SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Sababu inayopelekea kushindwa kuishi maisha ya ndoto zako

1. Hauko Tayari kuthubutu na kujiunga
2. Kutokujiamini
3. Kutopata sehemu sahihi ya kupata ushauri
4. Kutokuwa na sababu za msingi au malengo ya msingi ya kupigania ndoto zetu
5. Kukaa katika shauli la wasio haki na barazani pa wenye mizaha

Hizo ni baadhi ya sababu zinazopelekea watu wengi kushindwa kuishi maisha ya ndoto zao na kuishi maisha ya kawaida tofauti na fikra zao.

Kuthubutu ni jambo la muhimu sanaaa katika maisha ya mwanadamu kwa maendeleo ya kwake ,familia ,jamii pamoja na taifa kwa ujumla hivyo ndugu zangu nawasihi tuweze kua watu wanaothubutu.

Tuondoe uwoga katika maisha yetu Kwamaana Uwoga Ndio CHANZO CHA UMASKINI WETU tukiendeleea kuogopa mazingira yanayotuzunguka na jinsi gani watu watatuchukulia na kutusema atutaweza kupiga hatua.

Changamoto ni hali ya kawaida katika maisha ya mwanadamu , kuogopa changamoto nalo ni Kosa kubwa katika maisha yetu.

…………..Mwisho kabisa nipende kusema……………

USIJILINGANISHE NA MTU MWINGINE MAANA JUA NA MWEZI HAVIFANANI VYOTE UNG’ARA KWA WAKATI WAKE. TENGENEZA MAISHA YAKO ILI WATU PIA WATAMANI KUWA KAMA WEWE.

Namna nzuri ya kuhudumia nywele zako za asili kirahisi

Kwa wale ambao tuna nywele asilia (natural hair), tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo. Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia, karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.

Katika mada ya leo, nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi. Je,unazifahamu nywele zako vizuri?Una nywele za aina gani? Zina tabia gani? Zinataka nini?

Zifuatazo ndizo njia ya kuzihudumia nywele zako;

1. Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.

Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi. Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.T atizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako. Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri. Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako,zielewe,ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

2. Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.

Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.

3. Linda unyevu wa nywele zako

Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache,pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

4. Zifahamu nywele zako

Yani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi. Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu .Unajuaje?

Chukua kikombe,kijaze maji safi.Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.

Chomoa unywele mmoja kichwani,hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.

Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena,basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida.

(Wala usihofu,zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka,tutajuzana.)Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa,ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.

Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.

Mbadala,unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya vuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.Inasaidia sana.

Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.

5. Mafuta ya Kupaka kichwani.

Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia. Kwangu mimi,mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana. Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya olive(extra virgin) na ya tea tree.

6. Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.

Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako. Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana. sio kitana. Chanuo kubwa(wide toothed comb).

7. Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.

Kama unataka zikue haraka, usizisumbue sana. Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu. Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo. Kuchana mara kwa mara zinapukutika,zinaanguka. Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.

8. Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.

Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi. Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24

Kukosa hela sio tatizo bali ndio kigezo ya kutafuta hela

Ukimonyesha mtu fursa akakwambia hana hela mwambie hiyo ndio sababu ya wewe kumonyesha fursa ili awe na hela tukumbuke kuwa hela haitokani na hela hela inatokana na fursa

Nijukumu la mtu asiye na hela kutafuta njia ya kuwa na hela watu wengi tunachelewa kufanikiwa kwa kutojua majukumu yetu ili kupambana na UMASIKINI mwombe Mwenyezi MUNGU kwa imani yako akufungue akili…

To ur Success!

Sababu ya jamaa kujiita fara ugenini

MZEE:”sasa huyu mgeni sijui alale wap?”
MKE:”saa hizi ni usiku akalale na Bebi.”
jamaa akaona huyo Bebi pengne mtoto anakojoa kitandani au akalia asije msumbua usiku
JAMAA:”msipate tabu mi ntalala hapa kwenye kochi” akalala
asubh wanakunywa chai akaibuka mrembo,jamaa akapigwa bumbuwazi almanusra ajimwagie chai.
BINTI:”Naitwa BEBI,we unaitwa nani?”
Jamaa akasema mimi naitwa Fara…..!

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂

Angalia wadada walivyoumbuka kwenye hii test

Ticha katangaza test , Akatoa Masharti; Ukiandika jibu hamna kufuta au kukata.

Swali la kwanza,
Taja vyakula vi3 ambavyo ukienda hotelini umelipiwa utapenda kula (marks 1)

WAVULANA wakajaza; wali, ugali, mihogo.
WADADA wakajaza; burger, pizza, egg chop. Swali la

2: Eleza jinsi ya kupika kila chakula ulichotaja hapo juu. (marks 99)
wacha wadada waanze kuhangaika kukata majibu ya mwanzo!

Tikiti maji kama dawa ya kutibu nguvu za kiume

Mbali ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ‘Potassium’, ‘Magnesium’ na virutubisho vingine kibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili (Sex libido) na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction).

Wanasayansi wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.

Tikitimaji lina kirutubisho aina ya ‘arginine’, ambacho huchochea uzalishaji wa ‘nitric oxide’ kwenye mishipa ya damu na hivyo kuongeza nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa ya Viagra.

Kazi nyingine zinazofanywa na tikiti maji katika mwili wa mwanadamu;

Huimarisha mishipa ya damu.

Vyakula vyenye kiwango kingi cha madini aina ya ‘Potassium’ kama vile Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali, huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.

Husaidia kupunguza uzito wa mwili.

Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji.

Huimarisha kinga za mwili.

Kirutubisho cha ‘arginine’ kilichomo kwenye Tikitimaji mbali ya baadhi ya kazi zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa kinga ya mwili.

Huondoa sumu mwilini.

Kuondoa ‘ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.

Tunda hili hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.

Ishara 10 za mwanamke aliyekuzimia na anayekupanda

Ishara hizi zinaweza zikakusaidia kumgundua msichana anayekupenda, wasichana wanatofautiana ila wengi wao wana-share ishara tofauti. Mwanamke anayekupenda hatakosa kati ya hizi

 

Siyo kwamba ishara hizi zote anaweza kuwanazo msichana mmoja, ila kila mmoja kwa ishara zake.

Ishara hizo ni kama ifuatavyo

1. Mnapokutana na kuongea

Msichana anayekupenda anakuwa na tabasamu unapoongea naye kama amekuzoea, ila kama hajakuzoea anapokuona gafla tabasamu hutoweka maana anakuwa na aibu. Hawezi akakuangalia machoni atakuwa anakuangalia kwa kuibia. Sikiliza sauti yake, kama anaona aibu sauti yake itakuwa ya upole/laini anaweza akaanza kushika shika nywele zake au kuweka sawa mavazi yake.

 

2. Ajali za kijitakia

Anaweza akatafuta sababu yoyote ilimradi tu akushike. Anaweza akaona kitu kidogo tu au mdudu halafu anakurukia, au anakukumbatia.

3. Anaibia kukuchunguza

Unapokuwa umetulia zako unakuta anakuangalia kwa kuibia, ukigeuka anajifanya yuko bize na mambo yake kumbe anakuchunguza taratibu.

4. Anapenda mgusane

Mwanamke anayevutiwa na wewe mnapotembea naye mahali anapenda kushika mkono wako, au unapokutana naye anaweza kukukumbatia.

 

5. Anatafuta ukaribu

Mwanamke aliyevutiwa na wewe anapenda kuwa karibu na wewe muda wote. Mfano akiwa na marafiki zake halafu mkakutana gafla atakufuata halafu waangalie marafiki zake utakuta kama wanateta, ukiona hali hiyo kuna siri yao yeye na marafiki zake kuhusu wewe. Anapokuwa na marafiki zake akikuona anaweza akajitenga, hata kama mmeenda out pamoja na marafiki
zake utakuta yupo karibu na wewe.

6. Anapenda umjali

Anapokuwa na tatizo au anajisikia vibaya lazima akuambie, mfano mmeenda mahali kukawa na baridi hata kama si baridi sana atasema anahisi baridi ili mradi umsaidie koti lako, hata kama kuna watu hawezi kuona aibu kuvaa badala yake atajisikia vizuri anapovaa koti lako.

7. Hawezi kuzuia tabasamu

Unapomwonyeshea tabasamu lazima na yeye akuonyeshee, hata kama kuna kitu kimemwudhi atakuonyeshea tabasamu ili mradi aonyeshe umemkuta katika hali ya furaha.

 

8. Ishara za mwili

Anapopita mbele yako anaweza akafanya madoido mengi ambayo yatakuvutia ila kama anajiamini. Kama hajiamini anapokuona gafla anakosa amani, utamwona anashtuka gafla.

9. Anafurahishwa na vituko vyako

Mwanamke anayekupenda daima ni mwenye furaha mkiwa pamoja. Huwezi ukamboa, hata kama ukifanya kituko ambayo haichekeshi utakuta anafurahia.

10. Anakujali

Anakuwa anakujali, mfano akiona umeumia labda umejigonga, yupo radhi akuhudumie. unapokuwa naye anaweza kuuliza “unahitaji chochote? unaweza ukasema “nina kiu ngoja ninunue maji” utamsikia “nina maji, kunywa haya yangu kwanza”.basi ujue kwamba anakujali.

Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE

Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke

Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.

MADHARA YA SHISHA

Yafuatayo ni madhara ya shisha;

1.Kansa
Licha ya kupita ndani ya maji, moshi wa shisha huwa na kiwango kikubwa cha carbon monoxide na nicotine ambazo humfanya mtumiaji awe kwenye hatari kubwa ya Kupata Tatizo la kansa ya koo, ama mapafu.

2.Matatizo ya Moyo
Moshi na tumbaku husababisha mishipa ya damu ya artery Kuziba, Matokeo yakemoyo hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi wake.

3.Huharibu Fizi (periodontal disease)
Hii hutokana na kuongezeka kwa kiasi cha sumu ya nicotine kwenye damu na fizi matokeo yake ni kuharibika kwa fizi na kupata matatizo ya meno.

4. Fangasi na Kifua kikuu (TB)
Kutokana na kutosafishwa vizuri kwa bomba za kuvutia shisha (hasa kutokana na wengi kujali kipato kuliko afya za watu) Mtumiaji hujiweka kwenye hatari kubwa ya Kupata magonjwa ya kuambukizwa kama fangasi, au hata vidonda vya tumbo kwa kuvuta kimelea cha helicobacteria.

5.Kuzaa Njiti (mtoto mwenye uzito mdogo)
Hii ni kwa wanawake wanaotumia shisha wakiwa wajawazito. Pia mtoto huyo ni rahisi kuwa na magonjwa yanayohusiana na upumuaji.

6. “Nicotine Addiction”
Hii ni hali ya kuwa mtumwa wa Sumu ya Nicotine. Mtumiaji wa shisha huvuta kiwango sawa cha nicotine kama mvutaji wa sigara hii husababisha sumu hii hatari kuingia kwenye damu yake, matokeo yake hataweza kuishi bila kutumia shisha au sigara.

7.Kupoteza Uwezo za Kujamiiana.
Utafiti unaonesha kuwa, wanawake wanaotumia shisha hupoteza hamu ya kujamiiana kwa kiasi kikubwa. Hali ni mbaya zaidi kwa wanaume kwani huchangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa nguvu za kiume.

8.Kuchakaa kwa ngozi.
Kama ilivyo kwa watumiaji wa sigara, matumizi ya shisha huchangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa ngozi. Mtumiaji wa muda mrefu wa shisha huzeeka haraka zaidi ya asiyetumia.

9.Asthma na Allergy Zingine
Uvutaji wa shisha huharibu utando laini uliopo kwenye njia za pua na koo, uharibifu huu unaweza kusababisha matatizo ya allergy, na asthma.

10.Kwa kuwa Haina Ladha kama ya sigara, watu wengi (hasa vijana) huona shisha ni mbadala mzuri wa sigara, bangi, na madawa mengine ya kulevya wakihisi haina madhara kumbe wanajiangamiza wenyewe!

Faida za kunywa juisi ya ubuyu

Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

Faida za kunywa juisi ya Ubuyu

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.

  1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
  2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
  3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
  4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
  5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afya zaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
  6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
  7. Huongeza nuru ya macho
  8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
  9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
  10. 10Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo

Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi.

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About