Vituko Vya Kushare

Misemo 10 bora ya kuchekesha itakayokuacha mdomo wazi

1. Mwanaume hata awe bahili vipi, hawezi kumpa mwanamke mimba nusu.

2. Hata uwe na magari mangapi chooni utaenda kwa miguu.

3. Kama ubinadamu kazi mbona hatupewi mishahara?

4. Ukichanganya wali na choroko unapata mseto, lakini hautibu malaria.

5. Hata njiwa nae ana makinda, lakini hawezi kuwa spika wa Bunge.

6. Hata uwe na haraka vipi kwenda Zenj, huwezi kupanda Jahazi ya Yusuph Mzee.

7. Umeme hauna kiuno lakini unaongoza kwa kukatika.

8. Hata uwe kauzu vipi, huwezi kujamba wakati unatongoza.

9. Hata uwe na imani kali vipi, huwezi kusali wakati unafanya mapenzi.

10. Hata kizibo ni mfuniko lakini hauwezi
kufunika sufuria.

Mume mgonjwa kazua mpya baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospitali alipokuwa kalazwa

John aliruhusiwa kwenda nyumbani kutoka hospital ya
Vichaa, akapakiwa ktk ambulance hadi karibu na
nyumbani kwake, akaulizwa kwako unapakumbuka?

akajibu ndio nyumba yangu ilee, mara wakatoka
watoto wawili wamevaa uniform akasema watoto
wangu walee wanakwenda shule..
Akatoka mwanamke akasema na mke wangu yulee,
Ghafla akatoka mwanaume john akasema mimi
yuleeeeeeee…. naenda kazini!! JE, NI KWELI
AMEPONA??

Angalia kilichotokea baada ya dogo kupewa ada na kuitumia kubeti

Dogo kampigia simu baba yake;
DOGO: Baba katika zile shilingi laki mbili ulizonipa
nikalipe ada nimetumia shilingi alfu 30 kubeti
BABA : Unasema nini we mpumbavu mshenzi
mkubwa? Nimekukanya mara ngapi kuhusu kubeti?
DOGO : Lakini baba
BABA : Lakini baba nini ngoja urudi utaona
ntakachofanya.
DOGO : Nilitaka kukwambia kuwa nimeshinda
shilingi milioni 3
BABA : Ndio hayo ninayosema wewe mpumbavu
sana kwanini hukutumia laki nzima kubeti? Si
ungepata pesa nyingi zaidi? Ngoja urudi niwataarifu
ndugu zako kuhusu uulivyo na akili za kuamua
haraka mwanangu mpenzi…

😂😂😂😂😂😂😂😂😂

Alichofanya maasai baada ya kupanda Tax

Baada ya kupanda daladala aina ya DSM kutoka Mbagala chalambe mpaka Mwenge na kulipa sh 500.Masai akachukua tax wakati wa kurudi.walipofika sasa shughuli ilikuwa hivi.

Masai: we dureva? Naulisa Ng’ombe na mbusi ipi ngali?
Dereva: Ni ng’ombe ghali Masai.
Masai: kwanini Ng’ombe ngali?
Dereva: kwa sababu ni mkubwa zaidi ya mbuzi
Masai: umepata..na mbusi na kuku ipi ngali
Dereva: ni mbuzi kwa sababu nae ni mkubwa kuliko kuku.
Masai: Umepata..
Masai: sasa me nimekwenda kule mwenge kwa ngali kubwa nikalitoa sh. 500 hii yko ndogo unasema nikupe 40,000 wewe acha wizi.. Nitakupa 250 Tu..wee acha lbia morani…!!!

Alichofanya mke baada ya mme wake kupenda kumchunga sana

Alifanya hivi;
Siku ya kwanza

MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa blender nisikie…..mke­ akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja

Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha blender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili

Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na blender toka asubuhi

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About