Kama kote duniani, wanawake wengi Tanzania wanatumia vipodozi kama nyongeza ya urembo wao ya kiasili. Ila, kuna makosa maalum zinazofanyiwa kwenye kutumia vipodozi Tanzania. Kuwasaidia dada zetu, Yafuatayo ni makosa 10 ya kuweka vipodozi na jinsi ya kuzirekebisha.
1. Nyusi
Kuna tabia ya wanawake kunyoa nyusi zao sana, na wengine kuzitoa kabisa. Alafu, wanaishia kuzichora na rangi nyeusi.
Hii inamfanya mwanamke kuonekana kama kikatuni.
Sasa:
- Badala ya kunyoa nywele zote, zipunguze kwa kiasi kidogo
- Usituimie rangi nyeusi kuzijaza. Tumia rangi ya brauni
- Kwa muonekano wa kiasili zaidi, tumia nyusi, poda ya nyusi au gel badala ya penseli.
2. Tumia faundesheni inayofanana na rangi ya ngozi yako
Ingawa kupata faundesheni inayofanana na ngozi yako ni ngumu, hasa kwa wanawake weusi zaidi, wanawake wengi wanapata shida na kukubali rangi ya kiasili na wanajaribu kutumia vipodozi kubadilisa rangi yao.
Suluhisho:
- Kubali rangi yako ya kiasili
- Rangi yetu inaweza ikawa mweusi au mweupe zaidi kutegemea na msimu. Kwa hiyo ni bora kuwa na faundesheni inayoendana na mabadiliko hayo
3. Usitumie poda asana
Wanawake wengi wanfikiri kwamba kutumia poda nying ndio kupendeza zaidi. Matokeo yake, wanaishia kufanana na jinni.
Suluhisho:
- Tumia poda inayofanana na ngozi yako
- Usiweke poda nyingi. Kiasi kidogo kitakutosha
4. Tumia blush kwa usahihi
Kutumia kwa usahihi ni tatizo duniani.
Suluhisho:
- Tumia blush kwenye mifupa ya mashavu, sio kwenye mashavu yenyewe.
- Kama una ngozi yeneye uweusi zaidi, tumia blush ya rangi ya dhahabu au zambarau.
5. Burashi za vipodozi ni muhimu
Badala ya kutumia vidole vyako, utahitaji burashi zifuatayo:
- Burashi ya faundesheni
- Burashi ya poda
- Burashi ya blush
- Burashi ya nyusi
- Burahi ya eyeshadow
6. Tumia kope bandia kwa usahihi
Wanawake wengi wanatumia kope bandia zisizo na ubora. Matokeo yake wanafanana na dolli ya mtoto.
Suluhisho:
- Badala ya kutumia kope bandia, nunua wanja nzuri inayonyoosha na kunenepesha kope zako
- Nunua kope bandia zenye ubora (zilizotengenezwa na nywele za binadamu au yalisanidiwa)
- Jifunze jinsi ya kuweka kope bandia kwa usahihi.
7. Jifunze kuweka jicho la paka kwa usahihi
Jicho la paka ni njia moja ya kuongeza umaridadi kwa sura yako na kuvutia zaidi. Ila, wanawake wengi wanakosea kuiweka.
Suluhisho:
- Ni bora kutumia liner ya maji au mafuta kuliko kutumia penseli kama huna ujuzi wa kutosha
- Jifunze kuchora jicho la paka
8. Matatizo ya nyusi…tena
Wanawake wengi wanatumia konsila kwa nje ya nyusi zao. Tatizo linakuja pale ambapo konsila iliyotumiwa haiendani na ngozi yao. Hii inafanya konsila hiyo kuonekana sana, kwenye picha haswa!
Suluhisho:
- Tumia konsila inayoendana na ngozi yako
- Hakikisha una changanya konsila kwa kutumia burashi, ili ijichangaye vizure na ngozi/faundesheni yako
9. Eyeshadows
Wanawake wanatumia eyeshadow zinazo ng’aa au za rangi kali. Zaidi ya hapo, hawazichanganyi vizuri.
Suluhisho:
- Tumia eyeshadow za rangi ya dhahabu, brauni au zambarau
- Jifunze jinzi ya kuweka eye shadow vizuri, zikiwemo
- Rangi ya highlighter yakuweka chini ya nyusi zako
- Rangi ya msingi ya kuweka
- Rangi ya mpito
- Rangi kuu ya eye shadow
10, Mdomo
Kabla ya kuweka lipstick, hakikisha mdomo yako inaunyevu. Hii ni muhimu sana kwa lipstick yako kuseti vizuri.
Usiweke vipodozi kwa fujo
Kwenye swala la vipodozi, kutumia kidogo ni bora kuliko kutumia nyingi. Unataka urembo wako wa kiasili kuboreshwa, sio kubadalika kabisa.
Kwa kifupi, ukitumia vipodozi lakini unaonekana kama vile hujatumia vipodozi, basi hapo ndio utakuwa umepatia.
References:
Google ScholarResearchGate
Semantic Scholar
AckySHINE