Januari kweli ngumu, soma hii
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniโฆ๐
Januari kweli kiboko
Hii january sabuni za kuogea ni zile za kuoshea vyombo, yani unakutana mjini na mtu ana mchicha shingoniโฆ๐
Wasiopanda dalaladala wanakosa uhondo wa kauli hizi
1. nitakupa
2. Atapewa mbele
3. Hujapewa mbele?
4. Utapewa nyuma
5. Nitakupa nikikaa vizuri
6. Ngoja isimame nikupe
7. subiri asimamishe nikupe
8. hivi nlivyo kaa ntakupaje?
9. Utapewa tulia
10. Nikupe mara ngapi?
ย
Mchungaji kamfuata pedeshe moja maarufu kwa
kumwaga pesa kwenye kumbi za muziki;
MCHUNGAJI: Kijana, tuko katika harakati za
kujenga kanisa, jitafutie nafasi katika ufalme wa
mbingu kwa kuchangia ujenzi huu. Na Mungu
atakubariki zaidi
PEDESHE: Samahani Mchungaji haitakuwa vizuri
mimi kuchangia kanisa, fedha zangu ni haramu,
huwa nazipata kwa utapeli na kuuza madawa ya
kulevya.
MCHUNGAJI: Yote ni heri, pesa yako tutatumia
kwa kujenga eneo la choo we toa tu!!!
MUME: “Mke wangu nasikia John katembea na wake za watu wooote hapa mtaani kasoro mmoja tu!”
MKE: “Mmmh! basi huyo aliebaki atakuwa MAMA MBILINGE KISIKI, maana yule mama ndo ANAJIFANYAGA MGUMU sanaaa.!!”
Je, huyu mama angekuwa mkeo ungekuwa na swali lingine la kumuuliza?
Boss mmoja aliingia kazini kwake kasahau kufunga zipu ya suruali yake sasa secretary wake akamfuata na mazungumzo yakawa hivi:
SECRETARY: Boss leo umesahau kufunga geti nyumbani kwakoโฆ
Boss akabaki anashangaaโฆ Baadae wakati anakwenda chooni kujisaidia ile anataka kufungua zipu akaikuta iko wazi ndio akajua alichokuwa ameambiwa na Secretary wake.
Akarudi mpaka kwa secretary na mazungumzo yakaendelea:
BOSS: Bibie ulivyoona geti wazi je uliona benz langu lime paki auโฆ?
SECRETARY: Hapana Boss niliona kitoroli kidogo kimepaki kina matairi mawili
RAFIKI: Vipi mbona leo huna uchangamfu
JAMAA: Wanawake bwana, mwanamke hata umpendeje atakugeuka tu
RAFIKI: Nini tena ndugu yangu? Mbona shemeji mtu fresh sana
JAMAA: Hata mimi nilikuwa najua hivyo, leo nimegundua kumbe ana siri kubwa sana
ananificha, mi naita huu ni usaliti wa ndoa.
RAFIKI: Nini tena?
JAMAA:Nimegundua mke wangu kumbe anafanya biashara ya kitimoto na hajawahi hata kuniambia
RAFIKI: Kitimoto? We umejuaje?
JAMAA: Leo asubuhi nilichelewa kuamka niliamua nijipumzishe kidogo kabla ya kwenda kazini, simu ya mke wangu ikalia, nikaamua kuipokea, kabla hata sijafungua mdomo, nikasikia sauti ya mwanaume mmoja akauliza, โHuyo nguruwe umeshamuondoa?โ Hebu we fikiria nilivyoshtuka, yaani mpaka sasa nashindwa kuamini kuwa mke wangu ananizunguka anafanya biashara ya nguruwe hajaniambia hata siku moja
Pale unapokuwa umefulia sanaโฆ
Mgeni anakutembelea Maskani kwakoโฆ.Unaamua Kuchukua Ile Sh 600 iliyobaki na kwenda Dukani Kumnunulia Soda Unaondoka na Chupa Mbili Unanunua Fanta Moja kwaajil ya Mgeni na Ile Chupa ya Sprite Unaijaza Maji ili Ukirudi Uweze kumpa Kampani MgeniโฆโฆUnafika Seblen Unampa Ile soda ya Fanta Mgeni anakuambia Fanta huwa situmii Nipe hiyo sprite โฆ..Bwanaโฆ.Bwana. โฆBwanaโฆ.Weee ๐๐๐๐๐๐๐๐
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
Bosi wangu karudi safari yake kutoka serengeti..! Si akanitumia picha, lakini ilikuwa network yenyewe tabu.. kwahio picha haikufunguka na kwa vile niliona itachelewa kufunguka na ataona sikumjibu basi nami..
Nikampelekea msg nikamuandikia umependeza saana bosi mashaallahโฆ!!
sasa baada tu ya kumfika msg.. na huku picha ikafunguka kumbe picha ya Sokwe..!!
Basi Kaniambia kesho niende ofsini kwake kuna barua yangu..
Nahisi hyo barua ina pesa, hapa cjalala, nmekosa usingizi kabisa,nawaza ninunulie nn hyo pesa.Na kesho asubuhi sa 12 asubuhi atanikuta ofisini kwake naisubiri barua, sipendagi ujinga mimi.
Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;
JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi
Jana nateremka kwenye BASI UBUNGO nataka nichukue TEKSI hadi KIMARA naambiwa sh.15,000/=.
Wakati niponatafakari hiyo bei, nikasikia “Moro, Moro,Morogoro sh.6,000/=”
Nikaamua nipande niende zangu MOROGORO.
Kwenda na kurudi sh.12,000/=.
Wakati wa kurudi nikamwmbia KONDA aniteremshe KIMARA.
SIPENDAGI UJINGA MIMI NA BEI ZA TEKSI.
๐ย Jamaa kamuaga mkewe anaenda semina Songea kwa wiki nzima kumbe kahamia kwa demu nyumba ya pili toka kwake. Siku ya 1 kalala asubuhi alipoamka kachungulia kwake kukoje,
Si kamuona jamaa yuko nje ya nyumba yake kavaa taulo lake anapiga mswaki. Akapiga kelele, ‘We nani?’, Jamaa akajibu, ‘Mshikaji mambo ya mjini, mume wa huyu demu kasafiri kaenda Songea mi ndo najivinjari hapa’. Mume kajibu kwa uchungu, Shenzi mkubwa, ngoja nirudi toka Songea nakuua.๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
*Mniache mimi sipendi Ujinga Ujinga ๐๏ฟฝ๐๏ฟฝ๐๏ฟฝ๐
Recent Comments