Vituko Vya Mwaka Mpya
Wale wa kupenda kupewa pewa namba za simu soma hii
Unaomba namba ya simu ya mdada af anakunyima ila unalazimisha akupe anaona kuliko muendelee kuongea bora tu akupe anakutajia 071112016 unafuraahi unaondoka unafika nyumbani unajaribu kuipiga but kabla hujapiga unagundua alikutajia tarehe ya leoย Wadada acheni hizoย ๐๐๐๐๐๏ฟฝ๐๏ฟฝ๐๏ฟฝ๐
Hawa wanaume wanaopenda wanawake hovyo barabarani wamepatikana, hawatarudia ๐๐๐
Marafiki wawiliย (Jose na Ben)ย walikuwa wanatembea mtaani akatokea mwanamke akarusha busu kwa mmojawapo kupitia dirishani katika jengo la ghorofa tatu.
Wakaanza kujadiliana kama ifuatavyo:
Ben:ย Muone yule mrembo amenirushia busu
Jose:ย tafadhali achana na huyo mwanamke, usimjali..
(baadae yule mwanamke akamuashiria aende)
Ben:ย yule mwanamke ameniita!
Jose:ย Rafiki yangu, usiende. Nakutafadhalisha.
Ben:ย Kwa nini unaniambia nisiende Wakati mrembo kama yule ananiita? Huo ni wivu
Jose:ย Ben, Ninakutafadhalisha tena, usiende, tafadhali usiende kuleย (akihisi kutotiliwa maanani)
(Rafiki yake alimpuuza na alienda kwa yule mwanamke, mwanamke alishuka kukutana naye na wakapanda juu. Ghafla wakiwa wanataka kuanza taratibu za kula uroda, wakasikia mlio WA gari getini).. ๐๐
Lady:ย _(akiangalia kupitia dirishani)_
Oooh! Yule ni mume wangu!!
Ben:ย Mama yangu !
Nipo matatani, kweli ? ..!!
Lady:ย Usiwe na khofu, jifanye kuwa Dobi na anza kupiga pasi hizo nguo
(akimuonyesha lundo la nguo)
(Ben alitumia masaa matano kukamilisha kunyoosha zile nguo kwa sababu yule mume hakutoka tena siku ile)
(Siku iliyofuatia Ben alikwenda kwa Rafiki yake)
Ben:ย Kaka, unaweza kuamini Jana nimepiga pasi nguo kwa masaa matano???
Jose:ย Lakini nilikwambia usiende. Nguo zote hizo ulizonyoosha,ย Nilizifua Mimi Juzi!!
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
When an experienced person speaks โฆ ๐you must listen..!
Mzunguko wa elimu kiafrikaafrika
01.๐ Wale wanafunzi walioongoza Mashuleni, wanaenda kwenye Engineering na Medical school.
02.๐ Wale waliokuwa wa pili, wanachukua MBA na LLB na kuja kuwa Mameneja wa wanafunzi walioshika nafasi ya kwanza.
03.๐ Wale waliokuwa wa tatu, wanageukia Siasa na kuwaongoza wote hapo juu. Yaani wa kwanza na wa pili.
04.๐ Wale waliofeli, wanaenda Jeshi, hawa wakigoma, basi hao wa juu wote hawana raha.
05.๐ Wale waliopata Zero na waliokataa shule wanakuwa waganga wa kienyeji, wote hapo juu watamtafuta huyu, pale mambo yao yanapokwenda kombo. Tuache kudharauliana, kila mtu ni boss akiwa kwenye nafasi yake. ๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Maisha ya Pwani ni Shidaaaaah
๐๐ ๐๐๐๐๐๐ Jamaa kagombana na mkewe, akasusa kula๐ฝ๐จ kurudi kazini kamkuta mkewe amevaa kanga imeandikwaย ukisusa wenzio walaย ilipofika asubuhi mke akavaa kanga imeandikwaย ukitoka ๐ถ๐ถmwenzio anaingia๐๐
jamaa akagoma kwenda kazini ๐ฌ๐ฌ mke akabadili kanga na kuvaa iloandikwaย nimemdhibiti ndo mana hatoki๐ท jamaa akaenda kuomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa twende nyumbsni kwako, walipofika walimkuta mke kavaa kanga imeandikwaย ulidhani rafiki yako kumbe adui yako๐ค๐ค jamaa akaamua kusafiri siku tano ili kupunguza hasira. Aliporudi akamkuta mke amevaa kanga imeandikwaย ni bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
hata kama hupendagi ujinga kwa maneno ya kwenye kanga utasanda tu
Swali la kizushi kwa wadada wanaovaa mawigi
Hivi wadada mnaovaa mawigi.
๐๐ฝย Utajisikiaje siku Boyfriend wako anaingia chumbani halafu anatundika NDEVU kwenye henga๐คฃ
Cheki kilichotokea stesheni ya treni, mambo mengine ukipaniki inakula kwako kama huyu jamaa
Jamaa Wawili Walifika Stesheni, wakakuta Treni ndo kwanza inaondoka. Wakaanza Kuikimbiza. Mmoja akafanikiwa kupanda akaondokaโฆ
Yule aliyebaki akaanza kucheka sanaa mpaka machozi yakamtoka. Watu wakamuullza, unacheka nini sasa wakati umeachwa? Akawajibu: “kinachonichekesha, yule aliyepanda alikuwa ananisindikiza.
Wazo la asubuh – penzi la kuku
Wazo la asubui
๐Penzi la kuku sekunde 2 ila vifaranga kibao.Lakini binadamu masaa kibao mtoto 1 au 2. Sasa binadam na kuku nani JEMBE? Ukimwona JOGOO popote piga SALUTI!๐๐๐๐๐๐๐๐ukinuna poa tu!!!!!๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Wanaume wote ni waaminifu
Hii ni kwa wanaume ila mwanamke anaweza kusoma na kujifunza kuwa wanaume wote ni waaminifu.
Mwanaume mmoja alienda kukata miti kwa ajili ya mkaa, bahati mbaya panga likadondokea mtoni, akaanza kulia sana. Malaika akatokea na kumuuliza kwanini analia. Jamaa akajibu; “Panga langu limedondokea mtoni na ndilo ninalotegemea kuendeshea maisha yangu”.
Malaika akazama mtoni na kuibika na panga la DHAHABU na kumuuliza, ndio hili?
Jamaa: Hapana.
Malaika akazama tena na kuibuka na panga la SHABA na kuuliza, ndio hili?
Jamaa: Hapana.
Malaika akazama tena mara hii akaibuka na panga la CHUMA na kuuliza ndio hili?
Jamaa: NDIYO.
Malaika akafurahishwa sana na uaminifu wake hivyo akampa mapanga yote matatu. Jamaa akafurahi sana.
Siku nyingine jamaa alikuwa anatembea na mkewe njiani ghafla mke akadondokea mtoni, jamaa akaanza kulia. Malaika akatokea na kumuuliza: Kwanini unalia?
Jamaa: Mke wangu kadondokea mtoni na nampenda sana.
Malaika akazama mtoni akaibuka na WEMA SEPETU na kuuliza; “huyu ndiye mkeo?”
Jamaa: NDIYO.
Malaika akakasirika sana na kumuuliza: kwa nini umenidanganya?
Jamaa: Nimesema ndiyo kwa sababu ningesema hapana ungezama tena na kuibuka na AUNT EZEKIEL na ningesema hapana tena ungezama na kuibuka na MKE wangu alafu ningesema ndiyo ungenipa wote watatu!
Sasa mimi maskini sina uwezo wa kuhudumia wote hao, ndio maana nikasema NDIYO kwa Wema Sepetu.
*FUNDISHO*
Wanaume huwa hatusemi uongo bila sababu na inakuwa sababu maalumu kwa faida ya wote.
WANAUME WOTE NI WAAMINIFU. Hii ndiyo kauli mbiu yetu.
๐๐๐๐
Kilichotokea Leo mahakamani
Leo nimeenda mahakamani, mara judge akasema..
Order! Orderโฆ
Mimi na kiherehere changu nikasema.. Chapati .. Maziwa na ovacado tatu โฆ
Nimewekwa kwa karoom kengine hapa kanagiza..
i think wananiandalia chapati
๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Cheka na methali
1.Simba mwendapole =Huyo ni Sharobaro
2.Asiyefunzwa na Mamae= Ujue Mama hajapitia Ualimu
3.Zimwi likujualo= Lilikuona Sehemu.
4.Chelewa Chelewa= Ukizikusanya utapata Ufagio.
5.Hakuna Masika= Wakati wa Kiangazi.
6.Mpanda Ngazi= Asiwe Mwoga kuanguka
7.Dua la kuku=
Bismilah rahman rahim
11.Penye wengi= Pana Ajali au Tukio
12.Ukiona vyaelea= Ujue ni vyepesi.
13.Mwenye nguvu= amekula ugal wa dona(โฆ..)














































































I’m so happy you’re here! ๐ฅณ
Recent Comments