Visa Vya Kukuparaha
SMS Mafua ndiyo hii
JE UMESHAWAHI KUONA SMS MAFUA?
Cheki hii hapaโฆโฆ..
“Mabo dugu yagu mziba? Bwada nasubuliwa sada na bafua baka dashindwa kuadika beseji do hayo dugu yagu.
Diobeeni dipone
๐๐๐๐๐๐๐๐
Hapana Chezea
Bafua
Cheki huyu dingi alivyo mnoko
Unamtumia baba ako meseji ukiwa shule “Baba naomba unitumie 100,000 ya pckt mny” anakuuliza “pckt mny” ndo nini? Unamjibu ni kifupi cha “pocket money” af ankutumia 10,000, unamuuliza hiyo hela ni ya nini? Anakwambia ni kifupi cha 100,000.
Hapo ndo unatamani kuchoma shule ufe.
Angalia alichojibu huyu mwanafunzi, Ungekua wewe ni mwalimu wake ungemfanyaje?
Mwanafunz alikuwa kila siku anachelewa shule, na kila siku alikuwa anachapwa, basi siku moja mwalimu akaona ngoja amuulize.
Mwalimu: Mbona unachelewa kila siku?
Mwanafunzi: Nakaa mbali mwalimu
Mwalimu: (huku ana hasira akauliza)Mbali mbinguni?
Mwanafunzi: Mbinguni kwa mbele๐๐๐๐๐
Angalia kilichomkuta huyu msanii wa mziki na mashabiki wake
Msanii mmoja anaitwa ”KINYA” alikuwa ana perfom jukwaan..!!!
Kawaida kila msanii lazima ajitambulishe, mfano:-
”YEAH NI TEMBA hapa au
YEAH NI CHEGE hapaโฆ!!!
Yeye akasema: “YEAH NIKINYA HAPAโฆ!!!”
Watu wakapiga kelele ”UTAZOAAA” mwenyewe bwenge wee
JE, WEWE UNGEJITAMBULISHAJE NAITAJI JIBU LAKO TUONEโฅ
Gari na mke nini muhimu?
GARI YA MILIONI 50
UNALAZA NJEโฆ
mke wa laki sita
unalala nae ndaniโฆ.
BANGI SI NZURI JAMAN
๐๐๐๐๐๐๐๐
Njia 3 rahisi za kuondoa kitambi
JE, una KITAMBI na unataka kukiondoa?
FANYA HAYA;
1. Kopa mkopo mkubwa benki
2. Nunua gari bovu la biashara
3.Oana na mke mwenye kelele.
Ukiona miezi mitatu hakijaisha basi ujue umevimba BANDAMA sio kitambi..
Ikitokea hii kwenye chumba cha mtihani
Upo kwenye chumba cha mtihani,
maswalii yamekupiga kinyama
Unaamua kuchukua smartphone ugoogle kisha ucopy na kupaste kwenye booklet yako,
Ghagfla lecturer aningia na wewe kwa woga wako unaficha calculator na kuweka simu mezani,
Hapo ndo utajua shetani naye alikua anasimamia paper.
๐๐๐๐๐
Ungekua wewe ndio baba wa Huyu mtoto ungemjibu nini?
MTOTO: Hivi Baba wewe umezaliwa wapi?????
BABA: Mbeya
MTOTO: Mama nae kazaliwa wapi????
BABA: Tanga
MTOTO: Mimi jee?????
BABA: Dar
MTOTO: Sasa tulikutanaje????
๐๐ hapo wee kama baba ungemjibuje mwanao๐ณ๐ณ๐ณ
Angalia jamaa alivyouweza huu mchepuko wake
Kuna mchepuko nilimtumia nauli jana ili aje,.kwang sasa leo kaniambia eti ” nimesahau ile line yenye M-pesa home plz nitumie tena kwa tigo mpenz””!! Me nikajifanya chizi nikatuma Kule kule kwenye voda (aliosema kaacha home) Nikatuma huko message ivi “nikuongezee Sh. Ngapi tena mpenz..!!” Akanjbu “elfu 20,000 tu mpenzi” Mtuhurumie jamani ๐๐๐
Cheki huyu jamaa alivyoumbuka akiwa ndani ya dala dala baada ya kupokea simu ya mkewe
Jamaa kapokea simu kutoka kwa mke wake ndani ya daladala
jamaa: hellow hellow ( jamaa akawa hasikii vizuri ikabidi aweke loud speaker)
Mke: Umeweka wapi soksi zako yaani nyumba nzima inanuka.
Huyu Jamaa kawaweza polisi kweli
Et jamaa kawekwa jela kwa kosa la kupoteza mamiilion.ya kampun akiwa gerezan babayake alituma barua
Ikisema yan.mwanangu tumapata shida maana shamba halijalimwa na jatujii litalimwaje na msimu ndio huo nataman.ungekuwepo ningepata msaada wa kulimiwa hili shamba
Yule kijana alijibu tafadhal baba usilime hilo shamba maana pesa zote nilizo ibwa nimeficha.huko
Kwakuwa barua zote laxima zipite kwa mkuu wa gereza ndio xiende kwa muhusika kesho yake mzee alikuwa shamba lote limelimwaa na polisi
Akatuma ujumbe tena yule kijana
Nashukulu umepata msaada sasa nazan unaweza ukaendelea kupanda mazao shamban.kwetu๐๐๐๐๐
Maujanja ya kumkalisha mwanamme wako nyumbani weekend haya hapa
Siku hizi wa naume licha ya kukimbia nyumba zao kwa kisingizio cha kazi maajabu weekend hasa Jumamosi utasikia wanaaga nafika hapo njiani naja naenda kununua gazeti.
Kumbe wanaenda kunywa supu unasubiri wee mpaka alasiri au jioni
Hivyo wanandoa wengi hili limekuwa tatizo mwanaume kiguu na njia asb mchana na njia kumuacha mama na watoto.
Nini kifanyike hasa weekenda Mwanaume ashinde NYUMBANI akikupumzikia??
Zipo njia nyingi mojawapo SUPU YA WEEKEND NA MAZUNGUMZO NA MKAO
Ni kweli wanawake wengi hamjuagi kuwakalisha waume home.
Anza hivi
Siku uko home wewe amka mapema kabla yake anza makeke jikoniโฆ
Mara blenda priiiiiโฆ juiceโฆ ama milk shakeโฆ. hahahaha..Utaona anasogea jikoni..
Wakati anakunywa juice ama milk shakeโฆAnza kukuna naziโฆ
Chambua mnafuโฆ
Hapo jikoni kuna kanyama kanachemkaโฆ katia kitunguu tupia viazi 2 na ndizi.Hahaha..
ile harufu ikianza kutoka utasikia anafuata maji jikoniโฆ hahahaha kwenye frijiโฆ wala hatumi..
Hahaahhaโฆ utasikia nini kiko jikoni?Hahahaa.
Mmiminie supuโฆ
Na ndizi mbili na kiazi kimoja kapilipili mbuzi pembeni..
Muulize kuna chapatiโฆMpe.. hahahahaha..Akimaliza supu nakuapia atasinzia..
.Akishtuka ugali na mnafu na nyama umeivaโฆMpe ale..Mshushie na glass ya mtindiโฆHahahaha..
analewa full Hata kama kuna mama junior anaambiwa usipigeโฆ
Hahahahahahaโฆ.Baada ya hapo acha apumzikeโฆ aogeโฆ
Kisha funga ka khanga kako kepesi jilaze pembeni.. woiiiiiiiii..
Mkimaliza muombe pesa ya sokoniโฆ
NAKUAPIA HATA KAMA JANA YAKE ALIKUPA ATAKUPA TENA.
Hahahahaha.. jamaniโฆ
Hahahahahaโฆ yani kwa raha ya supuโฆ nakuapia utaambiwa hata mama alipiga simu janaโฆ hahahaha.. ama utasikia mamii.. njoo uone njooโฆ unaitiwa kitu cha kwenye tv.. hahaha.
Hata hujaona mwanzo ila kwa raha yakasupu utaitwaโฆ
Hata kama huna kalio nakuambia utapigwa kibao hata cha mgongoโฆ. hahahahahahahahahaha.
Sasa wewe unaamka chai na mkate kama chuo cha uhaziliโฆ
Wali maharage kama jeshi la j
Mkwe kazua mpya, Hii dunia ina mambo sana
Mama mkwe alimuuliza mkwewe “binti” samahani mbona mtoto hajafanana na mwanangu kabisa?
Binti akajibu, “bila samahani mama huku chini nina njia ya uzazi sio mashine ya photocopy”
mama mkwe hoii!! Chezea Wakwe Wa Bongo wewe.
Angalia huyu mvulana anachomwambia huyu daktari baada ya rafiki yake wa kike kupata ujauzito
๐๐๐๐
MVULANA:ย Daktari, rafiki yangu wa kike ni mjamzito, lakini mara zote nimekua nikitumia kinga. Inawezekanaje hii?
DAKTARI:ย Ngoja nikusimulie hadithi. Kulikua na Muindaji ambaye alikua anabeba bunduki kila aendako. Siku moja, alichukua mwamvuli badala ya bunduki na akaenda nayo. Ghafla akatokea Simba mbele yake. Ili amtishie Simba, muindaji akatumia mwamvuli na kummiminia risasi Simba. Simba akafa palepale!
MVULANA:ย Sio kweli!! Lazima kulikua na mtu mwengine pembeni aliyempiga risasi Simba.
DAKTARI:ย Nashukuru umeelewa somo!!๐
๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐๐
Haya nayo ni maajabu mengine kwa wazazi wa mabinti
BABA MWEUSI
MAMA MWEUSI
na ww walikuzaa mweusi lakini umefikisha miaka 20 umeanza kua mweupe
โฆ..HAPO NDO WAZAZI WANAJIULIZA hv mbegu ilkua ya kinyonga au๐๐๐๐
Angalia nilivyookoa maisha ya mtu leo
Nmeokoa maisha ya mtu asubuhi ya leo huwezi amini.Nmekutana na ombaomba nikamuuliza atajisikiaje nikimpa sh.30,000/-
Akasema ATAKUFA kwa furaha.Nikaondoka bila kumpa ili ASIFE.๐๐๐๐
Angalia huyu Jamaa alichomfanyia mke wake jana
Jana niligombana na mke wng, Akaniambia nibebe kila kitu changu niondoke, Bas kiustaarabu tu nikachukua nguo zangu,mwishoni nikambeba na yeye nikamuweka begani nikaanza kuondoka nae
hua sipendagi ujinga, amesahau na yeye pia ni wangu
Recent Comments