo hapa afrika. Angalia mtu kama Aliko Dangote kwa sasa zaidi ya kujishughulisha na uzalishaji wa cement na bidhaa nyingine za ujenzi na hata biashara zake kubwa nyingine kwa sasa ameenza kuzalisha nyanya na kuuza kwenye nchi yake huko nchini Nigeria. Ulitegemea mtu kama huyu ambaye ni tajiri wa kwanza afrika kuwaza kufanya biashara kama hiyo ya nyaya kwa sasa? Yawezekana wewe ulipoambiwa kuuza nyanya uliona ni biashara kichaa na haina maana ya kuifanya. Ukweli ni kuwa usipende kuanzia pakubwa bali anza na madogo ili kukupeleka kwenye kilele chako cha mafanikio na kutimiliza ndoto yako uliyonayo.

Hivyo hivyo kwa Bakhresa, Mengi, Dewji, Sheria Ngowi na wengine wengi tunaowaona nchini mwetu Tanzania wamefanikiwa kiuchumi, hii yote ni kutokana na kuamua kubuni kitu kipya kilichoweza kuwa msaada mkubwa kwenye jamii yao na kuweza kuwaletea wao mafanikio makubwa katika maisha yao. Sheria Ngowi pamoja na kusomea masuala ya Sheria nchini India lakini alijua bado ana kitu cha ziada ndani yake kinachoweza kumlipa na kumfanya awe na uhuru wa kifedha na maisha mazuri sawa na anavyotaka. Leo hii ni mbunifu wa mavazi Africa nzima inamjua na kumtazama. Jiulize kama asingetumia akili yake kwa kufikiri zaidi na kufuata ndoto yake aliyokuwanayo leo hii ingekuwaje kwake na kwenye jamii yake iliyohitaji mchango wake?

Nataka nikuambie huwezi kutoka kwa siku moja ni lazima uumize kichwa na akili yako leo hii na kujua ni nini cha kufanya kinachoweza kukupa uhuru unaoutaka kesho. Na suala la kuumiza kichwa chako na akili ni sasa na si kesho, narudia tena suala la kuumiza akili yako kwa ajili ya kubuni wazo la kukutoa kimaisha β€œni sasa na si kesho” kama unavyofikiri. Usiridhike na maisha yako unayoishi leo, usiridhike na kipato unachokipata huku sema ukweli ndani ya moyo wako na kwa uhalisia hakikutoshelezi kabisa kufikia kwenye kilele cha mafanikio makubwa unayoyataka. Usikubali kuwa mvivu wa kuumiza kichwa na kutumia akili yako kwa ajili ya kuja na kitu kipya kinachoweza kuleta manufaa kwako na kwa jamii yako iliyokuzunguka, anza kuwa mbunifu ili uweze kufikia ndoto yako ya maisha.

Umiza kichwa kuanzia sasa na amini katika wazo (idea) utakayoipata ndani ya moyo na akili yako ili kukusaidia na wewe kuwa miongoni mwa watatuzi wa matatizo katika ulimwengu huu. Unaweza kutumia matatizo yaliyopo kwenye jamii yako kama sehemu ya kukupatia wazo jipya na baada ya hapo kubuni njia na mkakati wa kulitatua tatizo ili kuleta matokeo chanya katikati ya watu waliokuzunguka na kwako pia. Mwombe Mungu akupe mwongozo wa kukusaidia kulitimiza na kulifanya hilo wazo (idea) kuwa wazi katika ulimwengu wa nje ili usibaki na wazo lililo kwenye akili na kichwa tu pasipo kuleta matokeo na mchango wowote makubwa kwa watu wako.

Nakusihi usisubiri kesho. Usione una siku nyingi za kuwaza au kuleta matokeo (ku_implement) ya hilo wazo lako (idea) uliyonayo au ndoto ya siku nyingi unayotembea nayo kila kukicha pasipo kuweka vitendo vya kuifanya izae faida na matunda kwako. Anza leo kuhidhilishia dunia kuwa nawe unauwezo mkubwa aliouweka Mungu ndani yako. Usijikatae wala usiogope kukataliwa na wengine pale utakapofanya uamuzi wa kuja na kitu chako kipya kwenye jamii yako, kumbuka kukataliwa ni sehemu ya kukupeleka katika mafanikio. Kadri unavyoongeza kukataliwa ndio unavyoongeza kufanikiwa.

Kama unahitaji kuwa mbunifu wa mavazi kama sheria ngowi anza kubuni leo hii au ikibidi mtafute na uwe chini yake na afanyike kuwa msaada na mshauri wako (mentor) wa hicho kitu unachotaka kukifanya. Amini inawezekana kwani watu waliofanikiwa si wachoyo unapojishusha na kuonesha uhitaji wa kujifunza kutoka kwao. Kama unataka kuwa mfanyabiashara mkubwa kama Dangote lakini bado huna wazo la biashara. Basi elewa una uwezo mkubwa wa kuumiza kichwa na akili kuanzia sasa na ukapata wazo linaloweza kuishangaza dunia yote hapo badae.

Lakini kumbuka si lazima ukaja na kitu kipya kabisa kwani tambua unauwezo pia wa β€œkuboresha wazo” au kitu fulani kinachofanyika na watu wengine ila wewe ukaleta ubunifu mpya kwenye hicho kitu na kuleta utofauti mkubwa kwenye eneo (industries) hiyo. Na hii ndio njia inayofanyika kwenye makampuni ya simu, magari, televisheni, nakadhalika. Leo hii samsung akileta simu yenye kamera yenye uwezo wa mega pixel 16 kesho yake utasikia Iphone ametoa simu yake mpya yenye kamera yenye uwezo wa mega pixel 20. Huu ni ubunifu tu ili kuzidi kutawala soko na kuteka wateja wa soko la simu ulimwenguni kote. Nataka nikuambie nawe unauwezo wa kufanya ubunifu mkubwa kwenye jambo lolote lile ili kukuletea mafanikio makubwa na hatimaye ukafanikiwa kufikia katika ndoto yako.

Nataka nikuambie una mawazo milioni na zaidi ndani yako ambayo hadi sasa dunia inayasubiri ili yaweze kuwa msaada kwa watu wengi na kufanyika kuwa faraja kubwa hata kwa watu waliokata tamaa. Ndio. usishangae wala sijakosea kusema ni mawazo β€œmilioni na zaidi” uliyonayo ndani yako. Ni wewe tu umejidharau, ni wewe unajiona huwezi kuwaza na kutoka na kitu kipya au kilichojaa ubunifu, ni wewe tu unajaa hofu ya kukataliwa kisa unaona utaonekana unaiga, huigi kwani hata waandishi wanaoandika kama mimi wanaandika kutokana na walichokipitia kwenye maisha na kujifunza kwa wengine, ni wewe tu unajiona huna lolote na si chochote katika ulimwengu huu hivyo huwezi kufanya mambo makubwa. Unajikosea heshima kwa kujiwiza mawazo hayo ya chini na kumkosea Mwenyezi Mungu yeye aliyekuumba na kukupa akili zote timamu ili uzitumie kwa ajili ya kuwaza na kubuni mambo mapya yanayoweza kuwa msaada mkubwa kwako na kwa jamii yako iliyokuzunguka. Anza kuwaza na kuumiza akili na kichwa chako leo hii, na amini kesho utafanikiwa.

JIAMINI NA AMINI UNAWEZA. ISHI NDOTO YAKO.

Mbinu 5 za kukunufaisha maishani

Mbinu 5 za kukufanikisha maishani Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu fulani kufanikiwa. Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha yako. Mbinu hizi ndizo wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani. Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi?

Hizo Ndizo Mbinu 5 Za Kukupa Maisha Ya Mafanikio:-
1. Kuwa na nidhamu binafsi.

Ili kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji sio suala la kufanya kazi kwa bidii tu, zaidi unachohitaji nikuwa na nidhamu binafsi ambayo itakuongoza kwenye malengo yako. Watu wengi hawana nidhamu binafsi kitu ambacho kinapelekea wengi ndoto zao zinaishia kati. Ni muhimu kuelewa kuwa ni lazima kufanya mambo yale yanayoendana na ndoto zako, hata kama kuna wakati unajihisi umechoka unalazimika kujikaza kufanya jambo hata dogo ambalo litakufikisha kwenye malengo yako. Ukishindwa kuwa na nidhamu binasi katk maisha yako elewa kuwa utashindwa kufikia mipango na malengo iliyo jiwekea.

2. Jifunze kila mara kwa watu waliofanikiwa.

Hii itakusaidia kujua vitu vingi usivovijua kuliko kukaa na kung’anga’nia mbinu zilezile ambazo hazikusaidii. Yapo mambo mengi sana usiyoyajua ambayo yanakufanya ushindwe kufanikiwa. Ikiwa utakuwa na uwezo wa kujifunza kwa wale waliofnikiwa utakuwa upo kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa na kusonga mbele. Maisha yako yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kutokana na kukosa kujifunza kwa wengine kwa kujua hilo badili mwelekeo wako na kuwa mtu wa kujifinza mwisho wa siku mafanikio yatakuwa makubwa kwako.

3. Jifunze kutokana na makosa uliyofanya.

Inawezekana kuna mahali utakuwa umekosea kwa namna moja au nyingine,badala ya kulaumu na kuumia moyo sana jifunze kutokana na hayo makosa liyoafanya ili isije ikawa kwako rahisi kufanya makosa yaleyale kwa mara nyingine. Ikiwa utajifunza kutokana na makosa na kufanyia kazi kile ulichojifunza hapo utakuwa umechukua hatua moja muhimu ya kuweza kukusaidia kusonga mbele kuyafata mafanikio unayoyataka. Unataka mabadiliko makubwa katika maisha jifunze kutokana na makosa yako na acha sana kulaumu.

4. Jenga tabia ya kujisomea kila siku.

Hili ni jambo ambalo nimekuwa nikiliongelea sana kuhusu huu umuhimu wa kujisomea. Unapojisomea unapata vitu vingi sana tena ndani ya muda mfupi. Kupitia huko utaweza kujifunza mambo mazuri yatakayoweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na kuwa mtu, tofauti kabisa. Acha uvivu jifunze vitu vipya kila siku. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu, ama mitandao mizuri inayoelimisha kama huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kupata maarifa bora na sahihi kabisa. Unapojifunza inakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi, ambapo kwako ingekuwa ngumu kuzikabili.

5. Kuwa na mahusiano sahihi na watu waliofanikiwa.

Katika kutafuta mafanikio ni vizuri ukawa na mahusiano ama mtandao na watu sahihi ambao watakusaidia kukufikisha kwenye lengo ulilojiwekea. Haina haja kuwa na watu ambao hawakusaidii kutimiza malengo yako. Watu hawa watakukwamisha na kukurudisha nyuma katika maisha yako tu siku zote. Jenga tabia ya kuwa na watu sahihi ambao utajifunza kitu kwao, utashirikiana nao na kujifunza mambo mengi huko ya mafanikio na hatimaye utamudu kusonga mbele

Sababu inayopelekea kushindwa kuishi maisha ya ndoto zako

1. Hauko Tayari kuthubutu na kujiunga
2. Kutokujiamini
3. Kutopata sehemu sahihi ya kupata ushauri
4. Kutokuwa na sababu za msingi au malengo ya msingi ya kupigania ndoto zetu
5. Kukaa katika shauli la wasio haki na barazani pa wenye mizaha

Hizo ni baadhi ya sababu zinazopelekea watu wengi kushindwa kuishi maisha ya ndoto zao na kuishi maisha ya kawaida tofauti na fikra zao.

Kuthubutu ni jambo la muhimu sanaaa katika maisha ya mwanadamu kwa maendeleo ya kwake ,familia ,jamii pamoja na taifa kwa ujumla hivyo ndugu zangu nawasihi tuweze kua watu wanaothubutu.

Tuondoe uwoga katika maisha yetu Kwamaana Uwoga Ndio CHANZO CHA UMASKINI WETU tukiendeleea kuogopa mazingira yanayotuzunguka na jinsi gani watu watatuchukulia na kutusema atutaweza kupiga hatua.

Changamoto ni hali ya kawaida katika maisha ya mwanadamu , kuogopa changamoto nalo ni Kosa kubwa katika maisha yetu.

…………..Mwisho kabisa nipende kusema……………

USIJILINGANISHE NA MTU MWINGINE MAANA JUA NA MWEZI HAVIFANANI VYOTE UNG’ARA KWA WAKATI WAKE. TENGENEZA MAISHA YAKO ILI WATU PIA WATAMANI KUWA KAMA WEWE.

Siri za mafanikio na Jinsi ya kufanikiwa

Tafuta fursa kila kona.
Tumia kipaji chako.
Kuwa na nidhamu katika fedha – matumizi mazuri ya pesa, nidhamu kwa watu wanaokuzunguka, usijikweze, usibague jamii, heshimu wote waliokaribu yako nk.

Kuwa na nidhamu katika afya yako: Afya ndio mtaji sahihi katika biashara yoyoteΒ – kuwa na mazoea ya kuangalia afya yako mara kwa mara nk.

Usipoteze mudaΒ – jali muda kuliko kitu chochote kwani muda ndio kila kitu, muda ni mali.
Shiriki kwenye makongamano au semina mbalimbali za ujasiriamali.
Kuwa na vyanzo vingi vya kukuletea kipato.

Tafuta maarifa kwa mamilionea mbalimbali dunianiΒ – soma historia za mamilionea jinsi walivyofanikiwa.

Jenga urafiki na taasisi za kifedhaΒ – mamilionea wengi hukopa fedha kutoka katika taasisi za kifedha – tembelea taasisi za fedha watakupa ushauri mbalimbali na watakupa mkopo, usisikilize maneno ya watu kuwa taasisi za pesa ni za watu matajiri hiyo sio kweli.

Kuwa na shauku, kuwa na fikra za kuwa milionea na wewe utakuwa.USIWAZIE KUSHINDWA

Kuwa na imani kwamba utakuwa milionea na itakuwa hivyo. KWA KUFANYA. SIO IMAN TU.

Wekeza ktk miradi au biashara mbalimbali. USIOGOPE KUTHUBUTU

Wekeza sehemu yenye mahitaji ya bidhaa inayotakiwa kuzalishwa – angalia fursa hapo ulipo na wekeza. SIO KUFUJA PESA

Kuwa na bajeti katika mapato na matumizi yako. NIDHAMU MUHIMU KATIKA PESA

Kuwa na wazo (Business idea):Β mamilionea wengi hutumia mawazo kutoka kwa watu mbalimbali kutengeneza pesa. Wazo ndio cheti cha kuwa milionea anza sasa fanyia kazi wazo lako ili kukuletea fedha.

Fanya vitu wewe mwenyewe – acha kufanya vitu kama fulani, usiige mtu, buni vya kwako, mamilionea huwa hawaigi, ukiwa mkweli kwako utakuwa mkweli kwa watu

Kuwa na malengo – kumbuka hakuna maendeleo pasipo na malengo, fahamu hilo.,, PLANS AND SELF COMMITMENT

Kuwa na moyo wa ujasiri – usiogope kushindwa jitahidi ktk kupambana na maisha usikubali kubezwa au kuvunjwa moyo. Ukianguka nyanyuka tena, usifikirie kutakuwa na mtu wa kukusaidia zaidi ya kujisaidia mwenyewe.UKIANGUKA USIOGOPE KUINUKA

Kuwa karibu na matajiri -usiogope kwani hao ni binadamu kama wewe, jaribu kuwadadisi ili wakupe mbinu mbali za kuwa tajiri hadi milionea. Ukiwa karibu nao unaweza ukapata nafasi ya kazi au kukuunganishia biashara ukaanza kufanya na kufanikiwa.

Mtangulize Mungu -mwabudu, msifu, mtolee sadaka, saidia masikini, wajane, wagonjwa, jenga nyumba za ibada. Mungu ndio kila kitu mtegemee yeye.

Fanya vitu kitofauti;Β fanya vitu vigeni, muonekano tofauti ingawa biashara ni ile ile, tumia lugha tofauti, panga bei tofauti, nk. Mfano aina tofauti za simenti, chupa za soda na juisi nk.

Acha wogaΒ – jaribu biashara yoyote, woga wako ndio umasikini wako, usiogope kukosolewa unapokosolewa ndio unajifunza. Usiogope mikopo, mamilionea wengi hufanya mambo ambayo wewe unayaogopa.

Kuwa na mtazamo chanya – usikubali mawazo hasi, marafiki zako wawe na mawazo chanya, usikubali kuvunjika moyo na usikubali mawazo yako yaingiliwe na mtu.
Anza kufanyia kazi wazo lako usisubiri mtu.

Kuwa na mipaka katika mambo yako – usifanye mambo kwa mkumbo, usiige, buni mambo yako. Mamilionea wengi wanabuni mambo yao hawapangiwi na mtu

Kuwa mwaminifu -mamilionea wengi ni waaminifu ktk mali za watu. Wengi walikuwa wakipewa mali wakauze ndio walipe pesa, wanadhaminiwa malighafi za viwandani hadi wanamiliki viwanda vyao. Uaminifu ndio njia ya kukufanya uwe milionea.

Pokea ushauri kwa watu hasa kuhusiana na biashara yako – waulize watu kuhusu huduma yako ya biashara wanaionaje na fanyia kazi ushauri wao.
Kuwa na plani katika kazi zako kila siku.

Kuwa na maono ya jinsi unavyotaka maisha yako yawe

Panua soko la bidhaa zako usitegemee soko la sehemu moja

Ubunifu ni muhimu sana – fanya ubunifu ktk kuuza bidhaa zako ili mauzo yasishuke, kuwa mbunifu ktk wateja wako kwani itakusaidia kugundua wateja wako wanataka nini – kuwa karibu nao, wasikilize, waheshimu nk.

Kuwa milionea kunaanzia kichwani mwako-ukiweka mawazo yako kichwani utakuwa milionea kweli utakuwa sio kusema tu mdomoni. Amini utakuwa milionea na utakuwa kweli
PIGA KAZI

Maneno ya walioshindwa yasikukwamishe safari yako ya kuwa milionea

Ondoa neno haiwezekani wewe kuwa milionea – kila binadamu anaweza kuwa milionea

Mshukuru Mungu kwa hicho alichokupa – kumbuka neema ya Mungu ndio imekufikisha hapo ulipo hivyo toa msaada kwa watu wasiojiweza, yatima, masikini, wajane, wagonjwa, toa sadaka, walemavu nk

HITIMISHO;
Shujaa mwenzangu, kuwa milionea inawezekana kama mimi na wewe tukifuata njia hizi 39 zinazotumiwa na mamilionea wengi duniani..

Ila kuthubutu ndo hatua ya kwanza.

Unashangaa kwa nini hufanikiwi?

Sikiliza, hakuna haja ya kuketi chini ili kuelewa ujumbe huu: Ukweli unabaki kwamba wengi wanajihusisha kupita kiasi na yale yasiyo ya msingi katika safari yao ya mafanikio. Kuna msemo wa kiingereza unaosema “mind your own business,” tunapaswa kujiuliza tufanyeje na ushauri huu. Fikiria, unaifuatilia maisha ya Ali Kiba kwa kina kiasi kwamba unajua hata mambo ya faragha kama vile bafuni mwake, unazifahamu ratiba zake za ziara za mwaka mzima, hata zingine unataka kumwekea mipango. Je, ni kweli wewe ni mwanamziki au?

Umeona eee Uko bize kujua simba na yanga mara mbeya city……. Hivi unataka kuwekeza kwenye soka?? Cha ajabu wewe ni mwalimu tena wa Bible knowledge halafu Uko bize na simba mara yanga. Uko kwenye biashara lakini unafatilia Lini bunge litakua live sijui unataka utangaze biashara yako bungeni . Mara Lema ataachiwa Lini, wewe ni mwanasiasa?? See hauko serious kufatilia biashara yako ya vitunguu ina Changamoto zipi, faida, lugha gani utumie kwa wateja au msimu wa soko ni Lini??

Mimi sijawahi kumuona Dewji ana comment kwenye page ya east Africa TV kuchangia Mada zisizohusiana na biashara zake. Unajua matajiri wako bize kufatilia yanayo wafanya kutajirika zaidi wewe Je?? Masikini unafatilia mambo ya kimasikini siyataji unayajua…….

Nimeshindwa kufahamu iwapo utakuwa na mafanikio katika kujua mahali anapoishi Lady Jaydee siku hizi. Wakati huo huo, vitunguu vyako viko nje katika ghalani Iringa, na viko hatarini kuharibiwa na wadudu bila wewe kujua jinsi ya kuchukua hatua ili kupata soko. Muda wako mwingi unaupoteza kwa kutumia vifurushi vya intaneti vya mega mix kutoka Tigo kufuatilia udaku wa Sudy Brown. Inashangaza kuona unajiona kama miongoni mwa waandishi wa umbea wa Shilawadu.

Utaishia kusoma story za mafanikio ya akina Mengi, Dewji, Dangote, shigongo lakini yako itakua tu HISTORIA YA MAREHEMU KWA UFUPI ulisoma darasa la kwanza hadi Saba shule ya msingi mwembengoma……
Historia inafutika hapo hapo….

BADILIKA : huu ni mwaka mpya

**Badilika huu mwaka. Kipenga kimeshapulizwa wenye mbio zao wameshatoka, wewe bado uko kitandani unaandika happy new year kwenye mitandao ya kijamii
Kipenga kimeshapulizwa wewe maliza bajet yote leo kwenye starehe alafu uanze kulalamika eti Mwezi wa kwanza Mgumu utadhani umeubonyeza

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda na kasi ya Magufuli, wewe bado unapiga vibomu alafu unalalamika uchumi mbovu

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaenda porini kutafuta pesa na kuja kuzitumia mjini wanaenzi ule msemo wa Mali utaipata shambani /porini wewe unatafuta pesa kati kati ya mji, my friend utapata nauli tu

Kipenga kimeshapulizwa wanasiasa wenzako wanaleta matokeo chanya kwenye jamii, wewe umekwama na siasa zako za Maigizo, utaisoma namba vizuri

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatengeneza ajira na kulipa mishahara, wewe umeajiriwa mwaka wa 10 unasubiri bonus, increment na kubagain ongezeko la mshahara alafu bado unataka kuwa celebrity, my friend labda celebrity wa mikopo

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta matatizo ili yawe fursa kwao, wewe ukiona changamoto unakimbia na kuilalamikia serikali, utasubiri sana

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanatafuta kazi kwa kufanya kazi za kujitolea kujenga nchi, wewe unasubiri interview, hiyo experience utaipata ndotoni

Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wanahojiwa na forbes magazine wamewezaje kuleta impact Africa nzima, we unakazana kujisifu unafollowers wengi instagram alafu Huna hata mmoja ambae ni rafiki wa kusaidiana.

Kipenga kimeshapulizwa wakati wenzako wakipost kwenye mitandao yao ya kijamii wanalipwa, wewe kazi yako ni kuretweet/kurepost na kulike siku nzima bila kupata faida yoyote

Kipenga kimeshapulizwa wenzako wanaoipenda nchi yao wanachangia matembezi ya tembo na faru yatakayofanyika Morogoro kwa kununua tshirt, wewe bado unazungusha bia na nyama choma alafu unalalamika watalii wamepungua, unataka waje wakuangalie wewe?

BADILIKA my friend.
😹😹😹😹😹

Elimu tuu haitoshi kukunufaisha maishani na kukupa mafanikio

EMBU SOMA HII KWA MAKINI SJUI NI KWELI? USIMAINDI LAKINI MAANA ITAKUGUSA TUU. MAFANIKIO YA MAISHA SIO ELIMU TU, UTHUBUTU, KUJIAMINI NA UJASIRI WA MAAMUZI
✍🏽Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa.

πŸ‘‰πŸΎKatika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa “darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa

πŸ™‡πŸ½πŸ“š Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishi 🏑 na πŸš— πŸš™magari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!)

πŸ‘‰πŸΎWapo πŸ™‡πŸ½πŸ“šwasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana

πŸ‘‰πŸΎLakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga

Hii inachangiwa na mambo mawili:-
πŸ‘‡πŸ½
I. Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli

πŸ‘‰πŸΎHata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio

πŸ‘‰πŸΎKadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa!

πŸ™‡πŸ½πŸ“šWasomi wengi kwa sababu ya “mentality” ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika
πŸ‘‡πŸΎ
II. Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani!

πŸ‘‰πŸΎKatika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha.

βœ‹πŸΎHuwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na “mentality” ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!

οΏ½Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninakwambia: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani

πŸ›£Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti

😎Ukitaka kufanikiwa ungana na waliofanikiwa wakuelekeze

πŸ˜€πŸ™πŸ½ Hii habari haitaki hasira, vumilia tu na jiongeze
….hata mimi sijawa tajiri badoπŸ˜œπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ‘†πŸΏβ€¦ But nakaza mwendo Bila kuangalia vipingamizi au ugumu wa safari…

Jinsi Muda Unavyopotea, Jifunze kitu hapa

Kila mtu ambaye ni hai amepewa muda Wa masaa 24 kila siku,168 kwa wiki,672 kwa mwezi,8064 kwa miezi 12 au kwa mwaka.

Katika hayo masaa 24 unayoyapata kila siku unayatumiaje katika suala zima la kukufikisha katika ndoto na malengo au mafanikio yako?

Kwa nini kuna matajiri na maskini na wote tunapewa masaa 24???
Tucheki mgawanyo Wa masaa 24 ulivyo….katika masaa 24 unayopewa kwa siku masaa 8 ni ya kazi,masaa 8 ni ya kulala na masaa 8 ni ya kufanya mambo yako mengine.

Tuseme katika Masaa 8 kwa ajili ya mambo yako mengine labda masaa manne yanapotea katika foleni au purukushani za maisha kama kula nk.
Je haya mengine manne yanaenda wapi?Tunayapotezea wapi?
Kwenye mpira?kwenye movie?kwenye TV?kwenye mitandao ya kijamii?kukaa na kuwajadili wengine na mashosti?

Hivi unajua kwa siku una wastani Wa kupoteza masaa manne kwenye masaa yako 24??
Kwa wiki unapoteza masaa 28 hali kadhalika masaa 112 kwa mwezi hupotea.
Kwa mwaka mmoja wenye masaa 8760 una wastani Wa kupoteza masaa 1344 ambayo ni sawa na siku 56 kwa mwaka kwa makadirio ya haraka haraka.

Kwa maana nyingine kwa kutumia hii “concept” kila miezi 12 ya mwaka mzima unapoteza miezi miwili kwa mambo ambayo sio “productive”.
Hii ni sawasawa na kupoteza mwaka mmoja ndani ya miaka 6…kwa maana nyingine kwa “the same concept” ya masaa 4 kwa siku kupotea ni kwamba unapoteza mwaka mmoja kwa mambo ambayo hayakusaidii chochote.

Hebu jiulize hapo ulipo una umri gani?umeshapoteza miaka mingapi kwa mambo ambayo sio productive??
Kama wewe ni mfanyakazi au muajiriwa ukifanya kazi kwa muda Wa miaka 40 au kwa muda Wa miaka 40 unapoteza miaka 6.6.

Je hebu jiulize muda wote huo unaoupoteza kwenye mambo ambayo sio “productive” ungekuwa ni muda ulioutumia vizuri kwa mambo ya uzalishaji mfano kuanza kidogo kidogo kujenga biashara yako sasaivi tungekuwa na mamilionea na mabilionea wangapi?
Ili uweze kujenga biashara ambayo ni “strong” inakuhitaji angalau uijenge kwa muda Wa miaka mitano kwa maana nyingine kwa kutumia masaa manne tu kwa siku ndani ya miaka 40 utakuta tayari wewe ni milionea na baada ya kustaafu ajira usingeanza kuangaishana na pensheni (kwanza ni shilingi ngapi) au kuanza kubembeleza kuomba uongezewe mkataba au kwenda kufanya tena part time employment…..kwa concept hiyo ni mamilionea wangapi tumewapoteza??

Ndio maana katika hii dunia yetu tunayoishi matajiri wote ni 3% na 97% ya watu waliobakia wanawafanyia kazi matajiri.
Matajiri waliweza kuiona hii concept kwa jicho la Tatu na wakaanza kuifanyia kazi and the rest is history.
Huwezi kumkuta tajiri anapoteza muda wake kwa mambo ya kizembe yasiyomuingizia chochote ndio maana matajiri wanazidi kuwa matajiri na maskini wanaendelea kuwa maskini.

Lakini bado muda na nafasi unayo sasa ukiamua na ukianza kuutumia muda wako ulio nao kwa ajili ya kuyatengeneza maisha yako.
Watu wengi hawako tayari kuumia na kujifunza biashara na kuielewa ndani ya miaka mitano itakayowapelekea kuwa matajiri na kuweza kuyafikia malengo na ndoto zao lakini wapo tayari kuajiriwa na kufa maskini ndani ya miaka 40.

Muda mzuri ndio sasa Wa kufanya maamuzi sahihi Wa kuyawekeza masaa manne kwenye biashara ili uje upate matokeo chanya.

Shopping Cart
45
    45
    Your Cart
    🏠 Home πŸ“– Reading πŸ–ΌοΈ Gallery πŸ’¬ AI Chat πŸ“˜ About