SMS Nzuri: Meseji za Vichekesho Vya Msimu

Kilichotokea baada ya mzungu na mbongo kukaa siti moja, bongo wasanii wengi

Mzungu akamdharau sana Mbongo nakujiona anajua kila kitu duniani!,
Akamwambia Mbongo waulizane maswali na Mbongo akishindwa anatoa sh.500 na endapo yeye atashindwa atatoa 100,000/=.
Mzungu akauliza ni nchi ipi ilishindwa kwenye vita kuu ya kwanza ya Dunia?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hajui.

Na yeye akamuuliza Mzungu ni kitu gani kikienda juu kina miguu minne na kikirudi chini kina miguu mitatu?

Mzungu akafikiria akakosa jibu akatoa 100,000/= kuashiria hajui ila akataka kujua, akauliza ni nini hicho?
Mbongo akatoa 500 kuashiria hata yeye hajui!.

SHARE na marafiki kama umemkubali Mbongo kwa ujanja. Lakini unafikiri Mbongo huyu kwa akili hizi atakuwa ametokea mkoa gani!?.

Hii ndiyo Ladha ya bia zote usiyoijua

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza ๐Ÿบ huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza kooโ€ฆ Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili ๐Ÿบ๐Ÿบ kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihiโ€ฆ.

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sanaโ€ฆ. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokezaโ€ฆ..

Bia ya nne ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikiaโ€ฆ.. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipuโ€ฆโ€ฆna kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; โ€˜Mi sipendwi mpaka leo sijaolewaโ€™ au โ€˜ Mume wangu sijui yukoje hanijaliโ€™

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ๐Ÿบ na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana. โ€ฆโ€ฆ. โ€ฆKuna watu husema ukilewa ndipo unakuwa mkweli, hivyo basi wakati huu hata bosi wako akitokeza unamueleza ukweli jinsi alivyo fala na hajui kuendesha kampuni.

Au unasema ukweli jinsi unavyompenda mke wa jirani yako ambaye mmekaa mnakunywa naye. Kimsingi uwezekano wa kutapika pia upo karibu na kama umekaa na mchumba wako huu ni muda ambao pia uchumba unaweza kuvunjikaโ€ฆโ€ฆ.

Angalia wadada walivyoumbuka kwenye hii test

Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.

Swali la kwanza,
Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)

WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop. Swali la

2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!

Mjini shule. Soma hii

Kuna mdada nilimkopesha pesa kwa ahadi kuwa baada ya wiki moja atanirejeshea pesa zangu.

Baada ya wiki moja nampigia simu hapokei simu zangu, nimempigia zaidi ya mara kumi (10) bila ya mafanikio!

Kila nikimpigia simu hajibu simu zangu, nikahamua kumwandikia message kwa WhatsAppโ€ฆ!

_Hello Mamu, Nakupigia simu sio kukudai pesa zangu, ila nataka kukwambia kuwa hapa Ubungo Plaza kuna wadada wawili walikuwa wanapigana kumgombea Mumeo (Baba Nang’oto). Ilikuwa vuta nikuvute na mumeo alikuwa kasimama tu anawaangalia akitabasamu. Baada ugomvi kwisha akaondoka na mmoja wao na kumwacha yule mwingine akitukana matusi kama ana akili nzuri._

โ€”
_*Kisha nikaituma ile message*_

Baada ya dakika kama mbili hivi, akanipigia simu nami wala sikupokea simu yakeโ€ฆ Akapiga tena na tena kama mara ishirini hivi wala sikupokea.

*Akatuma message akiniulizaโ€ฆ*

_Hao wanawake unawajuwa, โ€ฆmume wangu na huyo mwanamke wameelekea wapi, wewe unawajuwa hao wanawake waliopigana, yaani hapa nimechanganyikiwa kwa kweliโ€ฆ!_

Nikaisoma message yake wala sikuijibu, nikamchunia kimyaaaโ€ฆ!

Akanipigia tena simu mara tano, sikupokea simu zake, kimyaaaโ€ฆ! Akaniandikia message nyingineโ€ฆ.

*โ€ฆNakupigia jamani pokea simu basi nina pesa zako nataka nikupeโ€ฆ Naomba basi tukutane mjini unihadithie vizuriโ€ฆ!*

Nami nikamjibuโ€ฆ

_Nitumie hizo pesa kwenye Namba yangu ya Mpesa, ili nipitie sheli kujaza mafuta nije mjini kukupitia nikupeleke mahala walipoโ€ฆ!_

Baada ya dakika 2 message ikaingia, kuangalia balance yangu ya Mpesa, nikakuta kaingiza pesa zangu zote ninazo mdaiโ€ฆ!

Nikazima simu nikajilalia zangu kimyaaaโ€ฆ. Kama sio mie!

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.

Shopping Cart
๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About