Vihoja Vya Kutumia Watu

Kilichompata huyu jamaa mroho wa nyama, Hata kaa arudie tena

Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake Levi, kule sehemu za kwetu, akakaribishwa bonge ya ugali na nyama nyingi tu, wakati anakula akagundua kuwa shemeji yake, mke wa rafiki yake hali nyama;

JAMAA: Aise hili ni bonge ya lanchi hii, lakini Levi mbona sisi tu tunakula nyama shemeji Gulo hagusi kabisa anaishia mchicha tu? Tabia gani hii?
LEVI: Hapana sijamkataza, ila shemeji yako Mngoni halagi nyama ya FISI kama sisi

Mlevi kazua tafrani, angalia alichokifanya hapa

MLEVI mmoja aliingia baa akavuta kiti na kukaa mhudumu akatokea kumsikiliza.
MHUDUMU: Nikusaidie nini?
MLEVI: Eeh! nipe bia ya baridi kisaha wasikilize wote waliokaa hapa, wape bia na wao maana sipendi kunywa pombe wengine wananiangalia
Akaja mhudumu wa jikoni “nikusaidie nini?”

MLEVI: Niletee supu kisha wasikilize wote waliokaa hapa na wao wape supu sipendi kunywa supu watu wananiangalia
Safari hii watu wakapiga makofi
Baadae akamuita mhudumu
MLEVI: Niandikie bili zangu kisha waandikie wote bili zao sipendi kulipa huku watu wananiangalia

Wale wateja wakamvaa na kumshushia kichapo… teh teh teh teh teh hii kali hakuna cha bure mjini hahahaha na jasho la mtu haliliwi wandugu

Haya ndiyo madhara ya kulala kanisani

Tukiwa kanisani mdada alikuwa amelala , akaamka akasikia Pastor anasema
” SIMAMA”
Yule dada akasimama akashangaaa kanisa zima linamtizima kwa mshangao akiwemo mumewe, akaangalia kanisa zima akashtuka kujiona yeye peke yake ndiye aliesimama
Pastor akaendelea vizur endelea kusimama, tumepata mmoja hadi sasa aliyesimama narudia kwa mara ya mwisho kama hujasikia vizuri
” kama wew umewahi kumsaliti au bado unasaliti ndoa yako SIMAMA”
Binti akazimia

Tofauti ya ukopaji wa mzungu na mswahili

MZUNGU: Hi, I need $100, will pay back on Monday

MSWAHILI: Kaka vipi, shwari? Dah.. hatuonani mzee, mishe vipi, mnatunyima nini? Juzi nimekuona kwa mbaaali… mzee shavu dodo, full kipupwe! Sie tupo bwana, shida tu, afu misiba mingi tu, wife nae kajifungua ghafla. Sasa, kuna cheque naisubiri haijatoka hadi leo, wanasema itatoka next week, hapa nimekwama kweli. Naweza pata ‘Laki Moja’ ya karibu hapo nitarudisha mwisho wa mwezi…?😂😂😂😂😂

Shopping Cart
🏠 Home 📖 Reading 🖼️ Gallery 💬 AI Chat 📘 About