Umri unaofaa kuoa

Kuoana maana yake ni kuwajibika kwa maisha yako na mke au mume wako. Mara nyingi kuoana kunaambatana na kuzaa watoto. Ni vigumu sana kutambua umri sahihi wa mtu kuoa au kuolewa, kwa sababu watu wanatofautiana katika kuamua ni lini yuko tayari kujitegemea na kuwajibika kumtunza mtu mwingine. Wengine wanakuwa tayari katika umri wa miaka 20 na wengine katika umri mkubwa zaidi.

Kwa vile kuoa au kuolewa mara nyingi kunahusishwa na mtu kuwa mzazi, kuna vipengele vya kiafya vinavyofaa kuzingatia. Kwa mfano siyo vema msichana kuzaa kabla hajafikisha umri wa miaka 18, kwa sababu mwili wake hauko tayari kuzaa mtoto. Nyonga i nakuwa bado ni nyembamba, viungo vya uzazi ni vidogo na havijakomaa kiasi ambacho vinaweza kuharibika wakati wa kuzaa mtoto.
Kwa hiyo basi unashauriwa kusubiri i kuoana mpaka hapo utakapokuwa umejenga msingi i mzuri i wa maisha yako. Kabla hujawa tayari kuoa au kuolewa unaweza kuwa na urafiki na yule aliye mtarajiwa wake ili taratibu muweze kuelewana tabia, yale anayoyapenda na asiyoyapenda na kujenga msingi mzuri wa uhusiano.

Jinsi ya kumfanya mpenzi au rafiki yako asiwe na mwingine

Jambo la muhimu ni kuwasiliana kwa karibu i ili kuelewa mawazo na matatizo ya rafiki yako. Hakikisha unakuwa muwazi na mkweli. Mkielewana vizuri mnaweza kufurahia mazungumzo yenu vizuri. Vilevile mnaweza kusaidiana katika kutatua matatizo yanayoweza kumkabili mmoja wenu. Kwa kufanya hivyo mtajenga moyo wa kuaminiana.

Ili kudumisha urafiki wenu unashauriwa kuonyesha upendo wa hali ya juu. Jitahidi usiwe na marafiki wengine na mthibitishie kwamba yeye pekee ndiye unayempenda na uko mwaminifu kwake.

Utamfahamu vizuri rafiki yako iwapo mtazungumza mara kwa mara juu ya maisha yenu. Kwa mfano mnaweza kuzungumzia mipango ya uhusiano wenu, vitu anavyopendelea kufanya baada ya saa za kazi au masomo, watu anaowasiliana na kuandikiana nao. Iwapo mawasiliano yenu yatakuwa mazuri na iwapo utachunguza uhusiano wake na watu wengine utahisi kama kweli mnaaminiana.

Hata hivyo, iwapo hutaweza kumwamini rafiki yako na kama unahisi kwamba hata yeye hakuamini, jiulize kwamba kwa nini iwe hivyo. Je, inawezekana huyu mtu hanifai? Au, inaweza kuwa mapenzi yako ni kidogo kiasi ambacho siwezi kuzuia vishawishi vingine?

Jinsi ya kufanya wazazi wamkubali mchumba

Uhusiano mzuri na wazazi ni muhimu sana siyo katika masuala ya uchaguzi wa mchumba tu, bali katika masuala yote ya msingi maishani. Kwa hiyo, hatua ya kwanza ni kujaribu kuelewana nao.
Mara nyingi vijana hufikiri wazazi hawaelewi maisha ya vijana wa kisasa. Mara nyingine hufikiri kwamba mila na desturi zinamzuia kijana kufanya uamuzi ambao unafaa. Pia wengine hufikiri kwamba tofauti ya malengo kati ya vijana na wazazi huleta mgongano.

Hali kama hii ikijitokeza, ni vizuri kuwasiliana na wazazi kwa nia ya kuelewana. Usisahau kwamba wazazi wakati wote wanajaribu kujena maisha bora ya baadaye ya watoto wao. Unapowasiliana na wazazi jaribu kuwaeleza kwa heshima na upole kwa nini hukubaliani na mawazo yao na kwa nini unaona uamuzi wako unafaa. Inawezekana kwa kufanya hivi unaweza kupata ridhaa ya wazazi wako.
Kama hujawahi kuzungumza na wazazi wako kwa karibu, mara nyingi i i inakuwa vigumu kuanzisha mazungumzo. Jaribu kuanza kwa mazungumzo rahisi. Tafuta muda mzuri wa kuanzisha mazungumzo. Usianzishe mazungumzo na wazazi wakati wamechoka au wakati wametingwa na kazi nyingi; hawatakusikiliza. Jaribu kuwa wazi na mkweli, na waonyeshe wazazi wako kwamba unayajali mawazo yao. Kwa kufanya hivyo wazazi wako wanaweza kukuamini na kuafikiana na wewe katika maswali mazito zaidi. Vilevile onyesha kwamba unawaheshimu. Inachukua muda mrefu kufanikisha mawasiliano mazuri na wazazi, lakini ni vema kuyaanzisha mapema kwa ajili ya kufanikisha lengo la mawasiliano mazuri na wazazi.

Nikitafuta rafiki kwa nia ya kuoana (mchumba), je ni sifa gani niangalie kwa msichana/mvulana?

Kuchagua mchumba ni moja ya maamuzi ambayo kijana anahitaji kuyafanya kwa uangalifu mkubwa sana. Kwa sababu huyo ndiye atakayekuwa mwenzi wake wa maisha. Katika kuchagua mchumba kila mtu ana mawazo yake kuhusiana na kilicho muhimu kuzingatiwa. Mara nyingi mhemuko una nguvu zaidi kuliko uamuzi wa kimantiki

Hata hivyo, vifuatavyo ni kati ya vigezo ambavyo vinaweza kuangaliwa:

• Chagua mtu anayekuheshimu wewe na wengine; Chagua mtu unayemwamini;
• Chagua mtu ambaye unaweza kuongea, kujadiliana, na kuhojiana naye kwa uwazi bila kugombana;
• Chagua mtu mwenye umri unaokaribiana na wa kwako;
• Chagua mtu anayependelea vile unavyopendelea;
• Chagua mtu ambaye ataelewa matatizo yako na yuko tayari kukusaidia kuyatatua; na
• Chagua mtu mwenye afya nzuri.

Hii inamaanisha pia kumpata mtu ambaye kabla ya kuanza kujaamiana naye, atakuwa tayari kwenda kupima kwa hiari kujua hali yake ya VVU na pia kuwa tayari kutumia kinga kwa maana ya kondomu hadi hapo mtakapojua hali zenu.

Wafahamishe wazazi wako mtu uliyemchagua kama mchumba na mtambulishe kwao i ili wamfahamu na yeye awafahamu wazazi wako. Wakati huohuo na wewe jaribu kuwafahamu wazazi wake. Usifanye uchumba wa haraka. Pata muda wa kutosha kumwelewa rafiki yako.

Kufahamu tabia ya rafiki yako wa kike/kiume kabla ya kuoana hata kama anaishi mbali

Unaweza kufanya uchunguzi wa kutosha kuhusu tabia, muono na imani ya rafiki yako hata kama mnaishi mbalimbali. Unaweza kumuuliza maswali kuhusu mahali anapoishi na familia yake kwa ujumla. Jaribu kufanya mawasiliano ya karibu zaidi ili uweze kumdadisi, na yeye aweze kujieleza mwenyewe kwa undani zaidi kuhusu yeye mwenyewe.

Njia nyingine ni kutumia watu wengine walio karibu naye. Unapomchunguza mtu ambaye unafikiri anaweza kuwa mchumba wako inakubidi uwe na vigezo ulivyojiwekea ambavyo ungependa awe navyo.

Uchunguzi wa namna hiyo unaweza kukusaidia kujua tabia ya rafiki yako. Hata hivyo kufanya uchunguzi hakuna maana kwamba huhitaji kuwa naye kabisa. Bado unahitaji muda zaidi wa kuwa naye ili kumjua na kujenga uhusiano.

Jambo la kukumbuka ni kwamba tabia, siyo rahisi kufahamika na kuelezeka waziwazi, na hasa kama watu wako kwenye mapenzi. Mara nyingi katika mazingira haya siyo rahisi kuona kasoro. Vilevile tabia ya mtu huenda ikabadilika kulingana na umri.

Nifanye nini ili kuepuka kubakwa na mpenzi/ rafiki?

Kuna baadhi ya vidokezo ambavyo vinaweza kukusaidia:
1. Usikae faragha na mwenzi wako kabla hujawa tayari na kumwamini. Ongozana na marafiki wengine hasa mwanzoni mwa urafiki wenu. Msitoke tu nyie wawili hadi hapo utakapojisikia kuwa umemjua kiasi cha kumwelewa na kumwamini. Pia jiepushe kukaa sehemu za faragha naye.

2. Kama utatoka naye, hakikisha kuwa kuna mtu anayejua mnakokwenda na ni muda gani unakusudia kurudi nyumbani. Ikiwezekana kuwa na namba ya simu ya mmoja kati ya rafiki zako. Hii itakusaidia kama ikijitokeza hali ya kutaka msaada.
3. Usikubali yeye alipe gharama zote. Ni vizuri kugawa gharama hizo kati yenu. Kama mtakwenda kwenye tamasha au kupata kinywaji hakikisha kulipia nusu ya hizo gharama. Ukifanya hivyo utamzuia mwenzio mawazo ya kukufikiria “kuwa anakudai ngono“ kama malipo ya pesa yake aliyotumia.
4. Ni vizuri kutafakari na kuweka kichwani kabla ya kwenda naye popote juu ya nini unachotaka na kile usichotaka kitokee.
5. Onyesha wazi kuwa unaposema “hapana“ unamaanisha “hapana“ usimpe nafasi ya kuchukulia hiyo “hapana“ kuwa ndiyo.
6. Amini hisia zako. Kama unaona unalazimishwa usisite kueleza maoni yako / unavyojisikia. Ikibidi ondoka sehemu hiyo.

Kulambana sehemu za siri ni salama kiafya? Je, tendo hili ni la kawaida?

Si rahisi kusema ni kitendo kipi kilicho cha kawaida na kisicho cha kawaida. Kulamba ni jambo linalofanyika

na kama wahusika wote wanalipenda ni sawa. Inashauriwa kuosha sehemu za siri kabla ya kufanya hivyo. Kwa kufanya hivyo, yaani kunawa kunafanya tendo hili kufanyika katika hali ya usalama kiafya. KAMA wote mtakuwa wazima bila kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa hasa kisonono (gono).

Je, kuna matatizo yoyote kama mdomo wa msichana utagusana na shahawa?

Kama mpenzi wako hatakuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa hakuna madhara ya kiafya. kama shahawa i itagusana na mdomo wa msichana. Lakini, wasichana wengi hawapendi kupokea shahawa mdomoni na wanasikia kukerwa kufanya hivyo.

Wapenzi wajadiliane kati yao na kuamua kama tendo la kumwaga mbegu mdomoni wanalipenda au hawalipendi. Huu ni msingi mmojawapo wa kuonyesha kujaliana.

Hata hivyo, kama mwanaume ameambukizwa na magonjwa ya zinaa ni rahisi sana kwa mwanamke kuambukizwa magonjwa hayo wakati anapokea majimaji na shahawa mdomoni. Kwa hiyo, kutumia kondomu katika mtindo huu ni salama zaidi.

Je, madhara gani yatawapata wasichana na wavulana wanaojamiiana kwa kutumia sehemu ya haja kubwa?

Tunasema ngono kutumia njia ya haja kubwa pale ambapo uume uliodinda unaingizwa kwenye njia ya haja kubwa (mkunduni).

Tatizo kubwa la kujamii ana sehemu ya haja kubwa, ni kwamba kuna uwezekano wa kueneza magonjwa ya zinaa pamoja na maambukizi ya VVU na UKIMWI zaidi kuliko kutumia njia ya kawaida ya uke. Kujamii ana sehemu ya haja kubwa ni hatari kwa sababu hakuna yale majimaji kama ukeni na ngozi ni laini sana. Kwa hiyo michubuko i inaweza kutokea kwa urahisi. Michubuko hii i ii inasababisha maumivu na pia i inarahisisha kuambukizana magonjwa ya zinaa.
Kama bado umeamua kujamii ana kwa kutumia njia ya haja kubwa pamoja na usumbufu wote tulioutaja hapo juu, unashauriwa kutumia kondomu i li kuzuia uambukizaji wa magonjwa.

Je, mvulana anaweza akafikia mshindo kwa njia ya kusugua uume na vidole na kuna madhara gani ukisugua uume na vidole?

Ndiyo, mvulana anaweza akafikia mshindo kwa njia ya kusugua uume na vidole. Anaposuguliwa uume na vidole, msisimko wa mwili unaongezeka na damu zinaingia kwenye mishipa ya damu katika uume.

Basi, uume unasimama na mara nyingi ukiendelea kusuguliwa mvulana anamwaga mbegu zake. Kusugua uume ni njia salama ya kumaliza ashiki ya kutaka kujamii ana. Hakuna madhara yoyote ya kiafya wala kiakili kama uume unasuguliwa. Watu wengine wanasema kwamba kupiga punyeto inasababisha shida ya kisaikolojia kutokea na nguvu ya kiume kupungua. Wengine wanasema kwamba mtu anayepiga punyeto atashindwa kujamii ana na mwanamke. Lakini si kweli, ni uvumi potofu tu.

Je, kuna madhara msichana akifanya mapenzi wakati akiwa katika hedhi (siku zake)?

Kufanya mapenzi wakati msichana yuko katika hedhi hakuna madhara yoyote kiafya kwa mwanaume wala mwanamke kama kati yao hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa.

Ila kama mmoja wapo ana ugonjwa wa zinaa, huo ni wakati wa hatari sana kwa maambukizi, kwa sababu utando ndani ya mfuko wa uzazi unabomoka na mlango wa mfuko wa uzazi unakuwa wazi. Hivyo ni rahisi sana vijidudu vya magonjwa mbalimbali kuingia mwilini mwa msichana. Vilevile kama msichana tayari ameambukizwa na magonjwa ya zinaa, katika damu yake viko vijidudu vingi vinavyoweza kumwambukiza mvulana.

Kwa sababu mara nyingi ni vigumu kufahamu kama kati ya wapenzi hakuna mwenye ugonjwa wa zinaa, haishauriwi kujamii ana wakati wa hedhi na kama ndivyo basi kondomu i tumike.

Katika jamii nyingi kujamii ana wakati mwanamke yuko wenye hedhi haikubaliki kwa sababu ya mila au dini.

Je, uke wa mwanamke unaweza kupanuka kiasi gani?

Wakati wa kujifungua, uke wa mwanamke mzima hupanuka kuanzia kipenyo cha sentimeta kumi mpaka kumi na mbili i i ili kuruhusu kichwa cha mtoto kupita. Kwa kawaida, mwanamke anayejifungua, uke na mlango wa mfuko wa uzazi hupanuka vya kutosha.

Kwa wasichana wa umri mdogo, kuzaa mtoto kunaweza kukaleta matatizo, kwa sababu viungo vyake vya uzazi bado ni vidogo na havina nguvu ya kutosha. Mara kwa mara wasichana wanapata uchungu wa muda mrefu kwa sababu fupanyonga ni nyembamba hivyo kutoruhusu mtoto kupita kiurahisi na kwa haraka. Mara nyingine hata i inabidi kufanyiwa operesheni i i ili kumtoa mtoto.

Wasichana ambao hawapati huduma ya wataalamu ambao wanaweza kugundua matatizo ya msichana na mtoto haraka wakati wa kujifungua, mara nyingi wanapata ulemavu wa kudumu. Yaani ulemavu wa kuharibika ama njia ya mkojo au njia ya haja kubwa au hata njia zote mbili kwa pamoja. Uharibifu wa njia hizi unajulikana kana fistula, unamfanya mama kushindwa kuzuia haja kubwa au ndogo hivyo kuvuja ovyoovyo kwa kupitia ukeni.

Wakati mwingine msichana na mtoto ambaye hajazaliwa hufa wakati wa kujifungua, kwa sababu wanakuwa hawajapata huduma kutoka kwa mtu mwenye stadi za kutosha.

Kwa nini mara nyingine uume hausimami?

Ili mwanaume aweze kujamii ana, ni lazima uume usimame na kuweza kupenya ukeni. Kama mvulana anasisimka kimapenzi, damu nyingi inaenda katika mishipa ya damu ndani ya uume. Halafu uume husimama kutokana na msukumo wa damu. Hivyo kama msukumo wa damu hautoshi, hii husababisha uume kutosimama au kusimama kwa unyonge.

Kutokuwa na msisimko wa kutosha kwa ajili ya kusimamisha uume kunaweza kusababishwa na mambo mengi, mojawapo ni i i ile hali ya kutokuwa tayari kwa kujamii ana, kuwa na wasiwasi mwingi, kutompenda mpenzi wako, ulevi wa pombe au dawa za kulevya, kuvuta sigara, lishe duni au maradhi mbalimbali.
Kama una shida ya uume kutosimama wakati wa kujamii ana, jaribu kuangalia ni sababu zipi kati ya hizi zilizoorodheshwa juu zingeweza kuwa sababu kuu ya shida yako. Halafu, jaribu kurekebisha matatizo.

Nini kifanyike nini kwa mtu ambaye hafikii kilele au mshindo wakati anapofanya mapenzi?

Kwa mwanaume, dalili ya kufikia mshindo ni uume kusimama halafu kumwaga manii . Manii kutotoka wakati wa kujamii ana inaweza kusababishwa na mambo mengi. Kutoa manii kunatumia nguvu nyingi za mwili.

Kwa hiyo chochote kile kinachompunguzia mwanaume nguvu za mwili kama vile maradhi mbalimbali, ulevi wa pombe au dawa za kulevya, njaa au lishe duni kunasababisha mwanaume ashindwe kutoa manii . Sababu nyingine muhimu ni kutokuwa tayari kimawazo au kutokuwa na huruma katika tendo la kujamii ana. Kama ulevi ni sababu ya shida yako, jitahidi kuyaacha mambo haya. Jaribu kutulia na kuongeza muda wa kutayarishana kimapenzi mpaka mtakapoona mko tayari.
Kwa mwanamke, kutofikia mshindo pia kuna sababu mbalimbali. Lakini mara nyingi i i inasababishwa na kutokuwa na subira katika maandalizi ya kujamii ana, kutokuwa tayari kimawazo au kuogopa matokeo ya kufanya mapenzi. Mwanamke akiwa tayari kimawazo kwa kujamii ana na mwanaume akijitahidi kumstarehesha vizuri, mwanamke atafikia mshindo bila shida. Pia kuwa wazi juu ya unachokipenda na usichokipenda i inasaidia sana katika kuwa na ngono ya kuridhisha kwenu wote wawili.

Kwa nini mwanaume akiona mapaja ya mwanamke uume wake husimama?

Mapaja na nyonga ni sehemu ya mwili i i iliyo karibu na viungo vya uzazi vya mwanamke. Kwa sababu ya mvuto wa kijinsia kati ya mwanaume na mwanamke, ambao ni wa asili, mwanaume anapoona kilicho na uhusiano wa karibu na viungo vya uzazi au viungo vyenyewe hupata msisimko.

Mara nyingine hata i inatosha mwanaume kufikiria kuhusu mwanamke au viungo vyake vya uzazi, uume wake ukasimama. Kusimama uume ni kielelezo kimojawapo cha msisimko wa mwili na mchango mkubwa katika msisimko huo ni mawazo.

Kwa nini mara nyingi mvulana ni mwepesi sana katika kuanzisha kufanya mapenzi? Na kwa nini mwanaume mara nyingi anafikia mshindo kabla ya mwanamke? Mwanaume anawahi kufika kileleni kwa nini?

Kwa kawaida i inakubalika kuwa wavulana ndiyo waaanze kuonyesha ishara za kujamiaana na tafiti zimeonyesha kwamba mara nyingi mwanaume anafikia mshindo kabla ya mwanamke. Hii ni ukweli katika sehemu nyingi za dunia.
Baadhi ya wavulana wanatumia vibaya uwezo wao wa kufanya mapenzi. Wanafuatafuata wasichana na kuwatongoza i ili wafanye mapenzi katika umri mdogo. Hata hivyo kujamii ana katika umri mdogo kunaweza kusababisha athari nyingi kama vile mimba isiyotarajiwa au kuambukizwa magonjwa ya zinaa. Kwa hiyo, wavulana wanashauriwa kuwa wavumilivu licha ya mivuto hiyo ya kutaka kujamii ana, kwa sababu kwa njia ya kujamii ana ovyo mnahatarisha maisha yenu ya baadaye. Kuna njia nyingine za kuonyesha mapenzi, kama vile kubusu, kukumbatia, kushikana mikono na hata kupiga punyeto.
Kimaumbile, mara nyingi mwanaume anafikia mshindo haraka zaidi kuliko mwanamke. Lakini, mkihakikisha kwamba mwanamke ni tayari kwa kujamii ana na kama mmechukua muda wa kutosha kujiaanda vizuri, mnaweza kufikia mshindo pamoja. Hivyo kuwaletea raha na starehe wote wawili.

Njia zipi zinaweza kumletea mwanamke mshindo haraka, na zipi zinamletea mwanaume mshindo haraka? Njia za kufika kileleni

Jambo la msingi kabisa ni kwamba wote wawili kuwa tayari kwa kujamii ana. Yaani kupendana na kujaliana sana, halafu kuwa tayari kwa tendo hilo kimwili, kimawazo na kiakili. Kutokuwa tayari kwa kufanya mapenzi, kwa mfano kwa sababu ya kuogopa ujauzito, inamzuia mtu yeyote kufikia mshindo.
Kama wote wawili mpo tayari, kufikia mshindo au kutofikia kunategemea maandalizi ya awali ya mapenzi.
Mnatakiwa kukubaliana jinsi mtakavyofanya mapenzi i i ili kila mmoja wenu aweze kufurahia na kuridhika. Kwa uhakika, kila mwanamke na mwanaume anazo sehemu maalumu ambazo ukigusa basi ni rahisi sana kufikia mshindo.
Upeo wa hali ya kujamiiana pia unaweza kufikia kwa kupiga punyeto. Kwa mfano, mwanaume anaweza kugusa uume wake au mwanamke anaweza kusugua taratibu kinembe mpaka anafikia mshindo. Kupiga punyeto ni njia i iliyo salama ya kumaliza hamu ya kutaka kufanya mapenzi na haina athari mbaya kiafya.

Shopping Cart
2
    2
    Your Cart
    🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About