Hii bahati mbaya hii haifai kusema Samahani
(KIFO NI NIN)
KIFO ni pale unapokosea text na kumtumia
BABA yako kipindi mnakula
“hello Mrembo”๐๐
Kama utazubutu kusema Samahani ๐
(KIFO NI NIN)
KIFO ni pale unapokosea text na kumtumia
BABA yako kipindi mnakula
“hello Mrembo”๐๐
Kama utazubutu kusema Samahani ๐
Mimi Nimecheka sana
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
ZIARA ZA KUSHTUKIZA๐๐
Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti, na msikilizaji mzuri wa redio, huwa naangalia luninga mara chache sana kama nikibahatika kupita mahala kuna luninga. Sasa wiki hii nimesikia mengi kuhusu hizi ziara za kushtukiza za viongozi wetu, nikaona hili ni jambo zuri tena linafaa kuigwa na sisi wananchi wapenda maendeleo. Nikaona nijipange na mimi nifanye ziara kadhaa za kushtukiza katika sehemu mbalimbali zinazonihusu.
Nikaona nianze na ziara ya kushtukiza pale shuleni kwa huyu mwanangu, maana kila siku anakunywa chai na kuondoka na daftari zake na mie sijawahi kwenda shuleni kwao toka nilipomuandikisha shule mwezi Januari. Nilifika shuleni na kumuona mwalimu mkuu, ambae alianza kutetemeka nilipomuambia kuwa nimekuja pale kwa ziara ya kustukiza, sijui alidhani mi ni mmoja wa Mawaziri wapya, maana nilimuona jasho linamtiririka ghafla. Akanikaribisha ofisi yake iliyokuwa na vitabu kila kona, na kuita waalimu wote na kunitambulisha kuwa ni kiongozi nimekuja kwenye ziara ya kustukiza.
Nilipojitambulisha kuwa ni mzazi, waalimu wote nikawaona waanza kupumua kwa raha. Nikawaambia kuwa mimi nina mwanafunzi pale na nilikuja ziara ya kustukiza kujua maendeleo yake. Baada ya mwalimu mkuu kusaka jina la mwanangu nae akanambia, โMzee huyu mtoto hajaja shule mwezi wa tatu sasa, tulijaribu kukutafuta ikashindikana, hatujui yu wapiโ Jasho likaanza kunitoka mimi, yule mtoto kila asubuhi nampa nauli anaenda shule, na mara nyingi ananiomba michango kumbe hata shule haji. Niliondoka bila kuaga presha ikiwa juu.
Nikaona niende kwenye genge la mke wangu nae nikamfanyie ziara ya ghafla nimhadithie mambo ya mwanae, nilipofika pale nikakuta kuna mdada mwingine anauza genge. Nikamsalimu, na kumuuliza mwenye genge ntampataje, jibu lake lingeniua kama ningekuwa si mkakamavu, โMume wake kaja kumchukua na gari wameenda kununua shamba Bagamoyoโ. Nikaondoka nimechanganyikiwa, nikajuwa hapa dawa yangu moja tu, nayo ni Sabrina, mtoto wa Kinyaturu pale ambapo nikipata maudhi huwa naenda kubembelezwa.
Nikatwanga mguu kwa Sabrina nae nikamfanyie ziara ya ghafla ili anipoze moyo. Nilipogonga mlango wa chumba chake akatoka mbaba wa miraba minne, akanisalimia kwa upole, โSalama kaka unasemaje?โ Jibu likanitoka โSamahani mie nilimkopesha huyu dada wa chumba hiki vitenge, nilikuja kuuliza kama ameshapata hela yanguโ Ziara za kushtukiza zinataka moyo wa chuma jamani
Mapenzi ni balaa
Mapenzi ujue yanawez kukupa stress adi mama ako akikuuliz what’s wrong๐ค-โunawez kumjib MAMA WE BADO MDOGO UWEZ ELEW๐คฃ๐คฃ๐คฃ
Nimekuja kwa Rafiki angu kumtembelea kaacha maji jikon yeye kaenda kununua unga. Huku mm nikaongeza maji pale jikon. Kumbe yy aliweka maji saiz ya unga wake peke ykeโฆ Sasa hiv TUNAKUNYWA UJI hata hatuongeleshani. Kimbelembele changu kimeniponza.. ๐๐๐๐
Mchaga alinunua mbuzi akamwambia mpishi Nyama nusu ipike pilau na ingine itie kwenye friza. Kichwa fanya supu, miguu fanya mchuzi chukuchuku. Ngozi usitupe tutafanya mswala, utumbo pikia ndizi na mifupa tutawauzia wenye mbwa. Kinyesi kihifadhi kwa mbolea ya bustani.
Mpishi akamuuliza Hutaki na sauti ya mbuzi tufanye ring tone kwenye simu yako? Mchaga akajibu Yesuu! hivi inawezekana? bac fanya hivyo tuwauzie na wengine hiyo ringtone. Chezeya mchaga!
JE UMESHAWAHI KUONA SMS MAFUA?
Cheki hii hapaโฆโฆ..
“Mabo dugu yagu mziba? Bwada nasubuliwa sada na bafua baka dashindwa kuadika beseji do hayo dugu yagu.
Diobeeni dipone
๐๐๐๐๐๐๐๐
Hapana Chezea
Bafua
๐Ujinga wa ndoto ndiyo huu
โขโขUtaota umeokota dolla ukiamka emptyโฆ
โขโขUtaota umeokota dhahabu ukiamka kitandani patupu daadeeki OTA Sasa UMEKOJOAโฆ..
๐๐๐๐๐๐
Kitambo tukiwa watoto ulikuwa unaitwa uje ule kwa lugha tofauti kulingana na chakula kilichopikwa siku na muda husika
1. UGALI NA KUNDE
Mwitaji : ๐ฃJoniiiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Uje ukule
2. UGALI NA SAMAKI
Mwitaji: ๐ฃ we Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Unaitwa na Mama
3. WALI NA NYAMA/KUKU
Mwitaji: ๐ฃ Joniiii
Mwitikiaji : Eeeh
Mwitaji : Shauri yako!
๐๐๐๐๐๐
WALEVI WAWILI KATIKA MAZUNGUMZO YAO
MLEVI 1ย hivi rafiki yangu china ni mbali kweli
MLEVI 2ย sidhani mbona pale kazin kuna mchina anakuja na baiskeli
๐๐๐๐๐
Wanaume wana upendo kwa kweli.
Mwanaume hata akipewa kundi la wanawake 90 achague mmoja!! Hata akichagua mzuri kupita wote bado roho itamuuma kuwaacha wale 89 waliobaki!!*
Kwa namna hii wanaume wana Upendo Sana
๐๐๐๐๐๐
Recent Comments