Vituko Vya Kutumia Watu
Kilichompata huyu jamaa akiwa anaangalia mpira mechi kali na mke wake
WIFE: Baibie, yule ni nani? Ni Chris Brown??
HUSBAND: Yule ni Theo Walcott
WIFE: ile Yellow Card ni ya nini?
HUSBAND: ile ni ya Onyo, na Red Card inamaanisha mchezaji awache kucheza na atoke inje ya uwanja.
WIFE: Oooooh! Inakaa kama traffic light! Yellow- Ilani na Red – Simama
HUSBAND: Yeah yeah swity! Ndio hivyo.
WIFE: Na je Green Card??
HUSBAND: Aaaah! Hakuna kitu kama hicho.
WIFE: Nataka Arsenal ishinde world cup.
HUSBAND: [kimya]
WIFE: Ni nani yule mzee anakaa kama Mr. Bean??
HUSBAND: Yeees swity, yule ni kocha wa Arsenal, anaitwa Arsene Wenger.
WIFE: Oooooh! inamaanisha yule kocha mwengine ni Chelsea Wenger??
HUSBAND: [Kabadilisha channel]
Duh! Hiki nacho chombo cha moto?
_Sheria inasema kila anaetembea na chombo cha moto barabarani sharti awe na leseni._
_Sasa hawa wauza kahawa mbona wanatembea na chombo cha moto lakini hawakamatwi ๐ก._
_Hizi sheria zinapendelea._
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Punguzeni pombe. Cheki kilichompata huyu
Jamani punguzeni pombe,kuna jirani yangu amerudi amelewa sasa nachungulia dirishani naona anagonga mlango wake takribani masaa mawili,wakati hapa anaishi peke yake, kwakuwa sipendagi ujinga nimetoka nikamwambia mwenyewe kasafiri.Nae kaondoka.
Huyu panya wa tatu ni noma
๐ ๐ ๐ย Panya watatu walikua wakibishana nani Ni noma zaidi
Panya 1:ย jamani mimi ni noma Wiki hii nimekula rat rat(sumu ya panya) mara tatu na sijadedi !!!
Panya 2ย Wewe unasema nini, mimi nimekula nyama ikiwa
kwa mtego mara 5 nasijawahi dakwa
RAT 3ย Mmemaliza? Mie hata sijui mnabishana nini? Mimi hii mimba niliyo nayo ni ya paka !!!
Panya WA 1 na 2 wakazimia๐๐๐๐๐
Panya wa 3 huwa hapendi ujinga kabisa
Hii ndio ngoma droo kwa wanaume kati ya wanawake
{ NGOMA DROO}
Sikuizi utawasikia wadada wakisema kuachwa na mwanaume asie na pesa nisawa na kuluhusiwa hospital
{Sasa na sisi} wanaume tunasema
Kuachwa na demu mpenda pesa nisawa na kumaliza mkopo benk ๐๐๐๐๐๐
Wanaume atutakagi ujinga!!!! Wanaume heeeeee๐๐พโโ๐๐พโโ๐๐พโโ๐๐พโโ
Huyu mtoto kaongea point kweli, angalia anachomwambia baba yake
Mtoto alimwuuliza baba yake,
Mtoto: Baba unaweza kumwachia hilo gari lako house boy/girl akaliendesha?
Baba: siwezi kumwachia gari langu hili aliendeshe ni ghali sana.
Mtoto: je mnaweza kumwachia chumba chenu house boy/girl kikiwa wazi na mkaenda kazini?
Baba: haiwezekani kamwe kuna vitu vya gharama na pia heshima haitakuwepo.
Mtoto: unaweza ukampa house boy/girl ATM CARD yako na namba ya siri ukakuchulie pesa?
Baba: mtoto unatafuta balaa sasa, unataka siku akiiba hii card akachukue pesa zote tuwe maskini, sithubutu.
Mtoto: aahaaaaaa, kumbe hauwezi kumkabidhi chochote chenye thamani house boy/ girl, sasa kwa nini mnanikabidhi mimi kwa house boy/girl na nyie mnaenda kazini mpaka mnarudi kumbe mimi sina thamani kwenu eeeeh!
Kifahamu Kidada kimbea kilichofukuzwa kazi
Unafahamu?
Kile kidada kimbea kinachosemaga salio lako halitoshi kimefukuzwa kazi saivi kupiga simu ni bure mjulishe na mwenzako
๐ฒ ๐ฒ
Duh, hii sasa kazi
Wakati unafikiria dingi yako afe ili urithi nyumba, dingi nae anafikiria uanze kufa ili apangishe chumba unacholala.. hiyo inaitwa kufa kufaana.. ๐๐๐๐๐๐๐๐๐ #Hatutaki ujinga
Wazo la asubuh – penzi la kuku
Wazo la asubui
๐Penzi la kuku sekunde 2 ila vifaranga kibao.Lakini binadamu masaa kibao mtoto 1 au 2. Sasa binadam na kuku nani JEMBE? Ukimwona JOGOO popote piga SALUTI!๐๐๐๐๐๐๐๐ukinuna poa tu!!!!!๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Recent Comments