Sala ya Baba Yetu: Sala ya Bwana
Baba Yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe;
ufalme wako ufike,
utakalo lifanyike
duniani kama mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku,
utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina
SMS nzuri ya kumtakia umpendaye mchana mwema
Mpenzi kila tunapokuwa chumbani huwa napenda kuwa mbunifu, huwa najitahidi kuepuka udhaifu, ili mapenzi yangu yasikukifu, ENDELEA KUFURAHIA MAPENZI YANGU. Mchana mwema
Unaweza kutuma Ujumbe huu kwa Umpendaye hapa
MAFUNDISHO MUHIMU KUHUSU MWILI NA DAMU YA YESU KRISTU | BIBLIA INAVYOELEZA KUHUSU EKARISTI
Yesu alituambia nini kuhusu Mwili wake na damu yake?
Damu na Mwili aliotupa Yesu ni nini? Ekaristi ni nini hasa?
Fundisho hili la mwili na damu ya Yesu (Ekaristi) lilikua Agizo tunalopaswa kulitii mpaka leo?
Mitume walitii Fundisho la Ekaristi na waliliishi?
Je mkate na divai vilichukuliwa na Mitume kama nini hasa? walichukulia Ekaristi kama nini?
16Je, kikombe cha Baraka ambacho tunakibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17(Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja, kwa kuwa wote twashiriki mkate mmoja) (1 Wakorinto 10:16)
Je ni lazima Kwa Mkristu kupokea Mwili na damu ya Yesu (Ekaristi)?
Je ni kwa nini madhehebu mengine hawakubali mafundisho haya ya Ekaristi Takatifu, Je ni mara ya kwanza watu kukataa?
Hata wakati Yesu akiyasema maneno haya Wafuasi Wengi Walimwacha kama Biblia inavyosema; 60Wengi wa wafuasi Wake waliposikia jambo hili wakasema, โMafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?โโ (Yohana 6:60). Haishangazi hata leo weni hawaamini mafundisho haya japokua ndio msingi wa Imani ya Kikristo.
Mitume walifundisha nini kuhusu Mwili na Damu ya Kristu (Ekaristi)?
Je, Divai iliyotumiwa na Yesu na mitume pamoja na Wakristu wa Kwanza ilikua na Kilevi (pombe)?
Kwa hiyo hata Mitume na Wakristu wa kwanza walitumia divai yenye kilevi ndio maana kuna waliolewa na walionywa kuhusu hilo.
Je Yesu Yupo Mzima katika Ekaristi Takatifu? Na kwa nini Tunaabudu Ekaristi?
Ukisoma Yoh 6:51-57 inasema hivi;
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โโ 52Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, โMtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?โโ 53Hivyo Yesu akawaambia, โAmin, amin, nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu Yake, hamna uzima ndani yenu. 54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake. 57Kama vile Baba aliye hai alivyonituma Mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.
Mstari wa 51 Yesu alisema wazi Mkate huo ni Mwili wake.
Thamani na Uwepo wa Yesu Mwenyewe unaonekana katika Mstari wa 53 na wa 56. Kumbuka hapa amesema “Mimi nitakaa ndani yake” Hakusema Mwili wangu utakaa ndani yake. Kwa maana nyingine ni kwamba Ekaristi ni Yesu Mzima na Sio Mwili tuu.
54Mtu ye yote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho. 55Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli. 56Ye yote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.
Wale Wanaopinga fundisho la Ekaristi wanafikiri Yesu alivyosema Mimi ni Chakula Kutoka Mbinguni hakumaanisha Mwili bali Maneno na Imani Kwake lakini Tukisoma 51 Yesu alisema wazi kuwa Mwili wake ndio Mkate wenyewe.
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โโ
Mitume wa Yesu walielewa hivi fundisho hili ndio Maana walishiriki Meza ya Bwana kila walipokutana na waliheshimu kama Mwili na Damu ya Kristo.
7Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. (Mdo 20:7)
Ili kujua kuwa Mitume waliheshimu Mwili na Damu ya Yesu Biblia inatuambia hivi;
23Kwa maana mimi nilipokea kutoka kwa Bwana yale niliyowapa ninyi, kwamba Bwana Yesu, usiku ule alipotolewa, alitwaa mkate, 24naye akiisha kushukuru, akaumega, akasema โHuu ndio mwili Wangu, ambao ni kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ 25Vivi hivi baada ya kula, akakitwaa kikombe, akisema, โKikombe hiki ni agano jipya katika damu Yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo kwa ukumbusho Wangu.โ 26Maana kila mlapo mkate huu na kunywea kikombe hiki, mnatangaza mauti ya Bwana mpaka ajapo. 27Kwa hiyo, mtu ye yote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana. 28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe. 30Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. (1 Wakorinto 11:23-30)
Kwa hiyo Mitume walisisitiza kuhusu Mwili na Damu ya Kristu kuwa ni Mtakatifu.
51Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu ye yote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.โโ
Yesu alisema Mimi ni Mkate wa Uzima ambao alimaanisha upo katika Mwili wake. Mwili tuu hauna uzima kama hauna Yesu ndani yake. Kwa sababu Mwili ni Mzima na Unaye Yesu ndani yake ndiyo maana unaweza kuleta uzima kwa Wengine.
Tunaelewa kwamba Yesu alijitoa Msalabani Mwili Wake na Damu yake na ndicho alichotupa ktk Ekaristi. Na Mwili wake huo Ulikua umembeba yeye aliye Mungu ndiyo maana tunaabudu Ekaristi alipo Yesu aliye Mungu.
Kwa kuwa Yesu ni Mungu Kama tunavyosoma katika Yoh 1:1-12
1 Hapo mwanzo, kabla ya kuwapo kitu kingine cho chote, aliku wapo Neno. Huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye alikuwa Mungu. 2 Tangu mwanzo Neno amekuwa na Mungu. 3 Vitu vyote viliumbwa na yeye, wala hakuna cho chote kilichoumbwa ambacho hakukiumba. 4 Uzima ulikuwa ndani yake na uzima huo ndio ulikuwa nuru ya watuโฆโฆ..14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
Kwa hiyo Neno huyo huyo Ndiye aliyetukomboa kwa kuutoa mwili wake sadaka Msalabani na ndiye Aliyetupa Mwili Wake na Damu yake ktk Ekaristi na anaabudiwa kwa kuwa yupo katika mwili huo.
โKisha akachukua mkate, akashukuru, akaumega, akawapa akisema, โHuu ni mwili Wangu unaotolewa kwa ajili yenu, fanyeni hivi kwa ukumbusho Wangu.โ (Luka 22: 19). Kwa namna hii alitupa mwili wake.
Alisema fanyeni kwa ukumbusho wangu na Sio wa mwili wangu.
Hivyo Ekaristi ni Yesu Mwenyewe aliye Mungu. Ndiyo sababu tunaabudu Ekaristi Takatifu.
Ishi kama Penseli ili uwe mtu bora
Muumbaji wa penseli alipomaliza kuiumba penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi.
โKuna vitu sita unatakiwa uvitambue, โ Aliiambia penseli,
โKabla sijakutuma kwenda kutumika, unatakiwa uviweke akilini vitu hivyo na usivisahau kamwe. Vitakusaidia siku zote na utakuwa penseli bora maisha yako yote.โ
Alisema muumbaji wa penseli.
โMoja,โ alianza kuvitaja,โutakuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi, lakini kama utakubali na utaruhusu kuongozwa na mkono wa mtumiaji wakoโ
โMbiliโ aliendelea kutoa nasaha, โutapata maumivu makali kutokana na kuchongwa mara kwa mara. Lakini vumilia kwani itakusaidia kuwa penseli bora na kuandika vizuri.โ
โTatu, utakuwa na uwezo wa kusahihisha makosa utakayo yafanya.โ
โNne, kitu pekee cha muhimu katika maisha yako ni kile kilicho ndani yako kwa sababu ndicho chenye uwezo wa kuandika.โ
โTanoโ alisisitiza mtengenezaji penseli, โkwenye kila sehemu utakayotumika, utaacha alama yako. Hata ikiwa ni kwenye sehemu ngumu au mbaya kiasi gani, ni lazima alama yako ibaki.
โNa sitaโ, alimalizia muumbaji yule wa penseli, โipo siku utaisha na kupotea. Hivyo usiwe na hofu wala woga wala hudhuni uikaribiapo siku hiyo na ukaogopa kutimiza wajibu wako kwa kuhofia kuisha. Ukiogopa kuisha hautotumika na umuhimu wako hautonekana kwani hautatimiza wajibu uliombiwa kuufanyaโ
Penseli ilielewa na kuahidi kukumbuka na ikaingia sokoni ikiwa na dhamira yake moyoni.
Sasa tutumie mfano huo wa penseli katika maisha yetu halisi. Ukivikumbuka vitu hivyo sita ilivyopewa penseli, utaweza kuwa mtu bora kabisa kwenye maisha yako yote.
Moja, una uwezo wa kufanya mambo mengi na makubwa, kama utajiweka kwenye mikono ya Mungu.
Mbili, utakutana na magumu mengi ya kuumiza, lakini hayo ndiyo yatakufanya uwe mtu imara na bora, usiyakimbie.
Tatu, una uwezo wa kurekebisha makosa yote uliyoyafanya. Usijilaumu.
Nne, sehemu yako ya muhimu ni ile iliyo ndani yako kwani ndiyo inayoandika maisha yako. Ilinde.
Tano, kila sehemu utakayopita, acha alama yako kwa kufanya mazuri yatakayokufanya ukumbukwe daima, bila kujali mazingira. Timiza wajibu wako kwa kiwango cha juu.
Sita, tambua kuwa ipo siku utakufa. Usiwe na hofu yoyote juu ya kifo kwani ukiogopa kifo hutafanya lolote hapa duniani.
Tumia mfano huu wa penseli upate ujasiri wa kutambua kuwa wewe ni mtu muhimu hapa duniani na umeumbwa kwa madhumuni maalumu na umepewa uwezo mkubwa sana na Muumba wako! Ni wewe pekee mwenye uwezo wa kutimiza dhamira uliyotumwa na Muumba.
UBARIKIWE SANA.
Swala la Mapadri kutooa limeandikwa wapi katika Biblia?
JE,SHERIA YA MAPADRE KUTOOA NA KUISHI USEJA IMEANDIKWA WAPI KATIKA BIBLIA AU IMETUNGWA TU NA PAPA?
“Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke,8.Lakini nawaambia wale wasiooa bado na wajane heri wakae kama mimi nilivyo”
“32Lakini nataka msiwe na masumbufu.Yeye asiyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya Bwana ampendezeje Bwana;33.bali yeye aliyeoa hujishughulisha zaidi na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendeza mkewe.34-Tena iko tofauti kati ya mke na mwanamwali.Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana ili apate kuwa mtakatifu mwili na Roho.Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii,jinsi atakavyompendezesha mumewe.,35.Nasema hayo niwafaidie ninyi,si kwamba niwategee tanzi,bali kwaajili ya vile vipendezavyo,tena mpate kumhudumia Bwana pasipo kuvutwa na mambo mengine”
“Wanafunzi wake wakamwambia,kama mambo ya mme na mke yakiwa hivyo ni afadhali kutuooa kabisa.Lakini Yeye akawaambia ‘SI WOTE WAWEZAO KULIPOKEA NENO HILO,ILA TU WALE WALIOJALIWA,maana wako MATOWASHI waliozaliwa katika hali hiyo toka matumboni mwa mama zao;tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi,tena wako Matowashi WALIOJIFANYA WENYEWE KUWA MATOWASHI KWAAJILI YA UFALME WA MBINGUNI’,awezaye kulipokea neno hili na alipokee”
“Ndipo Petro akajibu akamwambia ‘Tazama sisi tumeacha vyote tukakufuata wewe,tutapata nini basi?29.Amini nawaambia,kila mtu aliyeacha nyumba au ndugu wa kiume au wakike,au baba au mama au watoto au mashamba KWAAJILI YA JINA LANGU,atapokea mara mia zaidi na kuurithi uzima wa milele”
Unayopaswa kujua Kuhusu Kipindi cha Majilio
madhehebu mbalimbali ya Ukristo (kama vile
Kanisa Katoliki, ya Waorthodoksi , Waanglikana
na Walutheri ) kinatangulia sherehe ya Noeli na
kuanza mwaka wa liturujia. Kinaweza kudumu
kati ya siku 22 na 40.
ujio (wa Yesu Kristo ), lakini jina la Kiswahili ni
sahihi zaidi kwa sababu linadokeza kuwa ujio
wa Yesu ni kwa ajili yetu na kuwa alikuja
zamani, anakuja kila siku na atakuja kwa
utukufu mwisho wa dunia.
Maana ya Majilio katika
maisha ya binadamu
Sisi binadamu hatuwezi kuishi daima katika
hali ileile bila ya matazamio. Hasa kijana
anatarajia mambo mapya tena mema. Hivyo
tunajitahidi kuyapata. Asiyetazamia chochote
amevunjika moyo, hana hamu ya kuishi. Lakini
matazamio ya kibinadamu yakimfikia mtu
hayamridhishi moja kwa moja. Kristo tu
anatimiza hamu zote kwa kumkomboa kutoka
unyonge. Majilio yanatukumbusha kila mwaka
matarajio ya kweli na hivyo yanaamsha hamu
ya kuishi kwa bidii ya kiroho.
Katika mwaka wa liturujia ya Kanisa la Roma ,
sherehe ya Noeli inaandaliwa na kipindi cha
Majilio ambacho kina mambo mawili:
kinakumbusha Mwana wa Mungu alivyotujilia
mara ya kwanza, na papo hapo kinatuandaa
kumpokea atakapotujilia tena siku ya mwisho .
Kufuatana na hayo kina sehemu mbili: hadi
tarehe 16 Desemba kinahusu zaidi kurudi kwa
Bwana; siku nane za mwisho kinatuelekeza
moja kwa moja kuadhimisha kuzaliwa kwake.
Urefu wa Majilio unategemea siku
inayoangukia Noeli, kwa kuwa ni lazima yawe
na Jumapili nne. Hivyo basi yanaanza kwa
Masifu ya Jioni ya kwanza ya Jumapili
inayoangukia tarehe 30 Novemba au tarehe ya
jirani zaidi; yanakwisha kabla ya Masifu ya
Jioni ya kwanza ya Noeli.
Kwa jumla ni kipindi cha toba: rangi yenyewe
ni zambarau; haziruhusiwi sherehe za fahari;
ala za muziki na maua vinaweza kutumika
kwa kiasi tu. Masharti hayo yanalegezwa
katika Jumapili ya tatu kwa sababu ya furaha
ya kuona tunakaribia sherehe yenyewe.
Katika kipindi hicho tunaadhimisha tumaini la
Israeli lililotimizwa Yesu alipokuja katika
unyenyekevu wa umbile letu; pia tunangojea
arudi kwa utukufu. Kama alivyotekeleza ahadi
mara ya kwanza, atazitekeleza pia mara ya
pili, ingawa kwake miaka elfu ni kama siku
moja tu. Kati ya majilio hayo mawili, Bwana
anatujilia mfululizo kifumbo katika sakramenti
(hasa ekaristi ) na katika maisha ya kila siku
kwa njia ya matukio na watu (hasa maskini ).
Basi tunapaswa kuwa tayari daima kumpokea
ili siku ya mwisho tukamlaki, naye
atukaribishe kwenye uzima wa milele. Pia
tunapaswa kumuomba aje kutukomboa, yeye
aliye tumaini letu.
wanatuongoza tukutane na Yesu:
1. Isaya
nabii wa tumaini, mwenye kipaji cha kutokeza
matazamio ya binadamu na kumhakikishia
atatimiziwa na Mwokozi
. 2. Yohane Mbatizaji ,
mwenye kuhimiza toba kwa kuwa tunapaswa
kupindua maisha yetu ili tukutane vema na
Kristo.
3. Maria , bikira aliyekuwa tayari
kumpokea Masiya kwa upendo na kushirikiana
naye katika kutimiza mpango wa wokovu .
Tukiwafuata hao watatu tunaweza kujipatia
maadili yale yanayotuandaa kumpokea
Mwokozi anapotujilia: ndiyo matunda maalumu
tunayotarajiwa kuyachuma wakati wa Majilio:
1. Kukesha katika imani, sala na kutambua
ishara za Bwana kutujilia katika nafasi yoyote
ya maisha na mwishoni mwa nyakati.
2.Kuongoka kwa kufuata njia nyofu.
3.Kushuhudia furaha inayoletwa na Yesu kwa
kuwa na upole na uvumilivu kwa wenzetu, kwa
tumaini la kuwa bidii zetu zinawahisha ufalme
wa Mungu wenye heri isiyo na mwisho.
4. Kutunza unyenyekevu kwa kufuata mifano ya
maskini wa Injili ambao ndio waliompokea
Mkombozi .
https://ludovicktmedia.blogspot.com/
Mahaba kwa wanawake wa siku hizi
Wanawake wengi siku hizi hawajui au hawataki kuonesha mahaba
Nimefanya kautafiti kangu kadogo nimegundua wanawake wengi siku hizi hawaonyeshi mahaba yani kwa ujumla hawako “Romantic”. Wanawake wengi siku hizi akipata mwanaume anaona amepata mtu wa kumsaidia shida zake kwa hiyo hata akiwa ndani ya mahusiano anafikiria zaidi kutatuliwa shida zake kuliko mahusiano yenyewe.
๐
Wanawake wa siku hizi wengi, kwa mfano umemtoa out kidogo mkapate walau msosi sehemu nzuri, mkianza kula mpaka mnamaliza hakumbuki hata kukulisha kidogo kimahaba. Unakuta anakula msosi kimpango wake utafikiri anakula na kaka yake. Mnatoka kidogo mnatembea unakuta anatembea na wewe utafikiri anatembea na kaka yake; yani unaweza ukamuacha nyuma kidogo au akawa mbele yako anashindwa kujiongeza kupitisha mkono wake kwenye kikwapa chako na kukushika kimahaba.
๐
Wakati mwingine anakuona jasho linakutoka usoni anashindwa hata kukufuta kimahaba anakutazama tu utafikiri wewe ni kinyago cha mpapure. Wakati anakuaga anaondoka utafikiri anamuaga kaka yake hakupigi hata busu. Mwanamke unazungumza nae hakushiki hata ndevu zako kimahaba, mwanamke unakuwa nae hakufunyii massage wala hakukati mara moja moja kucha zako kimahaba.
๐
Wakati mwingine unakuta umekaa nae mwaka mzima kwenye mahusiano lakini hajawahi kukwambia neno “Nakupenda”mpaka wewe uanze kumwambia kwanza.
๐
Wanawake wengi wa siku hizi wanapenda kudekezwa, kubembelezwa na kupewa pesa ndio maana wengi utasikia wakisema “nataka mwanaume Romantic na mwenye pesa” lakini hawajiulizi je, wao ni Romantic? Au sisi wanaume hatuhitaji hayo mahaba ya wanawake?
๐
Asili ya mwanamke ni mfariji mkuu wa mwanaume lakini siku hizi wanawake wengi wamekuwa stress kwa wanaume.
๐
Note: Hakuna mwanaume mbahili kwa mwanamke Romantic.
Yafahamu Mambo Mbalimbali kuhusiana na Wanawake kwa Ku-Download Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE
Kitabu hiki kina topiki Zifuatazo;
1. Mambo anayohitaji mwanamke kutoka kwa Mwanaume
2. Mambo yanayowavutia wanawake kutoka kwa wanaume
3. Mambo wanayoyapenda wanawake wakati wa kufanya mapenzi
4. Dalili za mwanamke kicheche
5. Maswali ya kujiuliza kama mwanamke anakupenda kwa dhati au anakudanganya
6. Tabia za mwanamke anayekupenda lakini hawezi kusema
7. Ishara za mwanamke aliyevutiwa na wewe
8. Dalili za mwanamke anayeelekea kukukubali
9. Mambo ambayo mwanamke hawezi kukwambia
10. Njia za kudumisha na kuamsha mapenzi na mwanamke
Kitabu hiki ni Soft copy [pdf] kwa hiyo unaweza kusoma moja kwa moja kirahisi kabisa hata kwenye simu yako. Utatumiwa Kopi ya kitabu hiki kwenye email yako na utaweza kukihifadhi na kusoma wakati wowote utakaotaka.
-
Familia, Mapenzi na Mahusiano
๐Kitabu cha SIRI ZA MWANAMKE๐ง๐๐
Original price was: Sh7,500.Sh3,000Current price is: Sh3,000. Download Now
Historia Fupi ya Ibada ya Rozari
huwa mwezi wa tano na mwezi wa kumi
ni miezi ambayo imewekwa kwa ajili ya
Bikira Maria na Mama Kanisa. Hivyo
hiyo miezi huwa inasaliwa rozari.
Wengi waweza kujiuliza kuwa ni kwa
nini ifanyike miezi hiyo? Yafuatayo nimajibu, mwezi wa tano umewekwa kwa
heshima ya Bikira Maria kutokana na
nini kilitokea katika historia hapo
nyuma.
watano kwa miaka yote ulikuwa ni
mwezi ambao sikukuu nyingi za
kiserikali ndo zilikuwa zikifanyika.
Kanisa kwa kutambua hilo nalo
likahidhinisha pia mwezi wa tano uwe
ni mwezi wa Rozari, na kwa makusudi
zaidi Kanisa lililenga kuwa sherehe hizo
ziendane na taratibu za wakristu, ni
kwa msingi huo sherehe hizo ziliendana
na mwezi wa rozari na kutokea hapo
ikahidhinishwa kuwa mwezi wa tano wa
mwaka ni mwezi wa Bikira Maria. Pia
mwezi wa kumi (October) pia ni mwezi
wa Bikira Maria na pia ni mwezi wa
Kusali Rozari kutokana na historia ya
hapo nyuma pia, na ilikuwa kwamba
baada ya ushindi wakristo walioupata
katika vita baina yao na yule aliyeitwa
Lepanto mnamo 7 October, 1571, Papa
wa wakati ule Papa Pius V aliufanya
huo ushindi kuwa ulitokana na
maombezi ya Bikira Maria, na alisema
kuwa rozari ni silaha kubwa hata kuliko
silaha kubwa za kivita. Ni Kwa msingi
huu tunaona kuanzia hapo mwezi wa
kumi ukawa mwezi uliotengwa na
Mama Kanisa kwa Bikira Maria, na pia
ukaitwa mwezi wa Rozari.
HISTORIA YENYEWE
kuanzishwa na Mt. Dominico
aliyezaliwa mnamo mwaka 1170 na
kufariki mwaka 1221 na hiyo sala Mt.
Dominico aliipata kwa njia ya ufunuo
ambapo Bikira Maria alimtokea na
kumwamuru awe anasali rozari. Bikira
Maria alimwamuru mtakatifu Dominico
kusali rozari kwa kipindi hicho iwe
kama silaha yake ili kupambana na
uzushi uliokuwa umeibuka ukipingana
na mafundisho ya Kanisa, na huo
uzushi uliitwa โ Albigensiaโ hili ni kundi
lilokuwa na imani kuwa Duniani kuna
nguvu nguvu mbili zenye uwiano sawa
lakini hupingana na kupigana moja
baada ya nyingine, nazo nguvu hizo ni
Mungu na Shetani. Hivyo hawa
waliamini kabisa kuwa Mungu na
Shetani wana nguvu sawa ( Dualistic )
waliamini pia kuwa dunia hii imejaa
uovu kwa kuwa iliumbwa na mwovu. Ni
kwa msingi huu Kanisa liliamua
kupambana na hawa wazushi ambao
pia walionekana kupotosha mafundisho
ya Kanisa. Ndipo tunaona Bikira Maria
anamtokea Mtakatifu Dominico na
kumwambia asali rozari ili kupambana
na mafundisho hayo ya kizushi. Ni Papa
Pio V ambaye mnamo mwaka 1569
alihidhinisha rasmi kusali rozari kwa
kanisa nzima na kuhidhinisha rozari
iwe jinsi tunavyoiona sasa. Katika zile
zama za kati, watawa wamonaki
walizoea kusali zaburi 150, na kwa
upande wa waumini walei ambao kwa
kipindi hicho hawakujua kusoma zaburi
iliwabidi wasali sala ya Baba yetu mara
150 baadala ya zaburi 150 na hizo baba
yetu walizisali kwa kuhesabu punje 150
zilizokuwa zimefungwa kwenye kamba
ndefu ambayo kwa lugha ya kitaalamu
iliitwa โ Corona โ au kwa Kiingereza โ
Crown โ kadiri ibada kwa Bikira Maria
ilivyoendelea kushamiri mnamo Karne
ya 12, sala kwa Bikira Maria
ilianzishwa na hivyo kuanza kusali
salamu maria 150 baadala ya baba yetu
150.
Salamu Maria 150 hapo baadaye
zilikuja kugawanywa katika makundi/
mafungu na Mtawa mdominica
aliyeitwa Henry Kalkar ( 1328-1408),
ambapo kila tendo la rozari lilikuwa na
mafungu 50 ya salamu Maria ambapo
pia kila fungu liligusia maisha ya Bikira
Maria na Yesu katika historia ya
wokovu wetu. Zaidi ya hapo, mtawa
mwingine wa mdominican aliyeitwa
Alanus de Rupe aliendelea kugawanya
hiyo historia ya matendo ya wokovu
wetu katika matendo ya furaha ,uchungu,
na utukufu kama tunavyoyaona sasa.
(NB Matendo ya mwanga hayo ni ya
majuzi siyo ya wakati ule). Na
nikuanzia hapo Bikira Maria amepewa
nafasi kubwa katika shirika la watawa
wa Dominican. Hivyo utamaduni wa
kusali rozari umeendelea karne hata
karne, mfano Papa Leo XIII (1878-1903)
aliweka msisitizo mkubwa juu ya ibada
ya rozari kwa Bikira Maria. Kuanzia
September 1, 1883 Baba Mtakatifu Leo
XIII aliandika jumla ya barua za
kichungaji 11 zote zikiwa zinaweka
mkazo juu ya rozari. Hivyo rozari ni
sala inayotokana na maandiko
matakatifu( Biblia). Mafumbo ya rozari
yote yanapatikana katika agano jipya
ambapo ndo tunaona matendo ya Bikira
Maria na Yesu Kristo katika wokovu
wetu.
tunakumbushwa uchungu aliopata
Bikira Maria Katika maisha yake hasa
ule utabiri wa Simeoni kwa Bikira
Maria juu ya mateso na kifo cha
mwanae Yesu, Matendo saba ya furaha
kwa Maria ambapo yaananza na
kupashwa habari kwa Bikira Maria na
Malaika wa Bwana, kupalizwa
mbinguni, na matendo ya huruma ya
Bikira Maria kwa wale ambao
wanaendelea kuteseka hapa duniani.
JE, WAKATOLIKI WANABUDU SANAMU?
KUNA TOFAUTI KATI YA KUABUDU NA KUHESHIMU
KWA NINI MUNGU PEKE YAKE ANASTAHILI KUABUDIWA?
MAMBO MAKUU NA MUHIMU KATIKA IBADA YA SANAMU
JE, BINADAMU TUNAHITAJI SANAMU AU PICHA?
KWA NINI WAKATOLIKI HAWAABUDU SANAMU AU PICHA?
IBADA YA KWELI YA SANAMU INAKUWAJE?
JE, MUNGU ANACHUKIA KILA SANAMU NA PICHA?
UBAYA WA SANAMU AU PICHA UKO WAPI?
BIBLIA INAWEZA KUTUSAIDIA KUIELEWA IBADA YA SANAMU?
JE, IJUMAA KUU WAKATOLIKI WANAABUDU NINI?
NINI HASA KINAFANYIKA SIKU YA IJUMAA KUU?
Mafundisho Kuhusu Bikira Maria
DOGMA ZA KANISA KATOLIKI KUHUSU BIKIRA MARIA.
kumhusu Bikira Maria ambayo ni lazima
kila Mkatoliki ayasadiki kutokana na
ufunuo wa Mungu: 1. B. Maria
mkingiwa dhambi ya asili 2. B. Maria
Mama wa Mungu 3. B. Maria Bikira
daima 4. B. Maria kupalizwa mbinguni
mwili na roho
MKINGIWA DHAMBI YA ASILI
neemaโ (Lk 1:28) maana ndiye tunda
bora la ukombozi ulioletwa na Yesu. Ni
imani ya Wakatoliki kwamba kwa stahili
za Mwanae alikingiwa asirithi kwa wazazi
dhambi ya asili na madonda
yanayotokana nayo, wala asitende
dhambi maisha yake yote. Kwa maneno
mengine, Bikira Maria tangu atungwe
mimba Mungu alimkinga na kila doa la
dhambi kwa kutazamia stahili za Yesu
Kristo aliye Mkombozi wa binadamu
wote. Ndiye aliyekombolewa kwa namna
bora kushinda viungo vyote vya Kanisa.
Maisha yake yote hakutenda dhambi
hata moja. Mapokeo ya mashariki
yanamuita โA Panagiaโ = โMtakatifu tuโ.
Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX
mwaka 1854, halafu mwaka 1858 Bikira
Maria alijitambulisha kama Mkingiwa
kwa Bernadeta Soubirous huko Lurdi
( Ufaransa ). Tena mwaka 1917 huko
Fatima ( Ureno ) aliwafunulia Lusia,
Fransisko na Yasinta Marto moyo wake
safi usio na doa.
MAMA WA MUNGU
โHapo mwanzo kulikuwako Neno, naye
Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno
alikuwa Munguโ (Yoh 1:1). Huyo Mungu
Mwana alitwaa ubinadamu katika Bikira
Maria akazaliwa mtoto, jina lake Yesu,
maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni
binadamu kama sisi katika yote
isipokuwa dhambi. Ubinadamu wa Yesu
unategemea Nafsi yake ya Kimungu:
akisema, โMimiโ, ni kwa Nafsi yake hiyo.
Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi,
โKweli nawaambia, kabla Abrahamu
hajazaliwa, nalikuwepoโ (Yoh 8:50).
โKama vile Baba alivyo asili ya uhai,
ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili
ya uhaiโ (Yoh 5:26).
Mtume Paulo akaeleza, โWakati
maalumu ulipotimia Mungu alimtuma
Mwanae aliyezaliwa na mwanamkeโ (Gal
4:4). Bikira Maria ni Mama wa Mungu
kwanzia wakati huo: tangu Bikira Maria
alipojaliwa kumchukua mimba, kumzaa,
kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye
kwa asili ni Mungu. Cheo hicho
kimemuinua juu kuliko hata malaika.
โMalaika alimwambia, โHicho
kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu,
Mwana wa Munguโโ (Lk 1:35).
Dogma ilitangazwa mwaka 431 kwenye
Mtaguso wa Efeso uliomuita โMzazi wa
Munguโ, ukisema Maria anastahili
kuitwa hivyo kwa sababu Mwana wa
milele wa Mungu, ambaye ni Mungu
sawa na Baba, alifanyika mtu toka
kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa:
โUmebarikiwa wewe katika wanawake,
naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Limenitokeaje neno hili, hata mama wa
Bwana wangu anijilie mimi?โ (Lk
1:42-43). Ungamo hilo la Elizabeti
likakamilishwa na Mtume Thoma
aliyemuambia Yesu mfufuka: โBwana
wangu na Mungu wangu!โ (Yoh 20:28).
BIKIRA NA MAMA
kuwa Yesu alitungwa bila ya mchango
wa mwanamume. La ajabu zaidi katika
imani hiyo ni kwamba hata uzazi
wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali
uliutakasa: ni Bikira daima. Ingawa akili
inasita, ni lazima kukiri na malaika,
โHakuna lisilowezekana kwa Munguโ (Lk
1:38). Yosefu , ingawa kisheria alikuwa
mume wake, hakutenda naye tendo la
ndoa.
Ni imani ya Wakatoliki na Waorthodoksi
kuwa Mama wa Yesu anastahili kuitwa
โBikira daimaโ kwa sababu alimchukua
mimba akiwa bikira, akamzaa bila ya
kupotewa na ubikira, akabaki bikira hadi
mwisho wa maisha yake. Hamu yake ya
kuwa bikira hata kisha kuchumbiwa
inajitokeza katika jibu alilompa malaika
aliyemtabiria mimba: โLitakuwaje neno
hili, maana sijui mume?โ (Lk 1:35). Ni
kielelezo cha Wakristo ambao Mtume
Paulo aliwaandikia: โNawaonea wivu,
wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea
mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira
safiโ (2Kor 11:2), โmpate kumhudumia
Bwana pasipo kuvutwa na mambo
mengineโ (1Kor 7:35).
Wanaosemwa katika Injili โndugu zake
Yesuโ si watoto wa Bikira Maria, bali
ndugu wa ukoo waliokuwa jirani sana
na familia hiyo takatifu. Kama Bikira
Maria angekuwa na watoto wengine,
Yesu angekuwa amefanya kosa la
kuwanyangโanya Mama yao na
kumfanya awe Mama wa mtume
Yohane alipomkabidhi msalabani,
โโMwana, tazama Mama yakoโ. Na tangu
saa ile huyo mwanafunzi alimchukua
akae nyumbani kwakeโ (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo
anayeitwa na mtume Paulo โndugu yake
Bwanaโ (Gal 1:19): Yakobo huyo alikuwa
maarufu katika Kanisa la Yerusalemu
(Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal
2:9). Yakobo huyo si mtume Yakobo
kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni
Yakobo ndugu yake Yose na mama yao
kwenye Injili anaitwa โMaria mwingineโ,
si Maria Mama wa Yesu. โWalikuwepo
pia wanawake waliotazama kwa mbali.
Miongoni mwao akiwa Maria
Magdalena , Salome na Maria mama wa
akina Yakobo mdogo na Yoseโ (Mk
15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida
kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa
wengi hivyo, tujue kuwatofautisha
kwenye Injili, ambazo zinamtaja Bikira
Maria kama โMama wa Mungu”
KUPALIZWA MBINGUNI MWILI NA ROHO
Maria alipalizwa mbinguni mwili na
roho, ishara ya mwanamke mshindi.
โIshara kubwa ikaonekana mbinguni,
ambapo mwanamke aliyevikwa jua , pia
na mwezi chini ya miguu yake, na taji la
nyota kumi na mbili juu ya kichwa
chakeโ (Ufu 12:1). Maneno ya shangilio
lake yametimia: Mungu โamewaangusha
wakuu katika viti vyao vya enzi; na
wanyonge amewakwezaโ (Lk 1:52).
Imani hiyo ya mapokeo ya kale,
yanavyoshuhudiwa na Mababu wa
Kanisa, ilitangazwa rasmi na Papa Pius
XII kwa niaba ya ma askofu wote mwaka
1950.
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake

35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Je Bikira Maria Alizaa Watoto Wengine?
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Yosefu likufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni โBikira daimaโ.
Ndugu wa Yesu wanaosemwa katika Injili ni kina nani?
wa Bikira Maria wala Yosefu mtakatifu, bali ndugu wa kiukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama
Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, je, Yesu Bwana wetu asingekuwa amefanya kosa la kiudugu
kuwanyangโanya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, โโMwana, tazama
Mama yakoโ. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwakeโ (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo โndugu yake Bwanaโ (Gal 1:19): Yakobo huyo
alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume
Yakobo mwana wa Alfayo, wala mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na
mama yao kwenye Injili anaitwa โMaria mwingineโ, si Maria Mama wa Yesu. โWalikuwepo pia wanawake
waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo
na Yoseโ (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue
kuwatofautisha kwenye Injili. Bikira Maria Injili zinamtaja kama โMama wa Yesuโ.

MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA BIKIRA MARIA
Leo nimeamua kutoa makala kuhusu Bikira Maria Baada ya maswali mbalimbali kuibuka kuhusu nafasi yake kwetu sisi. Chanzo cha makala hii ni www.alfagems.com
MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA B. MARIA
imani yao ama wenyewe wanavyojisikia kwa namna fulani, tunajikuta tukichanganyikiwa na pengine kuona aibu ya
kumheshimu Mama Bikira Maria. Tunapoanza kuchunguza nafasi yake katika fumbo la ukombozi wa mwanadamu,
tunakiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49). Halafu tunakiri kwa unyenyekevu
wote pamoja na Yohane Mbatizaji, โMtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Munguโ (Yoh 3:27). Hivyo yale yote
tunayoyasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia mwenyewe bali amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kuitikia kwa
hiari fumbo la mpango wake.
MAANDIKO YANASHUHUDIA UMUHIMU WA WATU UNAOTOFAUTIANA
ajili ya taifa lake. Abrahamu alimuamini na kuwa tayari kumtolea sadaka mwanae Isaka, tukio lililomfanya apate
baraka ya pekee ya kuwa baba wa waamini (Mwa 22:15-18). Yosefu, kipenzi wa Yakobo, alikuwa mwaminifu hata
akaliokoa taifa lisiangamie kwa njaa (Mwa 50:20). Musa ndiye mkombozi wa taifa la Mungu katika Agano la Kale:
aliongoza Israeli kutoka utumwani Misri akalipatia sheria kutoka kwa Mungu katika mlima Sinai. Maandiko ya
Agano la Kale yanakiri, โWala hajainuka kiongozi kama alivyokuwa Musaโ (Kumb 34:10-12). Kwa kuwa watu hao ni
wengi mno tunaorodhesha wafuatao: Yoshua, Debora, Gideoni, Samsoni, Samweli, Ruthu, wafalme Daudi na
Solomoni, manabii Eliya, Yeremia na Ezekieli. Nabii Isaya ana sifa ya pekee katika kumchora Masiya. Mwishoni
Bwana Yesu mwenyewe anamsifu Yohane Mbatizaji akisema, โNi mkuu kati ya uzao wa wanawakeโ (Lk 7:24-28).
Bikira Maria ana nafasi gani kati yao? Hao tuliowataja walitenda kweli mambo makuu kwa imani, lakini Bikira
Maria yuko juu sana kupita hao wote, tena kwa mbali: yeye ni malkia wa makundi yote ya mbinguni, sio ya watu
tu, bali hata ya malaika. Mapokeo ya mashariki humuita โdaraja linalounganisha dunia na mbinguโ, โmfano
aliouona Yakoboโ (Mwa 28:12).
BIKIRA MARIA KATIKA BIBLIA
1. UTABIRI KUHUSU BIKIRA MARIA, EVA MPYA
Kwa sababu Eva wa kale alidanganywa na kuangushwa na Shetani, hivyo alitenda dhambi. Kumbe Maandiko
matakatifu yanatupatia utabiri kuhusu Eva mpya atakayemshinda adui (Shetani) kwa kumponda kichwa: โNitaweka
uadui kati yako na huyu mwanamke, kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa chakoโ (Mwa 3:15).
โTazama Bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamuita jina lake Emanueli, yaani Mungu
pamoja nasiโ (Isa 7:14). Dondoo hilo lilinganishwe na Lk 1:34-35, โMariamu akamwambia malaika, Litakuwaje
neno hili, maana sijui mume? Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu akakujilia juu yako, na nguvu zake
Aliye juu zitakufunika kama kivuli. Kwa sababu hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Munguโ.
Utabiri mwingine wasema, โLitatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa
matunda. Na Roho wa Bwana atakaa juu yake, Roho ya hekima na ufahamu, Roho wa shauri na uwezo, Roho wa
maarifa na ya kumcha Bwanaโ (Isa 11:1-2). Je, shina hilo si yeye Mama Bikira Maria, na tawi alilochipusha si
Mwanae Bwana wetu Yesu Kristo?
โUmebarikiwa wewe katika kila hema la Yuda na katika kila taifa, nao wanaposikia jina lako watafadhaika.
Imani yako haitatoka mioyoni mwa watu wanaoukumbuka uweza wa Mungu mileleโ (Yudithi 14:7; 15:9).
Linganisha dondoo hili na Lk 1:42, โAkapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe kuliko wanawake wote,
na yeye utakayemzaa amebarikiwaโ. Je, utasema Bikira Maria ni mtu wa ziada katika mpango wa Mungu?
Tena tunasoma, โImba, ee binti Sion, piga kelele, ee Israeli, furahi na kushangilia kwa moyo wako wote, ee binti
Yerusalemu. Mfalme wa Israeli, naam, yeye Bwana yu katikati yakoโ (Sef 3:14-15). Linganisha dondoo hilo na
Injili: โMalaika akaingia nyumbani mwake akamwambia, Furahi Maria, umejaliwa neema kubwa, Bwana yu pamoja
naweโ (Lk 1:28).
2. BIKIRA MARIA KATIKA AGANO JIPYA
Maria alipokubali fumbo la umwilisho wa Mwana wa Mungu, akisema kwa hiari, โMimi ni mtumishi wa Bwana, na
iwe kwangu kama ulivyonenaโ (Lk 1:38).
Je, Bikira Maria ni bahasha? Siku hizi kuna baadhi ya waheshimiwa ambao wanadhani kujua Maandiko kuliko
watu wengine, tena wanadai wanaye Roho Mtakatifu; kumbe wanadiriki kumuita Mama huyo mtakatifu, eti ni
โbahashaโ ambayo ikileta barua haina kazi! Jambo hili linasikitisha sana na sio tu kumkosea heshima Mama yetu
mpendwa wa mbinguni, bali inaweza pia kuwa kufuru kwa Mwenyezi Mungu aliyemuumba kama msaidizi wa
Mkombozi aliyejaa neema.
Manabii mbalimbali kwa mwanga wa Roho Mtakatifu walimuagua kwa heshima; Mama Elizabeti alijiona hastahili
kutembelewa naye akamuita, โMama wa Bwana wanguโ; mzee Simeoni alimuagulia mateso yenye uchungu kama
upanga yatakayopenya moyowe. Bwana Yesu aliyefurika Roho Mtakatifu tangu nukta ya kuchukuliwa mimba,
wakati alipokaribia kufa pale msalabani alimuita, โMamaโ; jumuia ya Mitume na wafuasi wa kwanza walimtaja
kipekee ilivyo ishara ya heshima. Je, Roho Mtakatifu ndiye anayewaongoza hawa ndugu zetu wamuite bahasha? Je,
ni Roho yuleyule aliyewaongoza Mitume na manabii ama roho ya aina nyingine? โWapenzi wangu, msisadiki kila
mtu asemaye kwamba ana Roho wa Mungu, bali chunguzeni kwa makini kama huyo mtu anaongozwa na Roho wa
Mungu au la, maana manabii wengi wa uongo wamezuka ulimwenguniโ (1Yoh 4:1).
Bikira Maria sio โchomboโ tu, bali mshiriki wa kazi ya ukombozi ya Mwanae. Kadiri ya mtume Paulo kuteseka ni
kutimiliza yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya Kanisa, โNa sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu,
maana kwa mateso yangu hapa duniani nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristoโ (Kol
1:24). โโฆ maana tukiyashiriki mateso yake Kristo, tutaushiriki pia utukufu wakeโ (Rom 8:17b). Katika hilo la
kumfuata Mwanae katika mateso Bikira Maria alitabiriwa wazi na mzee Simeoni, โTazama huyu amewekwa kwa
kuanguka na kuinuka wengi katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Nawe mwenyewe uchungu ulio kama
upanga utauchoma moyo wakoโ (Lk 2:34-35).
Bikira Maria alishiriki mateso ya ukimbizi huko Misri kwa lengo la kumficha Mwanae asiteswe na Herode, โHivyo
Yosefu aliamka akamchukua mtoto pamoja na Mama yake akaondoka usiku akaenda Misri akakaa huko mpaka
Herode alipokufaโ (Math 2:14-15).
3. BIKIRA MARIA MWOMBEZI KATIKA HARUSI YA KANA:
huruma wenye shida: kwa ombi lake huko Kana ya Galilaya Yesu aligeuza maji kuwa divai, na wanafunzi wake
wakamwamini (Yoh 2:1-12).
4. BIKIRA MARIA AFANYWA EVA MPYA:
akamwita mkewe jina lake Hawa, kwa kuwa ndiye aliye Mama wa walio haiโ (Mwa 3:20). Hata hivyo Agano Jipya
linaonyesha Adamu na Eva wa zamani wametuletea kifo (Rom 5:12).
Yesu, aliye Adamu mpya, alipokuwa anakamilisha sadaka ya ukombozi pale msalabani alimfanya Bikira Maria
awe Eva mpya kwa kitendo cha kumkabidhi mwanafunzi, tena yule aliyempenda zaidi. โBasi Yesu aipomwona
Mama yake na yule mwanafunzi aliyempenda amesiMama karibu akamwambia Mama yake, Mama, tazama
Mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama Mama yakoโ (Yoh 19:26-27). Zaburi yasema, โLakini juu
ya Sion itasemwa, Sion ni Mama yao wote; Mungu mkuu ameuthibitisha. Mwenyezi Mungu ataorodhesha mataifa
na kuandika juu ya kila moja, Huyu chanzo chake ni Sionโ (Zab 87:5-6).
Pale msalabani Bikira Maria:
โข alifanywa Mama wa wote wanaompenda Mwanae;
โข alifanywa malkia wa wafiadini;
โข kisha kumzaa pasipo uchungu Bwana wa uzima, pale alituzaa sisi kwa uchungu wa kutisha uliotokana na
kumuona Mwanae akifa msalabani. Hata hivyo Bikira Maria aliendelea kumuamini Mwanae aliyeonekana
ameshindwa;
โข katika kuteswa kwa Yesu Bikira Maria alishuhudia hatua kwa hatua; wanafunzi wa Yesu walipokimbia na
kumtazama kwa mbali, Bikira mtakatifu alikuwa karibu akaona vema kila teso lililompata. Tena
kutokana na fungamano la upendo wa ajabu lililokuwepo kati ya Yesu na Mamaye, aliposhuhudia mateso
ya Mwanae aliteseka sana katika moyo wake safi usio na doa, kiasi kwamba baadhi ya watakatifu
wanasema, Msalaba wa Yesu uliwasulubisha wote, Yesu mwilini na Mama yake moyoni. Uaguzi wa mzee
Simeoni ulitimia hivyo.
JE, BIKIRA MARIA ALIZAA WATOTO WENGINE?
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Alikufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni โBikira daimaโ.
Ndugu wa Yesu wanaosemwa katika Injili ni kina nani? Wanaosemwa katika Injili โndugu zake Yesuโ si watoto
wa Bikira Maria wala Yosefu mtakatifu, bali ndugu wa kiukoo waliokuwa jirani sana na familia hiyo takatifu. Kama
Bikira Maria angekuwa na watoto wengine, je, Yesu Bwana wetu asingekuwa amefanya kosa la kiudugu
kuwanyangโanya Mama yao na kumfanya awe Mama wa mtume Yohane alipomkabidhi msalabani, โโMwana, tazama
Mama yakoโ. Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwakeโ (Yoh 19:27).
Katika Agano Jipya yupo Yakobo anayeitwa na mtume Paulo โndugu yake Bwanaโ (Gal 1:19): Yakobo huyo
alikuwa maarufu katika Kanisa la Yerusalemu (Mdo 12:7; 15:13-21; 21:18-20; Gal 2:9). Yakobo huyo si mtume
Yakobo mwana wa Alfayo, wala mtume Yakobo kaka yake Yohane (Lk 6:12-16), bali ni Yakobo ndugu yake Yose na
mama yao kwenye Injili anaitwa โMaria mwingineโ, si Maria Mama wa Yesu. โWalikuwepo pia wanawake
waliotazama kwa mbali. Miongoni mwao akiwa Maria Magdalena, Salome na Maria mama wa akina Yakobo mdogo
na Yoseโ (Mk 15:40). Maria lilikuwa jina la kawaida kwa Wayahudi: akina Maria wakiwa wengi hivyo, tujue
kuwatofautisha kwenye Injili. Bikira Maria Injili zinamtaja kama โMama wa Yesuโ.
JE, WAKATI WA KUFANYA UTUME YESU ALIMDHARAU MAMA YAKE?
Hivyo hukwazwa na semi kadhaa za Bwana Yesu ambazo kimsingi hazimpingi Mama yake, bali zinampongeza.
โAlipokuwa akisema hayo, mwanamke mmoja katika lile kundi la watu akasema, โHongera kwa mwanamke
aliyekuzaa na kukunyonyeshaโ. Yesu akamjibu, โBarabara, lakini heri yake zaidi yule anayelisikia Neno la Mungu na
kulishikaโโ (Mk 11:27-28).
Tena lingine lasema, โBasi, mtu mmoja akamwambia, โMama yako na ndugu zako wako nje, wataka kusema
naweโ. Lakini Yesu akamjibu huyo mtu aliyemwambia hivyo, โMama yangu ni nani, na ndugu zangu ni akina nani?โ
Kisha akanyosha mkono wake juu y aweanafunzi wake akasema, โHawa ndio Mama yangu na ndugu zangu, maana
yeyote anayefanya anavyotaka Baba yangu aliye mbinguni, huyo ndiye kaka yangu na dada yangu na Mama
yanguโโ (Math 12:46-50).
Je, sehemu hizi za Maandiko zinampinga kweli Bikira Maria au zinampongeza? Sababu:
โข Jamaa yake Elizabeti alimpongeza, tena akiongozwa na Roho Mtakatifu, โHeri yako wewe uliyesadiki
kwamba yatatimia yale uliyoambiwa na Bwanaโ (Lk 1:45).
โข Bikira mtakatifu alipopashwa habari na malaika hakukataa mpango wa Mungu, bali kwa hiari yake
alikubali fumbo la mpango wake. โMaria akasema, โMimi ni mtumishi wa Bwana, na iwe kwangu kama
ulivyonenaโ. Kisha malaika yule akaenda zakeโ (Lk 1:38).
โข Bwana Yesu alitaka kuwainua wasikilizaji wake wafuate mambo ya Kiroho kuliko ya mwilini. Hivyo ni
kweli, Bikira Maria anasifiwa kwanza kwa imani yake, iliyokuwa ya juu zaidi kushinda hata ile ya
Abrahamu, kuliko kwa kumchukua Yesu tumboni tu. Hata hivyo tusisahau kuwa Yesu, kama mtu yeyote
mcha Mungu, aliwaheshimu wazazi wake, tena tunasikia aliwatii. โBasi, akarudi pamoja nao Nazareti,
akawa anawatiiโ (Lk 2:51).
Naomba, kabla hujahukumu neno moja, angalia ujumla wake.
Yesu alizaliwa na Bikira mtakatifu, ndiye aliyemlea na kuhangaika naye huko na huko hata Misri ili kumuepusha
na kifo. Ishara ya kwanza kwenye maisha ya hadhara iliyongozwa na Bikira Maria huko Kana. Maria alikuwepo hata
wakati wa Yesu kuteswa, akiteseka pamoja naye. Pale msalabani alikabidhiwa Kanisa kwa njia ya Yohane mtume.
Bikira Maria alikuwepo hapo mwanzo wa Kanisa, na ndiye aliyelivutia zaidi Roho Mtakatifu kwa njia ya sala yake.
โHao wote walikusanyika pamoja kusali, pamoja na wanawake kadha wa kadha, na Maria Mama yake Yesu na
ndugu zakeโ (Mdo 1:14).
DOGMA ZA KANISA KUHUSU BIKIRA MARIA
ufunuo wa Mungu:
1. B. Maria mkingiwa dhambi ya asili
2. B. Maria Mama wa Mungu
3. B. Maria Bikira daima
4. B. Maria kupalizwa mbinguni mwili na roho
MKINGIWA DHAMBI YA ASILI
Yesu Kristo aliye Mkombozi wa binadamu wote. Ndiye mwanakanisa aliyekombolewa kwa namna bora kushinda
viungo vyote vya Kanisa. Maisha yake yote hakutenda dhambi hata moja. Mapokeo ya mashariki yanamuita A
Panagia = Mtakatifu tu. Dogma hiyo ilitangazwa na papa Pius IX mwaka 1854, hata mwaka 1858 Bikira Maria
alijitambulisha huko Lurdi (Ufaransa) kwa Mt. Bernadetta Soubirous kama Mkingiwa. Tena pale Fatima (Ureno)
tumefunuliwa moyo wake safi usio na doa.
MAMA WA MUNGU
naye Neno alikuwa Munguโ (Yoh 1:1). Huyo Mungu Mwana ndiye aliyetwaa ubinadamu katika Bikira Maria
akazaliwa mtoto, jina lake Yesu, maana yake Mungu Mwokozi. Huyo ni binadamu kama sisi isipokuwa hana
dhambi. Ubinadamu wa Yesu unategemea Nafsi yake ya Kimungu, hivyo akisema, โMimiโ, anamaanisha Nafsi yake
ya Kimungu. Ndiyo maana aliwaambia Wayahudi, โKweli nawaambia, kabla Abrahamu hajazaliwa, nalikuwepoโ
(Yoh 8:50). โKama vile Baba alivyo asili ya uhai, ndivyo alivyomjalia Mwanae kuwa asili ya uhaiโ (Yoh 5:26).
Je, Bikira Maria ni Mama wa Mungu tangu lini? Mtume Paulo anaeleza, โWakati maalumu ulipotimia Mungu
alimtuma Mwanae aliyezaliwa na mwanamkeโ (Gal 4:4). Ni kwanzia wakati huo: sasa imepita miaka 2006 tangu
Bikira Maria ajiliwe na sifa hiyo ya kumchukua mimba, kumzaa, kumnyonyesha na kumlea mtu ambaye kwa asili ni
Mungu. Cheo hicho kimemuinua juu kuliko hata malaika, akawa malkia wao. โMalaika alimwambia, โHicho
kitakachozaliwa kitaitwa Kitakatifu, Mwana wa Munguโโ (Lk 1:35). Dogma ilitolewa mwaka 431 kwenye Mtaguso wa
Efeso uliomuita โMzazi wa Munguโ.
BIKIRA NA MAMA
ya mchango wa mwanamume, kumbe la ajabu zaidi ni kwamba hata uzazi wenyewe haukuondoa ubikira wake, bali
uliutakasa. Ingawa akili yetu inakataa, sisi tunakiri na malaika, โHakuna lisilowezekana kwa Munguโ (Lk 1:38).
Ndiyo maana tunamkiri ni Bikira daima.
KUPALIZWA MBINGUNI MWII NA ROHO
mwanamke mshindi. โIshara kubwa ikaonekana mbinguni, ambapo mwanamke aliyevikwa jua, pia na mwezi chini
ya miguu yake, na taji la nyota kumi na mbili juu ya kichwa chakeโ (Ufu 12:1).
HESHIMA ZA LITURUJIA KWA MARIA
zinavyozidiana:
SHEREHE
1 Januari โ Bikira Maria Mama wa Mungu
25 Machi โ Bikira Maria Kupashwa Habari
15 Agosti โ Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni
SIKUKUU
8 Septemba โ Kuzaliwa kwa Bikira Maria
KUMBUKUMBU
15 Septemba โ Mama Yetu wa Huzuni
22 Agosti โ Bikira Maria Malkia
7 Oktoba โ Bikira Maria wa Rozari
21 Novemba โ Bikira Maria Kutolewa Hekaluni
KUMBUKUMBU YA HIARI
16 Julai โ Mama Yetu wa Mlima Karmeli
5 Agosti โ Kutabaruku wa Kanisa la B. Maria
Tena kila Jumamosi isiyo na adhimisho maalumu, Kanisa huadhimisha kumbukumbu ya Mama wa Mungu.
Pia zipo heshima za binafsi kwa Bikira Maria mwenye heri: mashariki tenzi na nyimbo (k.mf. Akatistos, tenzi za
mt. Efrem shemasi, na nyingine); magharibi (Roma) tunamheshimu binafsi na hata kijumuia kwa kusali rozari
takatifu. Ndiyo ibada ya binafsi inayompendeza sana baada ya zile za liturujia hata akatokea sehemu mbalimbali
duniani akihimiza tusali rozari ili tupate amani binafsi, kitaifa na kimataifa. Mwezi wa tano ni mwezi wa Maria.
Mwezi wa kumi ni mwezi wa Rozari. Mtu aliyeonja matunda ya kumheshimu Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
anajua uwezo wa maombezi yake. Kanisa linakiri neema zote za Mungu zaja kwetu kwa njia ya Maria.
Je, tunamuabudu Bikira Maria? Hapana, Bikira Maria hatumuabudu hata kidogo, bali tunamtolea heshima ya juu
kuliko watakatifu wengine. Mungu tu tunampa heshima ya โlatriaโ (kuabudu), watakatifu tunawaheshimu (dulia) na
Bikira Maria tunampa heshima sana (yuper-dulia).
Kweli Mama Bikira Maria ni โkina kisichochunguzika kwa macho ya malaikaโ (Akatistos). Ni fumbo la ajabu
alilolifanya Mungu katika mpango wa wokovu kwa ajili yake na kwa ajili yetu. Katika Injili ya Yohane Bwana Yesu
alisema, โNinayo bado mengi ya kuwaambieni, ila kwa sasa hamwezi kuyastahimili, lakini atakapokuja huyo Roho
wa ukweli atawaongoza kwenye ukweli woteโ (Yoh 16:12-13). Kwa msaada wa Roho Mtakatifu heshima kwa Bikira
Maria ilienea katika Kanisa lote tangu zamani kabisa. Tena katika Injili ya Luka kuna utabiri wa kumheshimu Bikira
Maria vizazi vyote, โKwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mdogo, hivyo tangu sasa vizazi vyote
wataniita mwenye heriโ (Lk 1:48).
Je, Bikira Maria ni Bikira Daima au alizaa watoto wengine?
Tunaweza kuthibitisha kuwa Bikira Maria hakuzaa watoto wengine kwa kunukuu Biblia Kama ifuatavyo;
1. Bikira Maria Alikuwa Bikira Kabla ya kumzaa Yesu
26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, “Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe.” 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, “Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” 34 Maria akamjibu, “Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?” 35 Malaika akamjibu, “Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. (Luka 1:26-35)
2. Biblia Haiwataji ndugu wa Yesu wakati Yosefu na Maria walipokimbilia Misri kumficha Yesu na wakati waliporudi
19 Baada ya kifo cha Herode, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto kule Misri, 20 akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, urudi tena katika nchi ya Israeli, maana wale waliotaka kumwua mtoto huyo wamekwisha kufa.” 21 Basi, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akarejea katika nchi ya Israeli. 22 Lakini Yosefu aliposikia kwamba Arkelao mwanawe Herode alikuwa mfalme wa Yudea mahali pa baba yake, aliogopa kwenda huko. Naye baada ya kuonywa katika ndoto, alikwenda katika mkoa wa Galilaya, 23 akahamia katika mji uitwao Nazareti. Ndivyo yalivyotimia maneno yaliyonenwa kwa njia ya manabii: “Ataitwa Mnazare.” Matayo 2:19-23
3. Biblia haituambii kuwa Yesu alikua na wadogo zake alipokuwa na miaka 12
41 Wazazi wa Yesu walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. 42 Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. 43 Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. 44 Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. 45 Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta. 46 Siku ya tatu walimkuta Hekaluni kati ya walimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. 47 Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. 48 Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutenda hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” 49 Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” 50 Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. 51 Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. 52 Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu. (Luka 2:41-52).
4. Kukosekana kwa neneo “Binamu” kwenye lugha ya Yesu
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
5. Biblia haitumii neno Ndugu, kaka au dada ikimaanisha ndugu wa kuzaliwa mama mmoja na baba mmoja
6. Undugu wa Yakobo, Simoni, Yosefu na Yuda kwa Yesu Sio wa mtu na kaka zake
55 Je, huyu si yule mwana wa seremala? Je, mama yake si anaitwa Maria, na ndugu zake si kina Yakobo, Yosefu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake je, si wote wako hapa pamoja nasi? Basi amepata wapi haya yote?” (Mathayo 13:55-56)
35 Yakobo na Yohane, wana wa Zebedayo, walimwendea Yesu wakamwambia, “Mwalimu, tunataka utufanyie kitu tutakachokuomba.” (Marko 10:35)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56)
19 Lakini sikuwaona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. (Wagalatia 1:19)
1 Mimi Yuda, mtumishi wa Yesu Kristo, ndugu yake Yakobo, nawaandikia ninyi mlioitwa na Mungu na ambao mnaishi katika upendo wa Mungu Baba, na katika ulinzi wa Yesu Kristo. (Yuda 1:1)
25 Karibu na msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mama yake, na dada ya mama yake, Maria mke wa Kleopa, na Maria Magdalene. (Yohana 19:25)
55 Mahali hapo walikuwapo wanawake wengi wakitazama kwa mbali. Hao ndio wale waliomfuata Yesu kutoka Galilaya wakimtumikia. 56 Miongoni mwao walikuwa Maria Magdalene, Maria mama yao Yakobo na Yosefu, pamoja na mama yao wana wa Zebedayo. (Matayo 27:55-56).
7. Yesu alimwacha Mama yake kwa Yohane kwa kuwa hakuwa na Kaka na dada wakumwachia mamaye
26 Yesu alipomwona mama yake, na karibu naye amesimama yule mwanafunzi aliyempenda, akamwambia mama yake: “Mama! Tazama, huyo ndiye mwanao.” 27 Halafu akamwambia yule mwanafunzi: “Tazama, huyo ndiye mama yako.” Na tangu saa ile huyo mwanafunzi alimchukua akae nyumbani kwake.
Angalia huyu jamaa alivyowafanyia watu uhuni bar
Jamaa kaingia Bar;
Jamaa: Muhudumu, nipe kinywaji na mpe kila mtu humu ndani kinywaji, maana wakati napata kinywaji lazima kila mtu apate kinywaji. Haraka sana muhudumu akagawa vinywaji,
Jamaa: Muhudumu nipe supu na kila mtu humu ndani mpe supu maana ninapokunywa supu kila mtu lazima anywe supu. Watu wakapewa supu tena safari hii wakapiga makofi.
Jamaa: Muhudumu nipe bili, na kila mtu humu ndani mpe bili maana wakati nalipa bili yangu kila mtu lazima alipe yake. Zogo lilianzia hapoโฆโฆ.
Baada ya kumkuta mwanamme mwingine chumbani kwake na mke wake cheki huyu anachokifanya
NAKUA(BABA) karudi kazini mwanae mdogo akamuwahi,
DOGO: Baba usiingie ndani kina jini chumbani kwenu
NAKUA: Hakuna kitu kama hicho
DOGO: Kweli baba kuna jini liko kwenye kabati lenu la nguoโฆ.
NAKUA kaingia ndani kamkuta mkewe kalala kitandani kajifunika shuka gubigubi hadi kichwani. Kaenda kwenye kabati kufungua mlango , akamkuta rafiki yake wa miaka mingi yuko uchi ndani ya kabati
NAKUA: Aise unajua we fala sana, we rafiki yangu miaka yote hiyo halafu unamtisha mwanangu eti wewe jini, hebu toka huko nenda kwenu kacheze michezo hiyo na mwanao.
SALA YA MATUMAINI
Mungu wangu,
natumaini kwako nitapewa kwa njia ya Yesu Kristu,
neema zako duniani na utukufu mbinguni,
kwani ndiwe uliyeagana hayo nasi,
nawe mwamini. Amina
Tofauti ya mke na mchepuko!!!
Mke ni kama Tv na Mchepuko ni kama Simu.
Nyumbani unaangalia Tv lakini ukitoka unatoka na simu.
Mara chache unafurahia Tv lakini Muda mrefu unacheza na simu yako.
Tv ni bure kwa maisha yako yote, lakini Simu kama hujalipia hupati huduma.
Tv ni kubwa nzito na wakati wote ni ya zamani. Lakini simu ni nzuri, nyembamba, na ni rahisi kubeba.
Gharama za huduma za tv ni ndogo sana, Lakini gharama za huduma za Simu ni kubwa na pia ni lazima kuzitimiza.
Tv ina remote lakini Simu haina.
Kitu muhimu zaidi simu ina njia mbili za kuwasiliana unaongea na unasikiliza lakini Tv unalazimika kusikiliza hata kama hutaki au unataka.
Unaweza kununua Tv mara moja na ukatumia kwa kipindi kirefu lakini Simu mara zote unabadilisha inategemea na fasheni.
Ya mwisho na ya kuzingatia
Tv haina Virusi lakini Simu inayo.
KUWA MAKINI.
Maujanja ya kumkalisha mwanamme wako nyumbani weekend haya hapa
Siku hizi wa naume licha ya kukimbia nyumba zao kwa kisingizio cha kazi maajabu weekend hasa Jumamosi utasikia wanaaga nafika hapo njiani naja naenda kununua gazeti.
Kumbe wanaenda kunywa supu unasubiri wee mpaka alasiri au jioni
Hivyo wanandoa wengi hili limekuwa tatizo mwanaume kiguu na njia asb mchana na njia kumuacha mama na watoto.
Nini kifanyike hasa weekenda Mwanaume ashinde NYUMBANI akikupumzikia??
Zipo njia nyingi mojawapo SUPU YA WEEKEND NA MAZUNGUMZO NA MKAO
Ni kweli wanawake wengi hamjuagi kuwakalisha waume home.
Anza hivi
Siku uko home wewe amka mapema kabla yake anza makeke jikoniโฆ
Mara blenda priiiiiโฆ juiceโฆ ama milk shakeโฆ. hahahaha..Utaona anasogea jikoni..
Wakati anakunywa juice ama milk shakeโฆAnza kukuna naziโฆ
Chambua mnafuโฆ
Hapo jikoni kuna kanyama kanachemkaโฆ katia kitunguu tupia viazi 2 na ndizi.Hahaha..
ile harufu ikianza kutoka utasikia anafuata maji jikoniโฆ hahahaha kwenye frijiโฆ wala hatumi..
Hahaahhaโฆ utasikia nini kiko jikoni?Hahahaa.
Mmiminie supuโฆ
Na ndizi mbili na kiazi kimoja kapilipili mbuzi pembeni..
Muulize kuna chapatiโฆMpe.. hahahahaha..Akimaliza supu nakuapia atasinzia..
.Akishtuka ugali na mnafu na nyama umeivaโฆMpe ale..Mshushie na glass ya mtindiโฆHahahaha..
analewa full Hata kama kuna mama junior anaambiwa usipigeโฆ
Hahahahahahaโฆ.Baada ya hapo acha apumzikeโฆ aogeโฆ
Kisha funga ka khanga kako kepesi jilaze pembeni.. woiiiiiiiii..
Mkimaliza muombe pesa ya sokoniโฆ
NAKUAPIA HATA KAMA JANA YAKE ALIKUPA ATAKUPA TENA.
Hahahahaha.. jamaniโฆ
Hahahahahaโฆ yani kwa raha ya supuโฆ nakuapia utaambiwa hata mama alipiga simu janaโฆ hahahaha.. ama utasikia mamii.. njoo uone njooโฆ unaitiwa kitu cha kwenye tv.. hahaha.
Hata hujaona mwanzo ila kwa raha yakasupu utaitwaโฆ
Hata kama huna kalio nakuambia utapigwa kibao hata cha mgongoโฆ. hahahahahahahahahaha.
Sasa wewe unaamka chai na mkate kama chuo cha uhaziliโฆ
Wali maharage kama jeshi la j
Hizi hapa, Aina 10 za ndoa usizozijua
Karibuni tuangalie aina hizi 10 za ndoa.
1. NDOA YA MKEKA
Inatokana na kufumaniwa na Binti wa watu.
Ndoa hii huwa Haina mahari. Hii huvunjika
mwaka mmoja tu,baada ya wanandoa kugundua
hawakuwa wakipendana!
2. NDOA YA MIHEMKO (NYEGE)
Hufungwa na vijana wenye umri wa miaka kati
mume18 mke 16.Huvunjika baada ya miaka 3 au
4 ya ndoa.
4. NDOA YA MAONYESHO
Wenye ndoa Hii hupenda kujionyesha
barabarani.Ila ndani hazina utii.Hupigana kila
wanaporudi kutoka kwenye mizunguko. Cha
kushangaza huwa hazivunjiki lakini ndiyo ndoa
zinazoongoza kwa kuchepuka!
5. NDOA YA UHAMISHO.
Hufungwa na watumishi wa vijijini na mjini. Ili wa
kijijini ahamie mjini.Mahari utoa anaetaka
kuhamia mjini. Hata kama mahari atatoa mume
lakini hii ndiyo ndoa yenye ukakasi
zaidi.Huvunjika mara tu wanapoanza kuishi wote
mjini. Salama ya hii ndoa ni kuhama kutoka mjini
kwenda kijijini.
6. NDOA YA MIMBA.
Hufungwa kwa sababu wanaoowana hawataki
kuonekana makwao kuwa wamezaa nje. Au
muolewaji alikuwa hampendi muoaji kwa
dhati.Muoaji hutumia mimba kama mtego wa
kuingia ndoani. Hii huvunjika mtoto akizaliwa na
kufikisha mwaka 1.
7. NDOA YA MALI (UTAJIRI)
Muolewaji miaka 18 au 28 Muoaji 65 au 70.Ndoa
hii pia huitwa ndoa ya babu na mjuukuu. Ndoa ya
aina hii hudumu, kwasababu mwenye kauli ni
mwenye mali. Asilimia kubwa ya waume wa ndoa
hizi hulea watoto wasio wao.
8. NDOA YA KWASABABU.
Hufungwa ili mradi muoaji au muolewaji
aonekane tu kwa jamii kuwa naye kaoa au
kaolewa.Huwa hazina utii wala upendo dhati.
Ndoa ya aina hii ikifikisha miaka 4 huwa
hazivunjiki wahusika huishi kwa mazoea.
9. NDOA YA UPENDO.
Ndoa hizi ziliishia mwaka 1978 kabla ya vita vya
kagera.Muoaji na muolewaji hawakuangalia vitu
ila utu tu ambao uliwaunganisha na kutengeneza
upendo wa kudumu. Hii ilidumu miaka yote.
10. NDOA KUCHUMA
Ndoa hii ufungwa ili mradi muoaji au muolewaji
akapate kitu au vitu fulani kutoka kwa upande
mmoja wapo. Hii hudumu miaka kadhaa
kutegemea na malengo ya mhusika. Wengine
husubiri mpaka mhusika afe,lkn hujikuta
wanakufa wao kwanza.
Kuwa mwangalifu!
Mafundisho ya kumfundisha mtu mzima kabla ya ubatizo wa hatari
- Mungu yupo mmoja. Bwana wetu na Baba yetu, mwenye kuwatunza watu wema mbinguni na kuwaadhibu watu wabaya motoni milele (Mt. 15:41,46)
- Katika Mungu mmoja kuna nafsi tatu: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu (Yoh. 14:16, 17).
- Nafsi ya pili alishuka duniani akajifanya mtu, akatuokoa utumwani mwa shetani, akatufundisha mambo gani tusadiki, mambo gani tutende, akatupa alama ya ukombozi wetu ndio ubatizo.
- Ubatizo wafuta kabisa uovu wa mtu na kutakasa roho zetu.
- Mwenye kubatizwa atubu na kurudisha alichoiba na kupatana na maadui n.k
Recent Comments