Ujumbe wa salamu kwa mpenzi kumjulia hali
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Furaha ni kawaida yangu, kununa si busara kwangu, kuishi nawewe vizuri ni sehemu ya Maisha yangu, kukusalimia ni hulka ya Moyo wangu, Uhali gani mpenzi?
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
Tambua kuwa nakujali
Furahia kwamba nitakuwa na wewe
Katika siku zote za maisha yangu
Nitakupenda bila kikomo milele
kama ni usafiri wewe ni gari salama,kama ni kiwanda wewe
ni namba moja ,kama ni maji kwako kuna chemchem,kama ni
mapenzi kwako nimefika,niahidi utakuwa nami siku zote
maishani mwangu.
Imani hufanya mambo yote yawezekane, Matumaini hufufua
yaliyopoteza uhai, lakini mapenzi hufanya mambo yote
yaonekane mazuri. Sina linalonihuzunisha maishani mwangu
kwa kuwa tunapendana!
nimetuma ndege wangu auzunguke ”moyo” wako kwa ” upendo
” auguse ”uso” wako kwa ”faraja” na mwisho
akunong’oneze sikioni taratibu kuwa nakupenda.
penzi linaweza kuelezewa kwa namna nyingi. Namna moja
niijuayo nikumtumia mapenzi hayo mtu asomaye meseji hii
Asali wa moyo wangu, fahamu kuwa unaweza kuamini kwamba
mwanga wa nyota unaweza kuunguza nyumba, jua linaweza
kusimama, lakini usiwaze hata siku moja kuwa naweza
kukuacha.
Mapenzi ni upepo,mimi sivumi na kupotea,mapenzi ni mahaba
sili nikamaliza,nikimaliza nitakula nini kesho?nakuahidi
kukupenda leo hata kesho ukiwepo na hata usipokuwepo.
Kama busu ni maji ningekupatia bahari, kukumbatia ni
majani, ningekupa msitu. Mapenzi ni maisha ningekupa yangu
bure.
Recent Comments