Dondoo za Urembo na Mitindo

Mambo ya Kuzingatia ili uwe mrembo siku zote

Katika Jamii nyingi duniani, dhana ya urembo imekuwa na mitazamo tofauti kwa watu wengi. Kila mmoja anautafakari urembo kwa namna yake kulingana na malezi na tamaduni za mahali husika. Wako wanaoamini kuwa mrembo ni lazima awe na ngozi nyeupe, wengine hudhani kuwa ili kuonekana mrembo, lazima uwe na nywele ndefu, lakini pia wapo wanaodhani kwamba ili uwe mrembo ni lazima uwe na umbo namba nane na wapo wanaojua urembo ni kuwa mwembamba (kimbaumbau au Miss) au kuwa mrefu na wapo wanaoamini urembo ni kuwa mnene.

Hiyo yote ni mitazamo tu, lakini tafsiri halisi kutoka kwa wataalamu wa urembo ni kwamba; urembo ni hali ya kuwa na afya bora.

Je, Mpenzi msomaji ulikuwa unajua hili? Nakuomba Kabla hujafanya chochote kuhusu afya yako, unatakiwa kuamini kwamba wewe ni mrembo. Ikiwa utasimama katika hilo ni kweli utakuwa mrembo siku zote. Basi ili kubaki kuwa mrembo tujifunze haya machache leo ya kufanya:

1. SAFISHA NGOZI YAKO:

Hakikisha ngozi yako inakuwa safi muda wote. Unaweza kutumia njia mbalimbali kama vile kuondoa ngozi zilizokufa mara kwa mara. Kuondoa mafuta yaliyogandamana katika ngozi kwa kufanyia masaji ngozi yako ili kurahisisha mzunguko wa damu yako.
Ikiwa hili litafanyika kwa umakini ni wazi kuwa matatizo ya kuwa na chunusi au weusi katika ngozi yako havitakuwepo kwako.

2. SAFISHA NYWELE ZAKO:

Tumia bidhaa za nywele, ambazo zinaendana na nywele zako na hakikisha unazingatia mambo muhimu katika uboreshaji wa nywele zako.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kutokutumia vifaa vinavyounguza vywele.

Epuka kuosha nywele kwa maji ya moto, pia kuchana nywele zikiwa na maji, kwani unaweza kusababisha kukatika kwa nywele zako.

3. USIPAKE VIPODOZI MARA KWA MARA:

Tumia vipodozi pale inapobidi, usipendelee kutumia vipodozi mara kwa mara kwani wakati mwingine matumizi ya mara kwa mara ya vipodozi, husababisha madhara katika ngozi yako, hasa unapotumia bila kufuata maelekezo ya wataalamu.

4. PATA USINGIZI WA KUTOSHA:

Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku. Kwa mujibu wa wataalamu, unatakiwa kulala si chini ya saa nane kila siku. Ikiwa utapata usingizi wa kutosha ni wazi kuwa macho yako yataonekana yenye nuru siku zote. Pia utazidi kuonekana kuwa mrembo zaidi.

5. FANYA MAZOEZI YA VIUNGO:

Hakikisha mazoezi yanakuwa sehemu ya maisha yako, hii itasaidia kukufanya uonekane siyo tu mrembo, bali pia mwenye kujiamini.

6. SAFISHA MENO YAKO:

Usafi wa meno pia ni miongoni mwa mambo ya kuzingatia unapoamua kuboresha urembo wako. Hakikisha unapiga mswaki walau mara mbili kwa siku kila siku au kila baada ya kula.

Haya yameorodheshwa na wataalamu mbalimbali kuwa ni mambo yanayochangia urembo wa asili na mvuto wa ngozi na mwili.

Umuhimu wa kuvaa soksi

Miguu ni sehemu mojawapo inayotoa jasho sana hivvo ni vema kuiweka mikavu kuzuia ukuaji wa bacteria au fungus.Wakaka tunajua umuhimu wa soksi au tunavaa bila kujua na wengine hatuvai? Hii ni kwa wadada pia wanaovaa viatu kama raba au hata nyumbani. Ni vema sana kufahamu kwanini tunavaa soksi na mda mwingine soksi gani tuvae.

1. KUZUIA MAGONJWA YA NGOZI MIGUUNI.

Tumia sekunde tatu tu kuvaa soksi na ujikinge na maradhi haya ya fungus na bacteria, kama sio mpenzi was soksi nashauri ufikirie tena maamuzi yako ya kutovaa soksi.

2. EPUKA HARUFU MBAYA YA MIGUU

Image result for atletes foot
Kwa kweli hii ni kero kwako na wanaokuzunguka.Usipovaa soksi jasho lote la miguu litaenda kwenye viatu na ivo viatu kutoa harufu.Soksi hunyonya lile jasho na huzuia harufu iyo. Aya basi tushtuke aibu hii ya nini katika karne ya watanashati sisi.Tuvae soksi na kubadili kila siku.

3. LAINISHA NGOZI YA MIGUU YA YAKO

Nani hapendi miguu soft?? wadada kutwa kusugua miguu saloon.Simple ukirud nyumban kama sakafu ni ngumu vaa soksi zako nyepesi safi miguu iwe laini.Baadhi ya viatu pia vina surface ngumu kwa chini (wakaka) ukiweka soksi zako safi hamna maneno.

4. KUPUNGUZA MAUMIVU MIGUUNI

Hii hasa kwa watoto wadogo ..tuwazoeze mapema kuvaa soksi.Mtoto anatembea ndani Mara akanyage maji mara vitu vya ncha Kaliโ€ฆ.Pia kuna viatu ukivaa bila soksi lazima upate maumivu na kupata zile sugu nyeusi.

5. KUPATA JOTO NYAKATI ZA BARIDI

Wale was mikoa iliyo na baridi kwa sasa naamini tuna soksi za kutosha za miguuni na mikono.Kama kuna sehemu inayongoza kutoa joto ni miguuni na mikononi.Basi vaa soksi ili kuzuia joto lisipotee.

6. MVUTO

Ili sio geni, mi mtu akivaa viatu bila soksi kwa kweli napunguza maksi za utanashatiโ€ฆwengine wanasema kuna viatu vya kutovaa soksi. .hakuna kitu kama icho kuna soksi ndogo ambazo hazionekani kwa juu zimejaa tele madukani tutafte.Ebu mtu kavaa kiatu chake safi akiweka na soksi safi inaonekana mvuto lazima uwepoโ€ฆ.Nani hapendi kuvutia??basi sote tunapenda tuvae soksi

Siandiki mengi sana, soksi sio jambo geni, tubadilike tujijali,.Ok unavaa soksi Je?unavaa soksi pea moja mara ngapi, unafua na kukausha vizuri maana soksi mbichi ni janga jingine la uchafu na maradhi.Kitu kingine ujue aina ya soksi nyakati za joto usivae soksi ambazo ni nzito sana vaa nyepesi, ambazo ni nzito vaa nyakati za baridi. Na soksi za watoto tununue ambazo hazibani sana.

Jinsi ya kutunza kucha kujiepusha na maradhi shambulizi ya Kucha

Mikono, viganja na vidole ni kati ya sehemu muhimu katika mwili wa msichana. Mikono hutumika kufanya shughuli nyingi za nyumbani, shuleni na sehemu mbalimbali katika maisha kuanzia kutandika kitanda, kupika, kufanya usafi, kuandika, kujiremba pamoja na majukumu mengine mengi.

Mikono isipotunzwa vizuri ni rahisi sana kuharibika, kupoteza mvuto wake wa asili na kuharibu afya ya kucha. Hitaji la urembo wakati mwingine humsukuma msichana katika matumizi ya vipodozi vya kupaka kwenye kucha zake ili kukamilisha urembo wake.

Urembo wa vidole na kucha sio lazima ufanyike katika saluni au kwa wataalamu wa kupamba kucha, msichana anaweza kushughulikia afya na urembo wa vidole na kucha zake kwa gharama nafuu na kwa muda ambao mwenyewe anaona unafaa kufanya hivyo hata akiwa nyumbani.

Hii pia itamsaidia Msichana kuchagua vipodozi salama kwa afya ya kucha zake na mwili kwa ujumla. Ni jambo la muhimu kufahamu kuwa baadhi ya vipodozi vinavyotumika katika urembo wa kucha, vina rangi na sumu zisizofaa kwa afya. Sumu kama vile โ€˜Formaldehyde na Tolueneโ€™ zinazopatikana katika baadhi ya rangi za kucha zina madhara kwa afya ya msichana.

Ni kweli kuwa kucha nzuri huongeza urembo, mvuto na furaha ya msichana lakini pia ni busara kukumbuka kuwa afya ni muhimu kuliko urembo na uzuri. Afya ya mwili na kucha za msichana kwa ujumla hutegemea chakula bora chenye protein, madini na vitamini na siyo rangi na vipodozi.

Upungufu wa vitamini A, B Complex, proteni, madini ya chuma na chokaa (kalishiamu) mwilini husababisha kucha zipoteze afya yake ya asili. Kucha ambazo hazina afya zinaweza kuoza, kukauka, kupinda, kupasuka au kuwa na umbo kama kijiko. Magonjwa ya kuvu (fungus), na baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi pia huharibu afya ya kucha. Mojawapo ya athari za dawa za kupunguza makali ya VVU aina ya Zidovudine (ZDV) ni kucha kuwa na rangi nyeusi.

Kwa ajili ya afya bora ya kucha msichana anashauriwa kula mboga za majani, maharage, korosho, asali na matunda kwa wingi kila siku. Usafi wa kucha kila siku kwa kuziosha kwa maji ya uvuguvugu na sabuni laini pamoja na brashi ndogo ya mikono huimarisha afya ya kucha. Kucha pia zinaweza kusafishwa kwa maji ya mmea wa mshubiri (Aloevera), kitunguu saumu kilichopondwa pondwa au kitunguu maji kisha viganja na vidole vikaushwe vizuri na kupaka losheni.

Kucha za msichana zinatakiwa zisiwe ndefu ili kuepuka utunzaji wa vimelea vinavyosababisha magonjwa na kurahisisha utunzaji na usafi wa kucha. Kucha ndefu zinaweza kuwa chanzo cha hatari kwa afya ya msichana na familia yake hasa pale msichana anapohusika na uandaaji wa chakula cha familia. Katika familia nyingi, hasa familia za kiafrika wasichana ndio wanaobeba wajibu na majukumu ya kuandaa chakula cha familia.

Kwa afya nzuri ya kucha, msichana anashauriwa kukata kucha zake ili ziwe fupi kadri anavyotaka kwa kutumia โ€˜nail cutterโ€™ au mkasi mdogo au wembe mpya ambao haujatumiwa na mtu mwingine. Kuchangia nyembe za kukatia kucha si salama kwani kunaweza kuwa njia mojawapo ya kusambaza vimelea vya magonjwa hatari ya kuambukiza kama vile virusi vinavyosababisha UKIMWI na ugonjwa wa homa ya ini.

Ni vizuri kulainisha ncha za kucha baada ya kuzikata kwa kutumia tupa ya kucha (nail file) na kuzisugua kuelekea upande mmoja ili kuepuka kucha zisivunjike au zisisababishe michubuko ya ngozi wakati wa kujikuna. Kusugua kucha kwa kwenda mbele na nyuma kunaweza kusababisha kucha zivunjike kwa urahisi na haraka.

Kwa afya njema ya kucha, msichana pia anashauriwa asifungue pini za barua au kukwangua vocha za simu kwa kutumia kucha. Kucha zisikatwe kwa kutumia meno na zisilowekwe kwenye maji kwa muda mrefu hasa pale maji hayo yanapokuwa na kemikali au sabuni.

Kwa ajili ya afya njema ya kucha za miguuni, ni muhimu kuhakikisha kuwa, viatu kabla ya kuvaliwa vinakuwa vikavu na safi kabisa. Viatu visipotumiwa pia vihifadhiwe sehemu kavu isiyo na vumbi, maji au unyevunyevu ili kuepusha visiwe makazi ya kuvu (fungus)

Jinsi ya kuvaa viatu mbalimbali inavyotakiwa na ili upendeze

Viatu ni kinga kwa ajili ya kuhifadhi miguu. Vile vile viatu ni vazi ambalo linaongeza urembo na nakshi kwa mvaaji. Viatu vipo vya aina mbalimbali na vinavaliwa kulingana na mahali na mavazi yanayoambatana navyo. Tuangalie baadhi ya aina za viatu na wapi hasa na vipi vikitumika vinapendeza zaidi.

1.Viatu vya ngozi vya kufunika

Viatu vya kufunika vipo virefu sana, vyenye urefu wa wastani na vifupi kabisa. Mara nyingine haviwi vya ngozi kabisa bali ni kama vina plastiki na pia vingine huwa na uwazi mdogo kwa mbele.Viatu virefu zaidi mara hupendeza zaidi kuvaliwa kwenye sherehe na kanisani. Unaweza kuvaa kazini kama kazi yako haikulazimu kutembea tembea maana vitachosha miguu yako na kupunguza ufanisi.

Viatu vyenye urefu wa wastani unaweza kuvaa popote iwe kazini, kanisani, kwenye sherehe n.k. Viatu vya chini kabisa vinakuwa vyenye matumizi zaidi wakati unamatembezi mengi. Havifai sana kuvaa kwenye sherehe za usiku hasa kama unavaa nguo maalumu ya usiku. Vinafaa sana kwa mjamzito hasa katika miezi ya mwisho.

2.Viatu vya wazi virefu

Viatu hivi vipo vya aina mbili, vyenye rangi za mngโ€™ao na ambavyo ni mahususi kwa sherehe za usiku na vyenye rangi ngumu ambavyo waweza kuvaa kazini au kanisani. Viatu hivi vinapendeza kuvaliwa na nguo yoyote ila ikiwa ya urefu wa wastani ni nzuri zaidi maana huwezesha kuonekana urembo na uzuri wote wa kiatu. Viatu hivi vinakuja katika mitindo mbalimbali na unachagua ule ambao wewe unaupendelea zaidi mfano vyenye visigino vyembamba, visigino vinene au aina ya โ€˜wedgesโ€™.

3.Viatu vya wazi vifupi

Viatu hivi ni vizuri sababu vinawezesha miguu kupumua na kuโ€™relaxโ€™. Viatu hivi vipo vya aina tofauti tofauti na vinafaa sana kuvaliwa kwa matembezi ya jioni, wakati wa safari ndefu, wakati ukiwa na mizunguko mingi na pia hata kazini au kanisani pale unapokuwa umevaa nguo za kawaida (casual). Havivutii sana kuvaliwa na suti au nguo ya usiku. Pia mara nyingi viatu vya chini hupendezea kuvaliwa na nguo ndefu( hasa casual) na viatu virefu hupendeza zaidi kwa nguo yenye urefu wa wastani.

4.Viatu vya muda maalumu

Hivi ni viatu ambavyo vinavaliwa wakati wa kazi maalumu kama wakati wa kazi za mashambani, mgodini, wakati wa michezo au wakati wa baridi kali.

Ni vyema na inapendeza kama unauwezo uwe na viatu vya aina mbalimbali angalau aina tatu. Mfano viatu vyeusi vya urefu wa wastani, viatu vya usiku vya wazi, viatu vya chini vya kufunika na vya wazi.

Mambo ya kuzingatia kama una ngozi yenye Mafuta

Ngozi yenye mafuta kwa kawaida huwa inang’ara, nene na yenye rangi iliyotitia. Mara nyingi ngozi yenye mafuta mengi sana huwa na chunusi nyingi na vipelepele na mara nyingine huwa na chunusi zenye vichwa vyeusi. Katika aina hizi za ngozi mafuta hutokana na tezi za sebaceous na kuzalisha mafuta zaidi ya kiwango kinachotakiwa. Mafuta hayo husambaa katika ngozi na kuifanya iwe na mafuta mafuta.

Mafuta katika mwili yanatengenezwa na โ€˜sebaceous glandsโ€™,kwa hiyo kuna baadhi ya watu wana sebaceous glands ambazo zinatengeneza mafuta kwa wingi sana na hivyo kufanya ngozi zao kungโ€™aa kwa sababu ya hayo mafuta mengi.

Sebaceous gland zipo kwa wingi usoni(face) shingoni(neck), kifuani, kichwani na mgongoni, ndiyo maana hayo maeneo yanakuwa na mafuta kwa wingi.

Sababu zinazosababisha ngozi kuwa na mafuta:

  1. Kurithi.
  2. Lishe.
  3. Kiwango cha homoni mbalimbali mwilini.
  4. Ujauzito.
  5. Vidonge vya kuzuia mimba.
  6. Baadhi ya vipodozi.
  7. Hali ya hewa ya joto.

Namna ya kutunza ngozi zenye mafuta

Faida kubwa ya kuwa na ngozi yenye mafuta ni kuwa haizeeki kwa haraka ikilinganishwa na aina nyinginezo za ngozi. Miongoni mwa mambo yanayosaidia ili kuitunza ngozi yenye mafuta na kuiepusha na chunusi na hali isiyopendeza ni:-

Ngozi yenye mafuta inahitajia kusafishwa vyema kwa maji ya moto na sabuni ili kuzuia vinyweleo visizibwe na mafuta.

Epusha vifaa vigumu visikwaruze uso wako na kupelekea ngozi kubanduka, kwani suala hilo husababisha tezi za mafuta kufanya kazi zaidi ili kujaza sehemu iliyopotea ya mafuta.

Epuka kutumia vipodozi ambavyo huifanya ngozi yako ipoteze maji au kukauka. Kwani husababisha sehemu ya juu ya ngozi inyauke, na hivyo kusababisha mafuta kuziba vinyweleo na kupelekea kutokea vichwa vyeusi.

Jitahidi kuitunza vyema ngozi yako na kuisafisha vizuri. Jaribu kuosha uso mara mbili au tatu kwa siku. Usioshe mara nyingi kwani kufanya hivyo huufanya uso kutoa mafuta zaidi.

Chagua kile unachosafishia kwa makini, jiepushe kutumia cream nzito nzito au vifaa vugumu wakati wa kuosha uso wako. Ni bora utumie sabuni za kawaida zisizokuwa na madawa. Unaweza kutumia lotion ya kuua bacteria au sabuni zisizo na dawa nyingi (lightly medicated), au sabuni zenye madini mbalimbali. Ni bora usioshe au kutumia lotion au michanganyiko yenye alkoholi.

Tumia maji ya moto au ya vuguvugu wakati unaosha uso wako.

Wakati unapoosha uso wako, ukande kwa kutumia ncha za vidole, jiepushe kupaka sabuni moja kwa moja usoni, inaweza kuganda na kuzuia vinyweleo kuziba.

Kutumia mask za udongo (clay) na tope (mud) husaidia katika ngozi za aina hii. Ni bora utumie mask mara moja au mbili kwa wiki.

Jitahidi kutumia vipodozi vya uso ambavyo vimetengenezwa kwa ajili ya ngozi yenye mafuta.

Dawa za nywele zinazosababisha uvimbe kwenye Kizazi kwa wanawake

Dawa za kulainisha nywele (relaxer) zimekuwa zinapendwa na wanawake wengi wa Afrika kwa kuwa zina uwezo wa kulainisha nywele na kumfanya apendeze na awe wa kuvutia.
Hata hivyo, wataalamu wa afya wanadai kuwa dawa hizo zinasababisha uvimbe kwenye kizazi kutokana na kemikali za dawa hizo ambazo huingia mwilini kupitia majeraha au ngozi wakati wa kupaka.

Daktari wa Manispaa ya Ilala, Laurent Chipata alifanya utafiti na kubaini kuwa dawa za nywele na vipodozi zina kemikali ambazo husababisha uzalishwaji wa vichocheo kwa kiasi kikubwa na kusababisha uvimbe kwenye kizazi uitwao fibroids au leimyoma.

โ€œKemikali hizi hupenya kwenye ngozi na wakati mwingine hata kwa harufu tu, husababisha kuzalishwa kwa wingi wa vichocheo aina ya estrogen ambavyo huchangia kuota kwa uvimbe wa fibroids,โ€ anasema.

Dk Chipata anasema kukua kwa uvimbe kwenye kizazi hutokea katika kipindi ambacho mama yupo kwenye uzazi yaani kabla hajakoma hedhi.

Utafiti wa Dk Chipata ulifanywa nchini na kujumuisha wanawake wa kada tofauti tofauti wanaotumia dawa za nywele na wale wasiotumia na ukubwa wa tatizo hili ulibainika.

โ€œZipo kemikali tofauti tofauti zinazosababisha uvinbe kwenye kizazi, zipo za kwenye dawa za kilimo kama DDT na za kwenye mafuta ya ngozi kama vile mercury na hydroquionone,โ€ anasema.

Dk Chipata anasema madhara yanayopatikana katika kemikali za vipodozi ni makubwa siyo tu kwenye kizazi bali nyingine husababisha saratani au kufeli kwa figo. Anatoa mfano wa kemikali ya zebaki (mercury).

โ€œDawa za nywele zina madhara si lazima zipenye kwenye ngozi baada ya mtu kupata jeraha la kuungua bali zinaweza kupenya zenyewe kwenye ngozi kutokana na mfumo wa ngozi,โ€ anasema.

Anashauri kuwa ni vyema watu wakasoma kipodozi kimetengenezwa kwa nini kabla ya kukitumia na kuongeza kuwa ni salama zaidi kubaki na ngozi au nywele halisi badala ya kujibadilisha.

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekataza vipodozi vyenye kemikali kama biothionol, hexachlorophene, mercury, vinyl chloride, zirconium na bidhaa zenye aerosol, chloroquionone, steroids, methylene na chloroform.

Utafiti mwingine uliofanywa mwaka 2012 na Dk Lauren Wise na wenzake nchini Marekani na kuchapishwa kwenye jarida la afya la nchini Marekani ulibaini kuwa vipodozi vingi vina kemikali zenye vichocheo vya estrogen ambavyo kwa kawaida huchochea kasi ya kuota kwa uvimbe kwenye kizazi cha mwanamke na wakati mwingine kwenye mji wa mimba. Kitaalamu uvimbe au vivimbe hivi hujulikana kama fibroids au myoma.

Dk Wise anasema aliwafanyia uchunguzi wanawake wanaotumia dawa za kulainisha nywele na kuangali umri walioanza kutumia dawa hizo, mara ngapi, waliungua kiasi gani na walikaa na dawa hizo kichwani kwa kipindi gani.

Aliwafuatilia wanawake 23,580 wanaotumia dawa za kulainisha nywele na baada ya kipindi fulani walipimwa. Kati yao, 7146 waligundulika kuwa na uvimbe kwenye kizazi baada ya kupimwa kwa mionzi na wengine kufanyiwa upasuaji.

Kwa nini relaxer ni hatari kwa wanawake?
Dk Wise anasema mchanganyiko ulio kenye dawa za nywele hasa zilizoandikwa โ€œLye Relaxerโ€ ni sodium hydroxide wakati makopo ya dawa yaliyoandikwa โ€œNo Lye Relaxerโ€ yana calcium hydroxide na guanidine carbonate.

Bidhaa za kulainishwa nywele zilizoandikwa โ€˜no lye relaxerโ€™ zinadaiwa kusababisha majeraha kwa kiasi kidogo ukilinganisha na zile zilizoandikwa โ€œLye Relaxerโ€.

Jinsi ya kuchagua rangi sahihi wakati wa Kujipodoa

YAPO mambo mabalimbali katika tasnia ya urembo hasa katika vipodozi yanayopaswa kuzingatiwa katika kuboresha muonekano wa mtu.
Moja ya mambo hayo ni ujuzi na uelewa wa kutumia rangi katika kujipodoa kwani ni wanawake wachache wenye ujuzi huu.
Katika makala hii, nitakuelezea namna ya kuchanganya na kutofautisha rangi za vipodozi, lengo likiwa ni kuboresha muonekano wako.

Uchanganyaji wa rangi za vipodozi ni muhimu sana kwani katika kujipodoa, rangi zote za vipodozi unavyopaka zinatakiwa zioane ili kuleta muonekano ulio sawa na wa kueleweka.

Kwanza kabisa unatakiwa uwe makini katika kuoanisha rangi za vipodozi pamoja na rangi ya ngozi yako, hivyo katika hili unatakiwa kuwa na ujuzi maalumu ili usije ukafanya makosa na kuharibu muonekano wako.

Pia inabidi ufahamu hatua za upakaji vipodozi ili usije ukafanya vipodozi vingine visionekane katika uso wako.

Namna ya kuoanisha na kutofautisha rangi

Siku zote vipodozi vyako lazima viendane na mavazi yako ili kuleta maana zaidi kwa mfano, mara nyingi rangi ya mdomo โ€˜lipstickโ€™ huendana na vazi lako wakati shedo โ€˜eye shadowโ€™ zinatofautiana.

Kwa nguo za pinki

Katika mavazi haya, unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya pinki ambayo itaendana sawasawa na mavazi yako huku ukichanganya na shedo โ€˜eyeshadowโ€™, inaweza kuwa ya rangi ya bluu ili kuitofautisha na mavazi yako, hapo utakuwa sawa katika kanuni za urembo.

Vazi la kijani

katika vazi hili unatakiwa kupaka rangi ya mdomo yenye rangi ya kahawia huku ukichanganya na shedo ya rangi ya kijani au kahawia iliyoingiliana na pinki au rangi ya machungwa.

Kwa vazi la njano au kahawia

Katika vazi hili unatakiwa kupaka โ€˜lipstickโ€™ ya rangi ya kahawia iliyokolea, kwa upande wa shedo waweza kupaka ya rangi ya dhahabu.

Kwa vazi la bluu

Katika vazi hili unatakiwa kupaka โ€˜lipstickโ€™ yenye rangi ya pinki huku ukipaka shedo ya rangi ya bluu kwa mtindo huu utakuwa mwenye kuvutia siku zote.

Madhara ya Uvaaji wa Wigi au nywele Bandia

Katika miongo kadhaa iliyopita, uvaaji wa wigi umekuwa fasheni katika sekta ya urembo na hutumika hususani na wanawake. Ingawa uvaaji wa wigi huwafanya wanawake hao kuonekana mithili ya mtu aliyevaa kofia ngumu (helmet), lakini yaonekana ni mapendeleo ya wengi.

Wanaume wengi hujiuliza , “Ni kwanini kina mama hupendelea kuvaa wigi na kusuka nywele za bandia?, wakati hupendeza na kuwa warembo zaidi wakiwa na nywele zao za asili”?

Wigi huvaliwa zaidi na kinamama wenye asili ya Afrika au Wamarekani wa asili ya Afrika. Lakini tukiangalia moja ya chimbuko hasa la uvaaji wigi ni ubaguzi uliokuwepo wakati wa utumwa ambapo wale wenye ngozi nyeupe na nywele shombeshombe walipewa kazi za ndani na wale wasio na ngozi nyeupe na nywele zisizo shombeshombe walifanyishwa kazi ngumu za mashambani.

Watumwa waliopelekwa barani Amerika hawakuweza kuzihudumia nywele zao kutokana na hali ngumu, na mabwenyenye waliwashusha hadhi na kuwavunja moyo kwa kuwaambia hawakuwa na nywele bali ni “manyoya”.

Lakini sababu nyingine inayodhaniwa kuwaathiri wanawake wa asili ya Afrika ni fikra kuwa mwanamke mwenye nywele ndefu pengine hadi mgongoni ni mrembo zaidi. Pia siku hizi warembo na wanaoshiriki katika mashindano ya urembo hujaribu kurefusha nywele zao ili kuwa na viwango na aina za mitindo ya ughaibuni.

Pamoja na kuwa wanawake wanajaribu kuwa warembo kwa uvaaji wa wigi, zifuatazo ni baadhi ya hasara au madhara kiafya ya uvaaji wigi na usukaji wa nywele za bandia.

Uvaaji wa wigi au nywele za bandia waweza kukusababishia mzio (allergy), endapo malighafi au kemikali zilizotumika kutengeneza wigi hiyo zitasisimua mfumo wa kinga ya mwili wa mvaaji.

Kupata m-ba ni tatizo jingine kutokana na uvaaji wigi, hii hutokana na kukosekana kwa hewa ya kutosha ya Oksijeni katika ngozi ya kichwa (scalp hypoxia) na katika tishu za shina la nywele. Kwa hiyo kama utaamua kuvaa wigi uhakikishe imetengenezwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa na inapitisha hewa ya kutosha ya Oksijeni.

Pia waweza kunyonyoka nywele hata kama una nywele nzuri zenye afya, na kama utachagua kuvaa wigi na unataka kuepuka madhara hakikisha kuwa nywele zako ni safi, usilazimishe kuvaa wigi iliyo ndogo na yenye kubana sana, hakikisha unapata muda wa kupata hewa na nywele zako zinapakwa mafuta kuepuka ukavu wa ngozi ya kichwa na nywele kukatika .

Maumivu ya kichwa ni tatizo ambalo laweza kusababishwa na uvaaji wigi au usukaji wa nywele bandia. Wigi iliyo ndogo husababisha mkandamizo kichwani na kusababisha maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.

Upotevu wa muda na fedha ni dhahiri kwa kuwa ufumaji wa nywele za bandia waweza kuchukua muda mrefu, itamlazimu mvaaji wigi kubadili kwa kununua mpya kila baada ya muda fulani au kuwa na wigi nyingi kwa ajili kubadili kulingana na fasheni.

Harufu mbaya huweza kujitokeza endapo mba na jasho vitachanganyikana na hupelekea uwepo wa bakteria au fangasi na kusababisha muwasho mkali, hii yaweza kumkosesha raha mvaaji wigi na mwenye kufuma nywele za bandia hasa pale anapokuwa katika majumuiko ya kijamii.Kama utachagua kuvaa wigi hakikisha nywele zako zinasafishwa na shampoo au sabuni, zinakaushwa vizuri na kupakwa mafuta.

Endapo mwanamama atachagua kuvaa wigi,asisahau kuwa nywele zake za asili zinahitaji matunzo,na azingatie wakati wa kununua wigi au nywele za bandia, ahakikishe ananunua yenye ubora unaotakiwa ili kuepuka madhara ya kiafya anayoweza pata kutokana na uvaaji wigi au anapofuma nywele za bandia.

Benson Chonya

Uvaaji wa Tai kulingana na Umbo lako

Kuna mambo mengi ya kufanya ili tuwe watu wa kuvutia kila wakati.Mpangilio wa mavazi hufanya mtu kuonekana maridadi. Kama wewe ni mvaaji wa tai unapovaa unazingatia mambo yapi? Na je unafunga tai yako kwa namna inayokubalika?

Wengine huwa hawafahamu jinsi ya kufunga tai na hivyo kuleta mushkeri wakati wa kuvaa tai na kusababisha tai kukaa upande. Unapoamua kuvaa tai na shati ambalo halijanyooshwa ambalo linakuwa kwenye mikunjo au kuvaa tai na ndala unakuwa umeua maananzima na kulivunjia heshima vazi hili.

Tai ni vazi lawatu walio maridadi kama huwezi kuwa maridadi basi vazi hili halikufai kabisa.
Unapovaa taa unatakiwa kuzingatia aina ya umbo lako kama wewe ni mnene vaa tai inayoendana na mtu mnene na kama wewe ni mwembamba basi vaa tai inayoendana na mtu mwembamba.

Kuna wengine huvaa tai zinazofika magotini na kuwa kichekesho anapopita mtaani
Tai ni vazi ambalo huongeza heshima na hadhi ya mvaaji cha muhimu ni jinsi gani unavaa tai yako na ikiwezekana jaribu kumechisha tai na suruali kwa vile ili tai upendeze ni laima iendane na nguo unayovaa.

Ni vyema ukahakikisha kuwa unakuwa na tai zenye rangi tofauti ambazo zitaendana na nguo unazovaa.

Madhara ya kuvaa miwani ya Urembo maarufu kama miwani ya Jua

Miwani za urembo maarufu kama miwani za jua zimetajwa kuwa na madhara kwa watumiaji wake kutokana na watu kutofahamu saizi za namba ambazo wanapaswa kuzivaa kabla ya kununua.

Akifafanua kwenye kipindi cha Supamix kinachorushwa East Africa Redio, Daktari Ningwa wa Upasuaji wa macho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dk.Neema Daniel Kanyaro amesema watu wengi amekuwa wakivaa miwani pasipokjua kwamba zinaweza kuwasababishia matatizo ya kuona.

Dk. Kanyaro amesema kwamba watu wamekuwa wakivaa miwani za jua kama urembo pasipo kwenda kupima kujua ni aina gani ya miwani wanazotakiwa kuzitumia lakini pia bila kujua kama miwani hizo zina namba ambazo kila mtu ana namba kutokana na uono wake.

“Miwani ni dawa lakini usivae bila kupima kwani inaweza kukusababishia matatizo ikiwemo uoni hafifu. Unaweza kukuta unavaa miweani nyeusi lakini kumbe siyo namba yako. Kama hujijui unaweza kuta ukitazama unaona giza kumbe umeshaua macho kwa urembo” amesema.

Akizungumzia kuhsu presha ya macho Dk. Kanyaro amesema kwamba ugonjwa huo hauna dalili za moja kwa moja bali ni lazima kupima na huathiri watu wa rika zote.

Matumizi ya Asali kwenye Urembo wa ngozi na Nywele

Asali hutumika kulainisha Ngozi

Asali ina asili ya kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu hivyo ni faida kwa mtu mwenye ngozi kavu.

Jinsi ya kuandaa
Chukua asali mbichi kijiko kimoja cha chai kisha paka usoni, kaa nayo kwa dakika 15 hadi 20 kisha safisha uso wako.

Asali katika kusafisha ngozi, kutibu na kuzuia chunusi

Kutokana na uwezo wa asali katika kuua bacteria na kuvuta uchafu katika matundu ya ngozi asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.

Jinsi ya Kuandaa
Chukua asali mbichi Kijiko kimoja cha chakula changanya na mafuta ya nazi vijiko viwili changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara huku ukiepuka kufikisha machoni. ukimaliza kusugua uso na mchanganyiko wako osha uso wako.

Jinsi ya kuandaa kama kisafisha ngozi, exfoliator
Changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda. tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako. Asali inaongeza lishe na chembe chembe kuzuia madhara yanayotokana na sumu za hewani zinazozeesha ngozi. Baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi.

Asali inasaidia ngozi iliyoungua na jua kujirudi na kung’aa.

Jinsi ya kutumia asali katika nywele
Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani.

Jinsi ya kufanya
Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama conditioner kisha safisha nywele zako.

Unaweza kuchanganya asali kiasi cha kijiko kimoja mpk viwili katika maji vikombe vitano kisha safishia nywele zako taratibu, yaani yapitishe tu hayo maji kwenye nywele zako ambazo ni safi.

Tahadhari:ย Asali kwa kiasi kikubwa hupausha weusi wa nywele kutokana na Hydrogen Peroxide inayopatikana ndani ya asali.

Ni vema ukatumia asali mbichi kujihakikishia faida za asali katika mwili wako.
Iwapo unavutiwa na matumizi ya kitu cha asili katika urembo wako unaweza kuongeza kitu hicho katika kitu kingine unachotumia mfano katika steaming yako au scrub unayotumia.

Vipodozi Visivyo Salama/Vilivyopigwa Marufuku Na Madhara Yake

SEHEMU YA KWANZA

1.0 UTANGULIZI

Vipodozi visivyo salama ni vipodozi ambavyo vina kemikali zinadhuru au zinazoweza kuudhuru mwili na kuusababishia matatizo. Maana hii inaweza kuongezewa na kujumuisha vipodozi vyote ambavyo usalama wake unatia mashaka na vinaweza kuleta madhara kwa mtumiaji.

Hivyo hujumuisha :

-Vipodozi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
-Vipodozi vyenye viambata (kemikali) vya sumu na vilivyopigwa marufuku na mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA)
-Vipodozi ambavyo muda wake wa matumizi umeisha
-Vipodozi ambavyo havioneshi tarehe ya kuharibika (mwisho wa matumizi)
-Vipodozi ambavyo maelezo yake hayajaandikwa kwa Kiswahili au kiingereza

Vinaweza vikawa ni mafuta, losheni, krimu, pafyumu, poda na kadhalika.

1.1 VIAMBATA (KEMIKALI) VYA SUMU VILIVYOPIGWA MARUFUKU

Vingi vikiwa katika lugha ya kiingereza, hizi ndizo kemikali ambazo huongezewa katika vipodozi ili kufanikisha au kusaidia dhumuni lililolengwa kwa kipodozi husika. Viambato vyenye sumu vilivyopigwa marufuku ni:

  • Chloroquinone (Hydroquinone na kemikali zingine)
  • Steroids (Mifano ni Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol, na Dexamethasone)
  • Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo
  • Chloroform
  • Bithionol
  • Hexachlorophene
  • Mercury (Zebaki) na kemikali zinazotokana nayo
  • Vinyl chloride
  • Zirconium na kemikali zinazotokana nayo
  • Methyelene chloride
  • Halogenated salicylanilides (Dimetabromsalan, Trimetabromsalan na Tetrabromsalan)
  • Chlorofluorocarbons (Kwenye pafyumu na deodorants)

1.2 JINSI YA KUJUA KAMA KIPODOZI KINA KIAMBATO (KEMIKALI) CHA SUMU KILICHOPIGWA MARUFUKU

Angalia kwenye lebo ya kipodozi chako sehemu waliyoandika Ingredients au Contents au neno jingine lolote lenye maana ya Vitu vilivyomo ndani. Hapo angalia kama kuna kiamabato au kemikali yoyote ambayo nimeiandika hapo juu kuanzia namba 1 mpaka 12.

Kama kuna kiambato au kemikali ambayo imepigwa marufuku basi jua kipodozi chako sio salama. Acha kukitumia mara moja na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa Tanzania (TFDA).

Kama hakuna kiambato cha sumu basi kipodozi chako kinaweza kuwa salama. Tatizo linakuja pale watengenezaji wanapofanya uhuni kwa kudanganya au kuficha na kuacha kuandika baadhi ya viambato vilivyomo ndani. Ambalo pia ni kosa kisheria.

Mifano

  • Sabuni ya JARIBU ina kiambato MERCURY. Sabuni hii sio salama, haifai kwa matumizi na imepigwa marufuku.
  • Losheni/krimu ya MEKAKO ina kiambato HYDROQUINONE. Losheni/krimu hizi sio salama, hazifai kwa matumizi na zimepigwa marufuku
  • Krimu za FAIR & LOVELY SUPER CREAM, VISIBLE DIFFERENCE CREAM, SKIN SUCCESS FADE CREAM, DEMOVATE NA DIPROSON CREAM zina viambata Krimu hizi sio salama kutumika kama vipodozi na zimepigwa marufuku

SEHEMU YA PILI

2.0 MADHARA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA

Vipodozi visivyo salama vina madhara mengi sana kwa afya ya mtumiaji. Na kama mtumiaji ni mjamzito basi madhara hayo yanaweza kumpata na mtoto aliyepo tumboni.

Pia vipodozi hivi vina athari nyingi sana kiuchumi kwani vitapelekea mtu kutumia pesa tena kugharamia matibabu ya matatizo atakayopata. Madhara hayo ni pamoja na:

-Ugonjwa wa saratani (kansa) ya ngozi, maini, ubongo, mapafu, mfumo wa damu, utumbo mpana na kibofu cha mkojo
-Uharibifu wa ngozi, macho, ini, mapafu na figo
-Magonjwa ya moyo na kutopumua vizuri
-Kutokwa na chunusi kubwa kubwa
-Ngozi kuungua, maumivu makali, ngozi kuwa nyekundu na kutokwa na vipele
-Ngozi kuwa nyembamba sana na laini na endapo ngozi itapata jeraha au kufanyiwa upasuaji, kidonda kitachelewa kupona au hakitapona
-Mzio (Allergy) na muwasho wa ngozi
-Kichefuchefu, kutapika, kusikia usingizi na kizunguzungu
-Magonjwa ya akili, mishipa ya fahamu (hasa kichwani)
-Uharibifu wa ubongo na mtindio wa ubongo kwa watoto wachanga na waliopo tumboni
-Ngozi kuwa laini na kusababisha kupata magonjwa kama fangasi kwenye ngozi au maambukizi ya vimelea vya maradhi
-Kuchubuka kwa ngozi
-Ngozi kuwa na mabaka meusi na meupe au rangi mbalimbali
-Upofu, uziwi na upotevu wa fahamu wa mara kwa mara
-Kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu na kupoteza fahamu

2.2 USHAURI

Kama tulivyoona hapo juu mengi ya madhara ya vipodozi visivyo salama ni makubwa na huhatarisha kabisa afya za watumiaji na watoto. Hivyo ni vyema kuvijua na kuviepuka kabisa ili usiweze kupata madhara.

Pili msaidie kumuelimisha ndugu, jamaa na rafiki nay eye ajue na asitumie kabisa vipodozi visivyo salama

Pia ukiona mtu au duka ambalo linauza vipodozi visivyo salama acha kununua vipodozi kutoka kwake na toa taarifa kwa mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa

Epuka kabisa vipodozi visivyo salama. Hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.

SEHEMU YA TATU

3.0 ORODHA YA VIPODOZI VISIVYO SALAMA NA VILIVYOPIGWA MARUFUKU TANZANIA

Vifuatavyo ni vipodozi visivyo salama na vimepigwa marufuku kutumika. Epuka kabisa kutumia vipodozi hivi hata kama vinakuletea matokeo mazuri kiasi gani.

3.1 Krimu, Losheni na Jeli zenye kiambato cha Hydroquinone

  • Mekako Cream
  • Rico Complexion Cream
  • Princess Cream
  • Butone Cream
  • Extra Clair Cream
  • Mic Cream
  • Viva Super Lemon Cream
  • Ultra Skin Tone Cream
  • Fade-Out Cream
  • Palmerโ€™s Skin Success (Pack)
  • Fair & White Active Lightening Cream
  • Fair & White Lightening Cream
  • Fair & White Strong Bleaching Treatment Cream
  • Fair & White Body Clearing Milk
  • Maxi-Tone Fade Cream
  • Nadinola Fade Cream
  • Clear Essence Medicated Fade Cream
  • Peau Claire Body Lotion
  • Reine Clair Rico Super Body Lotion
  • Immediate Claire Maxi โ€“Beauty Lotion
  • Tura Lotion
  • Lkb Medicated Cream
  • Crusader Skin Toning Cream
  • Tura Bright & Even Cream
  • Claire Cream
  • Miki Beauty Cream
  • Peau Claire Crรจme Eclaircissante
  • Sivoclair Lightening Body Lotion
  • Extra Clair Lightening Body Lotion
  • Precieux Treatment Beauty Lotion
  • Clear Essence Skin Beautifying Milk
  • Tura Skin Toning Cream
  • Madonna Medicated Beauty Cream
  • Mrembo Medicated Beauty Cream
  • Shirley Cream
  • Kiss โ€“ Medicated Beauty Cream
  • Uno21 Cream
  • Princess Patra Luxury Complexion Cream
  • Envi Skin Toner
  • Zarina Medicated Skin Lightener
  • Ambi Special Complexion
  • Lolane Cream
  • Glotone Complexion Cream
  • Nindola Cream
  • Tonight Night Beauty Cream
  • Fulani Cream Eclaircissante
  • Clere Lemon Cream
  • Clere Extra Cream
  • Binti Jambo Cream
  • Malaika Medicated Beauty Cream
  • Dera Heart With Hydroquinone Cream
  • Nish Medicated Cream
  • Island Beauty Skin Fade Cream
  • Malibu Medicated Cream
  • Care Plus Fairness Cream
  • Topiclear Cream
  • Carekako Medicated Cream
  • Body Clear Cream
  • A3 Skin Lightening Cream
  • Ambi American Formula
  • Dream Successful
  • Symba Crรจme Skin Lite โ€˜Nโ€™ Smooth
  • Cleartone Skin Toning Cream
  • Ambi Extra Complexion Cream For Men
  • Cleartone Extra Skin Toning Cream
  • Oโ€™nyi Skin Crรจme
  • A3 Triple Action Cream Pearlight
  • Elegance Skin Lightening
  • Clere Cream
  • Clear Touch Cream
  • Crusader Ultra Brand Cream
  • Ultime Skin Lightening Cream
  • Rico Skin Tone Cream
  • Baraka Skin Lightening Cream
  • Fairlady Skin Lightening Cream
  • Immediate Claire Lightening Body Cream
  • Jaribu Skin Lightening Lotion
  • Amira Skin Lightening Lotion
  • A3 Clear Touch Complexion Lotion
  • A3 Lemon Skin Lightening Lotion
  • Kiss Lotion
  • Princess Lotion
  • Clear Touch Lotion
  • Super Max-Tone Lotion
  • No Mark Cream
  • Body Clear
  • Top Clear
  • Ultra Clear
  • Peau Claire Lightening Body Oil
  • G &G Dynamiclair Lotion
  • G & G Teint Uniforme
  • G & G Cream Lightening Beauty Cream
  • Dawmy โ€“ Lightening Body Lotion
  • Maxi White Cream
  • Bioclare Lightening Body Lotion

3.2 Vipodozi vingine vyenye Hydroquinone

  • Fair & White Powder (Exclusive Whitenizer & Serum)
  • New Youth Tinted Vanishing Cream
  • Skin Success Fade Cream Regular
  • Teint Clair Clear Cpmplexion Body Lotion
  • Mareme Cream
  • Si Clair Plus Cream
  • Clair & White Body Cream
  • Body White Lotion
  • Bio Claire Cream
  • Forever Aloe MSM Gel
  • Kroyons Baby Oil
  • 3.3 Sabuni zenye kiambato cha Hydroquinone
  • Body Clear Medicated Antiseptic Soap
  • Blackstar
  • Cherie Claire Body Beauty Lightening & Treating Soap
  • Immediate Claire Body Beauty Soap
  • Lady Claire
  • G.C Extra Clear
  • Top Clear Beauty Complexion Soap
  • Ultra Clear
  • 3.4 Vipodozi vyenye Hydroquinone pamoja na Steroid
  • Clear Essence Skin Beautifying Milk For Sensitive Skin
  • Fair & White Clarifiance Fade Cream
  • Fair & White Exclusive Whitenizer Body Lotion
  • Fair & White Exclusive Whitenizer Cream
  • Fair & White Exclusive Whitenizer Gel
  • Fair & White Maxitone Lightening Lotion Sun Block
  • Fair & White So White Skin Perfect Gel

3.5 Sabuni zenye kiambato cha Mercury (Zebaki) na michanganyo yake

  • Movate Soap
  • Miki Soap
  • Jaribu Soap
  • Binti Jambo Soap
  • Amira Soap
  • Mekako Soap
  • Rico Soap
  • Tura Soap
  • Acura Soap
  • Fair Lady
  • Elegance
  • Block & White Skin Whitener Germicidal Bath Soap
  • Rose Beauty Soap
  • Maxi-Tone Soap (Skin Lightening Soap)
  • Margostara Soap (New Tannin)
  • Rusty โ€“ Whitening Soap (New Formula)
  • Emani Natural Fair Pearls Soap

3.6 Krimu zenye kiambato cha Mercury na michanganyiko yake

  • Pimplex Medicated Cream
  • New Shirley Medicated Cream

3.7 Krimu zenye Steroids (Betamethasone, Beclomethasone, Hydrocortisone, Clobetasol,

Dexamethasone nk)

  • Amira Cream
  • Jaribu Cream
  • Fair & Lovely Super Cream
  • Neu Clear Cream Plus (Spots Remover)
  • Age Renewal Cream
  • Visible Difference Cream (Neu Clear Spots Remover)
  • Body Clear Cream
  • Sivo Clair Fade Cream
  • Skin Balance Lemon Cream
  • Peau Claire Cream
  • Skin Success Cream
  • M & C Dynamic Clair Cream
  • Skin Success Fade Cream
  • Fairly White Cream
  • Clear Essence Cream
  • Miss Caroline Cream
  • Lemonvate Cream
  • Movate Cream
  • Soft & Lovely Cream
  • Mediven Cream
  • Body Treatment Cream (Spots Remover)
  • Dark & Lovely Cream
  • Sivo Clair Cream
  • Musk โ€“ Clear Cream
  • Fair & Beautiful Cream
  • Beautiful Beginning Cream
  • Diproson Cream
  • Demovate Cream
  • Top Lemon Plus
  • Lemon Cream
  • Beta Lemon Cream
  • Tenovate Cream
  • Unic Clear Super Cream
  • Topifram Cream
  • First Class Lady Cream

3.8 Vipodozi vingine vyenye kiambato cha Steroid

  • Fashion Fair Gel Plus
  • Hot Movate Gel
  • Hyprogel
  • Mova Gel Plus
  • Secret Gel
  • Secret Cream
  • Peau Claire Gel Plus
  • Hot Proson Gel
  • Skin Success Gel Plus
  • Skin Clear Gel Plus
  • Soft & Beautiful Gel
  • Skin Fade Gel Plus
  • Ultra โ€“ Gel Plus
  • Zarina Plus Top Gel
  • Action Demovate Gel Plus
  • Prosone Gel
  • Skin Balance Gel Wrinkle Remover
  • TCB Gel Plus
  • Demo โ€“ Gel Plus
  • Regge Lemon Gel
  • Ultimate Lady Gel
  • Topifram Gel Plus
  • Clai & Lovely Gel
  • Fair & White Serum Exclusive Whitenizer
  • Maxi White Lightening Body Milk
  • Maxitone Cleansing Milk
  • Avoderm Cream
  • Niomre Cream
  • Niomre Lotion
  • Nyala Lightening Body Cream
  • Si Clair Cream
  • Cute Press White Beauty Lotion
  • White SPA Rose Lotion
  • White SPA UV Lightening Cream

3.9 Vipodozi vya kupunguza unene vilivyopigwa marufuku

  • Bio Valley Sliming Gel

3.10 Vipodozi vya nywele vilivyopigwa marufuku

  • African Gold Super Glo
  • Sofn Free Hair Foodblue Cap Shampoo
  • Marhaba Anti-Dandruff Hair Cream
  • Blue Cap Spray
  • Blue Cap Cream

3.11 Vipodozi vinginevyo vilivyopigwa marufuku

  • Bio Light Cream
  • Salon Dermaplex Amazon Clay 9Normal To Dry Skin)
  • Beauty Secrets Body Cream
  • Swiss Soft N White Lightening Gel
  • Whitening Complex Mask

3.12 Vipodozi Vinavyosababisha muwasho vikitumika karibu na macho

  • Eye Shadow Gel
  • Eye Shadow Gel 02
  • Eye Shadow Gel 07
  • Eye Shadow Gel 08
  • Eye Shadow Gel 09
  • Eye Shadow Gel 10

TAHADHARI : VIPODOZI VISIVYO SALAMA VIPO VINGI ZAIDI YA HIVYO AMBAVYO VIMEORODHESHWA HAPO JUU NA VINGINE VINGI ZAIDI VINAWEZA VIKAFIKA SOKONI.

Mara zote kuwa makini na vipodozi na pata taarifa, elimu na ushauri kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wataalam wa afya, urembo na vipodozi.

Mambo ya Kuzingatia ili uwe na ngozi laini

Takribani kila mtu angependa kuwa na ngozi laini, au hata laini zaidi. Watu wengi wamekuwa wakiitafuta ngozi nzuri au kujitahidi kuitunza ili isiharibike. Lakini je, wamefanikiwa?
Wachache hufanikiwa na wengi hushindwa. Na hata hao waliofanikiwa wengi wao hutumia vipodozi vikali ambavyo vingi huchubua na kuharibu ngozi zao na kuwaletea madhara makubwa sana baadae.

Vipi wewe, ungependa kuwa na ngozi nzuri bila kuidhuru afya yako? Karibu somo la leo ili uweze kuwa na ngozi nzuri bila kuidhuru afya yako.

Ngozi laini ni nzuri na inaongeza mvuto wa mwili. Ulaini wa ngozi hupotezwa na mambo mbalimbali kama vile seli za ngozi kupungukiwa na maji na kuanza kusinyaa na kunyauka, seli za ngozi kujeruhiwa, na seli za ngozi kufa. Matokeo yake ni michirizi, makunyanzi, makovu, chunusi, madoa, ngozi kufubaa na kuzeeka.

Kuifanya ngozi kuwa laini unahitaji kuupatia mwili virutubisho vyote vya kujenga mwili vizuri na kunywa maji ya kutosha ili seli zisikauke, kusinyaa wala kunyauka. Kula mlo kamili, matunda mengi na kunywa maji ya kutosha.

Pia unahitaji kuepuka jua kali ambalo litaunguza ngozi, kuikausha na kuifanya iwe na makunyanzi na vitu vingine vinavyoota kwenye ngozi kutokana na jua.

Tumia vipodozi vizuri vinavyosaidia ngozi kuwa laini bila kuidhuru. Hapa kuna vipodozi vya aina mbali mbali na vinavyofanya kazi kwa njia mbali mbali. Vipodozi vya muhimu ni

  1. Vipodozi vya kuongeza unyevu au maji kwenye (seli za) ngozi
  2. Kwa kiingereza vinaitwa โ€œMoisturizersโ€. Hivi hufanya kazi ya kufunika ngozi na kuzuia maji yasipotee kutoka kwenye ngozi, na pia husaidia kuongea maji kuingia kwenye seli za ngozi. Vipo katika mtindo wa sabuni, mafuta na losheni.
  3. Vipodozi vya kusaidia kuongeza kasi ya kuzalishwa kwa seli mpya za ngozi
  4. Hivi husaidia kuzalisha seli mpya za ngozi ambazo zitaleta ngozi mpya na nzuri na kuondoa ile ya zamani iliyochoka na kuzeeka. Mifano ni losheni na krimu zenye Vitamini A na Vitamini E.
  5. Vipodozi vya kusaidia kuondoa uchafu na seli (ngozi) zilizozeeka au kufa

Tumia sabuni zenye uwezo mkubwa wa kuondoa uchafu kutoka kwenye ngozi, na ukiweza tumia โ€œface washโ€ au โ€œfacial cleansersโ€. Hivi husaidia kusafisha kabisa ngozi na kuondoa uchafu.

Kwa upande wa seli zilizokufa na kubaki juu ya ngozi tumia โ€œscrubโ€. Scrub hufanya kazi kwa kuondoa seli zilizoharibika na zilizokufa na kuacha seli changa na ngozi nzuri.

USHAURI:

  1. Pata ushauri wa kulainisha na kupendezesha ngozi yako kutoka kwa wataalam wanaojua vizuri afya, urembo na vipodozi. Utashauriwa vizuri jinsi ya kufanya, vipodozi vya kutumia na jinsi ya kuvitumia vizuri kwa matokeo mazuri zaidi. Epuka wauza vipodozi wasio waaminifu au wasiovijua vizuri vipodozi, maana wanaweza kukupa vipodozi vya tofauti na mahitaji yako au vipodozi vinavyodhuru afya yako.
  2. Safisha ngozi yako vizuri, kila siku. Hakikisha unaondoa uchafu na vijidudu vyote vinavyotua na kukaa juu ya ngozi yako. Ondoa vumbi, seli zilizokufa, mafuta ya ziada, jasho nk Lala na pumzisha ngozi yako kiasi cha kutosha ili iweze kujitengeneza na kuwa nzuri. Ipumzishe kila siku kwa matokeo mazuri zaidi. Pata usingizi wa kutosha na ulio bora
  3. Tumia vipodozi vizuri vyenye uwezo wa kukupa matokeo mazuri unayoyataka na visivyodhuru afya yako. Pata ushauri mzuri kutoka kwa wataalam ili uweze kufanikisha hili vizuri. Tumia vipodozi vinavyoendana na ngozi yako. Kama ngozi yako ni kavu tumia vipodozi ambavyo ni maalum kwa ajili ya ngozi kavu, na kama ngozi yako ni ya mafuta basi tumia vipodozi ambavyo ni mahususi kwa ajili ya ngozi ya mafuta.
  4. Usitumie vipodozi vinavyoharibu ngozi na kuihatarisha ngozi yako. Epuka vipodozi vyote visivyo salama na vile visivyoendana na ngozi yako.
  5. Jihadhari na michubuko au majeraha mengine yoyote yatakayoweza kuharibu ngozi yako. Hii ni kwa sababu michubuko na majeraha hayo yatakuharibia uzuri wa ngozi yako na pia yatakuachia makovu baada ya kupona
  6. Kuwa na furaha, amani na tabasamu itakusaidia pia kuwa na ngozi nzuri, hususan ngozi ya usoni.

Jinsi ya kuondoa kitambi Kitaalamu

Hapo zamani kidogo tuliona na tulishuhudia watu wakisema ya kwamba mwanaume ambaye ana kitambi ndiye ambaye mwenye fedha, hiyo ni imani ambayo ilijengeka katika fikra na mitazamo yetu. Lakini katika karne hii mambo yamebadilika baada ya kuona baadhi ya madaktari wakieleza kwa kina ya kwamba kuwepo matumbo makubwa tanatokana na uwepo wa mafuta mengi katika kuta za tumbo.

Na mafuta hayo pindi ambao yanazidi huwa na athari sana kiafya, athari hizo za kiafya hupelekea mtu kuweza kupata magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu na magonjwa mengine mbalimbali.

Hivyo ili kuepukana na athari hizo zitokanazo na kitambi nakusihi ufanye yafuatayo:

1. Chakula

Huu ni msingi mwingine muhimu sana katika harakati za kupunguza unene na tumbo, kwa kifupi unahitaji kuzingatia yafuatayo:

  1. Kula mboga za majani kwa wingi kwani husaidia sana kiafya.
  2. Kunywa maji mengi sana
  3. Weka chakula cha kukutia hamu mbali na nyumba yako
  4. Kula vyakula ambavyo vitatumika kwa kiwango kikubwa katika kujenga mwili wako ila epuka kula vyakula vyenye mafuta kwa wingi.

2. Mazoezi ya viungo husaidia kupunguza tumbo.

Kwa kiwango kikubwa Unaweza kufanya mazoezi ya aina nyingi ili kupunguza tumbo. Mazoezi yoyote ya nguvu yatapunguza mafuta ya mwili wako pamoja na mafuta ya ndani (visceral fat).
Mazoezi ambayo nayazungumzia ni mazoezi ambayo yanasaidia kukata tumbo kwa kiwango cha juu sana. Mazoezi haya kwa karne hii ya teknolojia yapo wazi katika video mbalimbali.

Hivyo jaribu kutafuta video mbalimbali ambazo zitakusaidia kwa kiwango kikubwa katika kukata tumbo.

3. Hakikisha unapata usingizi Wlwa kutosha kwa siku.

Kupata usingizi kwa muda mzuri kumeonyesha kuwa na mchango katika kudhibiti kiwango cha mafuta katika mwili wa binadamu. Katika utafiti mmoja, watu waliopata usingizi kwa saa 5 hadi 7 kwa siku katika kipindi cha miaka 5, walionyesha kuwa na mafuta mwilini kidogo zaidi ukilinganisha na wale waliopata usingizi kwa pungufu ya saa 5 kwa siku.

Hivyo hakikisha unatenga muda wa kupumzika hasa pale unapokuwa una usingizi.

Jinsi ya kufanya ili uwe na umbo dogo la kuvutia

Unaweza kujiuliza, hivi inawezekanaje kuwa na umbo dogo la aina hii? Ukweli ni kwamba inawezekana, lakini inahitaji kazi ya ziada kufikia kwenye lengo hilo.

Unalifahamu umbile la sifuri au saizi zero?

Kwa wale wanaojali maumbo ya kupendeza saizi zero linatafsiriwa ni kuwa na kiuno kisichozidi inchi 23, nyonga 32 na kifua 31. Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni mazoezi na ulaji wako, kwa kuwa mwangalifu katika kiasi cha kalori unachoingiza mwilini kila siku.

Unatakiwa kuwa mwadilifu katika uchaguaji wako wa chakula, haimaanishi ukae na njaa. Inawezekana ikawa ni vigumu kuelewa makala haya.

Kinachosisitizwa katika mpango huu, ni kuwa waangalifu katika upangiliaji wa vyakula. Aina hii ya mpangilio wa ulaji inafahamika zaidi kitaalamu kama โ€˜crash dietโ€™ Kula kiasi cha kalori 400- 500 kwa siku. Lakini unatakiwa kufanya mazoezi angalau kwa saa mbili kwa siku, ili kupunguza mara mbili ya kiasi cha mafuta uliyokula katika siku hiyo.

Kunywa maji kwa wingi:

Kwa kunywa kiasi kikubwa cha maji itakusaidia kurahisisha umengโ€™enyaji wa chakula mwilini. Ni vyema mwili wako ukawa na maji ya kutosha ikiwa umeingia kwenye mpango huu wa ulaji Kula mboga za kijani: Zina Vitamini, protini na virutubisho vingine kwa wingi ambavyo ni muhimu kwa afya. Kama ilivyoainisha awali, utaratibu huu hauhamasishi kukaa na njaa, bali kula vyakula vilivyo bora kiafya.

Kula vyakula visivyokobolewa.

Mara nyingi vyakula vya aina hii, huwa na virutubisho muhimu na vinavyohitajika katika ustawi wa mwili.

Punguza wanga katika mlo wako.

Badala yake unaweza kula protini na kuingiza vyakula kama mayai na samaki kwenye mlo wako.

Epuka kula vyakula vya mtaani.

Vyakula kama chips, mihogo ya kukaanga na jamii yake vinachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzito wa mwili na pia hulifanya zoezi la umengโ€™enywaji wa chakula tumboni kuwa gumu.

Kula supu za mbogamboga;

Supu kama ya kabichi licha ya kujaza tumbo, husaidia katika kurahisisha mfumo wa umengโ€™enyaji chakula tumboni.

Kula saladi na matunda kwa wingi.

Hii itasaidia kukuweka sawa kiafya.

Jizuie kula vyakula vyenye sukari nyingi na hata vile vya mtaani unavyohisi vinaweza kukwamisha mpango wako wa kupungua.

Lakini pamoja na yote jipe mazoezi ya kutosha kama kukimbia, kuruka kamba au mazoezi ya kupunguza tumbo na maziwa

Faida za kuvaa saa ya Mkononi

leo tutajaribu kuongalia sababu kwanini tunatakiwa tuvae saa za mkoni yaani nini haswa kinatulazimisha kuvaa saa za mkononi , hebu kwa tujue saa za mkononi zilianza kuvaliwa mwaka gani.

Kabla ya vita ya kwanza ya dunia kulikuwa kuna saa za mfuko yaani pocket watch saa hizi zilipendwa sana enzi hizo. ila katika kipindi cha mapigano wanajeshi walihitaji saa ambayo itakuwa rahisi kuangalia sio mpaka watoe mfuko hivyo walianza kuvaaa saa mkononi na ikawa rahisi sana kuangalia wakati wa mapigano ..na vita ilivyoisha saa ikaonekana ni style sasa ikabidi watu waanze kuvaa kama fashion mitaani huko ulaya. sasa tuje sababu zinapelekea wewe au mimi kuvaaa saa japo simu zipo

SAA HUTUNZA MUDA VIZURI;

Japo kuna simu kuna computer hakuna kifaa kinachopita saa kwa utunzaji mzuri wa muda hasa saa za mabattery ya quartz za mwaka 1955 pia saa ya mkononi humpa mtu urahis wa kuangalia wakati muda wowote atakoa pia kuanza kufungua mfuko au bag

SAA ZINA NGUVU MBALIMBALI;

Saa mara nyingi huwa zina sifa mbalimbali kama uwezo wa kutoa ingia maji hivyo kufanya mtumiaji kuvaa popote atakapo hata kwenye maji kuna zingine ni ngumu kupasuka yaani shock resistant hasa kwa saa za company ya gshocK au skmei

SAA HAZIITAJI KUCHARGE’;

Kama tulipo sema saa ni simple sana hautaji wewe kuichaji maana kuna saa ambazo battery hukaa hata miaka mitano bila kuisha hasa saa kijapani pia kuna saa ambazo huwa hazitumii kabisa battery hizi huenda na mawimbi ya mkono wako

SAA NI FASHION;

Saa za mkononi pia ni fashion huongeza umaridadi na urembo wa mtumiaji au mmiliki wa saa husika. katika vitu wataalam wa fashion huwa wanashauri ni kuvaa saa mkononi ukitaka upendeze zaidi na mavazi yako wewe vaa saa ya mkononi muonekano wako utaongeza na utang’ara zaidi pia wanawake na wanapenda wanaume wanaovaa saa nzuri hahahahah natania sina uhakika ila well wanaume tuvaa saa ili tupendeze kitaa au maofisin wakuu

SAA HUTENGENEZA UHUSIANO KATI YA WEWE;

Asikwambie mtu watu wanao vaa saa mara nyingi huwa ni matime keeper wazur pia hujali muda wao tena ngoja nikukumbushe ndugu yangu we umeshahau kipindi tunasoma matime keeper wote walichagulia kisa anamiliki saa tu tena saa nzuri.. hivyo mara nyingi ukimiliki saa automatic utautunza muda wako sahihi ndugu yangu kuvaa saa.

Namna ya uvaaji wa mavazi mbalimbali kwa wanaume

Wanaume wanajali mavazi yao pia, sio wanawake tu. Ila, mwanaume anabidi aelewe kwamba badala ya kufuata mitindo, kupendeza kwenye tukio lolote kuna nguo ambayo utaihitaji. Nguo hizi ni kama:

1. T-Shirt ya Pamba

Ukitaka t-shirt itakayo dumu kwa muda mrefu, nunua t-shirt zilizotengenezwa kwa pamba tu. Pia, kuwa na t-shirt kadhaa zenye rangi tofauti, zikiwemo:

Za rangi ya kawaida kama Nyeupe, nyeusi, rangi ya kijivu
Za rangi kali kama Njano, bluu nyepesi na kijani
Uzuri wa t-shirt ni kwamba zinaweza kuvaliwa na chochote kile. Kwa hiyo, kuwa na aina nyingi kabatini.

2. Polo Shirts

Mwanaume yoyote anatakiwa kuwa na Polo Shirt (t-shirt zenya kola) kadhaa. Zinafaa sana kuvaliwa kazini kwenye siku za Ijumaa au weekend.

3. Mashati ya kawaida

Mashati ya kawaida, ya mikono mirefu au mifupi, ni mazuri kuvaa na jinzi na viatu au raba. Pia, zipo za aina na rangi tofauti kwa hiyo tafuta itakayokufaa.

4. Mashati ya shughuli/sherehe rasmi

Kutegeamea na ajira yako, shati ya aina hii inaweza ikawa nguo utakayoishia kuvaa kuliko zote. Kwa hiyo, lazima uwe nazo za kutosha za aina mbalimbali.

Pia hata kama huzihitaji kwa kila siku, utazihitaji kwa sherehekama harusi au mkutano mkubwa wa kikazi.

Muhimu kuliko vyote ni kuhakikisha unajua saizi yako na kwamba unavaa shati linalo kutosha vizuri kabisa. Zaidi ya hapo, fikiria tai utakayoivalia.

5. Bukta

Kwa kuzingatia joto lote la Tanzania, bukta ni muhimu.

Kuna aina nyingi za bukta na zenye rangi tofauti. Zinaendena na polo shirt pamoja na viatu vya kawaida. Ni mazuri kuvaa kwenye wikiendi ukiwa umetulia na washkaji.

6. Suruali za kawaida

Suruali za aina hii zina faraja na zinavaliwa kwenye mazingira mbalimbali. Pia, kama polo shirt zinapatikana kwa rangi nyingi kwa hiyo zinaweza kuvaliwa na mashati, viatu, kodia n.k za ain nyingi.

7. Jinzi

Jinzi zinaweza kuvaliwa kokote, siku yoyote.

Iwe ijumaa kazini au jumamosi usiku, hata kazini kwenye siku ya kazi (kutegemea na masharti ya kazini kwako), jinzi zitavaliwa tu. Zipo za aina nyingi, rangi tofauti na zinavaliwa na chochote kile.

Ila, ni muhimu kujua saizi yako ile upendeza unavyostahili. Pia, jinzi zenye ubora zitakuwa na bei zaidi ila bora ununue jinzi yenye ubora itakayodumu kwa miaka kuliko jinzi isiyo na ubora itakyodumu kwa miezi.

8. Koti la suti

Mwanaume yoyote anatakiwa kuwa na koti za suti za rangi ya bluu na kijivu kabatini. Rangi hizi zinaendana na sherehe rasmi na zisizo rasmi, na zinavaliwa na aina mbalimbali ya mashati na viatu.

Ila, muhimu zaidi ya rangi ni saizi. Hakikisha unajua saizi yako na kwamba koti zinakutosha vizuri.

9. Chupi na Soksi

Hakikisha chupi zako ni nzuri, zinakutosha na ni safi (usije ukajiaibisha). Kama zimechakaa, zitupe.

Soksi nazo ni vilevile. Ila, unahitaji kuwa na aina tofauti za soksi kwa ajili ya mavazi tofauti. Hakikisha rangi ya soksi zako zina ukali au ni nzito kidogo ya suruali yako.

10. Viatu

Kwa kawaida, viatu ni vitu vya kwanza vya mtu kuangalia akikuona, hasa na wanawake. Kwa, sio swala la kupuuzia.

Cha muhimu ni kwamba ni visafi na ziko katika hali nzuri.

Ndio, inabidi ujaribu nguo mbalimbali ila ujue kinachokupendeza. Ila, kuwa na mavazi yasiyo na mbwembwe nyingi si mbaya. Bahati nzuri, nguo tulizoorodhesha hapo juu zitakusaidia kupendeza bila kuweka juhudi saaaaana.

Tiba mbadala ya chunusi na vipele usoni

Kuna idadi kubwa ya watu wanao kabiliwa na tatizo la vipele vya usoni ( Chunusi ). Kuwa na chunusi ni jambo lenye karaha sana, kwani linakufanya upoteze mvuto wako wa asili na hivyo kukukosesha raha.

Zipo njia mbalimbali za asili zinazo weza kutumika kutibu tatizo la chunusi na vipele vya usoni.

Ifuatayo ni miongoni mwa njia bora kabisa na ya uhakika itakayo kusaidia kuondokana na tatizo la Chunusi au vipele kwenye uso.

Komamanga: Maganda Ya Mkomamanga yaliyosagwa, yakichanganywa na habbat sodah ya unga, hutengeneza dawa nzuri ya asili ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni ( chunusi )

Habbat Soda: Hii ni Habbat Sodah Ya Mbegumbegu. Habbat Sodah iliyosagwa ndio inayo hitajika katika kutengeneza dawa ya asili ya kuondoa tatizo la vipele vya usoni ama chunusi.

MAHITAJI:

Habbat Sawdah ya Unga iliyo sagwa.
Nusu kikombe ya maganda ya komamanga yaliyo sagwa.
Nusu kikombe ya siki ya tofaha(apple )

MATAYARISHO NA MATUMIZI

Changanya na pasha moto kwa dakika mbili kikombe kimoja cha Habbat-Sawdaa iliyosagwa, ยฝ (nusu)
kikombe cha maganda ya komamanga yaliyosagwa, na ยฝ (nusu) kikombe cha siki ambayo inatokana na juisi ya tofaha (apple).

Paka katika sehemu inayotakiwa kabla ya kwenda kulala kila siku usiku mpaka vipele (chunusi) vitakapoondoka. Mchanganyiko unaweza kukaa mpaka wiki tatu na ni lazima uwekwe katika hali ya ubarid.

Vyakula vya Kukuza nywele na kuzifanya ziwe na Afya

Kuwa na nywele zenye afya nzuri ni muhimu kwa wote bila kujali jinsi, hali hii husababisha wengi kutumia madawa ya aina mbalimbali ya kuhakikisha nywele zao zinastawi na kuwa na muonekano mzuri.
Kwa bahati mbaya, wengi waliotumia madawa yanayotengenezwa kwa kemikali hujikuta katika wakati mgumu siku za usoni wakikabiliwa na matatizo ya nywele kukatika na hata kupata madhara katika ngozi ya kichwa.

Njia bora na salama zaidi ya kustawisha nywele, kuzifanya ziwe na mvuto wa aina yake bila kujali wewe ni mtu wa asili ya bara Asia, Afrika au Marekani, ni kula vyakula vyenye virutubisho muhimu kwa afya ya nywele.

Vifuatavyo ni sehemu ya vyakula ambavyo hupatikana kirahisi barani Afrika na kwa bei nafuu, ambavyo vitakupa afya bora zaidi ya nywele zako.

1. Yai

Nywele za binadamu zina protini ambayo zimeumbiwa. Hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa zina protini ya kutosha, na hilo hufanyika kupitia vyakula. Protini ni nguzo kuu ya nywele za binadamu, na yai ni moja kati ya vyakula vyenye utajiri mkubwa wa protini. Hakikisha unakula yai angalau mara tatu kwa wiki.

2. Spinachi

Nywele zinahitaji madini ya chuma ili ziweze kuwa katika hali nzuri ya afya. Kukosekana kwa madini ya chuma husababisha nywele kunyonyoka. Mwili unapokosa madini ya chuma, hewa ya oxygen na virutubisho hushindwa kufika vizuri kwenye mizizi ya nywele hivyo hufanya nywele kuwa dhaifu na zisizo na muonekano mzuri.

Mboga za majani aina ya spinachi ni suluhisho, kwakuwa zina madini ya chuma kwa wingi ambayo seli za nywele huhitaji.

3. Jamii ya Machungwa, Limao

Mwili wa binadamu huhitaji vitamini C ambayo husaidia kuhuisha utendaji wa madini ya chuma. Hivyo, unapaswa kuongeza matunda ya jamii ya โ€˜citrusโ€™, kama vile machungwa, chenza, balungi na limao. Pia, unaweza kutumia na asali pamoja.

Vitamini C husaidia katika ukuaji wa nywele kusaidia usambaaji wa virutubisho na ukuaji wa haraka wa nywele.

4. Karoti

Ni muhimu sana kuhakikisha unakunywa juice ya karoti kila siku, kama unataka nywele zako zikue haraka zikiwa na mwonekano mzuri wenye afya. Vitamini A inayopatikana kwenye karoti ni muhimu sana kwa ukuaji wa seli za nywele. Kumbuka nywele zina tishu ambazo hukua haraka zaidi katika mwili.

Karoti ina mafuta asili yanayofahamika kama โ€˜sebumโ€™ na mizizi ambayo husaidia kukuza nywele kwa haraka.

5. Parachichi

Tunda aina ya parachichi lina kazi nyingi sana mwilini kama matunda mengine, lakini hili ni tunda la kipekee amnbalo lina utajiri wa vitamini E ambayo husaidia mzunguko wa damu na katika hilo husaidia mfumo wa ukuaji wa nywele kwa haraka.

Tunda hili husaidia kuhuisha na kurekebisha mafuta na kiwango cha PH (inayosafisha kemikalii mwilini) ambavyo kama vitazidi kwenye mwili vinaweza kusababisha kusimama kwa ukuaji wa nywele, yaani nywele hudumaa.

Kwa faida zaidi, vitamin E inayopatikana kwenye parachichi kwa wingi husaidia zaidi afya ya moyo wa binadamu na zaidi ngozi. Hakikisha unapata tunda hili kadiri iwezekanavyo.

Hivi ni baadhi tu ya vyakula na matunda kwa ukuaji mzuri wa nywele zako. Kama unatumia vizuri mlo wako, utakuwa adimu sana kutumia mafuta yenye kemikali ambayo yanaweza kukuletea madhara mabaya.

Jinsi ya Kujaza nywele kwa njia za Asili

Zingatia mambo haya yafuatayo;

  1. Chukua parachichi kubwa moja, asali vijiko vitatu na kiini cha yai.
  2. Osha nywele zako kwa shampoo na uzikaushe.
  3. Ponda ponda parachichi mpaka lilainike kabisa. Chukua vijiko vitatu vya asali na kiini cha yai kisha changanya yote kwa pamoja.
  4. Paka mchanganyiko huo kaa nao kwa muda wa dakika 15 kisha osha.
  5. Fanya hivyo kwa muda wa wiki moja hadi mbili na utaweza kuona matokeo mazuri katika nywele yako
Shopping Cart
16
    16
    Your Cart
    ๐Ÿ  Home ๐Ÿ“– Reading ๐Ÿ–ผ๏ธ Gallery ๐Ÿ’ฌ AI Chat ๐Ÿ“˜ About