Vichekesho vya Watoto
Watoto wa siku hizi ni shida! Angalia huyu mtoto anachomwambia baba yake
Ka ni wewe?
DOGO: baba mi siendi tena shule inaonekana walimu hawana uhakika na majibu yao.
BABA: Kwanini unasema hivyo?
DOGO: juzi walisema 3+4= 7, jana wakasema 1+6=7, halafu leo wanasema 5+2=7 sasa huoni kama wanatuchanganya.
ungekua wewe ungemjibu nini
Dingi kauzu kuliko wote duniani ndiyo huyu hapa
Mtoto:ย Baba nitumie pesa ya matumizi huku shuleni hali ni mbaya sana la sivyo najinyonga.
Baba:ย Huku nyumbani hali ni mbaya kuliko huko shuleni kwahiyo kama unajinyonga utapunguza Bajeti, kopa Kamba dukani kwa Mangi nitalipa nikija kuchukua Maiti yako, Mungu akulaze mahali pema peponi Mwananguโฆ..
Angalia huyu baba alichowafanya mtoto wake wa kike na boyfriend wake
BABA OYEEEEEE๐ช๐ช
Soma hiiโฆ
Msichana alikuwa amekaa na baba yake kibarazani, mara akamuona MVULANA friend wake akija, yule mvulana alipokaribia tu, yule msichana akamwambia hivi:-
MSICHANA: Umekuja kuchukua kile kitabu chako, kinachoitwa “DADDY IS AT HOME?” by Ngozi Okafor
MVULANA: Hapana!, Nimekuja kuazima kitabu cha maombi kama kinaitwa “WHERE SHOULD I WAIT FOR YOU?” by Ngลฉgฤฉ wa Thiong’o
MSICHANA: Aaah! Hicho sina ila ninacho kimoja kinaitwa “UNDER THE MANGO TREE” by Chimamanda Adichie
MVULANA: Ooh! Vizuri, Basi usisahau kuja nacho kesho kitabu cha Okot p’Bitek kile kinachoitwa “CALL ME IN 5 MINUTES BEFORE” Utakapokuja shule.
MSICHANA: Usijali, tena nina kitabu kipya kinaitwa “I WON’T LET YOU DOWN” by Chinua Achebe
Baba mtu akawatazama kisha akasema
BABA: Vitabu vyote hivyo, mbona vingi sana, atavisoma vyote kweli
MSICHANA: Ndio Daddy, huyu mvulana yupo smart sana na ana akili atavisoma vyote hivyo!
BABA: Sawa! Usisahau kumpatia na kile ambacho nimekiweka pale juu ya meza, kinaitwa “I AM NOT STUPID, I UNDERSTOOD EVERYTHING YOU’VE BEEN SAYING” by Shakespeare!
Na kuna kingine nimekiweka juu ya kabati la vyombo, kinaitwa “IF YOU GET PREGNANT PREPARE TO GET MARRIED” by Wole Soyinka.
Recent Comments