Vituko Vya Katikati Ya Wiki
Huyu jamaa kawaweza wapenda vya bure
Jamaa kaingia mgahawani kwa fujo
JAMAA :Β Nipe soda moja na kila mtu mpe yake maana ninapokunywa soda napenda kila mtu anywe
WATU :Β Ha! Ha! Ha! Haaaa!
JAMAA :Β Nipe mchemsho na kila mtu mpe wa kwake maana ninapokula mchemsho napenda kila mtu ale wake
WATU:Β Watu weweeee! Tena safari hii Na makofi juu..
JAMAA :Β Mhudumu, nipe bili na kila mtu mpe yake maana ninapolipa bili napenda kuona kila mtu analipa yake
πππππππ
Wanandoa wa Kijapani wakibishana
*Wanandoa wa Kijapan wakiwa wanabishana hadharani*
*Husband: Takamushi jiku.*
*Wife :hashi jiku mishihe*
*Husband: inamoto kushini hat a pi*
*Wife: jejeta takuna mota shinita*
*Husband: kituya sitina kutara*.
*Wife: totori yatika miniya*
_Uko busy kusoma utadhani unaelewa kijapan kuwaga serious saa zingine_
ππππππ
Unakumbuka haya enzi za shule?
Kama umesoma st Kayumba utakuwa una aidia na hayaβ¦
1.Unaenda shule umechelewa unakuta mwalim anakamata wachelewaj unaamua urudi nyumbani
2.unachukua kimbegu cha ubuyu unasugua sakafuni af unamuunguza mwenzio
3.mkiruhusiwa tu unakimbia unataka uwe wa kwanza kwenye njia yenu y kurudia nyumban
4.MTU akikukera unamfungia shule (mnapigana baada ya kufunga shule)
5.MTU akikunyima kitu chake unamwambia “Ahaa eeh utaona sa nne”
6.wadada wembamba ndo wanaongoza kwa kusuta wenzao
7.ukiibiwa daftar jipya unalia kuliko hata uliloandika
8.unajaza mapeni kwenye mkebe(compass) na mengine hayaandiki
9.vifaa vingine kwenye mkebe hujawahi hata kuvitumia mfano bikari labda utolee mwibaπ
10.hakuna habari nzur kama kuambiwa Leo hamna shule mwalim haupo
11.habari mbaya zaidi n kurud nyumban kutoka shule una njaa af unaambiwa chakula mgeni kaja tumempa
12.mtoto wa mwalim utamgundua tu kwanzia sweta begi na viatu vyake
13.usiombee umpige mtoto wa mwalim utataman uache shule
14.unatengeneza kifutio cha ndala af unatishia eti kinafuta hadi peniπ
15.ukaguzi na huna ufagio.. unaomba chelewa kwa watu af unaongeza kijiti katikati
16.siku ukienda na ufagio wanakagua maji, ukienda na naji wanakagua kuni au mboleaπ
π
Dah shule zetu hizi kiboko!!
Ipi umeipitia wewe
Share na wengine
Je, hili nalo ulilipitia ulipokua Shuleni?
Hakuna Kitu Kilikua Kinaniumizaga Kipindi Nipo Shuleni.
Time Mmetoka Kwenye Mitihani Wa Mathematics Halafu Mpo Kikundi Fulani Either Mnarudi Nyumbani Au Mnapumzika Kwa Ajili Ya Next Exam.
Unasikia Jamaa Wanabishana Pale Jibu Lilikua 4 Mwingine Anasema 5, Na Wewe Ulijaza 80.
Mvua zazua kasheshe! Soma hii..
Baba- : Halloo mke wangu.. yaani ni shida sitaweza kurudi nyumban, daraja limevunjika na kutoka morogoro kurudi dar haiwezekani
MAMA:- Mme wangu morogoro ulienda bila kuniaga! ?
BABA:- Ilikuwa ni ghafla sana mke wangu sikuweza kukwambia
MAMA:- kha! Sasa watoto nani atawaangalia
BABA:- Unasemaje! We uko wapi kwan
MAMA:- Niko bagamoyo na daraja limeondolewa na maji sitaweza kurudi.
BABA:- Unasemaje we mwanamke.. nakwambia nikukute nyumban ndani ya dk 15
Baada ya dk 15 Baba kafika nyumban.
MAMA:- Haya umefkaje kutoka morogoro?
BABA:- Nimepewa lift na helkopta ya Mbowe..
Kama umeipenda shea na rfiki zakoooβ¦..
Cheki tabia za kuandika vimaneno vya ajabuajabu kwenye pikipiki na bodaboda ilivyomponza huyu
Jamaa mmoja dereva wa bajaji alianguka, sasa bajaji ikawa imem’bana akawa anafurukuta bila mafanikio Cha ajabu watu wakawa wanampita bila kumsaidia, Kumbe Nyuma ya Bajaji yake alikua Kaandika “NIACHENI KAMA NILIVYO, HII NDIO STYLE YANGU”Β πππΒ Mpaka sasa nimemwacha bado yuko hapoΒ *Sipendagi Ujinga mimi* πΆπ½πΆπ½πΆπ½πΆπ½πΆπ½
Jambo la kufanya kama binti alikuachaga zamani na sahizi anakutaka
Kuishi kijijini kunahitaji moyo sana
..unaenda kuoga, unakumbuka kuwa umesahau sabuniβ¦unaenda kuchukua sabuni kurudi bafuni, unakuta ng’ombe amekunywa maji yote..unaamua kufuata mengne,unarudi unakuta mbuzi kala sabuniβ¦ππππ
Maisha ya kijijini hadi raha!!
Jamaa alimfumania mtu anazini na mkewe,
Akamtoza Faini ya sh 5000 tu,yule mtu akatoa 10000.
Jamaa akasema lala nae tena sina chenji!πππππππ
Majibu ya mkato ya kuchekesha Kutoka Kenya
Njeri:Β Roysambu ni ngapi?
Makanga:Β Roysambu ni moja tu. Pengine kama Chinese wamejenga ingine.
Odhis:Β Hii gari haina watu bana.
Makanga:Β Kwani hao wawili wenye wamekaa hapo ndani ni ngβombe?
Man:Β Wekeni nyimbo za Yesu tafadhali.
Makanga:Β Yesu bado hajatoa album. Akitoa tutaeka.
Mwikali:Β Excuse me condaβ¦gari za Mwingi zinapandiwa wapi?
Makanga:Β Ziliacha kupandwa juu hazimei.
Man:Β Kwani mwisho wa gari ni wapi?
Makanga:Β Mwisho ni hapo penye number plate iko.
Karis:Β Ruaka ni how much?
Makanga:Β Sijaskia Ruaka ikiuzwa. But nikiskia nitakwambia.
Passenger:Β Shukisha dere.
Makanga:Β Tukishukisha dere utaendesha gari?
Johnny:Β Maze, hii gari iko na joto sana.
Makanga:Β Basi shuka upande fridge
Recent Comments