Vichekesho vya Watoto
Soma huyu mtoto anachosema sasa, Ndoto za watoto bwana! Kazi ipo!
Mwalimu aliingia darasani na kuwauliza wanafunzi juu ya ndoto zao za baadae.
MWAL: John we unataka ukiwa mkubwa uwe nani?
JOHN: Nataka niwe daktari wa moyo niwasaidie watanzania wanaougua magonjwa ya moyo.
MWAL: vizuri. Na wewe Rose unataka kuwa nani?
ROSE: Nataka kuwa rubani, niweze kusaidia watu wanapenda kusafiri kw anga.
MWAL: Safi sana Rose. Utakua utakua mfano kwa wasichana wenzio kuwa na bidii kwenye masomo ya sayansi.
MWAL: Na wewe Nehemiah ??
Nehemiah : mimi nataka kuwa tajiri mkubwa sana. Niwe na nyumba Tanzania, S.Africa, Marekani na Dubai. Niwe na gari 7 za kutembelea. Kila siku nabadilisha. Leo nikipanda hii, siirudii hadi week iishe. Nataka niwe namiliki viwanda, Makampuni, ndege binafsi na mashamba makubwa. Nataka niwe na nguvu serikalini ya kuamua nani awe Rais na nani asiwe……”
Akameza mate kisha akaendelea….
“Nataka kuwa na walinzi 20 wenye silaha nzito wakinizunguka, na watumishi wakininyenyekea. Nataka kuwa bilionea ninayeogopwa. Lakini pia nataka kuwa na mke mzuuuri sana ambaye nitakuwa natembea nae kila mahali.”
MWAL: ndoto nzuri sn lakini unahitaji bidii sana kutimiza. Haya na wewe Jenny tueleze unataka kuwa nani??
JENNY: Nataka kuwa mke wa Nehemiah .!!
Kwa nini vitu vunavyoanza na “K” ni vitamu sana?
Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee wehu wako hapa!”
Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”
Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”
Alichokisema mtoto baada ya kusikia baba na mama wakiongea mambo yao usiku
MUME: Mke wangu naomba nikubusu
MKE: Sitaki
MUME: Ntakununulia pete ya gold
MKE: Staki
MUME: Ntakununulia gari
MKE: Sitaki….mtoto wao aliyekuwa kalala alisikia haya maneno ya mwisho
MTOTO: Baba basi nibusu mimi uninunulie baiskeli
BABA: Pumbafu lala huko mjinga mkubwa















































































I’m so happy you’re here! 🥳
Recent Comments