SMS ya kumwambia mpenzi wako hutomuacha na kumuonyesha umuhimu wake
Kama safari tumeianza,kama chakula sinto kusanza,kama
nyumba wewe kibaraza na kama ukingo wewe kiambaza.
Kama safari tumeianza,kama chakula sinto kusanza,kama
nyumba wewe kibaraza na kama ukingo wewe kiambaza.
naukunjua moyo wangu huishi milele maishani ,nafungua
nafsi nikupende wewe pekee,nafunga milango ya moyo wangu
ili
kutokupokea ugeni wowote wa moyo zaidi yako
mpenzi.nakupenda sana laazizi
nilivyokutana nawe siku ya kwanza nilikupenda kwa
dhati,nikakueleza ukweli ukanikaribisha moyoni
mwako,siwezi kuchezea nafasi hiyo laaziz,nitakushika
daima.
Uchungu wa kifo hauna tofauti na maumivu nitakayoyapata
ukiniachana, mpenzi usiniache nami siko tayari kukuacha
Siku zote kwangu ni sherehe ni wewe unishereheshaye,ukweli
usio na kejeli mapenzi yako yanatii kiu yangu,moyoni
mwangu nimeridhia⦠.nakupenda daima mpenzi!
Kumjali mtu ni rahisi, lakini kumfanya mtu akujali ni
vigumu, nashangaa umewezaje kunifanya nikujali?
Imara hautikisiki,kakamavu halishikiki penzi langu kwako
ni nuru daima halizimiki.upo juu katika mapenzi.
Mpenzi kwa mara ya kwanza nilipokuana niliogopa kukuambia,
hata nilipokuambia niliogopa kukupenda, nilipokupenda sasa
naogopa mno kukupoteza. Kusema kweli siko tayari kukukosa
katika maisha yangu.
Niseme nini ujue nakupenda? Nifanye nini ujue nakupenda?
Nikuite jina gani ujue ni wewe peke yako upo moyoni
mwangu? Hakika hakuna ila moyo wangu ndio unaosema kuwa
nakupenda, niamini mpenzi
Njoo pendo langu nikutembeze
katika milango ya furaha
Nikuwakilishe mbele ya majamaa zangu
Nikuonjeshe asali ya pendo langu
Recent Comments