SMS, Vichekesho, Mahusiano, Biashara na Ujasiriamali, Afya, Chemsha Bongo, Dini pamoja na Vitabu kwenye PDF

Karibu AckySHINE

🤣😃😂

Chagua Unachotaka Kusoma Hapa

BURUDANI MAKALA DINI VITABU

Unahakikishiwa kusoma kitu kipya kizuri kila saa unapotembelea ukurasa huu.

Jinsi msongo wa mawazo unavyoweza kukusababishia ugonjwa wa moyo

Kila mmoja wetu anaweza kuwa na sababu tofauti inayoweza kumsababishia msongo (stress). Sababu kubwa ambazo husababisha msongo ni masuala ya kazi hata pia masuala ya kijamii. Masuala ya kikazi ni kama kutokuwa na furaha kazini, kazi nyingi, kufanya kazi kwa masaa mengi, kutokuwa na mipangilio bora, kutokujiwekea malengo na mengine mengi.

Masuala ya kijamii ambayo hupelekea msongo ni kama kupoteza mtu umpendaye, ndoa kuvunjika, kupoteza kazi, kuongezeka majukumu ya kifedha, magonjwa sugu, matatizo ya familia na mengineyo mengi.

Wakati mwingine msongo waweza kutokana na nafsi ya mtu mwenyewe na siyo sababu za nje ya mtu. Mfano mtu kujitengenezea mazingira ya kufikirika yanayoogofya yamleteayo wasiwasi na msongo.

Jinsi msongo wa mawazo unavyosababisha Magonjwa ya moyo

Watu walio na msongo (Stress) wanakuwa katika hatari zaidi ya kupata magonjwa ya moyo kuliko wale wenye utulivu, hii ni kwa mujibu wa wataalam na watafiti mbalimbali wanaohusiana na magonjwa ya moyo. Magonjwa haya ya moyo ni kama shinikizo la juu la damu, moyo kwenda mbio na mengineyo.

Matabibu wanafahamu kuwa, msongo wa ghafla waweza kusababisha magonjwa hatari ya moyo kama shambulizi la moyo. Watu wenye matatizo ya moyo hawana budi kuepuka hali ya msongo na kujifunza jinsi ya kukabiliana na maisha katika hali ya utulivu kwa kadiri iwezekanavyo.

Hivyo ili uweze kuepuka ugonjwa huu unachoptakiwa kufanya ni kuhakisha unaepuka visababishi vyote vya ugonjwa huu vya msongo, ambavyo nimekwisha vielezea hapo awali.

Faida na jinsi ya kutumia mbegu ya Parachichi kiafya

Leo nimekuletea matumizi ya mbegu ya parachichi yenyewe yaani ile inayokuwa katikati ya tunda la parachichi.

Kwanza mbegu ya parachichi huweza kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘antioxidants’ hii ni kutokana mbegu hiyo na kuwa na zaidi ya asilimia 70 ya kirutubisho hicho.

Kwa mujibu wa utafiti uliowahi kufanyika mwaka 2004 chini ya chuo kikuu cha Singapore na kuchapishwa katika Food chemistry walibaini kuwa mbegu hiyo inakiwango kikubwa cha antioxidants ikiwa ni pamoja na mbegu za matunda mengine kama vile embe, stafeli n.k

Mbegu hii ya parachichi pia huweza kuwasaidia wale wenye uhitaji wa kupunguza uzito kwani matumizi ya mbegu hiyo husaidia kuunguza mafuta mwilini na hivyo kupunguza uzito mkubwa mwilini.

Matumizi ya unga wa mbegu hizo pia husaidia kupunguza shida ya maumivu ya mwili hasa kwenye maungio yaani ‘joint’ za mwili.

Lakini pia kwa wenye shida ya maumivu ya viungo hivyo wanashauriwa kutumia hata mafuta ya parachichi yenyewe kwani huweza kutoa ahueni kwa haraka zaidi.

Pamoja na hayo pia mbegu za parachichi husaidia kurekebisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula tumboni.

Jinsi ya Kutumia

Saga mbegu ya parachichi kisha changanya na maji ya uvuguvugu kisha koroga vizuri na utumie mchanganyiko huo kutwa mara 2 kwa siku kwa muda wa wiki 2 mfululizo.

Jinsi ya kutibu chunusi kwa kutumia papai

Dawa nyingine madhubuti ya chunusi ni papai. Tunda hili ni moja ya matunda yanayotumika kwa ajili ya urembo hasa kwa wanawake.

Chukua papai na uchanganye na asali kidogo, likoroge kidogo na ujipake sehemu yenye chunusi moja kwa moja kwa dakika 15 hivi hivi kisha jioshe uso wako na maji ya moto kisha malizia na kujisafisha na maji baridi mra baada ya kutumia maji ya moto.

Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa wiki.

Mambo ya Kuzingatia ili uwe mrembo siku zote

Katika Jamii nyingi duniani, dhana ya urembo imekuwa na mitazamo tofauti kwa watu wengi. Kila mmoja anautafakari urembo kwa namna yake kulingana na malezi na tamaduni za mahali husika. Wako wanaoamini kuwa mrembo ni lazima awe na ngozi nyeupe, wengine hudhani kuwa ili kuonekana mrembo, lazima uwe na nywele ndefu, lakini pia wapo wanaodhani kwamba ili uwe mrembo ni lazima uwe na umbo namba nane na wapo wanaojua urembo ni kuwa mwembamba (kimbaumbau au Miss) au kuwa mrefu na wapo wanaoamini urembo ni kuwa mnene.

Hiyo yote ni mitazamo tu, lakini tafsiri halisi kutoka kwa wataalamu wa urembo ni kwamba; urembo ni hali ya kuwa na afya bora.

Je, Mpenzi msomaji ulikuwa unajua hili? Nakuomba Kabla hujafanya chochote kuhusu afya yako, unatakiwa kuamini kwamba wewe ni mrembo. Ikiwa utasimama katika hilo ni kweli utakuwa mrembo siku zote. Basi ili kubaki kuwa mrembo tujifunze haya machache leo ya kufanya:

1. SAFISHA NGOZI YAKO:

Hakikisha ngozi yako inakuwa safi muda wote. Unaweza kutumia njia mbalimbali kama vile kuondoa ngozi zilizokufa mara kwa mara. Kuondoa mafuta yaliyogandamana katika ngozi kwa kufanyia masaji ngozi yako ili kurahisisha mzunguko wa damu yako.
Ikiwa hili litafanyika kwa umakini ni wazi kuwa matatizo ya kuwa na chunusi au weusi katika ngozi yako havitakuwepo kwako.

2. SAFISHA NYWELE ZAKO:

Tumia bidhaa za nywele, ambazo zinaendana na nywele zako na hakikisha unazingatia mambo muhimu katika uboreshaji wa nywele zako.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kutokutumia vifaa vinavyounguza vywele.

Epuka kuosha nywele kwa maji ya moto, pia kuchana nywele zikiwa na maji, kwani unaweza kusababisha kukatika kwa nywele zako.

3. USIPAKE VIPODOZI MARA KWA MARA:

Tumia vipodozi pale inapobidi, usipendelee kutumia vipodozi mara kwa mara kwani wakati mwingine matumizi ya mara kwa mara ya vipodozi, husababisha madhara katika ngozi yako, hasa unapotumia bila kufuata maelekezo ya wataalamu.

4. PATA USINGIZI WA KUTOSHA:

Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku. Kwa mujibu wa wataalamu, unatakiwa kulala si chini ya saa nane kila siku. Ikiwa utapata usingizi wa kutosha ni wazi kuwa macho yako yataonekana yenye nuru siku zote. Pia utazidi kuonekana kuwa mrembo zaidi.

5. FANYA MAZOEZI YA VIUNGO:

Hakikisha mazoezi yanakuwa sehemu ya maisha yako, hii itasaidia kukufanya uonekane siyo tu mrembo, bali pia mwenye kujiamini.

6. SAFISHA MENO YAKO:

Usafi wa meno pia ni miongoni mwa mambo ya kuzingatia unapoamua kuboresha urembo wako. Hakikisha unapiga mswaki walau mara mbili kwa siku kila siku au kila baada ya kula.

Haya yameorodheshwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni mambo yanayochangia urembo wa asili na mvuto wa ngozi na mwili.

Jiwekee Utaratibu utakaokuwezesha kuamua vizuri juu ya fedha utakazopata

Jiwekee utaratibu utakaokupa uzoefu wa kuamua vizuri juu ya fedha unazopata. Watu tumekuwa tukitumia fedha tunazopata bila kufikiria jinsi ya kugawa ktk matumiz badala yake baada ya kutumia ndio una/ninaanza kujuta Kwa nin nime/umetumia tofauti na mahitaji uliyonayo. Kiasi cha fedha ulichonacho chaweza kukufanya uwe maskini au tajir kutokana na maamuz unayofanya juu ya hiyo fedha. Ukitaka ufanikiwe na ukue kifedha jaribu kugawa fedha uliyopata Kwa mafungu yafuatayo:

A. Sadaka: ndani ya sadaka kuna; a. malimbuko, mith 3:9, b. zaka na c. dhabihu malaki 3:8. Hii inakusaida wewe kumpa Mungu nafasi ya kwanza mth 6:33
2.pia unaonyesha ya kuwa unahitaji msaada na hekima zaid ktk kugawa fedha zilizobaki. Hagai 1:2-11
3. Shukrani Kwa Mungu alivyokuwezesha kumb torat 8:11-20 4. Unaonyesha unahitaj msaada wa Mungu ktk kupata mbinu za kuongeza fedha ktk maisha yako mith 3:9,10. Ktk bahasha hii waweza kuweka 10% au zaidi kutokana na Roho mtakatifu akavyokuongoza.

B. Akiba, Uwe na tabia ya kujiwekea akiba Kwa ajil ya baadae au ukiwa mzee, kumb torat 28:8 na mwanzo sura ya 41 hadi 47 tunamwona Yusuphu alivyoweka akiba 20% ya mavuno ktk miaka saba ya baraka ambayo ilisaidia ktk miaka saba iliyofuata ya ukame. Hii inajusaidia kuweka akiba Kwa ajil ya maisha ya baadae Kwa kiwango maalum na Kwa mda Fulani zab 144:13a. Jifunze Kwa Chungu anayeweka akiba ya chakula wakati wa jua ambacho humsaidia wakati wa ukame mith 6:6-8. Omba Roho mtakatifu akuongoze kuweka akiba ili utumie pind ambapo hutakuw na pato.
C. Kuwekeza ;hii inakusaidia ili kujijengea tabia ya kuwa na mtaji wa kukusaidia kuzalisha pesa zaid Kwa kuanzisha mradi mwingine Luk 19:12.
D. Matumizi yaliyo ya lazima. Mungu ana uwezo wa kutupa tunachohitaji ila Mungu anataka tuwe na mahitaji Tito 3:14. Haya in matumiz ya kila siku kama chakula etc.

Unaweza ukaongeza bahasha maalumu Kwa ajil ya kuweka au kutunza fedha za kulipia madeni /ujenzi/ada kama kuna wanaosoma/ kodi ya nyumba/ maandalizi ya harusi etc.
Kugawa fedha katika Mafungu ya bahasha inakusaidia kuwa na utaratibu maalum wa kutumia fedha na pia inakusaidia kufanya maamuzi mazuri ju ya kila fedha unayopata.

SWALI: Je, fedha unayopata unagawaje kabla ya kutumia? Je, Unakumbuka bahasha no. 4 tu, au 4 &3 au 4 &2 au 1 &4 au 1,2& 4 au 1,3 &4 au 1,2,3&4. In Roho wa Mungu atakayekuongoza kugawa fedha na sio vinginevyo.

Unaweza sema sina mtaji wa kutosha au sina biashara yoyote au nimejaribu kufanya biashara au kuwekeza cjafanikiwa etc, hivyo ni visingizio. Unapingiza visingizio au manung’uniko unapelekea kukataa tamaa na pia unamzuia Roho Mtakatifu kukusaidia kuvuka ktk hali hiyo.
Jifunze kutoka Kwa watumwa hawa waliopewa mtaji na bwana wao na jinsi walivyotumia kuzalisha. Kila mmoja alipewa kiasi kadri ya uwezo wa uwezo wa mtu vivyo hivyo walitofautiana kupata faida ingawaje mmoja wao aliamua kufukia na mwisho alinyang’anywa na kupewa yule mwenye zaidi, Luka 19:12-26 na mth 25:14-29.

Sababu ya meno kubadilika rangi

Wapo baadhi ya watu wanashindwa hata kuachia kicheko chenye bashasha hii ni kwa sababu meno yao yamekuwa na rangi, hivyo kuwafanya watu hao kuona aiabu. Pia watu wengi wakiona meno yana rangi ya njano hudhani ni machafu, meusi yanahitaji kusafishwa ili yawe meupe.

Meno kubadilika rangi huweza kuwa ni sababu moja au muunganiko wa sababu mbalimbali kama ifuatavyo;

Matumizi ya vyakula na vinywaji vyenye kaboni, sigara na mvinyo (wine) kwa muda mrefu husababisha kubadilika kwa rangi ya meno kwa juu (extrinsic staining).

Utumiaji wa maji yenye madini mengi ya fluoride katika kipindi cha utoto (dental fluorosis).

Matumizi ya dawa aina ya tetracycline kwa mama mjamzito ambaye tayari meno ya mtoto aliye tumboni yameanza kuumbwa lakini hayapata madini ya kutosha.

Maumbile yasiyo sahihi ya sehemu ya juu ya jino (amelogenesis imperfecta). Iwapo sehemu hii imeumbwa ikiwa laini kuliko inavyotakiwa huwa rahisi kufyonza rangi na jino huota likiwa limebadilika rangi au hubadilika baada ya muda.

Kufa kwa sehemu hai ya jino hasa kutokana na kuumia kwa jino au ajali (pulp necrosis), hali hii huweza huchukua miaka mingi mpaka kutokea kubalika rangi ya jino..

Jino liliozibwa kwa kutumia material aina ya amalgam huweza kubadilika rangi na kuwa nyeusi.

Mara nyingne jino lililotibiwa kwenye mzizi wa jino (root canal treatment ) huweza kubadilika rangi baada ya miaka mingi.

Kuna njia mbalimbali ambazo hutumika kuyafanya meno yaliyo na rangi isiyo ya kawaida kuwa meupe.

Njia hizi hutofautiana kati ya mtu na mtu kutokana na jinsi alivyoathirika. Kuna njia nyingi ambazo huweza kuyang’arisha kwa ndani (internal bleaching) au kuyangarisha kwa nje (external bleaching).

Endapo una tatizo la meno yaliyobadilika rangi, muone daktari wa kinywa na meno kwaajili ya ushauri na matibabu kwani kinywa kizuri na chenye afya huongeza kujiamini.

Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu

Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU” 😂😂😂 Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapo *Sipendagi Ujinga mimi* 🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽🚶🏽

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About