Ujumbe mzuri wa kimapenzi wa kumwambia mpenzi mapenzi huanza na wewe na yeye
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Maneno huanza na ABC. Namba 123. Muziki na do re mi na
mapenzi huanza na mimi na wewe.
Naweza kukuazima mabega yangu upande, masikio yangu
usikilizie mikono yangu ushikie, miguu yangu, utembelee,
lakini si moyo wangu kwani tayari unao wewe.
Nenda sms taratibu kwa yule ma BEST nimpendaye,ukimkuta
amelala ucmuamshe mpige busu kisha mnong’oneze mwambie
nampenda sanaaaa
Nilivyokutana nawe cku ya kwanza nilikupenda kwa dhati
,nikakueleza ukweli ukanikaribisha moyoni mwako,cwezi
kuchezea nafac hyo laaziz nitakushika daima.
Kama safari tumeianza,kama chakula sinto kusanza,kama
nyumba wewe kibaraza na kama ukingo wewe kiambaza.
Fikra hutawala mtima wangu,
Kwa madhila yalojaa duniani,
Kwa muhali wa yanayojiri,
Kwa machweo na mawio,
Kwa totoro ama nuruni,
Nao moyo hukosa ukamilifu,
Kwa utashi wa zake hisia,
Zinipazo sababu kuu,
Ya upendo juu yako,
Ya kukufanya daima uwe,
Mawazoni mwangu.
Mawazoni ama ndotoni,
Daima wewe hutawala,
Kila asubuhi niamkapo,
Nao usiku nilalapo,
U chakula changu akilini,
Nalo tulizo langu moyoni,
Daima huuwaza upekee,
Wewe uliojaaliwa,
Na hivyo naihisi furaha,
Daima wewe uwapo,
Mawazoni mwangu.
pendo ni silaha kali zaidi duniani hu uwa wasio na hatia
na hujeruhi bila kutarajia,wengine hujitolea muhanga nayo
,silaha hiyo itumikapo vizuri huleta marafiki na kuongeza
furaha,je we unaitumiaje silaha hiyo?
Naweza kuishiwa ujumbe wa kukutumia. Naweza kuishiwa utani
pia. Naweza kuishiwa chaji lakini moyo wangu hauwezi
kukosa nafasi ya kukuweka.
sura yako haifutiki usoni mwangu kirahic,ingawa upo mbal
nami lkn penzi lako bado nalikumbuka,hakuna anayeweza
kukata kiu yangu zaidi yako,nakupenda mpenzi wangu!
Ikiwa penzi langu kwako litakufa halitazikwa,ikiwa moyo
wangu ni mwandiko hautafutika na kama dhati yangu ni
machozi daima hayatokauka na wewe kwangu ni damu ngozini
haitochuruzika ila mishipani… .
Najua kuna vishawishi vingi sana uko ulipo, lakini nikiwa
moyoni mwako, siku hii itakuwa nzuri zaidi kwetu,
tupendane daima lahazizi…
Recent Comments