SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Madhara ya Uvaaji wa Wigi au nywele Bandia

Katika miongo kadhaa iliyopita, uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususani na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana mithili ya mtu aliyevaa kofia ngumu (helmet), lakini yaonekana ni mapendeleo ya wengi.

Wanaume wengi hujiuliza , “Ni kwanini kina mama hupendelea kuvaa wigi na kusuka nywele za bandia?, wakati hupendeza na kuwa warembo zaidi wakiwa na nywele zao za asili”?

Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani.

Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni “manyoya”.

Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urembo hujaribu kurefusha nywele zao ili kuwa na viwango na aina za mitindo ya ughaibuni.

Pamoja na kuwa wanawake wanajaribu kuwa warembo kwa uvaaji wa wigi, zifuatazo ni baadhi ya hasara au madhara kiafya ya uvaaji wigi na usukaji wa nywele za bandia.

Uvaaji wa wigi au nywele za bandia waweza kukusababishia mzio (allergy), endapo malighafi au kemikali zilizotumika kutengeneza wigi hiyo zitasisimua mfumo wa kinga ya mwili wa mvaaji.

Kupata m-ba ni tatizo jingine kutokana na uvaaji wigi, hii hutokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya Oksijeni katika ngozi ya kichwa (scalp hypoxia) na katika tishu za shina la nywele. Kwa hiyo kama utaamua kuvaa wigi uhakikishe imetengenezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa na inapitisha hewa ya kutosha ya Oksijeni.

Pia waweza kunyonyoka nywele hata kama una nywele nzuri zenye afya, na kama utachagua kuvaa wigi na unataka kuepuka madhara hakikisha kuwa nywele zako ni safi, usilazimishe kuvaa wigi iliyo ndogo na yenye kubana sana, hakikisha unapata muda wa kupata hewa na nywele zako zinapakwa mafuta kuepuka ukavu wa ngozi ya kichwa na nywele kukatika .

Maumivu ya kichwa ni tatizo ambalo laweza kusababishwa na uvaaji wigi au usukaji wa nywele bandia. Wigi iliyo ndogo husababisha mkandamizo kichwani na kusababisha maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.

Upotevu wa muda na fedha ni dhahiri kwa kuwa ufumaji wa nywele za bandia waweza kuchukua muda mrefu, itamlazimu mvaaji wigi kubadili kwa kununua mpya kila baada ya muda fulani au kuwa na wigi nyingi kwa ajili kubadili kulingana na fasheni.

Harufu mbaya huweza kujitokeza endapo mba na jasho vitachanganyikana na hupelekea uwepo wa bakteria au fangasi na kusababisha muwasho mkali, hii yaweza kumkosesha raha mvaaji wigi na mwenye kufuma nywele za bandia hasa pale anapokuwa katika majumuiko ya kijamii.Kama utachagua kuvaa wigi hakikisha nywele zako zinasafishwa na shampoo au sabuni, zinakaushwa vizuri na kupakwa mafuta.

Endapo mwanamama atachagua kuvaa wigi,asisahau kuwa nywele zake za asili zinahitaji matunzo,na azingatie wakati wa kununua wigi au nywele za bandia, ahakikishe ananunua yenye ubora unaotakiwa ili kuepuka madhara ya kiafya anayoweza pata kutokana na uvaaji wigi au anapofuma nywele za bandia.

Benson Chonya

Jinsi ya Kulima Mgagani: Kilimo bora cha Mgagani

Utangulizi

Migagani, migange, mikabili au miangani ni mimea ya jenasi Cleome katika familia na oda Brassicales (kabichi). Mgagani (Cleome gynandra) au Spider plant kwa kingereza, ni mmea wa asili ya Afrika unaostawi vizuri kwa kumwagiliwa hapa afrika ya mashariki wakati wa joto. Pia huchumwa mashambani ikiwa imeota yenyewe zao hili hushambiliwa na magonjwa na wadudu mara chache. Majani na Matawi machanga yana virutubisho kuliko Sukuma wiki na kabichi. Mahitaji yake yanaongezeka kwenye miji midogo na mikubwa kila siku.

Mgagani wa kawaida, huliwa takriban kila mahali pa Afrika na katika mabara mengine pia. Wanawake wengi wenye mimba au waliozaa hula mmea huu, kwa sababu una chuma nyingi kiasi na husaidia kuongeza damu. Mboga ya mgagani huitwa magagani.

Aina Za Mgagani

Kwa Afrika kuna aina 50 za mgagani , lakini ni aina nne tu zinazoliwa. Aina bora zinazalishwa na kituo cha AVRDC-THE WORLD VEGETABLE CENTER zina majani mapana, uchungu kidogo na ina majani mengi Zaidi na huvunwa kwa muda mrefu. Aina hizi ni pamoja na PS ambayo ina shina na matawi ya zambarau na GS I yenye shina na matawi ya kijani, mbegu za aina bora zina weza kupatikana toka kwenye kituo cha the world Vegetable Center, Arusha Tanzania. Ikumbukwe kuwa wakilima wengi wa nchi za Tanzania na kenya wanalima na kuuza mbegu za aina hizi na pia baadhi ya makampuni ya mbegu yameanza kuuza.

Mazingira Mgagani Unapoota

Kwa asili mgagani unastawi vizuri sehemu zenye joto na udongo wa aina mbalimbali kama tifutifu. Zao hili halikui vizuri katika udongo unaotuamisha maji, au katika maeneo ya baridi au kivuli. Katika eneo la mita za mraba 1-2, familia inaweza kupata mgagani wa kula kwa muda wa miezi minne.

 


Kutayarisha Shamba La Kuotesha Mgagani

Anza kwa kutifua ardhi vizuri na changanya na mbolea ya samadi kwa kiwango cha kilo moja hadi mbili kwa mita mraba. Mgagani waweza kuoteshwa peke yake au kwa kuchanganywa na mazao mengine kama mnavu au mchicha.

Uoteshaji Wa Mgagani

Baada ya kuandaa shamba lako sia mbegu kwa kutawanya au katika mstari ya umbali wa sm 30-50, majira ya mvua au kwa kumwagilia, kina cha mstari kisizidi sm1, funika kwa udongo kidogo na mwagilia kama hakuna mvua. Punguza miche iliyosongamana inapokuwa na majani manne hadi matano na iwe katika nafasi ya sm 15-20 toka mche hadi mche kwa upandaji wa kutawanya.

Palizi Ya Mgagani

Hakikisha shamba ni Safi hasa mwezi wa kwanza baadae magugu yanaweza kuzuliwa Na kivuli cha mgagani umeota vizuri.

Umwagiliaji Wa Mgagani

Unyevu wa kutosha ni muhimu kwa zao hili na inashauriwa kumwagilia ni majira ya kiangazi angalau mara mbili kwa wiki. Mgagani hustahimili ukame kuliko nyanya au mchicha lakini mimea isiachwe ikanyauka.

Uvunaji Wa Mgagani

Kwa uvunaji wa moja kwa moja mimea inaweza kung’olewa baada ya wiki nne hadi sita, kwa kuvuna majani, uchumaji unaweza kufanyika kila mara hadi miezi minne, Mimea iliyo na umri wa Zaidi ya miezi minne, inaweza kukatwa shina na kuchipua na kuendelea kuvunwa baada ya wiki nne hadi miezi minne kulingana na hali ya hewa na matunzo.

 

Uzalishaji Wa Mbegu Za Mgagani

Kwa kawaida mgagani hutoa mbegu kwenye shina au matawi vifuko vya mbegu vikikauka huwa mbegu imekomaa. Mimea ikatwe usawa wa ardhi na kutungiwa kwenye sakafu. Safi na ngumu, kuondoa mbegu toka kwenye maganda. Ondoa maganda, mashina na majani yaliyochanganyika na mbegu. Uchafu mwingine mbegu zihifadhiwe katika mifuko ya plastiki au ya karatasi au makopo na kuweka sehemu iliyo kavu. Kwa kuwa mbegu zina mafuta ya asili ya dawa za kuua wadudu ni vigumu sana kushambuliwa na wadudu waharibifu.

Mauzo Ya Mbegu Za Mgagani

Makundi ya wakulima yaliyopata mafunzo ya uzalishaji wa mbegu sasa yanazalisha kwa ajili ya wakulima wengine. Katika nchi ya kenya ambapo mgagani unaliwa sana, uzalishaji wa mbegu hupatia wakulima mapato Zaidi kuliko kuzalisha mboga mbegu za mgagani zinaptikana madukani.

Mauzo Ya Mgagani

Matawi malaini na machanga yenye majani yanaweza kuvunwa na kuwekwa kwenye mafungu ya uzito wa gramu 100-200. Majani yaliyo kaushwa kwa jua na kuwekwa kwenye vyombo mbalimbali huuzwa.

Kuwa na kawaida ya kujiwekea Akiba ni njia na Siri ya kuwa tajiri

Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Je ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida.

Kuwa na lengo la kifedha, kuweka akiba, na kutumia fedha kwa hekima ni muhimu sana katika safari ya kuelekea utajirini. Kuweka malengo kunamaanisha kuwa na mpango madhubuti wa kifedha unaolenga katika kupata matokeo mazuri ya uwekezaji na matumizi ya fedha. Watu wenye mafanikio katika eneo la utajiri mara nyingi hutumia mipango ya muda mfupi, kati, na muda mrefu kuhakikisha kuwa wanafikia malengo yao.

Aidha, kuweka akiba ni nguzo muhimu. Hii inamaanisha kujinyima baadhi ya matumizi yasiyo ya msingi na kuhakikisha kuwa unaweka kando sehemu ya mapato yako kwa ajali ya siku zijazo. Akiba hii inaweza kutumika kama mtaji wa kuanzisha biashara au kuwekeza katika fursa zenye faida kubwa.

Kuwekeza ni hatua inayofuata baada ya kuwa na akiba ya kutosha. Hapa, elimu juu ya masoko ya fedha, biashara, na uwekezaji katika rasilimali kama hisa, mali isiyohamishika, na biashara huja kuchukua sehemu kubwa. Ni muhimu kujifunza na kuelewa ni wapi na lini kuwekeza. Kutafuta ushauri kutoka kwa wataalamu wa fedha kunaweza kusaidia kuepuka makosa na kupata mwelekeo sahihi.

Kwa kutumia mbinu hizi – kuweka malengo, kuweka akiba, na kuwekeza kwa hekima – mtu anaweza kujenga msingi imara wa kuelekea utajiri. Ni safari inayohitaji uvumilivu, nidhamu, na uelewa mpana wa maswala ya kifedha, lakini inawezekana kwa yule aliye tayari kujifunza na kuchukua hatua.

Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na huendelea kuificha.
Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua siri ya utajiri.Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate manufaa kwa kununua kitabu hiki nimeamua kuiweka siri hii wazi:—

Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza kuitoa ziada na faida.

Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia ya kuweka akiba-

Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi ambavyo vinazalisha faida endelevu.

Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha biasharayako ili iwe indelevu.

Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika.

Njia ya kwanza ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka akiba, anza kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawana TShs 30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000 (Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka itazaa na kukuletea TShs 2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii inaweza ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine njia hii inaweza kuwa ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.Dundulizo la akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia kwani utaweza kukidhi hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya dharura gharama za likizo na hata kutumia mbinu hii kama mpango wa elimu kwa watoto wako iwapo utawaanzishia hivi mara tu kila mmojawapo anapozaliwa au unaweza kuutumia kama upanga wa siku zijazo kwa mirathi ukianza hivyo leo kwa kupangilia namna hiyo kwa kila kusudio lako la baadaye.

Tuangalie njia ya pili.- Njia ya pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama wewe ni mtu mwenye shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako kinaweza kuwa kinaongezeka kila mara. Badala ya kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku jiwekee malengo ya kuweka akiba ya TShs 10,000. Anza kwa kutenga asilimia10% ya mapato yako hadi utakapofikia lengo la TShs 10,000 au zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa miaka sitini na tano (65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka akiba ya TShs 10,000 kwa siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita bila riba yoyote utapataTShs. 23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa miaka sita na miezi sita utapata TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo utaendelea kuweka akiba kwa riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka kumi utapata TShs. 63,112,201.43.Kwa kuwa kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo katika kitegauchumi chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze kwenye kitega uchumi chenye kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa mambo ya fedha wanashauri kuwa uwekeze fedha yako kwenye kitegauchumi chenye kutoa faida ya angalau asilimia 10% Kwa mfano unaweza kuwekeza kwenye Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered Bank” inatoa riba ya asilimia kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa katika soko la hisa na mitaji.Kwa wastani wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato yatokanayo na hisa kwa gawio pamoja na kukua kwamtaji ni zaidi ya asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa kiwango cha kawaida chaasilimia kumi (10%).

Eti wanadamu walikuja vipi duniani

Mtoto wa miaka sita alimuuliza babake:
MTOTO: Baa, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
BABA: Mungu alimuumba Nabii Adam na Hawa.
Kisha wao wakaanza kuzaa watoto na watoto
wakazaa mpaka tukazaliwa sisi. (Mtoto hakuridhika
akamfuta mamake)
MTOTO: Mma, eti sisi wanadamu tulikuja vipi
duniani?
MAMA: Wanasayansi wamesema sisi tulitokana na
manyani baadae tukawa binadamu. (Mtoto akarudi
kwa baba)
MTOTO: Baa mbona mama ansema sisi tulikuwa
manyani mwanzo?Au wanidanganya?
BABA: Mwanangu, mimi nimekuelezea kuhusu ukoo
wetu. Mamako amekuelezea kuhusu ukoo wao😂😂🚶🏼🚶🏼🚶🏼

Faida za Korosho Kiafya

Korosho zina faida hizi zifuatazo;

1. Zinakinga Maradhi ya Saratani Haswa kwenye matumbo mapana.

2. Korosho zinasaidia Afya ya moyo kufanya kazi vizuri.

3. Korosho zinasaidia Kuzifanya nywele na ngozi ya mwili kuwa na Afya nzuri.

4. Korosho zinasaidia mifupa yako kuwa imara na afya nzuri.

5. Korosho ni nzuri kula kwa ajili ya mishipa ya mwilini mwako.

6. Korosho zinakukinga usipatwe na mawe kwenye nyongo yako.

7. Korosho ukila zinapunguza uzito mwilini.

Ufugaji wa nguruwe kazi, Cheki jamaa hawa wake walivyompa mtihani

MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalishanini?
.

MFUGAJI: Nawalisha mabaki ya chakula toka migahawa mbalimbali
.
MWANAHARAKATI: Hayo ni makosa unawatesawanyama kwa kuwalisha chakula kichafu. Akapigwa faini… Baada ya siku chache wakaja wanaharakati toka Umoja wa Mataifa
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.

MFUGAJI: Huwa nawaanzia siku na uji wa ulezi, halafu mikate, mchana ugali kwa kabeji na usiku viazi
.
MWANAHARAKATI: Loh watu wanakufa kwa njaa wewe unalisha nguruwe, akapigwa faini….siku chache baadae wakaja wanaharakati wa Mazingira
.
MWANAHARAKATI: Hawa nguruwe unawalisha nini?
.
MFUGAJI: (Kwanza akasita kidogo) Hawa huwa nawapa shilingi alfu tano kila mmoja kila siku halafu wao wenyewe wanaenda kununua chakula wanachokitaka.. .

Kingereza sio mchezo, angalia huyu anavyojichanganya

Jamaa fulani alikuwa ame2lia beach mzungu akapita akamuliza “Are u relax ? Jamaa akawa hamuelewi akamjibu No! Mzungu mwengine akapita akamuliza vilevile akajibu No!

Akaona hapa anasumbuliwa akasogea mbele kidogo ya maji akamuona mzungu mmoja alikuwa ame2lia. Akamuliza “are u relax? Mzungu akajibu yes jamaa akamkata makofi mawili na kumwambia kumbe we ndo relax inuka unatafutwa na wenzako…..Shenz mkubwa mie nasumbuliwa na wenzako kule we umejikausha!!

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?

Kwa mujibu wa Biologia, baada ya tendo la kukutana kimwili takribani mbegu milioni 200 hadi 300 hutolewa na mwanaume…halafu zote huanza kupiga mbizi kuogelea kwenye njia safarini kukutana na yai la kike.

Ajabu ya kwanza ni kwamba sio zote 200 – 300 ambazo hufanikiwa kulifikia yai( nyingi huchoka na kufia njiani maana si mashindano ya mchezo mchezo).
Ajabu ya pili ni kwamba kati ya hizi 300 zinazofanikiwa kufikia yai, ni moja tu..moja tu itakayoshinda nakufanikiwa kupenya na kurutubisha yai, na kwa mantiki hii ILIYOSHINDA NI WEWE HAPO.

Umewahi kuwaza kuhusu hili vizuri?
Yaani ulishindana mbio hizo ukiwa huna macho na ulishinda, ulishindana bila elimu na ukashinda,ulishindana bila hata cheti chochote wala msaada wa yeyote ….na UKASHINDA.

Nini kinachokufanya udhani utashindwa sasa?
Tena sasa uko na macho yote, miguu, sasa Unamjua Mungu, sasa ukiwa na mipango,ndoto na maono.
Kumbuka ULISHASHINDA toka tumboni huna sababu ya kuwa na hofu yeyote, PAMBANA

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About