SMS kwa mpenzi kumwambia unampenda kwa moyo
unaweza ukafunga macho kwa usilolitaka kuliona lakini
hauwez kufunga moyo wako kwa Unalo Lipenda. Nakupenda
Mpenzi
unaweza ukafunga macho kwa usilolitaka kuliona lakini
hauwez kufunga moyo wako kwa Unalo Lipenda. Nakupenda
Mpenzi
mapenzi ni hisia zilizopo moyoni mwetu,hujidhihirishe pale
unapopata umpendaye,utamu wake ni zaidi ya sukari uchungu
wake ni zaidi ya shubiri je kwako yapo je?
yapitayo mdomoni yametokea moyoni ,uyaonayo hadharani
nimeagizwa na manani yakuridhishayo nafsini ni utamu wa
yakini.
moyo wangu saafi kama upole wa tausi wingi wa baridi kama maji ya mtungi ,yote ni kutokana na mapenzi unayonipatia. ASANTE KWA KUNIPENDA MPENZI
Nakupenda sana P tafadhari usinikasirikie, nimekukumbuka nahitaji kukuona unipoze moyo wangu, njooo mwandani wangu nakusubiri daktari wangu.
Lazima utakuwa mwizi sababu umeiba moyo wangu, umechoka
sababu unakimbia mara zote akilini mwangu, na labda mimi
sina shabaha sababu mara zote nikikulenga nakukosa.
Napenda ufahamu kuwa wewe ndiye nikupendae tu
Uzuri wako sio sababu ya mimi kukupenda
Ila nakupenda kwa matendo yako na jinsi ulivyoumbika.
Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata
ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
Recent Comments