SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Mambo ya kufanya ili kupona majeraha mapema

Hakuna mtu anayependa kupata majeraha au kuchelewa kupona majeraha. Kwa kuwa uhai na uzima wetu haupo mikononi mwetu, ni vyema tukafahamu kuwa kuna wakati tunaweza kuumia.

Kwa kutambua hili karibu nikufahamishe mambo matano unayoweza kuyafanya ili kuharakisha kupona majeraha.

1. Kula vizuri

Lishe bora ni muhimu wakati wote, lakini ni muhimu zaidi mara unapokuwa na majeraha. Ili uweze kupona majeraha mapema unahitaji ule matunda na vyakula vyenye protini, vitamini C, B12 pamoja na madini ya chuma kwa wingi.

Vyakula na matunda hayo ni kama vile machungwa, mapapai, mayai, maziwa, samaki, maharage, n.k. Kwa kula vyakula hivi mwili utaweza kutibu majeraha kwa haraka zaidi.

2. Pumzika vya kutosha

Kupumzika ni njia ya kuupa mwili nafasi ya kujijenga na kujitibu wakati wa majeraha. Kutokana na mtindo wa maisha au changamoto za kiuchumi, baadhi ya watu hawapati muda wa kupumzika wapatapo majeraha.

Hivi leo utamkuta mtu akiendelea na shughuli zake huku akiwa na plasta, au bandeji bila hata kujali. Ili uweze kupona mapema unahitaji kuupumzisha mwili kwa kiasi cha kutosha ili upone vyema.

3. Fuata maelekezo

Kutokana na majeraha uliyoyapata daktari anaweza kukataza usile au sifanye kitu fulani lakini wewe hutaki; je unafikiri utaweza kupona mapema?

Watu wengi hukatazwa vitu kama vile pombe au kazi ngumu mara wapatapo majeraha, lakini ni wachache ndiyo wanaoheshimu hili.

Ni lazima ufuate ushauri wa daktari ikiwa unataka kupona mapema.

4. Kunywa maji mengi

Maji huchukua takriban asilimia 70 ya mwili wa binadamu. Kunywa maji mengi uwapo na majeraha kutakuwezesha kupona majeraha yako mapema.

Maji huboresha kinga mwili, huboresha misuli pamoja na viungio (joints) mbalimbali hivyo kukuwezesha kupona majeraha mapema.

5. Ogea maji ya baridi

Tafiti mbalimbali zilizofanywa zimeonyesha kuwa kuna manufaa makubwa ya kuogea maji ya baridi. Manufaa haya pia yapo kwa mtu aliyepata majeraha.

Kuogea maji ya baridi kutasababisha mzunguko mzuri wa damu, hivyo viini lishe na tiba vitasafirishwa vyema kwenda kuponya majeraha; pia maji baridi hupunguza maumivu ya vidonda au majeraha.

Kwa hakika lishe bora ni tiba ya maradhi takriban yote. Katika makala hii umeona jinsi lishe bora pamoja na kuzingatia kanuni chache za msingi za afya kunaweza kukusaidia kupona majeraha mapema.

Bongo usanii mwingi!!!

BONGO USANII UMEZIDI DAAH!!

…yani nakupeleka dinner unakula sana vipaja vya kuku na chips yai halafu nakupeleka bar unakunywa sana tu, tukitoka hapo nakupeleka club, Masaa yote hayo hakumbuki kuniambia upo periods hadi mdaa wakwenda kulala ndo beiby nipo kwenye siku zangu!! jamani jamani… Hapo ndo unaanza kupiga hesabu pesa iliyopotea buree😂😂😂😂

Ndooo maana mabinti wa kibongo 🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻

Ujumbe wa kuasa kuhusu upendo

UPENDO ni ubeti wa maneno yaliyo tamkwa mpaka sasa hajulikan nani alietunga!
PENZI ni hadithi iliyocmuliwa lakin mpaka sasa hafahamik nan muhucka, ndio maana kila mwenye KUPENDA au KUPENDWA hana uhakika muda wote huhis anasalitiwa.
PENZI Ni kama jengo lilokosa nguzo muda wowote unahic litadondoka… Ucnielewe vibaya ckukatazi KUPENDA au KUPENDWA, ila tazama wap UMEPENDA au UMEPENDWA!je eti nikweli kumpenda asie kupenda ni sawa na kusubiri boti airport

Majibu ya mkato ya kuchekesha Kutoka Kenya

Njeri: Roysambu ni ngapi?
Makanga: Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.

Odhis: Hii gari haina watu bana.
Makanga: Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ng’ombe?

Man: Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.
Makanga: Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.

Mwikali: Excuse me conda…gari za Mwingi zinapandiwa wapi?
Makanga: Ziliacha kupandwa juu hazimei.

Man: Kwani mwisho wa gari ni wapi?
Makanga: Mwisho ni hapo penye number plate iko.

Karis: Ruaka ni how much?
Makanga: Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.

Passenger: Shukisha dere.
Makanga: Tukishukisha dere utaendesha gari?

Johnny: Maze, hii gari iko na joto sana.
Makanga: Basi shuka upande fridge

Aina ya vyakula vinavyotakiwa kwa wajawazito

Kwa ajili afya ya mama na mtoto ni muhimu sana, mwanamke anatakiwa apate chakula bora kilicho na madini yote kama vitamini na protini. Mama mjamzito anatakiwa apate gramu 100 za protini kila siku. Ifuatayo ni mlo kamili anaotakiwa apate mama mjamzito kila siku ya ujauzito wake kwa afya bora.

Hivi ndivyo vyakula bora ambavyo mama mjamzito na mtoto wake wanastahili kula;

1. Jamii Kunde

Mbegu za kunde ni sehemu muhimu ya chakula kwa mama mjamzito kwa sababu huwa na kiwango kikubwa cha protini. Kwa watu wasiokula nyama au wana uwezo mdogo tu kujipatia nyama mbegu za jamii kunde zinatosheleza mahitaji ya protini. Hivi ni vyakula vya mimea kama Soya,Peas,Karanga, Alfa alfa,Mikunde, maharage.

2.Mayai

Mayai mawili kwa siku husaidia kuupa mwili protini, vitamini A na madini ambayo itasaidia kuzuia kupatwa na maradhi ya magonjwa mbali mbali.

3. Maziwa na vyakula vya jamii ya maziwa

Glasi nne au zaidi ya maziwa ya aina yoyote pamoja na/au vyakula vyenye jamii ya maziwa kama jibini, mtindi na siagi. Maziwa ni muhimu kwa protini, calcium, vitamini na virutubisho vingi. Vitasaidia ukuaji wa mifupa na misuli, Ni muhimu kwa damu yenye afya, kusaidia usingizi na kusawazisha mdundo wa moyo.

4. Viazi tamu

Viazi vitamu vina vitamini A ambayo husaidia ukuaji wa macho ya mtoto,ngozi na mifupa

5. Nyama

Nyama ya kuku au ngombe huwa na protini nyingi sana na husaidia katika ukuaji wa mwili wa mtoto hasa kwa mama mjamzito wa miezi minne

6. Nafaka na vyakula vya Wanga

Vyakula hivi huipa mwili nguvu ya kufanya kazi na pia ukuaji wa mtoto tumboni.Vyakula hivi ni kama mahindi,mtama ,mihogo,vyakula vya ngano kama mkate n.k.

7. Avocado

Ni matunda ambayo yana mafuta mengi maarufu kama fatty acid. Avocado inasaidia katika ukuaji wa ubongo,ngozi nyororo na ukuaji wa misuli ya mtoto tumboni.

8 .Mboga za majani

Mboga za majani kama spinach, kabeji, mchicha na matembele. Mboga hizi zinafaa ziwe zenye rangi ya kijani iliyokolea kwa sababu hizi ndizo zenye virutubisho vya kutosha. Mboga hizi zitampa mama na mtoto wake Vitamin A na B, pia virutubisho vitakavyosaidia mwili kupata protini ya kutosha, ukuaji wa mwili, na utengenezaji wa damu. Kutopata mboga za kutosha kunaweza sababisha mama kupata ugonjwa wa Anemia.

9. Mafuta ya samaki

Mafuta ya maini ya samaki huwa na Omega fatty acids ambayo inasaidia ukuaji wa ubongo na macho ya mtoto.

10.Maji

Maji ni muhimu kwa mwili kwa sababu inasaidia kwenye mmenyenyo na unyonywaji chakula na pia husaidia kuzia choo ngumu Maji pia huzuia uvimbe wa mwili na maambukizi ya mfumo wa mkojo(UTI)

Kweli shilingi yaua, Huyu jamaa kapatikana, angalia anachomjibu mke wake,

Jamaa alikuwa anagombana na mkewe,hatimae
akamwambia kwa ukali
“Unajua nimechoka sasa, haya kusanya nguo
zako na……..

Kabla hajamalizia sentensi simu
ya mkewe ikaita, kumbe alikuwa ni baba yake.
Basi mzee akaanza kuongea na binti yake huku
jamaa anasikia

“Aisee mwanangu nimebahatika kuuza ile
nyumba yangu sasa nimeona niwatumie milioni
20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio.
Haya mwambie yeye nitampigia kesho kama
ana mradi mwingine nimpe hela kidogo”.Baada
ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa
akamuuliza,”eeenhee!!! ulikuwa unasema
umenichoka nikusanye nguo zangu halafu
iweje? Jamaa kwa upole akajibu “Nilikuwa
nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue”.

Usiyoyajua kuhusu pesa haya hapa

Habari za Leo Rafiki yangu wa Muhimu sana. Ni furaha yangu kujua unaendelea vyema sana na majukumu yako.

Ni wakati mwingine tena tunaenda kujifunza pamoja juu ya mambo mbalimbali ili tuweze kufikia mafanikio kila siku. Leo tunakwenda kujifunza kuhusu pesa na utajua mambo mengi sana juu ya pesa.

Ni siri gani ipo ndani ya fedha na wengi hawaijui?

Kwanini watu wengi wanakua matajiri halafu wanapoteza utajiri wao wote na kuwa maskini tena?

Ulishawahi kuona watu maarufu wamekua na pesa nyingi lakini baada ya muda wanapotea na pesa zao zinapotea na kurudi kuwa watu wa kawaida kabisa?

Hujawahi kuona watu wakiuza mashamba ya urithi kwa mamilioni ya pesa na wakabadilisha aina ya maisha wanayoishi lakini baada ya muda pesa zinapotea na wanarudia hali yao ya zamani?

Hujakutana na vijana waliochimba madini wakajikuta wamepata mawe wakawa milionea lakini ghafla baada ya muda Fulani wanarudi kule kule walipokua?

Wengi wakiona hayo utawasikia wanasema pesa za mashamba hazika! Pesa za madini zina mashetani! Ni siri gani ipo kwenye hii pesa?

Inawezekana umeshajiuliza sana maswali haya na hata kuogopa kuwa nayo. Ukaamua kuwa mtu wa kawaida tu kwasababu ya hofu hizi zinazokujia unapofikiri kuwa tajiri kisha uje upoteze pesa zako zote!

Watu wengi wamekuwa na fikra kwamba pesa ni mbaya, zinaharibu watu, zinawafanya watu kuwa wachoyo, zinawafanya watu kuwa na tamaa pamoja na mengine mengi unayoyafahamu.

Ukweli ni kwamba pesa haina tatizo lolote pesa haina shetani wala pepo lolote linaloifanya imharibu mtu anapokuwa nayo nyingi. Pesa sio kiumbe hai. Pesa tunaitumia kununua bidhaa mbalimbali au kulipia huduma tunazozihitaji katika maisha yetu ya kila siku.

Ukweli kuhusu pesa ni huu hapa. Kwanza pesa haimbadilishi mtu bali inamfanya awe Zaidi ya vile alivyokuwa mwanzo yaani kama mtu alikuwa ni mchoyo akipata pesa atakuwa mchoyo maradufu, kama alikua mlevi akipata pesa anazidisha kuwa mlevi Zaidi.

Na wengine wakiwa hawana pesa kuna tabia nyingi wanakuwa nazo ndani zimejificha hawazionyeshi wakishapata pesa zile tabia zinafunguka na kuwa wazi.

Kama mtu alikuwa Malaya akipata pesa ndio utaona anaanza kubadilisha wanawake. Pesa zinabaki kuwa pesa na tabia za mtu zinabakia kuwa tabia za mtu.

Kama mtu alikua mtoaji akipata pesa atakuwa mtoaji Zaidi.
Kama alikua mcha Mungu akipata pesa atakwenda kuabudu Zaidi.
Hivyo pesa sio tatizo watu ndio wenye matatizo ndani yetu.

“Having more money won’t change you as a person. It will, however, magnify
the person you already are.” – Bob Proctor

Huwa napenda kuutumia mfano wa chombo. Watu wengi wanaopata pesa nyingi ghafla na kuzipoteza zote ni kama maji yaliyojaa kwenye ndoo utake kuyaweka yote kwenye kikombe cha chai.

Ukweli ni kwamba kikombe kitajaa lakini yale yaliyobaki yatamwagika yote chini hivyo hivyo na pesa zinazopatikana ghafla ni sawa na kuziweka kwenye kikombe ambacho ni uwezo wa akili yako.

Kama Akili yako bado haijaweza kupangilia milioni ishirini hivyo hata ukipewa leo zote zitapotea na zitabaki kile kiwango ambacho akili yako inaweza kutawala na kuendesha. Hivyo njia sahihi ya wewe kuweza kumiliki mamilioni ya shilingi na kubakia nayo ni kuanza kubadili ufahamu wako. Kuza ufahamu wako kidogo kidogo ili uweze kuendesha utajiri mkubwa. Na hili halitokei ndani ya siku moja ni kadiri unavyojifunza kila siku. Kwa kusoma vitabu na kufanyia kazi yale unayojifunza.

Jambo moja na muhimu la kufanya ni kutokuweka akili yako yote kwenye pesa. Usiweke malengo yako kwenye pesa unapofanya biashara unafanya ili upate pesa lakini siku zote pesa hazikai huwa zinaisha hivyo badala ya wewe kuweka nguvu zako na mawazo yako kwenye pesa weka Zaidi katika kuwasaidia watu kama unauza nguo kazana Zaidi katika kuwafanya watu wafurahie huduma yako pesa zitakuja.

Kama unatoa huduma hakikisha unatoa huduma bora ili kuvutia wateja Zaidi kila siku. Pesa utaziona kwako na zitaongezeka kila wakati.

Wekeza pia muda wako kwenye kutengeneza mifumo mbalimbali ambayo itakuwa inakuingizia pesa bila kuwa na kikomo. Unapotegemea mfereji mmoja wa kipato lazima utabakia pale pale siku zote.

Jambo la muhimu la kufanya ili uweze kubakia juu kwenye mafanikio siku zote ni kujifunza na kujijengea misingi ambayo itakuwezesha wewe usiyumbe na ubakie na utajiri wako.

Kuwa mwaminifu, kua mtoaji, wapende wengine, kuwa muadilifu, usidhulumu mtu, kabla hujafanya lolote angalia lina manufaa gani kwako na kwa wengine.

Nikutakie wakati mwema Asante sana kwa kusoma Makala hii.

Kisa cha kusisimua cha kijana na mke wake na mama yake

Kuna kijana mmoja daktari alikwenda kuposa. Binti aliyemposa akamuwekea masharti mazito. Akamwambia chagua mawili imma kunioa mimi au kukaa na mama yako, kwa sababu ukinioa mimi sitokubali mama yako aje hata harusini kwangu! Yule kijana aliemewa. Hakujua la kufanya. Mke anamtaka, lakini mama yake pia anampenda.

Hivyo aliamua kuomba ushauri kwa mwalimu wake wa chuo kikuu. Alimwambia: moyo wangu unampenda mno binti niliyekwenda kumposa, lakini pia siwezi kuishi mbali na mama yangu. Nifanye nini?

Yule mwalimu mwenye hekima ambaye alikuwa anajua tabu alizopitia mama wa kijana yule, alimjibu kwa kumwambia: Kabla ya kukueleza uchague yupi kati ya wawili hao, rudi nyumbani, na leo usifanye chochote, ila kuikosha mikono ya mama yako. Yule kijana alifanya kama alivyotakiwa na mwalimu wake. Alipofika nyumbani aliomba idhini kwa mama yake amruhusu kuikosha mikono yake, na yule mama alimkubalia bila ya ajizi yoyote.

Yule kijana alipoanza kuikosha mikono ya mama yake na kuona jinsi ilivyogugutaa kwa kazi za sulubu, alilia sana. Muda wote huu alikuwa hajawahi kuangalia viganja vya mama yake. *Je, na wewe umewahi kukaa na kuangalia viganja vya mama au baba yako kuona tabu walizopitia kukulea?* Kumbe baba wa yule kijana alifariki dunia yeye akiwa bado mdogo, yule mama aliamua kusamehe kila kitu kwa ajili ya mustakbali wa mwanawe. Alijitolea kufanya kazi za sulubu. Alikubali kuwa mtumishi wa ndani, kukosha nguo, kupiga deki na kila kazi ambayo alihisi ingelimletea chumo la halali bila ya kujali ugumu wa jkazu hiyo.

Juhudi zake zilizaa matunda na kufanikiwa kumlea na kumsomesha mwanawe hadi chuo kikuu na sasa ni daktari ambaye ana mustakbali mzuri. Baada ya yule kijana kukumbuka yote hayo, alifanya haraka kumpigia simu mwalimu wake huku macho yakiendelea kububujikwa na machozi akimwambia, siwezi kusubiri hadi kesho. Jibu nimeshalipata. Siwezi kumtupa mama yangu kwa ajili ya mtu asiyejua thamani ya mama. Ahsante sana kwa kunionesha njia sahihi! Kamwe siwezi kumuuza mama yangu kwa ajili ya leo yangu wakati yeye ameuza maisha yake yote kwa ajili ya mustakbali wangu.
NANI KAMA MAMA?!? Maa! Tabasamu lako ni ufunguo wangu wa ofanisi.
Kama umeipenda.

Share kwa wengine ili nao wazinduke.

Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Nia yako isishindwe

Nimejifunza jambo kubwa sana ambalo sote tuna lijua nalo ni “NIA”.
Nimemtazama mwendesha pikipiki anaiwasha pikipiki kwa muda mrefu kwa kupiga kiki kwa kurudia rudia, akiamini lazima iwake ili aende anakotaka kwenda. Anajaribu kuwasha kwa kiki ikikataa anajaribu kwa starter, ikigoma anajaribu kuchomoa plug na kuangalia kama kuna tatizo, anajaribu tena na tena mpaka inawaka, anaanza safari yake.

Ingawa ametumia muda mwingi kuhangaika kuiwasha pikipiki yake lakini hakuzimia moyo na kuamua kuitelekeza ili atembee kwa miguu, ila alikua na “NIA” isiyozimika haraka mpaka atakapoona imewaka kwakua anaamini jana iliwaka, lazima na leo iwake hata kama imelala kwenye hali ya hewa ya namna gani.

Ikiwa tunakua na “NIA” ya kufanya mambo madogo madogo yatokee, na tunayasimamia kwa “IMANI” kabisa mpaka yanakua kweli, kwanini tunaogopa kusimamia mambo makubwa yatokee maishani mwetu?. Kwanini unadiriki kusema kwenu hakuna aliyewahi kufanikiwa, hakuna anae miliki gari ya thamanani, hakuna aliyejenga nyumba ya kifahari, hakuna…hakuna….

Kwanini “NIA” yako uilinganishe na kushindwa kwa hao wengine kwenu? Wewe ni mmoja wa tofauti, na ukiamua kujitenga kifikra mbali nao, na kufanya mambo makubwa kwa bidii bila kuzimia moyo, hakika utakua wewe kama wewe kuitwa MABADILIKO ya mafanikio katika hao wengi walioshindwa.

“NIA YAKO ISISHINDWE”

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About