SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Vyakula vinavyosaidia macho kuongeza uwezo wa kuona

Je unakula chakula bora ambacho ni bora pia kwa ajili ya macho yako? Kula vizuri kuna manufaa mengi kwa ajili ya miili yetu; macho nayo yakiwemo. Kuna virutubisho mbalimbali vinavyohitajika kwenye macho kuliko tu vile vinavyofahamika na wengi vilivyoko kwenye karoti.

Jifunze ni vyakula gani vitayapa macho yako na kuyawezesha kupata virutubisho ambavyo vitayalinda dhidi ya kupungua kwa uwezo wa kuona.

Mboga za majani

Watu wengi hufikiri kuwa kula mboga za majani ni umaskini; lakini ukweli ni kuwa mboga za majani zina manufaa makubwa kwenye miili yetu. Mboga za majani zina kemikali ya luteini na zeaxanthini ambazo ni muhimu katika kulinda na kujenga uwezo wa macho kuona vizuri.

Mayai

Mayai yana manufaa kwa ajili ya afya ya macho na miili yetu kwani yamejaa vitamini. Vitamini A inayopatikana kwenye mayai hulinda macho dhidi ya kutokuona usiku pamoja na kukauka kwa macho (macho angavu).

Samaki

Samaki ni chakula bora kwa afya ya macho hasa wale wa maji baridi, kwani wamejaa asidi ya mafuta ya omega-3 ambayo ni muhimu kwa ajili ya kuzuia macho angavu (kunyauka kwa macho), kudhoofu kwa misuli ya macho na hata mtoto wa jicho. Kama umeshindwa kula vyakula hivi vya baharini unaweza kula matunda kama vile matunda damu ili kupata asidi ya mafuta ya omega-3.

Matunda jamii ya mchungwa na zabibu

Matunda kama vile malimao, machenza, machungwa na zabibu yamesheheni vitamini C. Hivyo yatakuwezesha macho yako kujikinga na magonjwa kama vile mtoto wa jicho pamoja na kudhoofu kwa misuli ya macho.

Karanga na jamii zake

Vyakula hivi vimejaa mafuta ya omega-3 na vitamini E ambavyo ni muhimu kwa ajili ya afya ya macho.

Vyakula vya jamii ya kunde

Vyakula vya jamii ya kunde vina kemikali kama vile Bioflavonoidi na Zinki ambavo ni muhimu kwa ajili ya ulinzi wa retina na kuzuia kudhoofu kwa misuli ya jicho.

Alizeti

Ulaji wa mbegu za alizeti utakuwezesha kupata madini ya zinki pamoja na vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya macho yako.

Matunda ya rangirangi

Chakula kama karoti, nyanya, pilipili hoho, boga na mahindi ni vyanzo bora vya vitamini A na C. Inaaminika kuwa kemikali ya carotenoids inayoyapa matunda haya rangi zake ni muhimu kwa afya ya macho. Ikumbukwe pia vitamini C na A zina manufaa kadha wa kadha kama tulivyoona kwenye hoja zilizopita.

Nyama ya ng’ombe

Nyama imejaa madini ya zinki ambayo huuwezesha mwili kufyonza vitamini A ambayo ni muhimu kwa macho pia. Ikumbukwe kuwa vitamini A huuwezesha mwili kukabiliana na matatizo yatokanayo na umri au uzee.

Kwa hakika maradhi mengi humpata mwanadamu kutokana na kuharibu au kuacha mfumo wa ulaji wa asili. Ni kweli kuwa matunda na mboga vina manufaa makubwa kwa ajili ya macho yetu pamoja na mwili mzima kwa ujumla. Jitahidi kufanya angalau nusu ya mlo wako uwe ni matunda na mboga. Usisahau pia kumwona daktari mara kwa mara ili kupima afya ya macho yako pamoja na kupata ushauri wa kitabibu.

Ujumbe kwako wewe mwajiriwa au uliyejiari

Kama umeajiriwa au pia umejiajiri ni mojawapo ya njia zinazokuingizia kipato maana wengi wanaanzia hapo mpaka kuja kufikia kule wanakohitaji.
Ila kuna maswali machache ya kukupa changamoto ambayo nataka ujiulize:-

Kwako muajiriwa

👉🏿Umeshawahi kujiuliza huo mshahara unaolipwa unakutosha kukutimizia Yale yote unayohitaji maishani mwako??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ukifukuzwa au ukipunguzwa kazini utafanya nini?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ofisi au kampuni unayofanyia ikifilisika wewe utafanya nini?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kuhama au kuacha kazi hapo unapofanyia uende ofisi nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwanini hupapendi hapo unapoishi lakini bado unaendelea kuishi hapo?

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini huo usafiri unaoutumia huupendi lakini kila siku unautumia huo huo??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza ni kwa nini wanao au watoto wako hawapendi shule wanayosoma lakini wewe uwezo wako ndipo ulipoishia??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini hupendi mikopo lakini bado unaendelea tu kukopa??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza unaipenda kwa dhati tena kutoka moyoni kazi unayoifanya??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unaomba kila Mara kuongezewa mshahara kama sio kuandamana??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unatamani ukasome uongeze elimu??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini mkubwa wako kazini hataki uache kazi au ukasome au uhamie ofisi nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini kila siku uko “busy” kazini au ofisini mpaka unakosa muda wa kufurahia na ndugu,jamaa,na marafiki na familia na mifuko yako au akaunti yako benki haiko “busy”??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka kufungua kibiashara chako au unataka ufanye kilimo Fulani kwa sababu umesikia kinawatoa watu???

👉🏿Umeshawahi kujiuliza usipokwenda kazini kwa muda Wa wiki au mwezi au mwaka je kipato hicho hicho unachokipata utaendelea kukipata??

Hebu jiulize hayo maswali na mengine mengi yanayofanania na haya ujaribu kuona kama majibu yake unayo na kama majibu yapo ni njia gani unatumia au unategemea kutumia ili kuondokana na hayo??

Kwako wewe uliyejiajiri

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini biashara yako haikui kwa muda wote huo uko pale pale??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini unataka uachane na hiyo biashara ufanye nyingine??

👉🏿Umeshawahi kujiuliza kwa nini kila kitu unafanya wewe mwenyewe haumruhusu msaidizi kuwepo??

👉🏿Kwa nini huthubutu kumuachia mtu biashara yako kwa muda tu ukiondoka unafunga??

👉🏿Kwa nini unawaumiza wengine au wengine wanaumia ndipo wewe utengeneze faida yako??

👉🏿Kwa nini huwezi kuwasaidia wengine waweze kutengeneza kipato kama chako??

👉🏿Kwa nini akija mwenzako pembeni yako kufungua biashara kama yako unachukia???

👉🏿Kwa nini unachukia kulipa kodi ya pango lakini inakubidi tu ufanye hivyo??

👉🏿Ni watu wangapi wanaichukia au kuipenda biashara yako??

👉🏿Wangapi wanakuongea vizuri au vibaya kutokana na Huduma yako unayotoa??

👉🏿Kwa nini unatamani usiwe unalipa kodi??

👉🏿Kwa nini hupendi kuwaonyesha wengine njia unazotumia katika kuijenga biashara yako??ikiwa ni pamoja na upatikanaji Wa mizigo,unavyouza na unavyopata Wateja??kwa nini?

👉🏿Kwa nini hupendi kuona aliyeanza nyuma yako akifanikiwa kabla yako??

Hayo ni baadhi ya maswali ya kujiuliza wewe kama mjasiriamali au uliyejiajiri ingawa yapo na mengine unaweza kujiuliza tu uone kama utapata majibu yake na yawe ya kueleweka

Njia nzuri ya kufanikiwa katika maisha

Kuna tofauti kubwa sana kati ya mtu anayejenga GHOROFA na yule anayejenga Nyumba ya KAWAIDA.

Anayejenga Ghorofa anatakiwa achimbe msingi Mrefu kwenda chini kabla hajaanza
kuinua Ghorofa yake juu. Hivyo wakati huyu mwingine anapokuwa anajenga Nyumba ya kawaida atakapokuwa tayari anakaribia hata kuezeka, unaweza kukuta yule anayejenga Ghorofa bado yuko kwenye Msingi.
Ila siku akianza kuinua Ghorofa lake, kila mtu atashangaa urefu wa juu atakaoenda nao.

Kwenye maisha ndivyo ilivyo- “If want to go so high, you need to go so deep” (Kama unataka kwenda juu sana ni lazima ukubali kwenda chini sana). Ni lazima ufanye kitu cha tofauti kitakochokujengea Future imara.

Ukweli ni kuwa Watu wengi wanaokuzunguka wanajenga maisha ambayo ni kama Nyumba ya kawaida.
Na wewe kama unataka kujenga maisha yanayofanana na Ghorofa,
Ni lazima ukubali kuonekana unachelewa kwenye baadhi ya mambo.

Hii inamaanisha nini?…
Hii inamaanisha kuwa utalazimika kufanya vitu vya TOFAUTI na kuwa TAYARI kusubiri.
Utatakiwa Kuwekeza wakati wengine wanaenda kununua nguo mpya waendane na Fashion,
Utatakiwa Kusoma vitabu wakati wengine wanaangalia movie na kupiga stories,
Utatakiwa Uanzishe Biashara yako wakati wenzako wamesharidhika na mshahara wanaopata n.k

Unachofanya kuanzia unapoamka hadi unapoenda kulala kitajulisha kama unajenga Maisha GHOROFA ama Maisha KAWAIDA.

Ukijiona unapoteza muda hovyo,
ukiingia Facebook/instagram ni kusoma umbea tu,
Unalalamika unasema utafanya na hakuna unachofanya, ujue unajenga Maisha ya KAWAIDA tena ni kama Nyumba ya UDONGO.

Ukitaka kujenga maisha GHOROFA;
1. _Jifunze kitu kipya leo._
2. _Chukua hatua kuelekea Ndoto yako._
3. _Usiwe mtu wa kulalamika bali tafuta suluhisho kwa kila changamoto._

Je, LEO utajiunga na wanaojenga Maisha GHOROFA ama wale wanaojenga Maisha ya KAWAIDA?

Twende zetu tujenge Maghorofa !!!

Cheki huyu jamaa alivyoumbuka kwenye harusi

Jamaa mmoja alialikwa ktk harusi. Akafika mlango Wa 1 umeandikwa kulia ni ndugu Wa maharusi, kushoto ni wageni waalikwa, akaenda kushoto maana yy alialikwa. Akakuta mlango wa2 umeandikwa kulia wenye zawadi kushoto wasionazawadi yy hakuwa na zawadi. Mlango Wa 3 umeandikwa kulia wanawake kushoto waume akapita kushoto akajikuta ametokea mtaani

😄😄😄😄😄😄😄😄. Tujifunze kutoa wandugu

*hatupendagi ujinga sisi*
🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿🚶🏿

Umuhimu wa kupata chanjo

Siku zote sisi wanadamu huwa tunaambizana kuwa, kinga ni bora kuliko tiba, tukiwa na maana kwamba, ni vyema mtu ukachukua tahadhari mapema kabla haujafikwa na jambo au tatizo fulani.

Vivyo hivyo katika chanjo, hii ni kinga ambayo hutolewa kwa binadamu na katika umri tofauti tofauti ili kuuwezesha mwili kutengeneza ulinzi asilia (antibodies) ambao utauwezesha mwili uwe na nguvu zaidi za kupambana na magonjwa au visababishi vya matatizo mbalimbali ya kiafya ambavyo siku zote vimekuwa ni sehemu ya maisha ya mwanadamu.

Mpenzi msomaji, ni vyema ukafahamu kuwa chanjo SIYO tiba, na siku zote hutolewa kwa watu ambao hawana ugonjwa au tatizo husika linaloendana na chanjo hiyo, mfano, kama mtoto anao ugonjwa wa surua, basi itabidi apate matibabu ya surua na siyo chanjo ya surua. (Ila kumbuka kuwa matatizo mengine ya kiafya kama vile kukohoa, kuharisha au mafua, havimzuii mtu kupata chanjo).

Pengine utajihoji ni kwa nini inakuwa hivi?, hii ni kutokana na kwamba, chanjo siku zote dozi za dawa zake huwa ni kidogo ukilinganisha na dozi endapo hiyo dawa itatumika kutibu ugonjwa husika mfano surua au kifua kikuu, hivyo kwa kuwa dozi ni ndogo, basi haitakuwa rahisi kutibu mtu ambaye tayari anao ugonjwa.

Kitu kingine katika chanjo ni kwamba, baadhi ya chanjo huwa ni chembe chembe maalumu ambazo hufanana na aina ya ugonjwa ambao umekusudiwa kuzuiliwa au kukingwa, hivyo chembe chembe hizi huwa katika kiwango kidogo sana ambacho hakiwezi kukusababishia matatizo yoyote ya kiafya, ila mwili wako utaamshwa utengeneze kinga za kutosha ili endapo mazingira uliyopo yatakuwa na ugonjwa huo husika, wewe mwili wako utakuwa tayari kupambana ila chembe chembe hizi maalumu hazitaweza kukutibu endapo tayari unao ugonjwa husika.

Mambo ambayo huweza kujitokeza baada ya mtu kupata chanjo ni pamoja na hali ya joto la mwili kupanda au homa, ingawaje siyo lazima mtu apatwe na hali hiyo cha kufanya ni kutumia dawa za kushusha homa na baada ya muda mwili wako utarejea katika hali yake ya kawaida, hivyo endapo hali hiyo itajitokeza kwako usiwe na shaka.

Chanjo itakuwezesha kujikinga dhidi ya magonjwa, kukupunguzia gharama za matibabu na utapata muda ya kuendelea na shughuli zako za kila siku, kwani wewe au familia yako mtakuwa na afya bora.

Jinsi ya kujua kama mwanamke anakupenda kweli kwa dhati

Yafuatayo ni maswali ya kujiuliza ili kujua kama mwanamke anakupenda kweli.

Anajitoa kwa ajili yako?

Mwanamke anayekupenda atakuwa tayari kujitoa muhanga kwa ajili yako. Mwanamke anayekupenda atakua tayari kufanya chochote kile kwa ajili yako kitu ambacho hawezi kufanya kwa ajili ya mtu mwingine yoyote.

 

Atakupa kipaumbele?

Mwanamke anayekupenda atakupa kipaumbele katika vitu na mambo yake yote. Mbele ya Marafiki zake wewe utakuwa ni bora zaidi.

Anakuchukulia tofauti na wanaume wengine?

Mwanamke anayekupenda atakufanyia mambo ambayo hawezi kuwafanyia wanaume wengine.

Anakupa nafasi na muda wake?

Mwanamke anayekupenda anakupa nafasi na muda wake. Anauwezo wa kuacha mabo mengine ili aweze kuwa na wewe.

 

Anakuhangaikia?

Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako, Kawaida mwanamke anayekupenda atahangaika juu ya usalama wako, raha yako, heshima yako na maendeleo yako. Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke uliyemlenga anakupenda kweli.

Ana wivu juu yako?

Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa. Anaogopa usije ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa. Wivu ni ishara kuwa anakupenda wewe na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza, anaogopa usije ukatoka katika maisha yake.

 

Anakushirikisha furaha yake?

Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia wewe macho namaanisha uso wake haraka sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia wewe kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake, zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.

Anakuangalia sana?

Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine, atakuangalia na kutabasamu vizuri. Hii ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia kuwa anakuhitaji katika maisha yake.

 

Anavaa vizuri mkutanapo?

Mwanamke anayekupenda atajitahidi apendekeze kwa kuvaa vizuri pale anapojua kuwa atakutana na wewe, atajali sana juu ya nywele zake, nguo zake na hata anavyonukia. Hii ni ili kukuvutia wewe na kuonyesha uwepo wake kwako.

Anapenda kuwa karibu na wewe?

Mwanamke anayekupenda ataonyesha dalili za kupenda kuwa karibu yako katika mazungumzo au maeneo mengine, atapenda mara nyingi kuwepo katika maeneo unayopendelea na pia sauti yake itabadilika kuashiria hali ya kukupenda na kutaka kukuvuta kwa sauti yake.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

Baadhi ya misemo mikali ya leo

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi kufunika sufuria.

Kwa nini watu wanapenda pesa

Watu wengi tunapenda sana Pesa lakini hatuko tayari kuzifanyia Pesa kazi nikiwa na maana kutumia njia sahihi kuzipata na tunapozipata hatuna Akili ya kuweza kuwa nazo muda mrefu zisiondoke.
Kama tujuavyo katika maisha yetu haya Pesa ndio kila kitu,tunahitaji Pesa ili tuweze kufanya mambo mengi mazuri na makubwa.Kitu kinachotukwamisha hatujui tufanye nini ili tuweze kuzipata hizi Pesa na tunapozipata tunakosea tena cha kuzifanyia ili zisipotee tena au zisiishe.

Kitu kikubwa kinachotugharimu ni kwamba hatuna elimu ya Pesa.Wengi wetu tumesoma tena sana lakini huko shuleni na vyuoni hatufundishwi jinsi gani ya kuzitafuta Pesa,uzifanyie nini,na nini kifanyike ili zisiishe.
Elimu hii kuhusu Pesa haitolewi shuleni zaidi ni ya kujifunza kutoka mtaani hasa kwa watu wanaomiliki Pesa nyingi au ambao wamefanikiwa ndio watakupa utaalam halisi na elimu kuhusu Pesa.

Kuna watu wengi sana tumeshawahi kuwasikia wamepata Pesa nyingi sana lakini sasaivi hawana kitu.Wengi tumewasikia kwenye bahati nasibu wamejishindia Pesa nyingi,wengine kwenye mashindano mbalimbali wamejishindia Pesa kibao lakini cha kujiuliza hao watu mpaka sasa wapo wapi?hela zao ziko wapi?wamezifanyia kitu gani?bado wanazo??Jibu rahisi ni hapana na hii ni kutokana na kwamba hawakupata elimu ya Pesa ndio maana.

Inatakiwa kabla ya kuwapa watu Pesa lazima wapate elimu kuhusiana na Pesa hapo ndipo watakapokuwa na ujuzi Wa kuweza kuzifanyia kazi na kuziongeza.
Matajiri wote unaowafahamu wana elimu juu ya Pesa ndio maana Pesa zinazidi kuwafuata wao na sisi ambao hatuna elimu ya Pesa tunazidi kuhangaika kuzitafuta.

Lakini sifa nyingine ya Pesa kadiri unavyotoa ndivyo unavyozidi kuzipata yaani ni kama vile unabarikiwa….kama unajua au unavyoona matajiri wengi sana ni watoaji Wa hela kusaidia sehemu mbalimbali hasa kwa wasiojiweza au miradi ya kimaendeleo ndio maana unaona wanazidi kufanikiwa.

Watu wengi tunazifanyia Pesa kazi badala ya Pesa kutufanyia sisi kazi. Hii ni kutokana na kwamba hatujaelewa au hatujui jinsi gani ya kutengeneza mfumo utakaokuwa unakuingizia tu Pesa hata kama haupo.Umeshawahi kujiuliza hicho unachokifanya kama ukipumzika kwa muda Wa kama miezi sita utaendelea kupata kiasi kilekile cha Pesa ulichokuwa unakipata kabla ya kupumzika?Kama huwezi hivyo basi wewe unazifanyia Pesa kazi.

Kwa muajiriwa ukipumzika miezi sita utaendelea kulipwa mshahara wako?
Kwa mfanyabiashara labda Wa duka ukipumzika wiki moja bila kufungua duka lako utapata kipato kile kile unachokitengeneza kila siku?Kama hauwezi basi ujue unazifanyia Pesa kazi.

Tukiangalia kwa upande mwingine wafanyabiashara wakubwa wanaweza kupumzika hata mwaka mzima na wakaendelea kupata hela zilezile kwani wameshatengeneza mfumo ambao sisi wengi hatunao na ndio watu ambao Pesa zinawafanyia kazi.Ana uwezo Wa kwenda kupumzika Marekani mwaka mzima na Pesa zikaendelea kuingia huu ndio Uhuru Wa Pesa.

Jiulize wewe unazifanyia Pesa kazi au Pesa zinakufanyia wewe kazi?
Unaufanyia mfumo kazi au mfumo unakufanyia wewe kazi?
Kipato chako ni endelevu au sio endelevu?
Ukipumzika mwaka mzima bila kufanya au kugusa chochote utaendelea kupata kipato hichohicho?

Kama jibu ni hapana basi ni muda muafaka Wa kubadilika na kubadilisha unachokifanya.

……Shtuka na changamkia fursa……

Shopping Cart
1
    1
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About